Jumapili, 2 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 23

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 23
Kwa ndugu wote ambao wameisikia sauti Yangu: Mmeisikia sauti ya hukumu Yangu kali na mmevumilia mateso yaliyokithiri. Hata hivyo, mnapaswa kujua kwamba katika sauti Yangu kali kumejificha nia Zangu! Ninawafundisha nidhamu ili muweze kuokolewa. Mnapaswa kujua kwamba kwa wana Wangu wapendwa, Nitawafundisha nidhamu na kuwapogoa na kuwafanya muwe wakamilifu hivi karibuni. Moyo Wangu una hamu sana, lakini ninyi hamuelewi moyo Wangu na hamtendi kulingana na neno Langu. Maneno Yangu leo yanawajia ninyi na kuwafanya kutambua kweli kwamba Mungu ni Mungu mwenye upendo na nyote mmepitia upendo wa dhati wa Mungu. Hata hivyo, pia kuna idadi ndogo ya watu ambao wanajifanya na wanapoona huzuni ya watu wengine pia wao watakuwa na machozi machoni mwao. Kuna wengine ambao—kwa juu—wanaonekana kuwa wadeni wa Mungu na wanaonekana wenye majuto, lakini ndani yao, hawamwelewi Mungu kwa kweli na wala hawana uhakika kumhusu Yeye; badala yake, ni sura ya kinafiki tu. Ninawachukia watu hawa zaidi! Siku moja, watu hawa wataondolewa kutoka katika mji Wangu. Nia Yangu ni kwamba Nataka wale wanaonitaka kwa ari, na wale tu ambao wananifuatilia kwa moyo wa kweli wanaweza kunipendeza—kwani wao Nitawaunga mkono bila shaka kwa mikono Yangu mwenyewe na kuhakikisha kuwa hawatapata majanga yoyote. Watu wanaomtaka Mungu kwa kweli watakuwa tayari kujali mzigo wa Mungu kwa vyovyote vile na wenye huruma kwa moyo wa Mungu na kutekeleza mapenzi Yangu. Kwa hiyo, ninyi mnapaswa kuingia katika ukweli hivi karibuni na kukubali neno Langu kama maisha yenu—huu ndio mzigo Wangu mkubwa zaidi. Ikiwa makanisa na watakatifu wote wanaingia katika uhalisi na wote waweze kushiriki na Mimi moja kwa moja, wawe uso kwa uso na Mimi, na kutenda ukweli na haki, ni hapo tu ndipo wao ni wana Wangu wapendwa, wale ambao wananipendeza sana, na juu yao Nitawapa baraka zote kubwa.

Chanzo: Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 23
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

0 评论:

Chapisha Maoni