Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kutenda-ukweli. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kutenda-ukweli. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 8 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (10)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (10)


Kwa wanadamu kuendelea mbele kiasi hiki ni hali isiyo na kigezo. Kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu vinaendelea bega kwa bega, na hivyo kazi ya Mungu, pia, ni tukio kubwa lisilo na kifani. Kuingia kwa mwanadamu hadi sasa ni ajabu ambayo kamwe haijawahi kufikiriwa na mwanadamu. Kazi ya Mungu imefikia upeo wake—na, kufuatia, “kuingia” kwa mwanadamu[1] pia kumefikia kilele chake. Mungu amejishusha kwa kadiri Anavyoweza, na kamwe Hajawahi kuwalalamikia wanadamu au vitu vyote katika ulimwengu.

Jumapili, 3 Machi 2019

Neno la Mungu | Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa


    Katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili ili kufanya kazi Aliyopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja yeye mwenyewe ili kufanya kazi kati ya wanadamu kwa lengo la kuwakamilisha wale watu ambao wanaipendeza nafsi Yake. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo Yeye hufanya tu hiyo kazi wakati wa siku za mwisho. Ni wakati wa siku za mwisho tu ambapo Mungu alipata mwili ili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa. 

Jumatano, 27 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)


  Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)


Katika nyakati zilizopita, watu walijifundisha wenyewe kuwa na Mungu na kuishi katikati ya roho kila wakati, ambao, ukilinganishwa na utendaji wa leo, ni mafundisho rahisi ya kiroho tu. Utendaji kama huu huja kabla ya kuingia kwa watu katika njia sahihi ya maisha, na ni mbinu ya juujuu zaidi na rahisi zaidi kati ya mbinu zote za utendaji. Ni utendaji wa hatua za mwanzoni kabisa za imani ya watu kwa Mungu. Ikiwa watu wataishi kila mara kwa utendaji huu, watakuwa na hisia nyingi sana, na hawataweza kuingia katika uzoefu ambao ni wa kina na wa kweli.

Jumanne, 26 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (3)


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (3)


    Mungu amewaaminia wanadamu vitu vingi sana na Amezungumza bila kikomo juu ya kuingia kwao. Lakini kwa sababu ubora wa tabia ya watu ni duni mno, maneno mengi ya Mungu yameshindwa kuanza kustawi. Kuna sababu mbalimbali za huu ubora duni wa tabia, kama vile uharibifu wa mawazo na maadili ya binadamu, na kutokuwa na malezi mazuri; imani za usihiri zilizojaa moyoni mwa mwanadamu; mitindo ya maisha iliyopotoka ambayo imeweka maovu mengi katika sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu;

Jumanne, 25 Septemba 2018

Worship and Praise Dance | "Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu" | The Kingdom of Christ Is Paradise for the Honest (Swahili Subtitles)


Worship and Praise Dance | "Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu" | The Kingdom of Christ Is Paradise for the Honest (Swahili Subtitles)

Safi na mwaminifu kama mtoto, asiye na hatia na mchangamfu, aliyejawa na nguvu za ujana,

wao ni kama malaika wanaokuja ulimwenguni.

Hakuna uongo, udanganyifu au hadaa, na moyo ulio wazi na mwaminifu, wanaishi na heshima.

Wanaitoa mioyo yao kwa Mungu, Mungu anawaamini, na wao ni watu waaminifu ambao Mungu anapenda.

Wale wanaopenda ukweli wote wana mioyo ya uaminifu.

Watu waaminifu hufurahia kutenda ukweli, na kwa kumtii Mungu mioyo yao ina amani.

Wanamcha Mungu, wanaepuka maovu na wanaishi kulingana na maneno ya Mungu.

Wanaishi katika maneno ya Mungu na wamewekwa huru na kuachiliwa.

Wanakubali uchunguzi wa Mungu na kuishi mbele Yake. Kumpenda Mungu ni kuwa na furaha na mwenye shangwe.

Ndugu, tumemwamini Mungu tangu tulipokuwa wadogo. Je, tuna furaha?

Ndiyo, tuna furaha!

Nina furaha pia!


Ninapompenda Mungu, moyo wangu una utulivu na una furaha,

na ninaishi kwa urahisi ninapotenda kulingana na maneno ya Mungu.

Moyoni mwangu kuna Mungu tu, kuna ukweli tu, maneno ya Mungu yamekuwa maisha yangu.

