Jumatatu, 11 Desemba 2017

Swahili Christian Video | Nyendo za Mateso ya Kidini "Kuficha Uhalifu"


Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Filamu hii ya hali halisi inayoonyesha kifo cha ghafla na kisichotarajiwa cha Mkristo Mchina aliyeitwa Song Xiaolan–kifo ambacho kwacho polisi wa CCP walitoa maelezo yasiyopatana na yaliyogongana. Baada ya kuchunguza, familia ya Song iligundua kwamba polisi walikuwa wakidanganya wakati wote huo. Jamaa wa familia ya Song alipata habari kutoka kwa jamaa aliyemfahamu katika Ofisi ya Usalama wa Umma ya kwamba Song Xiaolan alikuwa akifuatiwa kwa siri na polisi wa CCP kutokana na imani yake kwa Mungu na utendaji wa majukumu yake. Polisi walipomkamata, walimpiga hadi kufa. Ili kuepuka lawama, polisi walifunika ukweli kwa kubuni eneo la kifo la Song Xiaolan....
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

0 评论:

Chapisha Maoni