Jumapili, 6 Mei 2018

Mimi Sistahili Kumwona Kristo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

Mimi Sistahili Kumwona Kristo

Huanbao    Mji wa Dalian, Mkoa wa Liaoning
Tangu kwanza nianze kumwamini Mwenyezi Mungu, daima nimewapenda wale ndugu wa kiume na wa kike ambao wanaweza kupokea huduma ya kibinafsi ya Kristo, ambao wanaweza kusikia mahubiri Yake kwa masikio yao wenyewe. Katika moyo wangu, nimewaza jinsi ingekuwa vizuri sana kama siku moja katika siku zijazo ninaweza kusikia mahubiri ya Kristo, bila shaka kumwona Yeye kungekuwa kwa ajabu hata zaidi. Lakini hivi karibuni, kwa njia ya kusikiliza ushirika Wake, nimekuja kuhisi kwa undani moyoni mwangu kwamba mimi sifai kumwona Kristo.
Ilikuwa wakati ambapo Ushirika na Kuhubiri Kuhusu Kuingia kwa Maisha Juzuu ya1 hadi 3 zilipotolewa. Niliposikia juzuu ya kwanza, nikahisi mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu alizungumza vizuri mno. Niliposikia ushirika wa dada mmoja kwa juzuu ya pili (hii ilikuwa kabla mtu yeyote kuniambia huu ulikuwa ushirika wa Kristo), nilidhani dada huyu alikuwa ni kiongozi tu chini ya mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu, na hasa wakati alifanya ushirika kuhusu shida kuhusu jinsi ya kutazama maarifa, sikusikia mijibizo ya shauku ya ndugu zangu wa kiume na wa kike, kwa hiyo nilikuwa na hakika kuwa dhanio langu lilikuwa sahihi, na kwa sababu nilihisi kuwa huyu dada hakuzungumza vyema kama yule mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu, sikuwa nikisikiliza kwa uangalifu. Baada ya kusikia juzuu ya tatu, baada ya ushirika na mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu, nikamsikia dada huyo akisema, "Kuhusu ushirika wa ndugu huyu wa kiume sasa hivi ...," na nilikuwa na uhakika zaidi kwamba dada huyu alikuwa kiongozi chini ya mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu, kwa sababu katika ulimwengu wetu, viongozi daima huzungumza kwanza, na wasaidizi wao huzungumza baadaye. Kwa hiyo nikazima kpaaza sautii , nikifikiri, "Nitaisikiliza hii baadaye nitakapokuwa na nafasi." Siku ambayo nilipata habari kuwa huyo dada kwa kweli alikuwa Kristo nilishtuka, na hatimaye nikasikiliza kwa makini kila neno la mahubiri.
Baada ya hapo, nikaanza kutafakari: Kwa nini nilitamani sana hivyo kusikia ushirika wa Kristo mimi mwenyewe, lakini wakati alipozungumza nasi, sikuweza kuutambua? Nilianza kula na kunywa maneno ya Mungu yaliyofungamana na hali yangu, na kuona kwamba  Mungu alisema, "Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mtakuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mnamwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki kamwe mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa, mhenga, lakini hakuna yeyote anayemchukua Kristo kama binadamu wa nyama na mwili aliye na kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, huu si uovu kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umewafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si Mkubwa wa umbo, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida …. Na hivyo watu humchukulia kama mtu wa kawaida; wao kufanya wanavyopenda wanapokuwa pamoja Naye …. Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza" ("Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili). Ikilinganishwa na maneno ya Mungu, na kisha nilifikiri juu ya vile tabia yangu mwenyewe potovu ilivyojidhihirisha wakati hatimaye niliusikia ushirika wa Kristo. Nilipenda kusikia mahubiri ya Kristo na ushirika kwa masikio yangu mwenyewe, lakini wakati hatimaye niliusikia ushirika wa Kristo sikujali. Nilimwona Kristo kama mwanadamu wa kawaida tu. Hii ni kwa sababu sikuelewa kiini cha Kristo, sikuelewa yote ambayo Kristo huifanya kuendelea kuwa duni na huficha, na nilikuwa na mawazo mengi mno na fikira kumhusu