Nikiishi chini ya uongozi wa maneno ya Mungu kila siku, ninabarikiwa na Mungu na Roho Mtakatifu ananiongoza.

Wanakubali uchunguzi wa Mungu na kuishi mbele Yake. Kumpenda Mungu ni kuwa na furaha na mwenye shangwe.

Nikiishi chini ya uongozi wa maneno ya Mungu kila siku, ninabarikiwa na Mungu na Roho Mtakatifu ananiongoza.

Ufalme wa Kristo ni mbinguni kwa watu waaminifu,

na ni makao yao ya kupendeza.

kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Imba Nyimbo Mpya


    Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Alhamisi, 5 Julai 2018

Sura ya 9. Kutafuta Mapenzi ya Mungu na Kuuweka Ukweli Katika Vitendo Kwa Kiasi Kikubwa Zaidi Iwezekanavyo

Sura ya 9. Kutafuta Mapenzi ya Mungu na Kuuweka Ukweli Katika Vitendo Kwa Kiasi Kikubwa Zaidi Iwezekanavyo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Punde tu watu wanapokuwa na haraka wakati wakiutumiza wajibu wao, hawajui jinsi ya kuuzoea; punde tu wanaposhughulika na mambo, hali yao ya kiroho inakuwa na matatizo; hawawezi kudumisha hali yao ya kawaida. Inawezekanaje kuwa hivi? Unapoombwa kufanya kazi kidogo, haufuati ukawaida, unakosa mipaka, husogei karibu na Mungu na unajitenga mbali na Mungu. Hili linadhibitisha kwamba watu hawajui jinsi ya kuwa na uzoefu. Haidhuru nini ufanyacho, unapaswa kwanza kuelewa halisi kwa nini unalifanya hili na asili ya jambo hili ni lipi.

Ijumaa, 4 Mei 2018

64. Huku Ni Kuweka Ukweli Katika Vitendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, ushuhuda, Umeme wa Mashariki

