Ijumaa, 26 Januari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Mwenyezi Mungu alisema, Kila siku unayoiishi sasa ni ya maana sana na muhimu sana kwa hatima yako na majaliwa yako, kwa hivyo unapaswa kufurahia kila ulicho nacho na kila dakika inayopita. Unapaswa kutumia muda wako vizuri ili uweze kujinufaisha, ili usije kuishi maisha haya bure. Pengine unajihisi kukanganyikiwa unaojiuliza ni kwa nini Ninazungumza maneno haya. Kwa kweli, Sijapendezwa na matendo ya yeyote kati yenu. Kwa maana matumaini ambayo Nimekuwa nayo juu yako si vile tu ulivyo sasa. Kwa hivyo, Naweza kuelezea hivi: Nyinyi nyote mko hatarini kabisa. Vilio vyako vya kwanza kwa ajili ya wokovu na matamanio yako ya kwanza ya kufuatilia ukweli na kutafuta nuru vinakaribia mwisho. Hivi ndivyo utakavyonifidia mwishowe, ambacho ni kitu ambacho Sikukitumainia. Sitamani kuzungumza kinyume cha ukweli, kwa maana umenivunja moyo sana. Pengine hupendi kuiachia mada hapo na hutaki kuukabili ukweli, lakini ni lazima nikuulize swali hili: Kwa miaka hii yote, moyo wako umejawa na nini? Mioyo yenu inamwamini nani? Usiseme kwamba swali Langu limekuja ghafula sana, na usiniulize kwa nini Nauliza swali kama hilo. Unapaswa kujua hili: Ni kwa sababu Ninakufahamu vizuri, ninakujali sana, na Ninajitolea moyo Wangu sana kwa kile unachofanya, ndio maana Ninakuuliza kwa kurudiarudia na kubeba taabu isiyoelezeka. Hata hivyo, malipo Yangu yamekuwa ni kupuuzwa na kukataliwa kusikostahimilika. Hivyo mmekuwa na ajizi sana juu Yangu; Ninawezaje kutojua kitu kuhusu hilo? Kama unaamini kwamba hili linawezekana, inathibitisha zaidi ukweli kwamba hunitendei wema kabisa. Kisha Ninawaambia kwamba mnajidanganya nyinyi wenyewe. Nyinyi nyote ni werevu sana kiasi kwamba hamjui kile mnachofanya; sasa mtatumia nini ili kunipatia ufafanuzi?
Swali muhimu sana kwangu ni mioyo yenu inawamini nani. Pia Ningependa kila mmoja wenu afikiri vizuri na kisha ajiulize uaminifu wake uko kwa nani na anaishi kwa ajili ya nani? Pengine hujawahi kuliangalia swali hili kwa makini, hivyo nitakupatia jibu lake.
Wale wenye kumbukumbu nzuri wataukubali ukweli huu: Mwanadamu anaishi kwa ajili yake mwenyewe na ni mwaminifu kwake mwenyewe. Siamini kwamba jibu lako ni sahihi kabisa, kwa maana kila mmoja wenu anaishi maisha yake, kila mmoja wenu anapambana katika dhiki yake. Kwa hivyo, kile unachokuwa mwaminifu kwacho ni watu unaowapenda, na vitu vinavyokupendeza, na wala wewe si mwaminifu kwa nafsi yako mwenyewe. Kwa sababu kila mmoja wenu anaathiriwa na watu, matukio, na vitu vinavyomzunguka, kimsingi nyinyi si waaminifu kwa nafsi zenu. Sisemi maneno haya kwa kuwataka muwe waaminifu kwa nafsi zenu bali Nasema ili kufichua uaminifu wenu kwa kitu chochote kile. Maana kwa miaka yote hii Sijawahi kupokea uaminifu kutoka kwa mtu yeyote kati yenu. Mmekuwa wafuasi Wangu kwa miaka mingi sana, lakini hamjawahi kunionesha hata chembe ya uaminifu. Badala yake mmekuwa mkizunguka kwa watu mnaowapenda na vitu vinavyowapendeza sana, na kuviweka karibu na mioyo yenu na havijawahi kuachwa, wakati wowote, mahali popote. Unapokuwa na hamu ama shauku na kitu chochote kile unachokipenda, siku zote unakuwa ni wakati ambapo unanifuata, au hata wakati unaposikiliza maneno Yangu. Hivyo nasema, unatumia uaminifu ninaokutaka uuonyeshe, kwa kufurahia matamanio yako mwenyewe. Ingawa unaweza kutoa sadaka ya kitu kimoja au vitu viwili kwa ajili Yangu, hakuwakilishi vitu vyako vyote, na haionyeshi kwamba ni Kwangu ambako uaminifu wako uko kwa kweli. Unajiweka mwenyewe katika shughuli ambazo unazipenda: Wengine ni waaminifu kwa watoto, wengine kwa waume, wake, utajiri, kazi, wenye vyeo, umaarufu, au wanawake. Kwa maana kile ambacho unakuwa mwaminifu kwacho, hujawahi kuhisi kuchoshwa au kukerwa nacho, badala yake, unatamani kuwa na kiasi kikubwa zaidi na ubora wa vitu ambavyo u mwaminifu kwavyo na hujawahi kukata tamaa. Mimi mwenyewe na maneno Yangu daima hutupwa pembeni katika masuala ya vitu unavyovipenda. Na huna namna isipokuwa kuyaweka mwisho; wengi hata wanaondoka sehemu ya mwisho kwa ajili ya kuwa waaminifu kwa kitu ambacho hawajakigundua bado. Hawajawahi kuniweka mioyoni mwao kwa kiwango chochote kile. Pengine utafikiri kwamba ninahitaji mambo mengi sana kutoka kwako au Ninakuhukumu kimakosa, lakini je, umeshawahi kufikiri kuhusu ukweli huu kwamba unapotumia muda kwa furaha pamoja na familia yako, hujawahi kuwa mwaminifu kwangu hata mara moja? Wakati kama huu, hii haikuumizi? Mioyo yenu inapojawa na furaha kwa kupokea malipo kwa kazi zenu, haiwavunji moyo kwamba hamjajitweka kwa ukweli wa kutosha? Ni lini umewahi kulia kwa kukosa idhinisho langu? Unaitesa akili yako na kupata maumivu makubwa kwa ajili ya watoto wako, lakini bado hujaridhika, bado unaamini kwamba hujaweka jitihada za kutosha kwao, kwamba hujatumia nguvu zako zote. Lakini Kwangu, mmekuwa ajizi na wa kutojali, mkiniweka tu katika kumbukumbu zenu na wala Sidumu ndani ya mioyo yenu. Kujitolea Kwangu na jitihada zangu daima hupita bila nyinyi kuzihisi, na wala hamjawahi kuweka jitihada ili muweze kuelewa. Nyinyi hutafakari kidogo tu na kuamini kwamba hiyo itatosha. "Uaminifu" wa aina hii sio ule ambao Nimekuwa nikiutazamia, bali ni ule ambao umekuwa machukizo Kwangu kwa muda mrefu. Hata hivyo, licha ya kile Ninachokisema, mtaendelea kukubali kitu kimoja tu au vitu viwili na kushindwa kukikubali kwa ukamilifu, kwa maana nyote mnajiamini sana, na siku zote mnachagua kipi mtakachokikubali kutoka katika maneno Niliyoyasema. Kama bado mko hivi, Nina njia katika akiba za kukabiliana na kujiamini kwenu, na Nitazitumia ili muweze kuyatambua maneno Yangu yote kuwa ni kweli na sio upotoshaji wa ukweli.