Kristo. Ushirika wa Kristo, niliwaza, lazima uwe unawapendelea wale ndugu wa kiume na wa kike walio na njia yamara moja ya kumfikia Yeye, na wengine wakikosa kuruhusiwa kuusikia ushirika Wake na masikio yao wenyewe; Ushirika wa Kristo, niliwaza, ungeandamana na Kristo kutangaza hadharani utambulisho Wake; ushirika wa Kristo, niliwaza, ni lazima uongewe kwa sauti tofauti na ya wengine na katika zamu nyingi sanifu za msemo, kama aina fulani ya mtu wa ajabu; Ushirika wa Kristo, niliwaza, ungeandamana na vifijo vya msisimko, vyenye shauku vya ndugu zangu wa kiume na wa kike; na ikiwa ilikuwa mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu na Kristo wakiongea kwa zamu, kwamba Kristo angeongea kwanza, na mwanamume aliyetumiwa na Roho Mtakatifu angeongea mwisho …. Niliizuia kazi na maneno ya Kristo kwa mipaka ya mawazo yangu, kwa sababu nilimuwaza Kristo kwa namna fulani. Wakati ukweli ulitofautiana na jinsi nilivyoufikiria, nilimchukua Kristo kama mtu wa kawaida na maneno ya Kristo kama yale ya mtu wa kawaida, na wakati wengine walipata mengi kutoka kwa ushirika, sikupata chochote, na badala yake nilifichua kabisa asili yangu ya kishetani ya kiburi, ya majivuno, ya kuchukia ukweli, na nikajifanya mtu anayemkataa na kumpinga Kristo.
Baadaye, niliona katika neno la Mungu: "Kila mara mnatumaini kumwona Kristo, lakini Nawasihi msijiinue wenyewe hivyo; kila mtu anaweza kumwona Kristo, lakini Nasema hakuna ambaye ni wa kufaa wa kumwona Kristo. Kwa sababu asili ya binadamu imejazwa na uovu, kiburi, na uasi, unapomwona Kristo, asili yako itakuharibu na itakuhukumu hadi kufa" ("Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili). "Hamna moyo wa dhati katika kukabiliana na ukweli sembuse kutamani ukweli hata kidogo. Nyinyi huchunguza tu kama vipofu na kusubiri kwa utepetevu. Mtajifaidi na nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu? Kama hauwezi kuyang’amua matamshi ya Mungu, umehitimu vipi kushuhudia kuonekana kwa Mungu? … Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni hao tu waliowezeshwa kushuhudia kuonekana kwa Mungu" ("Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya" katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinifanya nielewe kwamba sikuweza kutambua sauti ya Mungu kwa sababu nilikuwa na kiburi mno, mwasi mno, na pia mwenye kupenda makuu mno, wa kujaribiwa kwa urahisi mno kusikiliza kwa makini na kukubaliana na wale walio na uwezo na hadhi, huku nikiwaangalia kwa dharau wale bila uwezo na hadhi, hivi kwamba hata kama wangesema ukweli singeusikia. Niliposikiliza ushirika sikuwa nimelenga ukweli na sikutamani kupata ukweli, na badala yake nilijitolea mawazo yangu kwa kisio na uchunguzi. Sikufichua chochote isipokuwa kiburi na uasi, fikira na mawazo. Mtu aliye na kiburi, mwasi, na asiyekubali ukweli kama mimi, mtu asiye na uchaji Mungu au shauku mbele ya ukweli kama mimi, ningewezaje kusikia na kujua sauti ya Mungu? Nilikuwaje wa kufaa kumwona Kristo?
Kupitia ufunuo huo hatimaye nilielewa kuwa ingawa nilitaka kumwona Kristo, sikuwa ninafaa kumwona Kristo kwa sababu upotovu wa Shetani kwangu ni wa kina sana, nina kiburi na ni mwasi kwa asili, sina ukweli na sina upendo wa ukweli, sielewi kiini cha Kristo, mimi huhukumu kwa ubaguzi wa upuuzi, nina fikira nyingi mno na mawazo, na Mungu ninayemwamini bado ni Mungu asiye yakini, mfano wa umbo lenye nguvu na umbuji. Na wakati kwa hakika ninapomwona Kristo, mawazo yangu yanaweza kukita mizizi na kiburi changu kinaweza kuchipua wakati wowote, asili yangu mwenyewe ya uasi kwa njia hiyo ikiniangamiza. Sasa ni lazima nijiandae na ukweli, nijitahidi kuelewa tabia yangu potovu na kiini cha Kristo katika maneno ya Mungu, na kuwa mtu anayemwelewa na kumwabudu Kristo.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

0 评论:

Chapisha Maoni