64. Huku Ni Kuweka Ukweli Katika Vitendo

Fan Xing    Mji wa Zhumadian, Mkoa wa Henan
Katika siku za nyuma, nilikuwa nimeunganishwa na dada mmoja kufanya kazi kwa wajibu fulani. Kwa sababu nilikuwa na majisifu na mwenye kiburi na sikutafuta ukweli, nilikuwa na mawazo kiasi ya kabla kuhusu dada huyu ambayo niliweka moyoni mwangu daima na sikuzungumza waziwazi naye. Tulipotengana, sikuwa nimeingia katika ukweli wa uhusiano wa kufanya kazi wenye kuridhisha. Baadaye, kanisa lilinipangia kufanya kazi na dada mwingine nami nikaweka azimio mbele ya Mungu: Kuanzia sasa kuendelea, sitatembea katika njia za kufeli. Nimejifunza mafundisho yangu na hivyo kwa sasa wakati huu bila shaka nitakuwa na mawasiliano ya wazi zaidi na dada huyu na kufikia uhusiano wa kufanya kazi wenye kuridhisha.
Kila wakati kulikuwa na mgongano au pengo kati yetu tulipokuwa tukifanya wajibu wetu pamoja, ningechukua fursa ya kwanza kuwasiliana na dada na kuzungumza kwa dhati. Ningemwuliza ni vipengele vipi nilikuwa nikifanya kwa njia isiyofaa. Dada huyo kisha angeonyesha kuwa nilikuwa na kiburi na mwenye majisifu na kwamba siku zote ningekataa mitazamo yake katika mawasiliano yetu. Alisema wakati mwingine ningeonyesha hali zake na kumpachika jina bila haki, na kwamba wakati wa mikusanyiko, nilifanya maamuzi yote kuhusu kusoma neno la Mungu. Nilikubali kwa kichwa mambo haya yote dada alisema juu yangu. Nilidhani: "Kwa kuwa unasema mimi nina kiburi, basi nitazungumza kwa unyenyekevu zaidi kuanzia sasa na kuendelea na kuzingatia kwa makini hasa kuzungumza kwa hekima na busara. Ikiwa nitatambua matatizo yoyote unayo, basi nitayadunisha wakati ninapoyataja. Ikiwa hutayatambua, basi sitayazungumzia. Wakati wa mikusanyiko, nitakula na kunywa chochote utakachoniambia nikule na ninywe, na nitasikia kila kitu unachosema. Si hili litatatua kila suala?" Baada ya haya, nilianza kuweka hili katika vitendo. Kabla ya kuzungumza, ningefikiri vile ningeweza kuepuka kukana wazo la dada. Wakati mitazamo yetu hayakulingana pamoja, ningekubali kushindwa na mtazamo wake na kutekeleza wazo lake. Nilipomwona dada akifanya jambo kwa njia isiyo sahihi, singemfafanulia kwa waziwazi. Lakini baada ya kipindi cha muda cha kutenda kwa namna hii, niligundua kuwa itikadi yangu ya "nyima mwili na weka ukweli katika matendo" haikuwa imebadilisha uhusiano wetu hata kidogo. Badala yake, iliimarisha mawazo yake yaliyotungwa kabla kunihusu. Kwa kuona matokeo hayo, nilihisi nimekosewa. Niliwaza: "Tayari nimejitahidi kadri niwezavyo kuweka ukweli katika matendo, mbona haifanyi kazi? Dada huyu si rahisi kupatana na yeye, hana wepesi wa kuhisi hata kidogo. "Kwa hiyo, nilizama katika uhasi na moyo wangu ukahuzunika sana.
Siku moja, kiongozi mmoja alitujia kukagua kazi yetu na kuuliza jinsi hali zetu zilivyokuwa wakati wa kipindi hiki. Kisha nikaeleza vile hali yangu ilivyokuwa. Baada ya kusikiliza, kiongozi huyo alisema: "Hii mbinu yako haiweki ukweli katika matendo. Wewe ni mchafu ndani. Unatenda hivi kwa madhumuni yako mwenyewe na hautendi kulingana na ukweli." Baada ya haya, tulisoma vifungu viwili vya maneno ya Mungu. Mungu alisema: “Upande wa nje, inaonekana kana kwamba unatia ukweli katika vitendo, lakini kwa kweli, hali ya matendo yako haionyeshi kwamba unatia ukweli katika vitendo. Kuna watu wengi walio na mienendo fulani ya nje, wanaoamini ‘Ninatia ukweli katika vitendo…,’ Lakini Mungu asema: ‘Sitambui kwamba unatia ukweli katika vitendo.’ Hii ni nini? Hii ni aina ya mwenendo. Kusema kweli, unaweza kuhukumiwa kwa hilo; halitasifiwa, halitakumbukwa. Hata kusema kweli zaidi, katika kulichangua hili, unafanya uovu, mwenendo wako unampinga Mungu. Kutoka nje, hukatizi, husumbui, huharibu chochote, au kukiuka ukweli wowote. Inaonekana kile ambacho unafanya ni chenye mantiki na cha maana, lakini unafanya uovu na kumpinga Mungu. Kwa hivyo unapaswa kutegemea chanzo jinsi Mungu amehitaji, kuona kama kuna badiliko katika tabia yako au kama umetia ukweli katika vitendo. Haihusu kukubali mawazo na maoni ya mwanadamu, au kwa hiari zako mwenyewe. Badala yake, ni Mungu ndiye husema kama unakubali mapenzi Yake; ni Mungu ambaye husema kama matendo yako yana ukweli na kama yanafikia viwango Vyake au la. Kujipima dhidi ya matakwa ya Mungu ndiyo njia sahihi tu” (“Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). “Mawazo ya binadamu kwa kawaida yanaonekana mazuri na sahihi kwa watu na yanaonekana kama hayakiuki ukweli kwa kiasi kikubwa. Watu wanahisi kwamba kufanya kwa jinsi hii ni kuweka kweli katika matendo, wanahisi kwamba kufanya kwa jinsi hii ni kumtii Mungu. Kwa kweli, watu hawamtafuti Mungu hakika na kumwomba Mungu kuhusu hili. Hawajitahidi kufanya vizuri kuridhisha mapenzi ya Mungu wala hawajitahidi kufanya vizuri kulingana na mahitaji Yake. Hawana hali hii ya kweli, na hawana hamu kama hiyo. Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo watu hufanya katika matendo yao, kwa sababu unamwamini Mungu, lakini Mungu hayupo moyoni mwako. Hii sio dhambi vipi? Huku sio kujidanganya mwenyewe vipi? Ni athari gani kuamini jinsi hii kutakuwa nayo? Uko wapi umuhimu wa matendo ya kumwamini Mungu?” (“Kutafuta Mapenzi ya Mungu na Kuuweka Ukweli Katika Vitendo Kwa Kiasi Kikubwa Zaidi Iwezekanavyo” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nilijaribu kuelewa maneno yake Mungu na kuyalinganisha na hali yangu inayodaiwa kuwa "kuweka ukweli katika matendo." Moyo wangu ulichangamka. Hivyo, njia niliyokuwa nikifanya mambo haikukusudiwa kukidhi Mungu. Ilikusudiwa kulinda hadhi yangu bure. Niliogopa kiongozi huyo angesema asili yangu ilikuwa na dosari, kwamba sikutafuta ukweli, na kuwa sikufanya kazi vyema na yeyote. Aidha, nilifikiri ilikuwa ni kisingizio cha kurahisisha uhusiano wangu na dada na kujinasua kwa aibu na uchungu uliosababishwa na mgogoro huo. Nilidhani ingekomboa ile taswira ambayo watu wengine walikuwa nayo kunihusu na kuwaruhusu kuona kuwa nilikuwa nimebadilika. Inaweza kuonekana kuwa kile kilichodaiwa kuwa "kuweka ukweli katika matendo" kwangu kilikuwa kwa madhumuni yangu mwenyewe. Yote yalitendwa mbele ya wengine na hayakuanzishwa kwa msingi wa kutafuta kumridhisha Mungu. Sikujidharau na kwa kweli kuunyima mwili kwa sababu sikuwa na ufahamu wa asili yangu ya majisifu na kiburi. Katika kutafakari juu ya kufanya kazi na dada, ni kwa sababu sikutambua asili yangu ya kujisifu na kiburi, na kwa sababu nilijiheshimu na nilikuwa nafikiri kila wakati kuwa nilikuwa bora zaidi kuliko wengine nilipozungumza, bila kujua nilikuwa nimesimama kwenye kiweko nikidunisha wengine. Wakati wa kushughulikia mambo, nilipenda kuwa msimamizi; nilifanya mambo kwa njia yangu mwenyewe, na kamwe sikuwahi kutafuta maoni ya watu wengine. Wakati dada alipoonyesha haya matatizo niliyokuwa nayo, sikutafuta ukweli uliofanana ili kuchambua na kuelewa hali ya asili yangu. Hata zaidi, sikutafuta jinsi ninapaswa kuiweka katika vitendo kulingana na mahitaji ya Mungu na kwa mujibu wa ukweli. Nilibadili tu matendo machache ya nje, nikifikiria kuwa kwa kuwa niliacha kufanya mambo ambayo yalikuwa mabaya, nilikuwa nikiweka ukweli katika matendo. Kwa kweli, kila kitu nilichokuwa nikifanya kilikuwa ukweli kulingana na mawazo yangu mwenyewe. Vyote vilikuwa ni vitendo vya nje na havikuwa na chochote kuhusu neno la Mungu. Mungu hangetambua kuwa nilikuwa nikiweka ukweli katika matendo. Kwa sababu sikuwa natenda kulingana na mahitaji ya Mungu na sikuwa natenda kwa mujibu wa ukweli, na kila kitu nilichofanya kilifanyika ili kukidhi tamaa zangu za kibinafsi na kufikia malengo yangu mwenyewe, kwa hiyo matendo yangu yalikuwa mabaya machoni pa Mungu; ilikuwa kumpinga Mungu.
Baada ya kutambua hili, niliunganisha neno la Mungu kwa makusudi ili nipate kuelewa asili yangu potovu katika maisha. Wakati nilionyesha upotovu wangu au nilipotambua kuwa hali yangu haikuwa sahihi, nilifichua waziwazi nafasi yangu na nikaichunguza na kutafuta chanzo kulingana na neno la Mungu. Nilipofanya hili, kunena kwangu na matendo yangu yakawa ya kawaida, na nilijua nafasi ambao nilipaswa kusimama. Nikawa na heshima kwa watu na kutii kwa uvumilivu. Kuunyima mwili kukawa sio kugumu sana na tukaweza kuwa mawasiliano ya dhati. Ushirikiano wetu ulikuwa umekuwa wa kuridhisha tena zaidi kuliko siku za nyuma.
Kupitia uzoefu huu, nimepata kuelewa kwamba kuweka ukweli katika vitendo lazima kuwekwe kwa msingi wa neno la Mungu na lazima kuanzishwe kwa kanuni za kweli. Mtu akiacha neno la Mungu, basi kila kitu kinakuwa kitendo cha nje, yaani, kuweka ukweli wa mawazo yao wenyewe katika matendo. Hata ikiwa ningefanya mambo vizuri na kwa usahihi, bado haingechukuliwa kama kuweka ukweli katika vitendo, na hata zaidi haingeleta mabadiliko kwa tabia ya maisha yangu. Kuanzia sasa kuendelea, bila kujali ni nini ninachofanya, nataka maneno ya Mungu kuwa kanuni za matendo yangu na kuweka neno la Mungu kikamilifu katika vitendo ili mwenendo wangu utalingana na ukweli na mapenzi ya Mungu na kupata kuridhika kwa Mungu. Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu!
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Ijumaa, 20 Aprili 2018

Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani. Suala hili si lile ambalo ni geni sana kwenu, lakini inaonekana kwamba hamwelewi au hamjazoea maana iliyomo kwenye suala hili. Wengi wanayo dalili ya ufahamu tu na mara nyingi maarifa ya juujuu kuhusu suala hili. Ili kuwasaidia kutenda kwa njia bora zaidi ukweli, yaani, kuwasaidia kuweka kwa njia bora zaidi maneno Yangu katika matendo, Nafikiri kwamba ni suala hili ambalo lazima kwanza mlijue. Vinginevyo, imani yenu itabakia isiyo wazi, ya unafiki, na iliyopambwa sana na dini. Kama huelewi tabia ya Mungu, basi itakuwa haiwezekani kwako wewe kufanya kazi unayofaa kumfanyia. Kama hujui dutu ya Mungu, ndivyo pia haitawezekana kubakiza hali ya kumcha na kumwogopa Yeye, utakuwa ni uzembe na kuepuka kusema ukweli wote kwa kutojali, na zaidi, kukufuru kusikorekebishika. Kuelewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, ilhali hakuna yeyote amewahi kuchunguza kwa umakinifu au kudadisi suala hili. Ni wazi kuona kwamba nyote mmepuuzilia mbali amri za kiutawala Nilizozitoa. Kama hamuelewi tabia ya Mungu, basi mtaweza kukosea kwa urahisi sana tabia Yake. Kosa kama hilo ni sawa na kumkasirisha Mungu Mwenyewe, na hatimaye linakuwa ni uhalifu dhidi ya amri ya kiutawala. Sasa unafaa kutambua kwamba unaweza kuelewa tabia ya Mungu unapokuja kujua dutu Yake, na kuelewa tabia ya Mungu ni sawa na kuelewa amri za kiutawala. Bila shaka, wingi wa amri za kiutawala zinahusu tabia ya Mungu, lakini uzima wa tabia Yake bado haujaweza kuonyeshwa ndani yao. Hili linawahitaji kuzoea zaidi tabia ya Mungu.
Ninaongea nanyi leo si katika hali ya mazungumzo ya kawaida, kwa hiyo lazima myajali maneno Yangu kwa bidii na, zaidi, kuyatafakari kwa kina. Kile Ninachomaanisha na haya ni kwamba mmetoa jitihada ndogo sana kwa maneno ambayo Nimeyazungumza. Tunapokuja kwa tabia ya Mungu, hamko radhi zaidi kutafakari juu ya suala hili, na wachache sana wanajitolea kufanya hili. Kwa hiyo, Nasema kwamba imani yenu ni maneno ya kujionyesha tu. Hata sasa, hakuna hata mmoja wenu ametoa jitihada yoyote ya kweli kwa udhaifu wenu mkuu zaidi. Mmenisikitisha baada ya maumivu yote Niliyoyapitia kwa ajili yenu. Si ajabu kwamba nyote hamjali Mungu na mnaishi maisha yasiyo na ukweli. Ni vipi watu kama hawa wanaweza kuchukuliwa kama watakatifu? Sheria ya mbinguni haitaweza kuvumilia kitu kama hiki! Kwa sababu mnao uelewa mdogo sana, basi itabidi Nitumie pumzi zaidi.
Tabia ya Mungu ni mada ambayo inaonekana kuwa dhahania sana na ambayo haikubaliwi kwa urahisi, kwani tabia Yake ni tofauti na hulka ya binadamu. Mungu, vilevile, anazo hisia za anasa, hasira, huzuni, na furaha, lakini hisia kama hizo zinatofautiana pia na zile za binadamu. Mungu anayo nafsi Yake mwenyewe na kile Anachokimiliki. Kila kitu Anachokidhihirisha na kukionyesha ni viwakilishi vya dutu Yake na utambulisho Wake. Nafsi Yake, kile Anachomiliki, pamoja na dutu na utambulisho vyote haviwezi kubadilishwa na binadamu yeyote. Tabia Yake inajumuisha upendo Wake kwa binadamu, kumtuliza binadamu, chuki kwa binadamu, na hata zaidi, uelewa wa kina wa mwanadamu. Hulka ya binadamu, hata hivyo, inaweza kuwa yenye matumaini mema, changamfu, au ngumu. Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa wale walio hai miongoni mwa vitu vyote, kwa Bwana wa viumbe vyote. Tabia Yake inawakilisha heshima, nguvu, uadilifu, ukubwa, na zaidi kuliko vyote, mamlaka ya juu kabisa. Tabia yake ni ishara ya mamlaka na kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, na kizuri. Aidha, ni ishara ya namna ambavyo Mungu hawezi[a] kukandamizwa au kushambuliwa na giza na kikosi chochote cha adui, pamoja na ishara ya namna ambavyo hawezi kuwa(na kwa kweli haruhusiwi kuwa)[b] kukasirishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi. Hakuna mtu au watu wanaoweza au wanaweza kutatiza kazi Yake au tabia Yake. Lakini hulka ya binadamu si zaidi ya ishara tu ya hali ya kuwa na mamlaka ya juu zaidi kiasi cha binadamu dhidi ya wanyama. Binadamu mwenyewe hana mamlaka, hana uhuru, na hana uwezo wa kuzidi nafsi, bali ni dutu tu inayotii kwa njia ya woga kutawaliwa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Anasa ya Mungu inatokana na uwepo na kuibuka kwa hali ya kuwa haki na mwangaza; kwa sababu ya kuangamizwa kwa giza na maovu. Anafurahia kwa sababu Ameuleta mwangaza na maisha mazuri kwa mwanadamu; furaha Yake ni ile ya hali ya haki, ishara ya uwepo wa kila kitu kilicho kizuri, na zaidi ya yote, ishara ya msaada. Hasira ya Mungu inatokana na uwepo wa dhuluma na vurugu inayosababisha ambayo inamdhuru mwanadamu Wake; kwa sababu ya uwepo wa maovu na giza, uwepo wa vitu vinavyoondoa ukweli, na hata zaidi kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyopinga kile ambacho ni kizuri na cha kupendeza. Hasira Yake ni ishara ya kwamba vitu vyote vibaya havipo tena, na fauka ya hayo, ni ishara ya utakatifu Wake. Huzuni Yake ni kwa sababu ya mwanadamu, ambaye kwake Ana matumaini lakini ambaye ameanguka katika giza, kwa sababu kazi Afanyayo kwa mwanadamu haifikii matarajio Yake, na kwa sababu binadamu Awapendao hawawezi wote kuishi katika mwanga. Anahisi huzuni kwa sababu ya mwanadamu asiye na hatia, kwa yule binadamu mwaminifu lakini asiyejua, na kwa yule binadamu mzuri lakini mwenye hisia kinzani. Huzuni Yake ni ishara ya wema Wake na huruma Yake, ishara ya urembo na wema Wake. Furaha yake, bila shaka, inatokana na kuwashinda adui Zake na kupata imani nzuri ya binadamu. Aidha, inatokana na kuondolewa na kuangamizwa kwa nguvu zote za adui na mwanadamu kupokea maisha mazuri na yenye amani. Furaha ya Mungu ni tofauti na furaha ya binadamu; badala yake, ni ile hisia ya kupokea matunda mazuri, hisia ambayo ni kubwa zaidi kuliko furaha. Furaha Yake ni ishara ya mwanadamu kuwa huru dhidi ya mateso na kuingia katika ulimwengu wa mwangaza. Hisia za mwanadamu, kwa upande mwingine, zote zipo kwa makusudio ya masilahi yake mwenyewe, na wala si za haki, mwangaza, au kile ambacho ni cha kupendeza, na kidogo kati ya vyote neema ya Mbinguni. Hisia za mwanadamu ni za ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo si za mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo binadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa kwa pumzi moja. Mungu siku zote anayo mamlaka ya juu zaidi na mwenye heshima kila wakati, huku naye binadamu siku zote akiwa chini na kila wakati akikosa thamani. Hii ni kwa sababu Mungu siku zote anajitolea mhanga na kujitoa Mwenyewe kwa mwanadamu; binadamu, hata hivyo, siku zote huchukua na hufanya kazi kwa ajili yake pekee. Siku zote Mungu anashughulikia uwepo wa mwanadamu, ilhali binadamu hachangii katu katika mwangaza au haki. Hata kama binadamu anashughulika kwa muda, yeye ni mnyonge na hawezi kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake na wala si wengine. Binadamu siku zote ni mbinafsi, huku naye Mungu siku zote si mbinafsi. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo na haki, wema, na urembo, huku naye binadamu akiwa mrithi na mwonyeshaji wa vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na urembo, ilhali binadamu anaweza, wakati wowote, kusaliti haki na kupotoka kutoka kwa njia ya Mungu.