Kama sasa Ningeweka utajiri mbele yenu na kuwaambia kuwa mchague kwa uhuru, huku Nikijua kwamba[a] sitawahukumu, basi wengi wangechagua utajiri na kuacha ukweli. Wazuri miongoni mwenu wangeacha utajiri na kuchagua ukweli shingo upande, ilihali wale ambao wako katikati wangekumbatia utajiri kwa mkono mmoja na kwa mkono mwingine kuukumbatia ukweli. Kwa njia hii, je, rangi zenu halisi si zingejidhihirisha? Unapochagua ukweli kwa kulinganisha na kitu chochote ambacho u mwaminifu kwacho, wote mtafanya maamuzi kama hayo, na tabia yenu itabakia kuwa ile ile. Si ndivyo ilivyo? Je, hakuna watu wengi miongoni mwenu waliobadilika badilika katika kuchagua baina ya wema na ubaya? Katika mashindano kati ya mazuri na mabaya, nyeusi na nyeupe, una uhakika na uchaguzi ulioufanya kati ya familia na Mungu, watoto na Mungu, amani na vurugu, utajiri na umasikini, hadhi na kuwa mtu wa kawaida, kusaidiwa na kutupiliwa mbali, na kadhalika. Kati ya familia yenye amani na familia iliyovunjika, wewe huchagua ya kwanza bila kusita; kati ya utajiri na wajibu, safari hii pia unachagua ya kwanza, bila kuwa na nia ya kurudi ufuoni[b] kati ya starehe na umasikini, tena ulichagua ya kwanza; kati ya watoto, mke, mume na Mimi, unachagua za kwanza; na kati ya dhana na ukweli, kwa mara nyingine tena ulichagua ya kwanza. Nikikabiliwa na kila namna ya matendo yenu maovu, karibu sana Nimepoteza imani Yangu kwenu. Ninashangazwa sana na kwamba mioyo yenu inapinga kulainishwa. Miaka mingi ya kujitolea na jitihada Yangu imeniletea kuvunjika moyo tu nanyi kupoteza imani Nami. Hata hivyo, matumaini Yangu juu yenu yanakua kila siku inayopita, kwa kuwa siku Yangu tayari imekwisha kuwekwa wazi kwa kila mtu. Lakini, bado mnaendelea kuyatafuata yale ambayo ni ya giza na maovu, na mnakataa kulegeza mshiko wenu. Kwa kufanya hivyo, mtapata matokeo gani? Mmewahi kutafakari kwa makini kuhusu hili? Kama mngetakiwa kuchagua tena, msimamo wenu ungekuwa upi? Bado lingekuwa ni chaguo la kwanza? Je, yale ambayo mngenipatia bado yangekuwa maudhi na huzuni ya majuto? Je, mioyo yenu bado ingekuwa migumu? Je bado mngekuwa hamjui cha kufanya ili kuufariji moyo Wangu? Kwa wakati wa sasa, chaguo lako ni nini? Utayakubali maneno Yangu, au yatakuchosha? Siku Yangu imewekwa wazi kabisa mbele ya macho yenu, na kile mnachokiona ni maisha mapya na mwanzo mpya. Hata hivyo, ni lazima niwaambie kwamba huu mwanzo mpya si mwanzo wa kazi mpya iliyopita, bali ni mwisho wa ya kale. Yaani, hili ni tendo la mwisho. Ninaamini nyote mtaelewa kitu ambacho si cha kawaida kuhusu mwanzo huu mpya. Lakini siku moja hivi karibuni, mtaelewa maana halisi ya huu mwanzo mpya, kwa hivyo hebu sote tuipite na kuikaribisha tamati inayofuata! Hata hivyo, kitu ambacho Ninaendelea kutofurahishwa nacho ni kwamba pale unapokabiliwa na mambo ambayo si ya haki na mambo ya haki, daima umekuwa ukichagua chaguo la kwanza. Lakini hayo yote yako katika maisha yenu ya zamani. Pia Ninatumai kuyasahau yale yote yaliyotokea katika maisha yenu ya zamani, kitu kimoja baada ya kingine, ingawa hili ni gumu sana kufanya. Lakini bado nina njia nzuri sana ya kulitimiza. Hebu wacha maisha ya baadaye yachukue nafasi ya maisha ya zamani na kuacha kivuli cha maisha yako ya zamani kiondolewe badala ya utu wako halisi wa leo. Hii ina maana kwamba nitakusumbua tena ili uweze kufanya maamuzi kwa mara nyingine tena na kuona uaminifu wako uko kwa nani.
 kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.


0 评论:

Chapisha Maoni