Kila sentensi Niliyoizungumza inaendeleza tabia ya Mungu. Mngefanya vizuri zaidi endapo mngetafakari kuhusu maneno Yangu kwa umakini, na kwa kweli mtafaidi pakubwa kutoka katika maneno haya. Dutu ya Mungu ni ngumu sana kuelewa, lakini Ninaamini kwamba nyinyi nyote mnayo angalau baadhi ya maarifa kuhusu tabia ya Mungu. Ninatumai, basi, kwamba mtanionyesha Mimi na kufanya mengi zaidi ya yale ambayo hayakosei tabia ya Mungu. Kisha Nitatuliza moyo. Kwa mfano, mhifadhi Mungu katika moyo wako siku zote. Unapochukua hatua, timiza neno Lake. Tafuta fikira Zake katika kila kitu, na usifanye kile ambacho kitavunjia heshima na kumdhalilisha Mungu. Vilevile, usimweke Mungu nyuma ya akili zako ili ukajaze uwazi wa baadaye katika moyo wako. Ukifanya hivyo, basi utakuwa umekosea tabia ya Mungu. Kama kamwe hutamki matamshi ya kukufanya kukufuru au kulalamika dhidi ya Mungu na unaweza kufanya kikamilifu kila kitu ambacho amekuaminia wewe katika maisha yako yote, pamoja na kutii maneno yote ya Mungu, basi umeweza kuepuka kwa ufanisi kukosea amri za kiutawala. Kwa mfano, kama umewahi kusema “Kwa nini sifikirii kwamba Yeye ni Mungu?” “Nafikiri kwamba maneno haya si zaidi ya kutiwa nuru fulani na Roho Mtakatifu,” “Sifikirii kwamba kila kitu Mungu anachokifanya ni cha kweli,” “Ubinadamu wa Mungu hauna ukubwa zaidi kuliko wangu,” “Neno la Mungu haliaminiki tu,” au matamshi mengine kama hayo ya kuhukumu, basi Nakushawishi wewe kukiri dhambi zako na kutubu. Vinginevyo, hutawahi kuwa na fursa ya msamaha, kwani unakosea sio binadamu tu lakini Mungu Mwenyewe. Unaweza kuamini kwamba wewe unahukumu mtu tu, lakini Roho Mtakatifu wa Mungu hachukulii hivyo. Wewe kutoheshimu mwili Wake ni sawa na kumvunjia heshima Yeye mwenyewe. Kama hali ni hivi, basi si kweli kwamba umekosea tabia ya Mungu? Lazima mkumbuke kwamba kila kitu kinachofanywa na Roho wa Mungu ni kusaidia kazi Yake katika mwili na kufanya kazi kama hiyo vizuri. Ukiyapuuza haya, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye kamwe hataweza kufaulu katika kumwamini Mungu. Kwani umechochea hasira ya Mungu, na kwa hivyo lazima Atumie adhabu inayofaa ili kukufunza adabu.
Kuzoea dutu ya Mungu si jambo dogo. Lazima uelewe tabia Yake. Katika njia hii, polepole utaanza kuzoea dutu ya Mungu na hivyo basi kusonga mbele wakati uo huo katika hali kubwa zaidi na ya kupendeza zaidi. Hatimaye, utaaibika kutokana na nafsi yako ya kuchukiza, kiasi kwamba unaaibika kuuonyesha uso wako. Wakati huo, ndipo utakapokosea tabia ya Mungu kwa kiwango kidogo na kidogo; moyo wako utakuwa karibu zaidi na zaidi na ule wa Mungu, na polepole upendo wako Kwake utaweza kukua ndani ya moyo wako. Hii ni ishara ya mwanadamu kuingia katika hali nzuri. Lakini kufikia sasa bado hamjapata hili. Nyinyi hujichosha mkisafiri huku na kule kwa ajili ya hatima yenu, kwa hiyo ni nani angefikiria kujaribu na kuzoea zaidi dutu ya Mungu? Kama hali hii itaendelea, nyinyi mtaweza kuikosea bila kujua amri za kiutawala kwani mnajua kidogo sana kuhusu tabia ya Mungu. Kwa hivyo, kile mfanyacho sasa hakiweki msingi kwa sababu ya makosa yenu dhidi ya tabia ya Mungu? Kwamba Ninawaomba muweze kuelewa tabia ya Mungu haipingani na kazi Yangu. Kwani mkienda kinyume cha amri za kiutawala mara nyingi, basi ni nani kati yenu anayeweza kutoroka adhabu? Je, kazi Yangu haingekuwa bure kabisa? Kwa hivyo, Ningali Naomba kwamba pamoja na kuchunguza matendo yenu binafsi, kwamba muwe makini zaidi na hatua mnazochukua. Hili ndilo ombi kubwa zaidi ambalo Nitawaomba, na Ninatumai kwamba nyote mtalitilia maanani kwa umakinifu na kuliona kuwa muhimu. Endapo siku itawahi kufika ambapo matendo yenu yatanichochea Mimi hadi kuwa katika hali iliyojaa hasira, basi matokeo yatakuwa yenu pekee kufikiria, na hakuna mwingine yeyote atakayevumilia adhabu hiyo kwa niaba yenu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatano, 31 Januari 2018

45.Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika | kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

45. Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika

Changkai Mji wa Benxi, mkoa wa Liaoning
Maneno ya kawaida "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho" ni ambayo mimi binafsi ninayafahamu sana. Mimi na mume wangu sote tulikuwa hasa watu wasio na hatia: Wakati wa masuala yaliyohusisha faida au hasara yetu binafsi, hatukuwa aina ya watu wa kubishana na kusumbuana na wengine.Pale ambapo tuliweza kuwa wavumilivu tulikuwa wavumilivu, pale ambapo tungeweza kuwa na fadhila tulifanya tulivyoweza kuwa na fadhila. Kama matokeo yake, mara nyingi tulijipata tukiwa tumedanganywa na kudhulumiwa na wengine.

Jumatatu, 29 Januari 2018

Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini

 Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe? Ni mara ngapi wewe umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu wewe kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake?

Ijumaa, 26 Januari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Mwenyezi Mungu alisema, Kila siku unayoiishi sasa ni ya maana sana na muhimu sana kwa hatima yako na majaliwa yako, kwa hivyo unapaswa kufurahia kila ulicho nacho na kila dakika inayopita. Unapaswa kutumia muda wako vizuri ili uweze kujinufaisha, ili usije kuishi maisha haya bure. Pengine unajihisi kukanganyikiwa unaojiuliza ni kwa nini Ninazungumza maneno haya. Kwa kweli, Sijapendezwa na matendo ya yeyote kati yenu.

Alhamisi, 18 Januari 2018

Kumpenda Mungu Tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kumpenda Mungu Tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli

Mwenyezi Mungu alisema, Mnapotaka kumpenda na kumjua Mungu leo, kwa upande mmoja ni lazima mstahimili mateso, usafishaji, na kwa ule upande mwingine, ni lazima mgharamike. Hakuna funzo lililo kubwa kuliko lile la kumpenda Mungu, na inaweza kusemwa kuwa funzo ambalo watu hujifunza katika maisha yao yote ya imani ni jinsi ya kumpenda Mungu. Hii ni kusema, kama unamwamini Mungu ni lazima umpende Mungu.

Jumatatu, 15 Januari 2018

Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini

Mwenyezi Mungu alisema, Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe?

Jumamosi, 16 Desemba 2017

Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yananayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake.