Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo makusudi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo makusudi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 29 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 98

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 98

Mambo yote yatakuja juu ya kila mmoja wenu, na yatawawezesha kujua zaidi juu Yangu na kuwa na uhakika zaidi juu Yangu. Yatawawezesha kunijua, Mungu mmoja Mwenyewe, kunijua Mimi Mwenye uweza, kunijua Mimi Mungu Mwenyewe mwenye mwili. Baadaye, Nitatoka katika mwili, Nirudi Sayuni, Nirudi katika nchi nzuri ya Kanaani, ambayo ni makazi Yangu, ndiyo hatima Yangu, na ndio msingi ambao niliumba vitu vyote. Sasa hakuna yeyote kati yenu anayeelewa maana ya maneno ambayo Ninasema, hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kuelewa maana ya maneno haya.

Jumamosi, 27 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 65

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 65

Maneno Yangu daima yanaendeleza barabara, yaani yanaonyesha udhaifu wenu wa jaala, vinginevyo bado mgekuwa mnakokota visigino vyenyu, bila wazo la muda gani ulioko sasa. Fahamu hili! Mimi Hutumia njia ya upendo ili kuwaokoa. Bila kujali jinsi nyinyi mlivyo, bila shaka Nitakamilisha mambo ambayo Nimekubali bila kufanya kosa lolote. Je, Ninaweza, Mwenyezi Mungu Mwenye haki, kufanya kosa? Je, hiyo siyo dhana ya mtu? Niambieni, kila kitu Mimi Hufanya na kusema si kwa ajili yenu?

Jumatano, 27 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)


  Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)


Katika nyakati zilizopita, watu walijifundisha wenyewe kuwa na Mungu na kuishi katikati ya roho kila wakati, ambao, ukilinganishwa na utendaji wa leo, ni mafundisho rahisi ya kiroho tu. Utendaji kama huu huja kabla ya kuingia kwa watu katika njia sahihi ya maisha, na ni mbinu ya juujuu zaidi na rahisi zaidi kati ya mbinu zote za utendaji. Ni utendaji wa hatua za mwanzoni kabisa za imani ya watu kwa Mungu. Ikiwa watu wataishi kila mara kwa utendaji huu, watakuwa na hisia nyingi sana, na hawataweza kuingia katika uzoefu ambao ni wa kina na wa kweli.

Ijumaa, 8 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Tatu

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Tatu

Namna Ambavyo Mungu Huanzisha Matokeo Ya Binadamu na Kiwango Ambacho Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu

Kabla ya kuwa na mitazamo au hitimisho zako binafsi, unafaa kwanza kuelewa mwelekeo wa Mungu kwako, kile ambacho Mungu anafikiria, na kuamua kama kufikiria kwako ni sahihi au la. Mungu hajawahi kutumia vipimo vya muda katika kuasisi matokeo ya mtu, na Hajawahi kutumia kiwango cha mateso yaliyovumiliwa na mtu katika kuasisi matokeo yake.

Alhamisi, 10 Januari 2019

Umeme wa Mashariki | Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Pili

Umeme wa Mashariki | Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Pili  

Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu
3. Sauti

Kitu cha tatu ni nini? Ni kitu ambacho mazingira ya kuishi ya kawaida ya wanadamu yanatakiwa kuwa nacho. Ni kitu ambacho Mungu alishughulikia alipoumba vitu vyote. Hiki ni kitu muhimu sana kwa Mungu na pia kwa kila mtu. Kama Mungu hakushughulikia suala hilo, ingekuwa kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ingekuwa na athari yenye maana sana kwa mwili na maisha ya mwanadamu, kiasi kwamba wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo.

Jumanne, 22 Mei 2018

Umeme wa Mashariki | 66. Ubia wa Kweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

Umeme wa Mashariki | 66. Ubia wa Kweli

Fang Li    Jiji la Anyang, Mkoa wa Henan
Hivi karibuni nilidhani nilikuwa nimeingia katika ubia wenye kuridhisha. Mshirika wangu na mimi tuliweza kujadili kitu chochote, wakati mwingine hata nikamwomba aonyeshe dosari zangu, na hatukupigana kamwe, hivyo nilidhani tulikuwa tumefanikisha ubia wenye kuridhisha.

Jumatatu, 21 Mei 2018

Maigizo Yaliyosimuliwa ya Hadithi za Kweli "Upendo wa Kweli wa Mungu" (Swahili Subtitles)

Maigizo Yaliyosimuliwa ya Hadithi za Kweli "Upendo wa Kweli wa Mungu" (Swahili Subtitles)

Ili kujitengenezea nafasi yake mwenyewe duniani, mhusika mkuu alilazimika kufuata mwenendo wa duniani humu, akihangaika na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya umaarufu na hadhi. Maisha yake yalilikuwa hasa matupu na yenye maumivu. Baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu, alipata maana ya maisha ya binadamu ndani ya maneno ya Mwenyezi Mungu, na akiwa amejawa na furaha, akamfuata Mungu na kutimiza majukumu yake. Hata hivyo, kwa sababu moyo wake ulikuwa chini ya udhibiti wa umaarufu na hadhi, katika kutekeleza majukumu yake mara kwa mara alitenda kwa mujibu wa mawazo yake mwenyewe, na alikuwa dhalimu na mwenye udikteta. Kwa sababu hii, alipogolewa na kushughulikiwa na ndugu. Kwanza, alibishana na hakukubali. Kupitia hukumu na kuadibiwa na maneno ya Mungu, alikuja kujua ukweli wa upotovu wake. Hata hivyo, kwa sababu hakuelewa nia ya Mungu, alimwelewa Mungu visivyo na kufikiri Mungu hangeweza kumwokoa. Kwa wakati huu, neno la Mungu lilimtolea nuru polepole, likamwongoza, na kumfanya kuelewa nia ya Mungu yenye ari ya kumwokoa mwanadamu, na alipitia upendo wa kweli wa Mungu kwa wanadamu …
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu
Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Alhamisi, 17 Mei 2018

Umeme wa Mashariki | 72. Nilijifunza Kufanya Kazi na Wengine

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Umeme wa Mashariki | 72. Nilijifunza Kufanya Kazi na Wengine

Liu Heng    Mkoa wa Jiangxi
Kupitia neema na kuinuliwa kwa Mungu, nilichukua jukumu la kuwa kiongozi wa kanisa. Wakati huo, nilikuwa na shauku mno na niliweka azimio mbele ya Mungu: Bila kujali kinachonikabili, sitayatelekeza majukumu yangu.

Alhamisi, 10 Mei 2018

Umeme wa Mashariki | Niko Tayari Kukubali Usimamizi wa Wote

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hukumu

 Umeme wa Mashariki | Niko Tayari Kukubali Usimamizi wa Wote

Xianshang     Mji wa Jinzhong, Mkoa wa Shanxi
Muda mfupi uliopita, kila wakati niliposikia kwamba wahubiri wa wilaya walikuwa wakija kwa kanisa letu, ningehisi kutaharaki kiasi. Sikufichua hisia zangu kwa nje, lakini moyo wangu ulijaa upinzani wa siri.

Ijumaa, 27 Aprili 2018

Ulinzi Bora Zaidi wa Mungu kwa Wanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maombi

Ulinzi Bora Zaidi wa Mungu kwa Wanadamu




Mji wa Kuiqian Rizhao, Mkoa wa Shandong
Kituo changu katika maisha, au hadhi, kilikuwa kitu ambacho sikuweza kamwe kukiachilia, na wakati Mungu alitengeneza mazingira yaliyonifichua, nilikuwa hasi, nikilalamika, na kukata tamaa tu. 

Ijumaa, 20 Aprili 2018

Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani. Suala hili si lile ambalo ni geni sana kwenu, lakini inaonekana kwamba hamwelewi au hamjazoea maana iliyomo kwenye suala hili. Wengi wanayo dalili ya ufahamu tu na mara nyingi maarifa ya juujuu kuhusu suala hili. Ili kuwasaidia kutenda kwa njia bora zaidi ukweli, yaani, kuwasaidia kuweka kwa njia bora zaidi maneno Yangu katika matendo, Nafikiri kwamba ni suala hili ambalo lazima kwanza mlijue. Vinginevyo, imani yenu itabakia isiyo wazi, ya unafiki, na iliyopambwa sana na dini. Kama huelewi tabia ya Mungu, basi itakuwa haiwezekani kwako wewe kufanya kazi unayofaa kumfanyia. Kama hujui dutu ya Mungu, ndivyo pia haitawezekana kubakiza hali ya kumcha na kumwogopa Yeye, utakuwa ni uzembe na kuepuka kusema ukweli wote kwa kutojali, na zaidi, kukufuru kusikorekebishika. Kuelewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, ilhali hakuna yeyote amewahi kuchunguza kwa umakinifu au kudadisi suala hili. Ni wazi kuona kwamba nyote mmepuuzilia mbali amri za kiutawala Nilizozitoa. Kama hamuelewi tabia ya Mungu, basi mtaweza kukosea kwa urahisi sana tabia Yake. Kosa kama hilo ni sawa na kumkasirisha Mungu Mwenyewe, na hatimaye linakuwa ni uhalifu dhidi ya amri ya kiutawala. Sasa unafaa kutambua kwamba unaweza kuelewa tabia ya Mungu unapokuja kujua dutu Yake, na kuelewa tabia ya Mungu ni sawa na kuelewa amri za kiutawala. Bila shaka, wingi wa amri za kiutawala zinahusu tabia ya Mungu, lakini uzima wa tabia Yake bado haujaweza kuonyeshwa ndani yao. Hili linawahitaji kuzoea zaidi tabia ya Mungu.
Ninaongea nanyi leo si katika hali ya mazungumzo ya kawaida, kwa hiyo lazima myajali maneno Yangu kwa bidii na, zaidi, kuyatafakari kwa kina. Kile Ninachomaanisha na haya ni kwamba mmetoa jitihada ndogo sana kwa maneno ambayo Nimeyazungumza. Tunapokuja kwa tabia ya Mungu, hamko radhi zaidi kutafakari juu ya suala hili, na wachache sana wanajitolea kufanya hili. Kwa hiyo, Nasema kwamba imani yenu ni maneno ya kujionyesha tu. Hata sasa, hakuna hata mmoja wenu ametoa jitihada yoyote ya kweli kwa udhaifu wenu mkuu zaidi. Mmenisikitisha baada ya maumivu yote Niliyoyapitia kwa ajili yenu. Si ajabu kwamba nyote hamjali Mungu na mnaishi maisha yasiyo na ukweli. Ni vipi watu kama hawa wanaweza kuchukuliwa kama watakatifu? Sheria ya mbinguni haitaweza kuvumilia kitu kama hiki! Kwa sababu mnao uelewa mdogo sana, basi itabidi Nitumie pumzi zaidi.
Tabia ya Mungu ni mada ambayo inaonekana kuwa dhahania sana na ambayo haikubaliwi kwa urahisi, kwani tabia Yake ni tofauti na hulka ya binadamu. Mungu, vilevile, anazo hisia za anasa, hasira, huzuni, na furaha, lakini hisia kama hizo zinatofautiana pia na zile za binadamu. Mungu anayo nafsi Yake mwenyewe na kile Anachokimiliki. Kila kitu Anachokidhihirisha na kukionyesha ni viwakilishi vya dutu Yake na utambulisho Wake. Nafsi Yake, kile Anachomiliki, pamoja na dutu na utambulisho vyote haviwezi kubadilishwa na binadamu yeyote. Tabia Yake inajumuisha upendo Wake kwa binadamu, kumtuliza binadamu, chuki kwa binadamu, na hata zaidi, uelewa wa kina wa mwanadamu. Hulka ya binadamu, hata hivyo, inaweza kuwa yenye matumaini mema, changamfu, au ngumu. Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa wale walio hai miongoni mwa vitu vyote, kwa Bwana wa viumbe vyote. Tabia Yake inawakilisha heshima, nguvu, uadilifu, ukubwa, na zaidi kuliko vyote, mamlaka ya juu kabisa. Tabia yake ni ishara ya mamlaka na kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, na kizuri. Aidha, ni ishara ya namna ambavyo Mungu hawezi[a] kukandamizwa au kushambuliwa na giza na kikosi chochote cha adui, pamoja na ishara ya namna ambavyo hawezi kuwa(na kwa kweli haruhusiwi kuwa)[b] kukasirishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi. Hakuna mtu au watu wanaoweza au wanaweza kutatiza kazi Yake au tabia Yake. Lakini hulka ya binadamu si zaidi ya ishara tu ya hali ya kuwa na mamlaka ya juu zaidi kiasi cha binadamu dhidi ya wanyama. Binadamu mwenyewe hana mamlaka, hana uhuru, na hana uwezo wa kuzidi nafsi, bali ni dutu tu inayotii kwa njia ya woga kutawaliwa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Anasa ya Mungu inatokana na uwepo na kuibuka kwa hali ya kuwa haki na mwangaza; kwa sababu ya kuangamizwa kwa giza na maovu. Anafurahia kwa sababu Ameuleta mwangaza na maisha mazuri kwa mwanadamu; furaha Yake ni ile ya hali ya haki, ishara ya uwepo wa kila kitu kilicho kizuri, na zaidi ya yote, ishara ya msaada. Hasira ya Mungu inatokana na uwepo wa dhuluma na vurugu inayosababisha ambayo inamdhuru mwanadamu Wake; kwa sababu ya uwepo wa maovu na giza, uwepo wa vitu vinavyoondoa ukweli, na hata zaidi kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyopinga kile ambacho ni kizuri na cha kupendeza. Hasira Yake ni ishara ya kwamba vitu vyote vibaya havipo tena, na fauka ya hayo, ni ishara ya utakatifu Wake. Huzuni Yake ni kwa sababu ya mwanadamu, ambaye kwake Ana matumaini lakini ambaye ameanguka katika giza, kwa sababu kazi Afanyayo kwa mwanadamu haifikii matarajio Yake, na kwa sababu binadamu Awapendao hawawezi wote kuishi katika mwanga. Anahisi huzuni kwa sababu ya mwanadamu asiye na hatia, kwa yule binadamu mwaminifu lakini asiyejua, na kwa yule binadamu mzuri lakini mwenye hisia kinzani. Huzuni Yake ni ishara ya wema Wake na huruma Yake, ishara ya urembo na wema Wake. Furaha yake, bila shaka, inatokana na kuwashinda adui Zake na kupata imani nzuri ya binadamu. Aidha, inatokana na kuondolewa na kuangamizwa kwa nguvu zote za adui na mwanadamu kupokea maisha mazuri na yenye amani. Furaha ya Mungu ni tofauti na furaha ya binadamu; badala yake, ni ile hisia ya kupokea matunda mazuri, hisia ambayo ni kubwa zaidi kuliko furaha. Furaha Yake ni ishara ya mwanadamu kuwa huru dhidi ya mateso na kuingia katika ulimwengu wa mwangaza. Hisia za mwanadamu, kwa upande mwingine, zote zipo kwa makusudio ya masilahi yake mwenyewe, na wala si za haki, mwangaza, au kile ambacho ni cha kupendeza, na kidogo kati ya vyote neema ya Mbinguni. Hisia za mwanadamu ni za ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo si za mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo binadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa kwa pumzi moja. Mungu siku zote anayo mamlaka ya juu zaidi na mwenye heshima kila wakati, huku naye binadamu siku zote akiwa chini na kila wakati akikosa thamani. Hii ni kwa sababu Mungu siku zote anajitolea mhanga na kujitoa Mwenyewe kwa mwanadamu; binadamu, hata hivyo, siku zote huchukua na hufanya kazi kwa ajili yake pekee. Siku zote Mungu anashughulikia uwepo wa mwanadamu, ilhali binadamu hachangii katu katika mwangaza au haki. Hata kama binadamu anashughulika kwa muda, yeye ni mnyonge na hawezi kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake na wala si wengine. Binadamu siku zote ni mbinafsi, huku naye Mungu siku zote si mbinafsi. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo na haki, wema, na urembo, huku naye binadamu akiwa mrithi na mwonyeshaji wa vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na urembo, ilhali binadamu anaweza, wakati wowote, kusaliti haki na kupotoka kutoka kwa njia ya Mungu.
Kila sentensi Niliyoizungumza inaendeleza tabia ya Mungu. Mngefanya vizuri zaidi endapo mngetafakari kuhusu maneno Yangu kwa umakini, na kwa kweli mtafaidi pakubwa kutoka katika maneno haya. Dutu ya Mungu ni ngumu sana kuelewa, lakini Ninaamini kwamba nyinyi nyote mnayo angalau baadhi ya maarifa kuhusu tabia ya Mungu. Ninatumai, basi, kwamba mtanionyesha Mimi na kufanya mengi zaidi ya yale ambayo hayakosei tabia ya Mungu. Kisha Nitatuliza moyo. Kwa mfano, mhifadhi Mungu katika moyo wako siku zote. Unapochukua hatua, timiza neno Lake. Tafuta fikira Zake katika kila kitu, na usifanye kile ambacho kitavunjia heshima na kumdhalilisha Mungu. Vilevile, usimweke Mungu nyuma ya akili zako ili ukajaze uwazi wa baadaye katika moyo wako. Ukifanya hivyo, basi utakuwa umekosea tabia ya Mungu. Kama kamwe hutamki matamshi ya kukufanya kukufuru au kulalamika dhidi ya Mungu na unaweza kufanya kikamilifu kila kitu ambacho amekuaminia wewe katika maisha yako yote, pamoja na kutii maneno yote ya Mungu, basi umeweza kuepuka kwa ufanisi kukosea amri za kiutawala. Kwa mfano, kama umewahi kusema “Kwa nini sifikirii kwamba Yeye ni Mungu?” “Nafikiri kwamba maneno haya si zaidi ya kutiwa nuru fulani na Roho Mtakatifu,” “Sifikirii kwamba kila kitu Mungu anachokifanya ni cha kweli,” “Ubinadamu wa Mungu hauna ukubwa zaidi kuliko wangu,” “Neno la Mungu haliaminiki tu,” au matamshi mengine kama hayo ya kuhukumu, basi Nakushawishi wewe kukiri dhambi zako na kutubu. Vinginevyo, hutawahi kuwa na fursa ya msamaha, kwani unakosea sio binadamu tu lakini Mungu Mwenyewe. Unaweza kuamini kwamba wewe unahukumu mtu tu, lakini Roho Mtakatifu wa Mungu hachukulii hivyo. Wewe kutoheshimu mwili Wake ni sawa na kumvunjia heshima Yeye mwenyewe. Kama hali ni hivi, basi si kweli kwamba umekosea tabia ya Mungu? Lazima mkumbuke kwamba kila kitu kinachofanywa na Roho wa Mungu ni kusaidia kazi Yake katika mwili na kufanya kazi kama hiyo vizuri. Ukiyapuuza haya, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye kamwe hataweza kufaulu katika kumwamini Mungu. Kwani umechochea hasira ya Mungu, na kwa hivyo lazima Atumie adhabu inayofaa ili kukufunza adabu.
Kuzoea dutu ya Mungu si jambo dogo. Lazima uelewe tabia Yake. Katika njia hii, polepole utaanza kuzoea dutu ya Mungu na hivyo basi kusonga mbele wakati uo huo katika hali kubwa zaidi na ya kupendeza zaidi. Hatimaye, utaaibika kutokana na nafsi yako ya kuchukiza, kiasi kwamba unaaibika kuuonyesha uso wako. Wakati huo, ndipo utakapokosea tabia ya Mungu kwa kiwango kidogo na kidogo; moyo wako utakuwa karibu zaidi na zaidi na ule wa Mungu, na polepole upendo wako Kwake utaweza kukua ndani ya moyo wako. Hii ni ishara ya mwanadamu kuingia katika hali nzuri. Lakini kufikia sasa bado hamjapata hili. Nyinyi hujichosha mkisafiri huku na kule kwa ajili ya hatima yenu, kwa hiyo ni nani angefikiria kujaribu na kuzoea zaidi dutu ya Mungu? Kama hali hii itaendelea, nyinyi mtaweza kuikosea bila kujua amri za kiutawala kwani mnajua kidogo sana kuhusu tabia ya Mungu. Kwa hivyo, kile mfanyacho sasa hakiweki msingi kwa sababu ya makosa yenu dhidi ya tabia ya Mungu? Kwamba Ninawaomba muweze kuelewa tabia ya Mungu haipingani na kazi Yangu. Kwani mkienda kinyume cha amri za kiutawala mara nyingi, basi ni nani kati yenu anayeweza kutoroka adhabu? Je, kazi Yangu haingekuwa bure kabisa? Kwa hivyo, Ningali Naomba kwamba pamoja na kuchunguza matendo yenu binafsi, kwamba muwe makini zaidi na hatua mnazochukua. Hili ndilo ombi kubwa zaidi ambalo Nitawaomba, na Ninatumai kwamba nyote mtalitilia maanani kwa umakinifu na kuliona kuwa muhimu. Endapo siku itawahi kufika ambapo matendo yenu yatanichochea Mimi hadi kuwa katika hali iliyojaa hasira, basi matokeo yatakuwa yenu pekee kufikiria, na hakuna mwingine yeyote atakayevumilia adhabu hiyo kwa niaba yenu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatatu, 2 Aprili 2018

Umeme wa Mashariki | Maonyo Matatu

Umeme wa Mashariki | Maonyo Matatu

Mwenyezi Mungu alisema, Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla ya kuuamua mwisho wenu, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu.

Jumatatu, 26 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Tano

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Tano

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu anapoweka mahitaji kwa wanadamu ambayo ni magumu kwao kueleza, na maneno Yake yanapogonga moja kwa moja katika moyo wa mwanadamu na watu wanatoa mioyo ya dhati ili Afurahie, basi Mungu huwapa watu nafasi ya kutafakari, kufanya uamuzi, na kutafuta njia ya kutenda.

Alhamisi, 22 Machi 2018

Tendeni Ukweli Mara Mnapouelewa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

Tendeni Ukweli Mara Mnapouelewa

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi neno la Mungu vina maana ya kuleta mabadiliko katika tabia zenu; lengo Lake si kuwafanya tu kulielewa au kulitambua na kufanya hilo kuwa mwisho wa jambo hilo. Kama mmoja wa uwezo wa kupokea, hampaswi kuwa na ugumu katika kuelewa neno la Mungu, kwa kuwa wingi wa neno la Mungu limeandikwa kwa lugha ya kibinadamu ambayo ni rahisi sana tu kuelewa. Kwa mfano, mnaweza kujua ni nini Mungu anataka muelewe na kutenda; hili ni jambo ambalo mtu wa kufaa ambaye ana uwezo wa uelewa anapaswa kuwa na uwezo wa kufanya. Maneno ya Mungu sasa ni hasa wazi na bayana, na Mungu husema mambo mengi ambayo watu hawajachukulia maanani au hali mbalimbali za mtu. Maneno yake yanajumuisha yote, angavu kama nuru ya mwezi kamili. Hivyo sasa, watu wanaelewa masuala mengi; wanachokosa ni kuweka neno Lake katika vitendo. Lazima watu wapitie vipengele vyote vya ukweli kwa kina, na kuutafiti na kuutafuta kwa undani zaidi, sio kusubiri tu kuchukua kile ambacho wamepewa bila shida; vinginevyo wanakuwa wadogo zaidi ya barakala. Wanajua neno la Mungu, lakini hawaliweki katika vitendo. Mtu wa aina hii hana upendo wa ukweli, na hatimaye ataondolewa. Kuwa na mtindo kama Petro wa miaka ya tisini inamaanisha ya kwamba kila mmoja wenu anapaswa kutenda neno la Mungu, kuwa na kuingia kwa kweli katika uzoefu wenu na kupata hata zaidi na hata nuru kubwa katika kushirikiana kwenu na Mungu, kuleta hata zaidi ya msaada Wake katika maisha yenu. Kama mmesoma sana neno la Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandishi na hamna maarifa ya kwanza ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu wa vitendo, hamtajua neno la Mungu. Ili mradi unahusika, neno la Mungu si maisha, lakini barua bila uhai. Na kama unaamini tu barua bila uhai, huwezi kufahamu kiini cha neno la Mungu, wala kuelewa mapenzi Yake. Wakati tu unapitia neno Lake katika uzoefu wako halisi ndio maana ya kiroho ya neno la Mungu itafunguka yenyewe kwako, na ni katika uzoefu tu ambapo unaweza kufahamu maana ya kiroho ya ukweli mwingi, na ni kwa kupitia tu uzoefu ndio unaweza kufungua mafumbo ya neno la Mungu. Usipoliweka katika vitendo, basi haijalishi jinsi neno Lake lilivyo wazi, jambo pekee ambalo umefahamu ukashikilia ni barua tupu na mafundisho, ambayo yamekuwa kanuni za dini kwako. Si hili ndilo Mafarisayo walifanya? Kama mtatenda na kupitia neno la Mungu, linakuwa vitendo kwenu; msipotafuta kulitenda, basi neno la Mungu kwenu ni kidogo zaidi ya hadithi ya mbingu ya tatu. Kwa kweli, mchakato wa kuamini katika Mungu ni mchakato wenu kupitia neno Lake pamoja na kupatwa na Yeye, au kuliweka wazi zaidi, kuamini katika Mungu ni kuwa na maarifa na ufahamu wa neno Lake na kupitia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake; huo ndio ukweli wa imani yenu katika Mungu. Kama mnaamini katika Mungu na mna matumani ya uzima wa milele bila kutafuta kutenda neno la Mungu kama kitu mlicho nacho ndani yenu, basi nyinyi ni wapumbavu; ni kama kwenda karamuni tu kuangalia yaliyo huko ya kula bila kweli kuyajaribu. Si mtu kama huyo ni mpumbavu?
Ukweli ambao mtu anahitaji kumiliki unapatikana katika neno la Mungu, ukweli ambao ni faida zaidi na manufaa kwa mtu. Ni lishe na riziki ambayo miili yenu inahitaji, kitu ambacho huwasaidia kurejesha ubinadamu wenu wa kawaida, ukweli ambao mnapaswa kujiandaa nao. Zaidi mnavyotenda neno la Mungu, kwa haraka ndivyo zaidi maisha yenu yatachanua; zaidi mnavyotenda neno la Mungu, ndio wazi ukweli unakuwa. Mnavyokua katika kimo, mtaona mambo ya ulimwengu wa kiroho wazi zaidi, na mtakuwa na nguvu zaidi ya ushindi juu ya Shetani. Sehemu kubwa ya ukweli ambao hamuelewi itakuwa wazi wakati unatenda neno la Mungu. Watu wengi wameridhika na kuelewa tu maandiko ya neno la Mungu na kuzingatia katika kujiandaa wenyewe na mafundishi bila kupitia kina chake katika vitendo; si hiyo ni njia ya Mafarisayo? Jinsi gani kirai “Neno la Mungu ni uzima” kikawa ukweli kwao, basi? Wakati tu mtu anatenda neno la Mungu ndio maisha yake yanaweza kweli kuchanua; maisha hayawezi kukua tu kwa kusoma neno Lake. Kama ni imani yako ya kwamba kuelewa neno la Mungu ni kila kinachohitajika kuwa na maisha, kuwa na kimo, basi kuelewa kwako ni potovu. Kuelea kwa kweli neno la Mungu hutokea wakati unatenda ukweli, na ni lazima uelewe ya kwamba “ni kwa kutenda tu ukweli kunaweza kueleweka siku zote.” Leo, baada ya kusoma neno la Mungu, unaweza tu kusema ya kwamba unajua neno la Mungu, lakini huwezi kusema ya kwamba unalielewa. Baadhi wanasema kuwa njia pekee ya kutenda ukweli ni kuelewa ukweli kwanza, lakini hii ni nusu tu ya haki na sio sahihi kabisa. Kabla uwe na maarifa ya ukweli, bado hujapitia ukweli huo. Kuhisi ya kwamba unaelewa unachosikia sio kitu kimoja kama kweli kuelewa. Kujiandaa mwenyewe na ukweli kama inavyoonekana katika maandishi si sawa na kuelewa maana halisi humo. Kwa sababu tu una ufahamu wa ukweli juu juu haina maana ya kwamba kweli unaelewa ukweli au kuutambu; maana halisi ya ukweli inatokana na kuwa na uzoefu wake. Ndio maana nasema ya kwamba wakati tu unapitia ukweli ndio unaweza kuuelewa, na wakati tu unapitia ukweli ndio unaweza kufahamu sehemu ya undani wake. Kuwa na uzoefu wa ukweli kwa kina ni njia pekee ya kufahamu kidokezo cha ukweli, na kuelewa kiini chake. Kwa hivyo, unaweza kwenda kila mahali na ukweli, lakini kama hakuna ukweli ndani yako, usifikirie hata kujaribu kuwashawishi watu wa kidini, kwa kiasi kidogo familia yako. Utakuwa kama kupepea kwa theluji bila ukweli, lakini kwa ukweli, unaweza kuwa na furaha na huru, ambapo hakuna awezaye kukushambulia. Haijalishi nadharia ina nguvu jinsi gani, haiwezi kushinda ukweli. Kwa ukweli, dunia yenyewe inaweza kutetemeka na milima na bahari kuhamishwa, wakati ambapo ukosefu wa ukweli unasababisha uharibifu na mabuu; huu ndio ukweli.
Cha muhimu sasa ni kujua ukweli kwanza, kisha uuweke katika vitendo, na kujiandaa wenyewe zaidi na maana halisi ya ukweli. Hilo ndio linapaswa kuwa lengo lako, sio tu watu kufanya wengine kufuata maneno yako lakini kuwafanya wafuate matendo yako, na ni katika hili tu unaweza kupata kitu cha maana. Bila kujali yanayokupata, bila kujali unayekutana naye, unaweza tu kusimama imara na ukweli. Neno la Mungu ndilo huleta maisha kwa mtu, sio kifo. Kama baada ya kusoma neno la Mungu hupati uzima, lakini bado umekufa baada ya kusoma neno Lake, basi kuna kitu kibaya na wewe. Kama baada ya muda fulani umesoma kiasi cha neno la Mungu na umesikia mahubiri mengi ya vitendo, lakini bado uko katika hali ya mauti, huu ni uthibitisho kuwa wewe si yule huthamini ukweli, wala mtu ambaye hutafuta ukweli. Kama kweli mngetafuta kumpata Mungu, hamngezingatia kujiandaa wenyewe na mafundisho ya juu na kuyatumia kuwahimiza wengine, lakini badala yake kuzingatia kupitia neno la Mungu na kuweka ukweli katika vitendo; si katika hilo ndio mnapaswa muingie ndani sasa?
Kuna muda mdogo kwa Mungu kufanya kazi Yake ndani yako, lakini kunaweza kuwa na matokeo yapi kama hushirikiani na yeye? Kwa nini daima Mungu huwataka kutenda neno Lake mara mnapolielewa? Ni kwa sababu Mungu amedhihirisha maneno Yake kwenu, na hatua yenu ifuatayo ni kweli kuyatenda, na Mungu atatekeleza kazi ya kutoa nuru na mwongozo wakati mnatenda maneno haya. Hivyo ndivyo jinsi ilivyo. Neno la Mungu linawekwa ili kuruhusu mtu kuchanuka maishani bila kusababisha kupotoka au ubaya. Unasema umesoma neno la Mungu na kulitenda, lakini hujapokea kazi yoyote ya Roho Mtakatifu—unachosema kinaweza tu kudanganya mtoto. Binadamu hajui kama nia zako ni sahihi, lakini unafikiri Mungu hawezijua? Ni jinsi gani basi wengine wanatenda neno la Mungu na wanapokea nuru ya Roho Mtakatifu, na bado kwa namna fulani unatenda neno Lake na hupokei nuru ya Roho Mtakatifu? Je, Mungu ni wa kihisia? Kama nia zako ni kweli nzuri na wewe ni mshirika, basi Roho wa Mungu atakuwa pamoja nawe. Mbona baadhi ya watu mara zote hutaka kuchukua nafasi maarufu, na bado Mungu hamruhusu kuinuka na kuongoza kanisa? Kwa nini baadhi ya watu hutimiza tu kazi yao na bila kuijua, wanapata kibali cha Mungu? Hilo linaweza kuwaje? Mungu huchunguza moyo, na watu ambao wanatafuta ukweli lazima wafanye hivyo kwa nia njema—watu ambao hawana nia njema hawawezi kusimama. Katika msingi wake, lengo lenu ni kuruhusu neno la Mungu kufanya kazi ndani yenu. Kwa maneno mengine, ni kuwa na uelewa wa kweli wa neno la Mungu katika kulitenda kwenu. Labda uwezo wenu wa kupokea neno la Mungu ni duni, lakini mnapotenda neno la Mungu, Yeye anaweza kubadilisha uwezo wenu duni kupokea, hivyo sio lazima tu mjue ukweli mingi, lakini pia ni lazima mtende huo ukweli. Hili ndilo lengo kubwa zaidi ambalo hauwezi kupuuzwa. Yesu aliteseka sana katika miaka yake 33½ kwa sababu Yeye alitenda ukweli. Kwa nini daima inasemwa katika rekodi ya kwamba Yeye aliteswa? Ni kueleza ni kiasi gani Yeye aliteseka kwa sababu Yeye alitenda ukweli na kutimiza mapenzi ya Mungu. Hangepitia mateso kama Yeye angejua ukweli bila kutenda ukweli huo. Kama Yesu angefuata mafunzo ya Wayahudi, na angefuata Mafarisayo, basi Yeye hangeteseka. Unaweza kujifunza kutoka kwa matendo ya Yesu ya kwamba ufanisi wa kazi ya Mungu juu ya mtu unatokana na ushirikiano wake, na hili ni jambo ambalo lazima mtambue. Je, Yesu angeteseka kama Yeye alivyofanya msalabani kama Yeye hangekuwa ametenda ukweli? Je, Yeye angeomba sala la huzuni kama hilo kama Yeye hangekuwa ametenda kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu? Basi hii ina maana ya kwamba hii ndio aina ya mateso mtu anapaswa kuvumilia.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatano, 14 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Utendaji (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Umeme wa Mashariki | Utendaji (1)

Mwenyezi Mungu alisema, kulikuwa na kupotoka kwingi katika jinsi watu walipata uzoefu, na kungeweza hata kuwa kwa ajabu. Kwa sababu tu hawakuelewa viwango vya mahitaji ya Mungu, kulikuwa na maeneo mengi ambayo uzoefu wa watu ulienda kombo. Sharti la Mungu kwa mtu ni kwao kuwa na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida. Njia za mtu wa kisasa kuhusiana na chakula na mavazi, kwa mfano. Wanaweza kuvaa suti na tai na wanaweza kujifunza kiasi kuhusu sanaa ya kisasa, na katika muda wao wa ziada wanaweza kuwa na kiasi fulani cha fasihi na maisha ya burudani. Wanaweza kuchukua baadhi ya picha za kumbukumbu na wanaweza kusoma na kupata kiasi cha elimu, na kuwa na mazingira mazuri kiasi ya kuishi. Haya ndiyo maisha ambayo yanastahili ubinadamu wa kawaida, ilhali watu wanayaona kama kitu kinachochukiwa na Mungu. Utendaji wao tu ni wao kufuata kanuni chache, na hii huwasababisha kuishi maisha yanayochosha sana, bila maana yoyote. Katika hali halisi, Mungu hajawahi kumhitaji mtu kufanya hivyo. Watu wanataka kukatiza tabia zao wenyewe, wakiomba bila kukoma katika roho zao ili wawe karibu na Mungu, mawazo yao daima yakiwa yamemilikiwa na kufikiria kuhusu mambo ya kimungu, macho yao mara kwa mara yakiangalia huku na kule, wakiangalia suala hili na suala lile, wakihofia kwa kiasi kikubwa kwamba uhusiano wao kwa Mungu utatengwa kwa namna fulani. Haya ni mambo yote ambayo mtu amejijumlishia mwenyewe; ni sheria ambazo zimewekwa kwa ajili ya mtu na mtu wenyewe. Usipoelewa kiini chako mwenyewe au kile kiwango ambacho mwenyewe unaweza kufikia, basi hutakuwa na namna yoyote ya kufahamu hasa viwango ni vipi ambavyo Mungu anahitaji kwa ajili ya mtu, na basi hutakuwa na namna yoyote ya kupata matendo ambayo yanatekelezwa katika hatua mwafaka. Akili yako daima inageuka upande huu na ule, unafikiria kila namna iwezekanayo kujifunza na kuhisi njia yako jinsi gani unaweza kusisimuliwa na kupata nuru kwa Roho Mtakatifu na matokeo kwamba unaweka muhtasari seti za njia za kutenda ambazo unadhani zitakusaidia kupata kuingia. Unapotenda kwa njia hii, hujui nini hasa ambacho Mungu anataka kutoka kwako; unatenda tu kwa njia yako mwenyewe, ukihisi starehe kabisa, bila kujali kuhusu matokeo wala kujali hata kidogo kuhusu iwapo kupotoka na makosa yapo. unapoendelea kwa njia hii, kutenda kwako kunakosa mambo mengi makubwa, kama vile pongezi ya Mungu, uthibitisho na Roho Mtakatifu na matokeo yanayopatikana kwa matakwa ya Mungu. Hata inakosa ubinadamu wowote wa kawaida au hisia za kawaida za mtu za mantiki. Kutenda kwako ni kufuata sheria tu, au kwamba uendelee kuongeza mzigo wako kimakusudi ili ujizuie, ili ujidhibiti. Na hata unafikiri kuwa kutenda kwako kuko sahihi, bila kujua kwamba sehemu kubwa ya kile unachotenda ni mchakato au utunzaji ambao si lazima. Kuna wengi ambao wanatenda hivi kwa miaka mingi bila mabadiliko kimsingi katika tabia zao, bila ufahamu mpya, na bila kuingia kupya. Wanazitekeleza kwa kutojua asili zao za kinyama, hata hadi hatua ambapo kuna mara nyingi wakati wanafanya mambo bila busara, mambo ya kinyama na mara nyingi wakifanya mambo ambayo huwapa watu kusita na ambayo hayaeleweki. Je, si aina hii ya mtu ni mtu ambaye amebadilika?
Sasa, kuzungumza kwa kiasi, watu huomba kidogo sasa ikilinganishwa na mbeleni kwa kuwa sasa si enzi ya kutafuta na kuhisi njia ya mtu ya kufuata. Sasa ni enzi ya ufunuo, Enzi ya Ufalme, ni maisha ya ufahamu ambapo vitu vyote vinaelezwa waziwazi kwa mtu, na mtu haachwi tena kuihisi njia katika maisha. Kuhusu masuala ya ndoa, mambo ya kidunia, maisha, chakula, mavazi na malazi, mahusiano kati ya watu, jinsi mtu anaweza kuhudumu katika njia ambayo inayakidhi mapenzi ya Mungu, jinsi mtu anavyoweza kuuacha mwili..., yepi kati ya haya hayajaambiwa kwenu? Je, bado mnahitaji kwenda kutafuta? Je, bado mnahitaji kuomba? Haina haja kweli! Kama bado unafanya vitu hivi, si unaongeza safu nyingine ya urasmi? Si lazima! Muhimu ni kama una azimio au la. Baadhi ya watu wanatenda kosa kwa kujua, na wanajua wazi kwamba kutembea njia ya dunia si vizuri, kwamba huleta hasara kwa maisha ya mtu na kuchelewesha maendeleo yao ya maisha, lakini wanasisitiza kulifanya, nao wanafanya hivyo baada ya kuomba na kutafuta. Je, si hii ni kutenda kosa kwa kujua? Kama wale wanaotamani sana anasa za mwili na kushikilia utajiri, ambaye baadaye anamwomba Mungu akisema: “Mungu! Je, Unaniruhusu nishikilie anasa za mwili na kushikilia utajiri? Je, ni mapenzi Yako nipate fedha kwa njia hii?” Je, hii ni njia ya kufaa kuomba? Ikiwa wanajua vizuri kabisa kwamba Mungu hafurahii mambo haya basi yanapaswa kuachiliwa, lakini mambo haya yameimarishwa katika mioyo nao wanaomba na kutafuta ili kumlazimisha Mungu kuwakubalia na kumfanya Mungu awape jibu. Kisha kuna wale ambao huwaleta ndugu wa kanisa upande wao na kuanzisha falme huru zao wenyewe. Unajua vizuri sana kwamba matendo haya yanamwasi Mungu, lakini bado unaenda kumtafuta na kumwomba Mungu. Wewe ni sugu na, ukifanya mambo hivi, bado unaweza kuonekana ukimwomba Mungu kwa ujasiri mkubwa na utulivu. Kweli huna aibu! Kuhusu kutembea njia ya dunia, hili limehubiriwa kwa muda mrefu mbeleni. Linachukiwa sana na Mungu, lakini bado unaomba, ukisema: “Ee Mungu! Unaniruhusu kutembea njia ya kidunia? Naweza kuyakidhi mapenzi Yako kwa njia hii? Kwa kweli, nia zangu ni sahihi. Sifanyi hivi kwa ajili ya mwili; nafanya hivi ili jina Lako lisitiwe aibu, nafanya hivyo kwa utukufu Wako, ili watu wa kidunia waweze kuona utukufu Wako ndani yangu. “Je, si njia hii ya kuomba ni upuuzi? Huoni aibu? Na si wewe unakuwa mjinga zaidi kufikiri kwamba hiki ni kitu cha thamani cha kufanya? Huna nia ya kupata uzoefu wa maisha ya mwanga, badala yake unakwenda kwa makusudi kuyaonja yale maisha katika giza na kuteseka. Hivyo si wewe unatafuta tu kuteseka? Umeambiwa jinsi ya kuishi maisha ya kiroho, maisha ya ubinadamu wa kawaida na umeambiwa kuhusu masuala yote ya ukweli. Kama huelewi kitu basi kiangalie moja kwa moja. Je, bado unahitaji kuyafunga macho yako na kuomba? Kama bado unaenda kutafuta kwa kuyaelekeza macho yako mbinguni, si bado unamwamini Mungu wa mashaka? Awali uliona matokeo kutokana na kutafuta kwako na kuomba na Roho Mtakatifu Aliisisimua roho yako kwa kiasi fulani kwa sababu wakati huo alikuwa Enzi ya Neema. Hukuweza kumwona Mungu hivyo hukuwa na chaguo lakini unaihisi njia yako mbele na kwenda kutafuta hivyo. Sasa Mungu Amekuja kati ya mtu na Neno limeonekana katika mwili. Sasa unaweza kumwona Mungu, na hivyo Roho Mtakatifu Hafanyi kazi tena kama Alivyofanya mbeleni. Enzi imebadilika na pia namna ambavyo Roho Mtakatifu hufanya kazi. Ingawa maombi yanaweza kutekelezwa kidogo zaidi kuliko awali, kwa sababu Mungu yuko duniani mtu sasa anayo nafasi ya kumpenda Mungu. Wanadamu wameingia katika enzi ya kumpenda Mungu nao wanayo ndani yao ukaribu sahihi kwa Mungu: “Ee Mungu! Hakika Wewe ni mzuri, nami niko tayari kukupenda!” Maneno machache tu ya wazi na rahisi hutoa sauti kwa upendo wa Mungu ndani ya moyo wako na ni kuimarisha tu upendo kati yako na Mungu. Wakati mwingine unaweza kujiona ukionyesha uasi kiasi, ukisema: “Ee Mungu! Mbona mimi ni mwovu sana?” Kweli unataka kujipiga, na machozi machoni mwako. Kwa wakati huu, moyo wako unahisi kujuta na kuwa na dhiki lakini huna namna ya kuionyesha. Hii ni kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, lakini hili ni jambo tu ambalo wale wanaotafuta maisha wanaweza kufikia. Unahisi kwamba Mungu anao upendo mkubwa kwako nawe unahodhi hisia maalum, lakini huna maneno ya kuomba kwa uwazi. Daima unahisi, hata hivyo, kwamba upendo wa Mungu ni kama kina cha bahari lakini huna namna ya kuonyesha hali hii, daima ukiuhisi katika moyo wako lakini kamwe huna maneno sahihi ya kuuonyesha. Hii ni hali ambayo mara nyingi hutokea katika roho. Aina hii ya maombi na ushirika ndani ya moyo wako kwamba inalenga kuwa karibu na Mungu ni ya kawaida.
Ingawa sasa maisha ya kuhisi njia ya mtu ya kwenda mbele na kutafuta yameisha, hii si kusema kwamba watu wasiombe kamwe, wala si kusema kwamba watu hawahitaji kuyasubiri mapenzi ya Mungu kujifunua kabla ya kuendelea na kazi; hizi ni baadhi tu ya mawazo ya mtu kabla ya kuona. Mungu amekuja miongoni mwa mtu kuishi naye na kuwa mwanga wa mtu, maisha ya mtu na njia ya mtu, na huu ni ukweli. Bila shaka, katika kuja kwa Mungu duniani ni muhimu Kwake kumletea mtu njia ya vitendo ambayo inafaa vimo vyao na maisha kwao kufurahia—Hajaja kuharibu njia zote za matendo ya mtu. Mtu haishi tena kwa kuihisi njia yake kwenda mbele na kutafuta kwa sababu hii imebadilishwa na kuja kwa Mungu duniani kufanya kazi na kunena Neno Lake. Amekuja kumweka huru mtu kutoka katika maisha ya giza na kumpa maisha ya mwanga. Kazi ya sasa ni kuonyesha mambo kwa uwazi, kusema kwa uwazi, kumwambia mtu moja kwa moja na kufafanua mambo waziwazi, ili mtu aweze kuweka mambo haya katika matendo. Kama vile Yehova alivyowaongoza watu wa Israeli, akiwaambia jinsi ya kutoa sadaka na jinsi ya kujenga hekalu, hivyo huna haja tena ya kuishi maisha ya kutafuta kama ulivyofanya Bwana Yesu alipoondoka. Je, ni muhimu kwenu kuihisi njia yenu kwa ajili ya kazi ya baadaye ya kueneza injili? Je, ni muhimu kwenu kuihisi njia yenu ili mjue jinsi mnavyopaswa kuishi? Je, ni muhimu kwenu kuihisi njia yenu ili mjue jinsi mnavyopaswa kutekeleza majukumu yenu? Je, ni muhimu kwenu kujisujudu ardhini na kwenda kutafuta ili mjue jinsi mnapaswa kutoa ushahidi? Je, ni muhimu kwenu kufunga na kuomba ili mjue jinsi mnapaswa kuvaa au kuishi? Je, ni muhimu kwenu kustahimili katika maombi yenu kwa Mungu mbinguni ili mjue jinsi mnapaswa kukubali kushindwa? Je, ni muhimu kwenu kuomba bila kukoma siku nzima na usiku kucha ili mjue jinsi mnapaswa kutii? Kuna wengi miongoni mwenu wanaosema kwamba hamwezi kutenda kwa sababu hamwelewi. Watu kweli hawaizingatii kazi ya leo! Mengi ya mambo haya nimeyasema muda mrefu uliopita, ni kwamba tu hamkuzingatia, hivyo si ajabu hamjui. Bila shaka, katika enzi ya leo Roho Mtakatifu bado Hajawasisimua watu ili kuwaruhusu kuhisi starehe, Naye anaishi pamoja na mtu. Hizi ni baadhi ya hisia maalum na zenye kuanisi ambazo mara nyingi hutokea katika maisha yako. Kila mara moja kwa wakati siku inakuja ambapo unahisi kwamba Mungu ni wa kupendeka sana nawe huwezi kutenda lingine ila kumwomba Mungu: “Ee Mungu! Upendo wako ni mzuri sana na picha Yako ni kubwa sana. Natamani kukupenda kwa undani zaidi. Natamani kutoa yote niliyo ili kuyatumia maisha yangu yote. Mradi ni kwa ajili Yako, natamani kutoa kila kitu kwako, ili tu kwamba iweze kukupenda Wewe....” Hii ni hisia ya furaha uliyopewa na Roho Mtakatifu. Si kupata nuru, wala mwangaza, ni kuchochea. Aina hii ya uzoefu itatokea mara kwa mara, kama vile ukielekea kazini. Utaomba na kujihisi karibu na Mungu, kiasi kwamba machozi yataulowesha uso wako, utaongozwa kiasi kwamba huwezi kujizuia nawe utakuwa na wasiwasi wa kupata mazingira ya kufaa ambapo unaweza kuonyesha hamasa zote moyoni mwako.... Wakati mwingine utakuwa katika shughuli ya umma nawe utahisi kwamba upendo unaofurahia ni mwingi mno, na kwamba bahati yako si ya kawaida, na zaidi utahisi kwamba wewe ni bora zaidi kuliko mwingine yeyote. Utajua kwa undani kwamba Mungu anakuinua, kwamba huu ni upendo mkuu wa Mungu kwa ajili yako. Katika maficho ya ndani kabisa ya moyo wako utahisi kuwa kuna aina ya upendo kuhusu Mungu usioelezeka na usiosomeka; ni kama unaujua lakini huna namna ya kuuonyesha, siku zote ukikufanya ufikirie kwa makini lakini ukikuacha usiweze kuuonyesha kabisa. Wakati kama huu, hata utasahau ulipo, hadi pale ambapo utazungumza: “Ee Mungu! Ni vigumu sana kukuelewa, lakini Wewe unapendwa sana! “Wakati mwingine unaweza hata kufanya baadhi ya vitendo vya ajabu na vya kipkee ambavyo watu kuviona visivyoelezeka, na haya ni mambo yote ambayo yanaweza kutokea mara nyingi .... Aina hii ya maisha ni magumu mno katika uzoefu wenu na mambo haya ni maisha ambayo Roho Mtakatifu amekupa leo, na maisha ambayo unapaswa kuishi sasa. Si kukufanya uache kuishi maisha, bali kwamba namna unavyoishi inabadilika. Ni hisia ambazo haziwezi kuelezeka au kuonyeshwa. Pia ni hisia ya kweli ya mtu na hata zaidi ni kazi ya Roho Mtakatifu. Inakufanya uelewe katika moyo wako, lakini huna namna ya kuionyesha wazi kwa mtu yeyote hata kidogo. Si kwa sababu wewe si mwepesi wa kusema au kwamba wewe ni kigugumizi, lakini kwa sababu ni aina ya hisia ambayo haiwezi kuelezwa katika maneno. Anakuruhusu kufurahia mambo haya leo kwa sababu haya ni maisha unayopaswa kuishi. Bila shaka, maisha yako mengine si matupu, kwamba tu kusisimuliwa kwa njia hii kunakuwa aina ya furaha katika maisha yako ambayo yanakufanya kutaka kufurahia misisimko ya Roho Mtakatifu siku zote. Lakini unapaswa kujua kwamba kuhamasishwa kwa namna hii sio kwamba uweze kujitenga kutoka kwenye mwili na kwenda mbingu ya tatu, au kusafiri duniani, bali ni kuwa uweze kupata uzoefu wa upendo wa Mungu leo, upate uzoefu wa umuhimu wa kazi ya Mungu leo, kumbukia utunzaji na ulinzi wa Mungu. Mambo haya yote ni kwa ajili yako kuwa na maarifa zaidi ya kazi ya Mungu hufanya leo na kuwa na uwezo wa kuhisi na kupata uzoefu zaidi wa upendo wa Mungu ambao unaufurahia leo—hili ni lengo la kazi hii.
Maisha ya kutafuta na kuihisi njia ya mtu yalikuwa wakati Mungu alikuwa bado hajakuwa mwili. Wakati huo watu hawangeweza kumwona Mungu na hivyo hawakuwa na chaguo lakini kutafuta na kuihisi njia yake kuendelea. Leo unaweza kumwona Mungu naye Anakwambia moja kwa moja jinsi unapaswa kutenda ili usihitaji tena kuihisi njia yako hapa na pale au kutafuta tena. Njia inayooongozwa naye ni njia ya ukweli na yale Anayomwelezea mtu, kile mtu anachokipata ni maisha na ukweli. Unaweza kuwa na njia nau kweli wa maisha, hivyo haja gani ipo kwenda kutafuta mahali popote? Roho Mtakatifu hawezi kufanya hatua mbili za kazi kwa pamoja. Kama, wakati Nimemaliza kuzungumza neno Langu, watu bado wanahitaji kuomba na kutafuta, hiyo haitamaanisha kwamba hatua hii ya kazi Ninayoifanya inafanywa bure? Ingawa Naweza kuwa nimemaliza kunena neno Langu, watu bado hawaelewi kabisa, na hii ni kwa sababu wanakosa ubora. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa njia ya maisha ya kanisa na kupitia kushiriki mmoja kwa mwingine. Mbeleni, Mungu aliyekuwa mwili hakuanza kazi, hivyo Roho Mtakatifu alifanya kazi kwa njia hiyo wakati huo na kuidumisha kazi. Wakati huo Roho Mtakatifu aliifanya kazi, lakini sasa ni Mungu aliyekuwa mwili Mwenyewe ambaye anaifanya, baada ya kuchukua nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu. Wakati watu waliomba mbeleni, walipata amani, furaha, lawama na nidhamu na hii yote ilikuwa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Sasa hali hizi ni chache na nadra. Mbona wakati Petro aliomba hakuwa na hisia za amani au za lawama, na kwa nini Paulo na wengine pia walihisi hivyo walipoomba? Hii ilikuwa kwa sababu ulikuwa ni wakati ambao kuonekana kwa Mungu hakukuwa kumeonekana, na zaidi ya hayo ulikuwa wakati wa Enzi ya Neema wakati Mungu alifanya kazi tofauti. Roho Mtakatifu anaweza tu kufanya aina moja ya kazi katika enzi yoyote ile. Kama Angefanya aina mbili za kazi wakati huo huo, mwili ukifanya aina moja na Roho Mtakatifu Akifanya aina nyingine ndani ya watu, na kama kile mwili ulisema haikuwa halali na kile Roho Alifany kilikuwa, basi Kristo asingekuwa na ukweli wowote, njia au maisha ya kuyataja. Huku kungekuwa kujipinga, na kungekuwa makosa katika chanzo hasa.
Watu walipotoka sana na walifanya makosa mengi mno katika uzoefu wao wa zamani. Awali kulikuwa na baadhi ya mambo ambayo watu wa ubinadamu wa kawaida walikuwa wamenuiwa kuwa nayo, na kunuiwa kufanya, au kulikuwa na makosa yasiyoepukika ambayo yalinuiwa kuonekana katika maisha ya binadamu, na wakati mambo hayo yalitendwa vibaya, waliliweka jukumu hilo kwa Mungu. Kulikuwa na dada ambaye alikuwa na wageni nyumbani kwake. Maandazi yake yaliyochomeka hayakuchemshwa vyema, hivyo akafikiri:: “Hii inaweza kuwa nidhamu ya Mungu. Mungu anaushughulika moyo wangu usiofaa. Mimi sifai kabisa.” Kwa kweli, alimradi njia ya kawaida ya mtu ya kufikiri inavyohusu, wageni wanapokuja unapata msisimko na kukimbia huku na kule, bila kujua nini cha kufanya kwanza na bila kuwa umepangwa unachofanya, matokeo yake ni kwamba ikiwa wali hautaishia kuungua, basi vyakula vyako vina na chumvi nyingi sana. Kwa kawaida, bila wageni uko sawa, lakini wakati ambapo watu wanakuja kila kitu kinakwenda mrama. Hali hii inasababishwa na hisia za msisimko, lakini watu huishia kudhania kuwa ni “nidhamu ya Mungu.” Kwa kweli, hii inafungamana na makosa katika maisha ya binadamu. Je, hungekumbana pia na aina hii ya kitu iwapo hukumwamini Mungu? Si aina hii ya kitu tukio la mara kwa mara? Kuna mambo mengi yanayofungamana na makosa ya watu; watu hufanya makosa, lakini hayafanywi na Roho Mtakatifu na hayamhusu Mungu. Kama unavyojiuma ulimi unapokula—yawezekana kuwa hii ni nidhamu ya Mungu? Nidhamu ya Mungu ina kanuni na kwa kawaida huonekana wakati unatenda kosa kwa kujua. Mungu humfundisha mtu nidhamu na mambo yanayohusu jina Lake, au wakati inahusu ushuhuda Wake au kazi Yake. Watu huuelewa ukweli vya kutosha sasa ili kuwa na ufahamu wa ndani wa mambo ya wanayoyafanya, kwa mfano: Je, unaweza kutohisi kitu unapozibadhiri fedha za kanisa au kuzitumia bila kujali? Utahisi kitu unapofanya hivyo. Haiwezekani kufanya kitu na kisha kuanza kuhisi kitu baadaye. Uko wazi moyoni mwako kuhusu mambo unayoyafanya ambayo yanaenda kinyume na dhamiri yako. Ingawa wanaweza kuujua ukweli kwa wazi, kwa sababu kila mtu anayo anayoyapenda, wao hujiingiza tu, hivyo baada ya wao kufanya kitu hawana hisia za wazi ya shutuma. Kama hawana nidhamu wakati wanapofanya makosa, nidhamu gani inaweza kuweko baadaye? Nidhamu gani inaweza kuweko baada ya fedha zote kubadhiriwa? Wao wana ufahamu kabisa wa nini wanachokifanya wanapofanya hivyo na kuhisi lawama. Usiposikiliza basi Mungu hatakupa usikivu. Utakapofika wakati ambapo hukumu ya haki inatokea, adhabu ataletwa juu ya kila mmoja kulingana na matendo yake. Kama mtu wa kawaida mwenye hisia ya mantiki, mtu ambaye ana dhamiri, una ufahamu wa kila kitu unachokifanya, hasa unapofanya kitu kibaya. Je, bado kuna watu wachache kanisani ambao hubadhiri fedha? Je, bado kuna watu wachache ambao hawaweki mipaka wazi kati ya wanaume na wanawake? Je, bado kuna watu wachache wanaohukumu, kupinga na kujaribu kuvunja mambo kwa siri? Kwa nini bado kila kitu kiko sawa nanyi? Nyote mnao ufahamu, hisia na aibu mioyoni mwenu na kwa sababu hii wakati mwingine mnateseka kuadibiwa na utakaso. Ni kwamba tu watu hawana aibu! Kama nidhamu kweli ingewafika, bado wangethubutu kutenda kwa njia hii? Wakati ambapo watu wa dhamiri hufanya mambo, wanahisi kufadhaika wakati dhamiri yao inachomwa kidogo tu, na kwa hiyo wana uwezo wa kuiacha miili yao. Kama wale wanaotenda dhambi kati ya wanaume na wanawake. Wanao ufahamu wa kile wanachofanya wakati huo, lakini tamaa yao ni kubwa mno na hawawezi kujidhibiti. Hata kama Roho Mtakatifu anatoa nidhamu, haitakuwa bure, hivyo Roho Mtakatifu hajishughulishi nawe tena. Wakati huo, kama Roho Mtakatifu hakukufundisha nidhamu, kukulaumu au kukifanyia chochote mwili wako, lawama gani ingeweza kutokea baadaye? Nidhamu gani inaweza kuwa baada ya tendo kufanyika? Inathibitisha tu kwamba huna aibu na unapuuzwa. Wewe ni fidhuli usiye na maana! Roho Mtakatifu hafanyi kazi bila sababu. Ikiwa unaujua ukweli vizuri sana lakini hushirikiani na una uwezo wa kufanya kitu chochote kabisa, basi unaweza kusubiri tu hadi siku ile ambayo inakuja wakati ambapoutaadhibiwa pamoja na yule mwovu. Huu ni mwisho bora kwako! Sasa Nimehubiri nikirudia kuhusu dhamira, kwa kuwa hiki ni kiwango cha chini zaidi. Bila dhamira, watu pia watapoteza nidhamu ya Roho Mtakatifu, na wanaweza kufanya chochote wanachopenda. Ikiwa kweli mtu ana dhamira, basi wakati ambapo Roho Mtakatifu anamshutumu anapitia vita vya ndani, na basi hana uwezekano wa kufanya kitu chochote kikubwa mno. Haijalishi jinsi Roho Mtakatifu anafundisha nidhamu ama kuadibu, kwa ujumla watu wote watakuwa na hisia kiasi wanapofanya kitu kibaya. Hivyo watu sasa wanaelewa kila aina ya ukweli na kama hawautendi basi hiyo ni shauri yao. Siwajibu watu kama hawa, wala sishikilii tumaini lolote kwao. Unaweza kufanya unavyopenda!
Baadhi ya watu huja pamoja na kuliweka neno la Mungu upande mmoja, daima wakizungumza kuhusu jinsi mtu huyu au mtu yule alivyo. Bila shaka ni vizuri kuwa na upambanuzi mdogo, kwa kuwa bila kujali unapokwenda hutadanganywa kwa urahisi, wala hautalaghaiwa au kupumbazwa kwa urahisi; hiki pia ni kipengele ambacho watu wanapaswa kumiliki. Lakini usilenge tu katika suala hili kwa kuwa linafungamanishwa na mambo ambayo ni hasi. Macho yasikaziwe daima kwa watu. Ufahamu wako wa jinsi Roho Mtakatifu anafanya kazi sasa ni kidogo mno, imani yako katika Mungu ni ya juujuu sana, nawe unayo mambo machache mno mazuri. Yule unayemwamini ni Mungu, Yule unayehitaji kumwelewa ni Mungu, si Shetani. Ikiwa unaelewa tu jinsi Shetani anafanya kazi na kuwa na ufahamu wa njia zote ambazo roho mbaya zinafanya kazi, lakini huna ujuzi wa Mungu kwa lolote, haya yatakuwa na maana gani? Je, si ni Mungu unayemwamini leo? Kwa nini ufahamu wako hauhusishi mambo haya mazuri? Hutilii tu maanani kipengele chanya cha kuingia na huna ufahamu wake, hivyo nini unachotaka kupata? Je, hujui jinsi unapaswa kutafuta? Unavyo vifaa vingi hasi “vya kufundishia” lakini unaambulia patupu na suala chanya la kuingia, hivyo ni jinsi gani kimo chako kitawahi kukua? Mtu akizungumza tu kuhusu vita na Shetani, ni matarajio yapi ya baadaye ya maendeleo mtu huyo atakuwa nayo? Si kuingia kwako kumepitwa na wakati sana? Mambo gani utakayoweza kupata kutokana na kazi ya sasa ukiendelea kwa njia hii? Kile ambacho ni muhimu sasa ni wewe uelewe nini Mungu anataka kufanya sasa, jinsi binadamu anapaswa kushirikiana, jinsi wanavyopaswa kumpenda Mungu, jinsi wanavyopaswa kuielewa kazi ya Roho Mtakatifu, jinsi wanavyopaswa kuingia katika maneno yote ambayo Mungu anasema leo, jinsi wanavyopaswa kuyaona, kuyaelewa na kuwa na uzoefu kwayo, jinsi yanavyopaswa kuyakidhi mapenzi ya Mungu, kushindwa kabisa na Mungu na kutii mbele za Mungu .... Unapaswa kulenga mambo haya kwa kuwa haya ni mambo yanayopaswa kuingiwa sasa. Je, unaelewa? Kuna faida gani kulenga tu juu kuhusu utambuzi wa watu? Unaweza kumtambua Shetani hapa, kuzitambua roho mbaya huko, unauweza kutambua mambo mengi, kuwa na ufahamu kamili wa roho mbaya na kuijua moja mara tu unapoiona. Lakini kama huwezi kusema chochote kuhusu kazi ya Mungu, utambuzi wako unaweza kuchukua nafasi ya ufahamu wako kuhusu Mungu? Hapo awali Nimeshiriki kuhusu maonyesho ya kazi ya roho mbaya, lakini hili si jambo kuu. Bila shaka watu wanapaswa pia kuwa na ufahamu kidogo kwa kuwa hili ni suala ambalo wale wanaomtumikia Mungu wanapaswa kumiliki ili kuepuka kufanya mambo ya kipuuzi na kuikatiza kazi ya Mungu. Lakini jambo muhimu zaidi linabaki kuwa na elimu ya kazi ya Mungu na kuelewa mapenzi ya Mungu. Ni ufahamu gani ulio nao wa hatua hii ya kazi ya Mungu? Je, unaweza kusema ni nini ambacho Mungu anafanya, mapenzi ya Mungu ni yepi, na unaweza kusema mapungufu yako ni yapi na mambo unayopaswa kujiandaa nayo? Je, unaweza kusema kuingia kwako kupya zaidi ni nini? Unapaswa kuelewa maingio yepi ya zamani yalikuwa mikengeuko na makosa, na maingio yepi yalikuwa yamepitwa na wakati. Unapaswa kupata tuzo na ufahamu katika maingio yako mapya. Usijidai kuwa ujinga; lazima ufanye juhudi katika maingio yako mapya ili uimarishe uzoefu na ufahamu wako mwenyewe, na hata zaidi lazima ufahamu sana hasa maingio yako mapya zaidi na njia sahihi zaidi ya kupata uzoefu. Lazima pia ujue jinsi ya kuzitupilia mbali mbinu zako za kutenda zilizopitwa na wakati na kuingia katika uzoefu mpya. Hata zaidi hivyo unapaswa kutambua kutenda kwako kulikopitwa na wakati kutokana na kazi mpya na kuingia. Haya ni mambo ambayo sasa unahitaji kuelewa kwa haraka na kuingia ndani yake. Lazima ufahamu tofauti na uhusiano kati ya maingizo yako ya zamani na mapya. Kama huna ufahamu wa hali ya juu wa mambo haya, basi hutakuwa njia ya yoyote ya kuendelea, kwa kuwa hutaweza kuendelea na kazi ya Roho Mtakatifu. Sehemu kubwa ya kuingia kwako kwa zamani na uzoefu iliungamanishwa na njia ya kutenda ya kupotosha na yenye makosa, na sehemu kubwa ya huku ilikuwa namna ya kupata uzoefu ambao ulikuwa wa wakati uliopita; lazima uelewe jinsi unavyopaswa kuwa na mtazamo wa vitu hivyo. Kwa njia ya kula kwa sahihi na kunywa neno la Mungu na kupitia ushirika mzuri, lazima uwe na uwezo wa kubadilisha dhana zako za kutenda za zamani na dhana zako za desturi za jadi, ili uweze kuingia katika kutenda kupya, na kuingia katika kazi mpya. Haya ni mambo unayopaswa kupata. Sasa Sikusihi kwamba ujielewe hadi kiwango kidogo zaidi; Sikusihi ulichukue hili kwa umakini sana.. Badala yake Nakusihi kuchukulia kwa umakini kuingia kwako na ufahamu wa kipengele chanya. Ingawa unaweza “kujijua,” haifuati kwa lazima kwamba hii ni kimo chako cha kweli. Lakini kama unaweza kupata uzoefu wa kutenda na kuingia kwa kazi mpya, hadi pale ambapo unaweza kufahamu na dhana zako binafsi zilikuwa nini au kutokuelewana, basi hiki ni kimo wako cha kweli nacho ni kitu unapaswa kumiliki. Haya ni mambo ambayo kila mtu kati yenu anapaswa kupata.
Kuna mambo mengi ambayo ninyi hamjui tu jinsi ya kutenda, hata zaidi kujua jinsi Roho Mtakatifu anafanya kazi. Wakati mwingine unafanya kitu ambacho kwa wazi hakimtii Roho Mtakatifu. Tayari una ufahamu wa kanuni ya kitu kupitia kula kwako na kunywa, hivyo unasumbuliwa kwa ndani na hisia ya lawama na kufadhaika na bila shaka hii ni hisia kuwa mtu ataihisi kwa misingi ya kuujua ukweli. Kutoshirikiana na kutofanya mambo kulingana na neno leo huipinga kazi ya Roho Mtakatifu na mtu lazima atahisi kufadhaika ndani mwake. Unaelewa kanuni za kipengele hiki lakini hutendi ipasavyo, hivyo unateswa na hisia ya lawama kwa ndani. Lakini kama huelewi kanuni hii, na hujala wala kunywa suala hili la ukweli, kama huijui kabisa, basi si lazima uhisi hali ya lawama katika suala hili. Kuzalisha shutuma ya Roho Mtakatifu ni kwa masharti. Unafikiri kwamba kwa sababu hujaomba, hujashirikiana na Roho Mtakatifu, hujauachilia mzigo unaoubeba ndani yako, umeichelewesha kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hali halisi haiwezi kucheleweshwa, na kama hutasema kitu basi Roho Mtakatifu Atamchochea mtu mwingine kukisema; Roho Mtakatifu Hazuiliwi nawe. Unahisi kutubu kwa Mungu na hili ni jambo unalopaswa kuhisi. Lakini Mungu hadhanii chochote na basi ni la zamani. Kama unaweza kupata kitu chochote au la ni shauri yako. Wakati mwingine dhamiri yako inahisi kama inateswa na shutuma, lakini hii si kupata nuru au mwangaza katika Roho Mtakatifu wakati huo, wala si lawama ya Roho Mtakatifu. Badala yake ni hisia katika dhamiri yako. Kama inahusisha jina la Mungu, ushuhuda wa Mungu au kazi ya Mungu, na wewe unatenda ovyo ovyp, basi Yeye hatakuachilia. Lakini ina kikomo, na kwa mambo ambayo ni vigumu kuyataja, Hatajishughulisha nawe, Atakupuuza, na hivyo hili ni jambo ambalo unapaswa kulihisi katika dhamiri yako. Baadhi ya mambo ni yale ambayo watu wa ubinadamu wa kawaida wanapaswa kuyafanya na baadhi ni mambo ya maisha ya binadamu ya kawaida. Kwa mfano, huchemshi maandazi vyema na kusema kuwa Mungu Anakuadhibu—hii ni kitu kisicho na mantiki kabisa kusema. Kabla ya kuja kumwamini Mungu, aina hii ya kitu hakikutokea mara nyingi? Je, ilikuwa ni Shetani akikuadhibu hapo awali? Kwa kweli unapotenda zaidi kuhusu jambo hili, hutakuwa na uwezekano wa kutenda makosa, ni ubongo wako tu ambao unafanya makosa. Unahisi kwamba inaonekana kuwa nidhamu ya Roho Mtakatifu wakati kwa kweli hivi sivyo (baadhi hali za kipekee kando), kwa sababu kazi hii haifanywi kabisa na Roho Mtakatifu, lakini badala yake ni hisia tu ambazo watu wanazo. Lakini kufikiri kwa namna hii kile wale ambao wana imani sahihi katika Mungu wanapaswa kufanya. Hungeweza kufikiri hivi wakati ambapo hukumwamini Mungu. Mara ulipokuja kumwamini Mungu, moyo wako unatumia juhudi zote katika suala hili na kwa kutojua ulianza kufikiri kwa namna hii. Hii inatokana na mawazo ya kawaida ya watu na pia inafungamana na mawazo yao wenyewe. Lakini acha Nikwambie, hiki si kitu ambacho kiko chini ya eneo la kazi ya Roho Mtakatifu. Jambo hili linafungamana na mjibizo wa kawaida aliyopewa mtu na Roho Mtakatifu kwa njia ya kufikiri kwake mwenyewe; lakini lazima uelewekwamba mjibizo huu si kazi ya Roho Mtakatifu. Kuwa na aina hii ya “maarifa” haithibitishi kwamba unayo kazi ya Roho Mtakatifu. Uwlewa wako haufungamani na kupata nuru kwa Roho Mtakatifu, kiasi kidogo ni kazi ya Roho Mtakatifu. Ni mjibizo tu wa kufikiri kwa kawaida kwa watu na hauhusiani kamwe na kupata nuru au mwanga wa Roho Mtakatifu. Hayo ni mambo mawili tofauti kabisa na halifanywi kabisa na Roho Mtakatifu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ili kuwapa watu nuru, Yeye kwa ujumla kuwapa ufahamu wa kazi ya Mungu, na ya kuingia kwao ya kweli na hali ya ukweli, na pia Huwapa azimio, huwaruhusu kuelewa kusudi la hamu la Mungu na mahitaji yake kwa ajili ya mtu leo, Huwapa azimio la kufungua njia zote. Hata wakati ambapo watu wanapitia umwagaji damu na sadaka ni lazima watende kwa ajili ya Mungu, na hata kama wanakumbana na mateso na dhiki, lazima bado wampende Mungu, na wasiwe na majuto, na lazima wawe shahidi kwa Mungu. Azimio la aina hii ni misisimko ya Roho Mtakatifu, na kazi ya Roho Mtakatifu—lakini jua kwamba hujamilikiwa na misismko kama hii kila wakati. Wakati mwingine katika mikutano unaweza kuhisi kuongozwa mno na kupata msukumo nawe unatoa sifa kubwa zaidi na unacheza. Unahisi kwamba una ufahamu usioaminika wa yale wengine wanashiriki, unahisi mpya kabisa kwa ndani, na moyo wako uko wazi kabisa bila hisia yoyote ya utupu—haya yote yanaungamanishwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kama wewe ni mtu ambaye huongoza, na Roho Mtakatifu anakupa nuru na mwangaza usio wa kawaida unapoenda kanisani kufanya kazi, akikufanya uwe mwenye bidii wa kushangaza, mwenye kuwajibika na kitilia maanani kazi yako, hii inafungamanisha kazo ya Roho Mtakatifu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Jumamosi, 10 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Njia… (5)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Umeme wa Mashariki | Njia… (5)

Mwenyezi Mungu alisema, Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu mbele ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba karibu watu wote wanaoamini katika Mungu hawamjui Roho, lakini tu wana aina ya imani iliyochanganyikiwa.Ni wazi kutokana na hili kwamba watu hawamfahamu Mungu, na hata ingawa wanasema wanaamini katika Yeye, kuhusu kiini chake, kulingana na matendo yao wanaamini katika wao wenyewe, sio Mungu. Kutokana na uzoefu Wangu binafsi wa kweli, Naweza kuona kwamba Mungu humshuhudia Mungu katika mwili, na kutoka nje, watu wote hulazimishwa kukubali ushahidi Wake, na inaweza tu kusemwa kwa shida kuwa wanaamini kwamba Roho wa Mungu hana kosa kabisa. Hata hivyo, Nasema kwamba kile ambacho watu wanaamini si mtu huyu na hasa si Roho wa Mungu, lakini wanaamini katika hisia zao wenyewe. Je, huko si kuamini tu katika wao wenyewe? Maneno haya Nisemayo yote ni ya kweli. Huko si kupachika watu majina, lakini nahitaji kueleza wazi kitu kimoja—kwamba watu wanaweza kuletwa katika siku hii, wawe wana uwazi au wamechanganyikiwa, hii yote inafanywa na Roho Mtakatifu na si kitu ambacho wanadamu wanaweza kuamuru. Huu ni mfano wa kile ambacho Nimetaja awali kuhusu Roho Mtakatifu kulazimisha imani ya watu. Hivi ndivyo Roho Mtakatifu hufanya kazi, na ni njia moja ambayo Roho Mtakatifu hufuata. Haijalishi yule ambaye watu huamini kwa asili, Roho Mtakatifu kwa nguvu huwapa watu aina fulani ya hisia ili waamini katika Mungu ndani ya mioyo yao. Hii siyo aina ya imani uliyo nayo? Je, huhisi kwamba imani yako katika Mungu ni kitu cha ajabu? Je, hudhani kwamba ni kitu cha ajabu kwamba huwezi kuepuka kutoka kwa mkondo huu? Hujaweka juhudi yoyote kulitafakari hili? Hii siyo ishara na ajabu kuu zaidi? Hata kama umekuwa na hamu kubwa ya kutoroka mara nyingi, huwa kila mara kuna nguvu ya maisha kuu inayokuvutia na kukufanya usite kuondoka. Na kila mara unapokabiliwa na hili unasongwa roho na kuwa na kikweukweu, na hujui la kufanya. Na kuna watu wengine ambao hujaribu kuondoka. Lakini unapojaribu kwenda, ni kama kisu kwa moyo wako, na ni kama kwamba nafsi yako imetolewa ndani yako na zimwi juu ya dunia ili moyo wako uwe na wahaka na ukose amani. Baada ya hilo, huwezi kufanya lolote bali kujitayarisha kukutana na jambo gumu na kurudi kwa Mungu…. Hujawahi kuwa na tukio hili? Naamini kwamba ndugu wadogo ambao wanaweza kuifungua mioyo yao watasema: “Ndio! Nimekuwa na matukio mengi sana kama haya; Ninaona aibu sana kuyafikiria!” Katika maisha Yangu ya kila siku Mimi huwa na furaha kila mara kuwaona ndugu Zangu wadogo kama wandani Wangu kwa sababu wamejawa na umaasumu—wao ni safi na wa kupendeka. Ni kama kwamba wao ni wenzi Wangu. Hii ndio maana kila mara Mimi hutafuta nafasi ya kuwaleta wandani Wangu wote pamoja, kuzungumza juu ya maadili yetu na mipango yetu. Mapenzi ya Mungu yatekelezwe ndani yetu ili sote tuwe kama mwili na damu, bila vizuizi na bila umbali. Hebu sote tuombe kwa Mungu: “Ee Mungu! Ikiwa ni mapenzi Yako, tunakusihi utupe mazingira yanayofaa ili sote tutambue matamanio yaliyo ndani ya mioyo yetu. Utuonee huruma sisi ambao ni wadogo na wanaokosa akili, ili tutumie kila tone la nguvu ndani ya mioyo yetu!” Naamini kwamba haya lazima yawe ni mapenzi ya Mungu kwa sababu zamani sana, Nilisema ombi hili mbele ya Mungu: “Baba! Sisi tulio duniani hukuita wakati wote, na kutarajia kwamba mapenzi Yako yatatimizwa hivi karibuni duniani. Niko radhi kutafuta mapenzi Yako. Fanya Unalotaka kufanya, na timiza kile Ulichonikabidhi Mimi mapema iwezekanavyo. Maadamu mapenzi Yako yanaweza kutimizwa mapema iwezekanavyo, Niko radhi hata Wewe ufungue njia mpya miongoni mwetu. Tarajio Langu pekee ni kwamba kazi Yako iweze kutimizwa hivi punde. Naamini kwamba hakuna sheria zinazoweza kuichelewesha kazi Yako! ”Hii ni kazi ambayo Mungu anafanya sasa. Hujaona njia ambayo Roho Mtakatifu anapitia? Ninapokutana na ndugu wazee, huwa kuna hisia ya ukandamizaji ambayo Siwezi kutambua kiini chake. Ni wakati Ninapokuwa nao tu ndio Ninaweza kuona kwamba wana uvundo mbaya wa jamii, na fikira zao za kidini, uzoefu wa kushughulikia mambo, njia zao za kuzungumza, maneno wayatumiayo, n.k., yote yanaudhi. Ni kama kwamba wamejawa na hekima na Mimi kila mara hukaa mbali nao kwa sababu Kwangu binafsi, falsafa Yangu ya maisha imepungukiwa sana. Nikiwa nao kila mara Mimi huhisi kuchoshwa na kulemewa, na wakati mwingine hilo huwa baya sana, la kukandamiza sana mpaka siwezi hata kupumua. Kwa hiyo katika nyakati hizi za hatari, Mungu hunipa Mimi njia bora ya kuepuka. Labda ni kuelewa Kwangu visivyo. Ninajali tu kuhusu kinachomfaidi Mungu; kutekeleza mapenzi ya Mungu ni muhimu zaidi. Mimi hukaa mbali sana na watu hawa, na ikiwa Mungu ananihitaji Nijihusishe nao, basi Mimi hutii. Katu sio kwamba wao ni wenye makuruhu, lakini ni kwamba “hekima,” fikira, na falsafa zao za maisha zinakera sana. Niko hapa kutimiza kile ambacho Mungu amenikabidhi Mimi, sio kujifunza kutoka kwa uzoefu wao namna ya kushughulikia mambo. Nakumbuka kwamba wakati mmoja Mungu aliniambia yafuatayo: “Hapa duniani, tafuta mapenzi ya Baba na utimize kile Alichokukabidhi. Mengine yote ni yasiyokuhusu Wewe.” Ninapofikiria juu ya hili Mimi huhisi amani kidogo. Hii ni kwa sababu Mimi huhisi kila mara kwamba mambo ya dunia ni yenye utata sana na kwamba Siwezi kuyafahamu hayo—huwa Sijui la kufanya. Kwa hiyo sijui ni mara ngapi Nimekuwa mwenye wasiwasi sana kuhusu hili na Nimechukia wanadamu—mbona watu ni wenye utata sana? Kuna tatizo gani na kuwa wa kawaida kidogo? Kujaribu kuwa mwerevu—ya nini kujisumbua? Ninapojihusisha na watu kwa kiwango kikubwa ni kwa msingi wa agizo la Mungu Kwangu, na hata kama kumekuwa na nyakati chache ambazo hali haikuwa hiyo, nani anaweza kujua labda ni nini kimejificha katika moyo Wangu?
Kuna nyakati nyingi ambapo Nimewashauri ndugu walio nami kwamba wanapaswa kuamini katika Mungu kutoka ndani ya mioyo yao wenyewe na sio kuhifadhi mambo wayapendayo wenyewe, kwamba wanapaswa kujali mapenzi Yake. Nimelia kwa uchungu mbele ya Mungu mara nyingi—kwa nini watu hawajali mapenzi ya Mungu? Je, yawezekana kwamba kazi ya Mungu ingepotea tu bila dalili bila sababu yoyote kabisa? Sijui ni kwa nini, na inaonekana kwamba kimekuwa kitendawili katika moyo Wangu. Kwa nini watu huwa hawatambui njia ya Roho Mtakatifu, lakini kila mara wao huwa wanadumisha mahusiano yasiyofaa kati ya watu wawili?Mimi huchafuka moyo Ninapowaona watu hivi. Wao hawaoni njia ya Roho Mtakatifu, lakini huzingatia tu kile ambacho watu hufanya. Moyo wa Mungu unaweza kuridhishwa kwa njia hii? Mimi huhuzunishwa mara kwa mara na hili. Inaonekana kwamba huu umekuwa mzigo Wangu kubeba. Roho Mtakatifu pia anasikitishwa kuhusu hili—je, huhisi lawama yoyote ndani ya moyo wako? Mungu na Afungue macho yetu ya kiroho. Kama yule Anayewaongoza watu kuingia katika roho, Nimeomba mbele ya Mungu mara nyingi: “Ee Baba! Naomba Nifanye mapenzi Yako kiini na kutafuta mapenzi Yako. Niwe mwaminifu kwa kile Ulichonikabidhi Mimi ili Wewe uweze kulipata kundi hili la watu. Utulete katika ulimwengu huru ili sote tuweze kukutana na Wewe na roho zetu. Amsha hisia za kiroho ndani ya mioyo yetu! ”Natarajia kwamba mapenzi ya Mungu yatatimizwa, kwa hiyo Ninamwomba bila kukoma ili Roho wa Mungu aendelee kutupa sisi nuru na kuturuhusu sote kufuata njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Hii ni kwa sababu njia Ninayotembea ni njia ya Roho Mtakatifu. Ni nani mwingine angetembea njia hiyo kwa niaba Yangu? Ni hili ndilo hufanya mzigo Wangu kuwa mzito zaidi. Nahisi kama kwamba Ninakaribia kuanguka, lakini Naamini kwamba Mungu bila shaka hatachelewesha kazi Yake. Labda wakati ambapo kile Alichonikabidhi kitatimizwa tutawachana. Kwa hiyo labda ni kwa sababu ya athari ya Roho wa Mungu ndio Nimehisi kila mara kuwa tofauti na wengine. Ni kama kwamba Mungu anataka kufanya kazi fulani, na sasa bado Sijapata ufahamu mzuri kuihusu. Hata hivyo, Naamini kwamba hakuna yeyote duniani aliye bora kuliko wandani Wangu, na Naamini kwamba wandani Wangu wataniombea mbele ya Mungu. Ikiwa hivyo, Nitashukuru kupita kiasi kuhusu hili. Natarajia kwamba ndugu Zangu watasema Nami. “Ee Mungu! Tunaomba mapenzi Yako yafichuliwe ndani yetu sisi katika enzi ya mwisho ili tubarikiwe na maisha ya roho, ili tuone matendo ya Roho wa Mungu na uso Wake wa kweli! ”Mara tuifikiapo hatua hii tutakuwa tunaishi kweli chini ya uongozi wa Roho, na ni wakati huo tu ndipo tutaweza kuuona uso wa kweli wa Mungu. Yaani, watu wataweza kufahamu maana ya kweli ya ukweli wote. Haufahamiki au kujulikana kupitia kwa fikira za wanadamu, lakini kupata nuru hufanyika kulingana na mapenzi ya Roho wa Mungu. Katika uzima wake wote, huyu ni Mungu Mwenyewe anayefanya kazi bila hata chembe kidogo ya wazo la mwanadamu ndani yake. Huu ni mpango Wake wa kazi kwa matendo Anayotaka kufichua duniani, na ni sehemu ya mwisho ya kazi Yake duniani. Uko radhi kushiriki katika kazi hii? Unataka kushiriki katika kazi hii? Una hiari ya kukamilishwa na Roho Mtakatifu na kufurahia maisha ya roho?
Kazi muhimu sana wakati huu ni kuzama ndani zaidi kutoka kwa msingi wetu wa asili. Ni lazima tuzame ndani zaidi katika hali za ukweli, maono, na maisha yetu. Kwa hali yoyote, lazima kwanza Niwakumbushe ndugu Zangu kwamba ili kuingia katika kazi hii, ni lazima uache fikira zako za awali. Yaani, ni lazima ubadilishe mwenendo wako wa maisha wa awali, ufanye mpango mpya, na kufungua ukurasa mpya. Ukiendelea kutetea kile ambacho kimekuwa cha thamani kwako katika maisha ya nyuma, Roho Mtakatifu hataweza kutembea ndani yako; Atakuwa na shida kuweza kuhimili maisha yako. Mtu asipotafuta au kuingia ndani, au kupanga, Roho Mtakatifu atamwacha kabisa. Hii inaitwa yule aliyekataliwa na enzi. Natarajia kwamba ndugu Zangu wote wataweza kuufahamu moyo Wangu, na pia Natarajia kwamba “washirika wapya” wengi zaidi wataweza kuinuka na kufanya kazi na Mungu kutimiza kazi hii pamoja. Naamini kwamba Mungu atatubariki, na pia Naamini kwamba Mungu atanipa wandani wengi zaidi ili Niweze kusafiri mpaka miisho ya dunia na tuwe hata na upendo mwingi zaidi kati yetu. Nimeridhika kabisa kwamba Mungu atapanua ufalme Wake kwa ajili ya juhudi zetu, na Natarajia kwamba kazi yetu ya bidii itafikia viwango visivyo na kifani ili Mungu apate vijana wengi zaidi. Sote tuombee hili zaidi na kumsihi Mungu bila kukoma ili maisha yetu yaendelee mbele Yake, na kwamba tuwe wandani na Mungu. Kusiwe na vizuizi vyovyote miongoni mwetu, na sote tule kiapo hiki mbele ya Mungu: “Kufanya kazi kwa umoja! Kuwa na moyo wa kuabudu mpaka mwisho! Kutotengana kamwe, kuwa pamoja kila mara!” Ndugu Zangu wekeni uamuzi huu mbele ya Mungu ili mioyo yetu isipotee na hiari yetu isiyumbeyumbe! Ili kutimiza mapenzi ya Mungu, Ningependa kusema tena: Fanya kazi kwa bidii! Ipatie kila kitu ulichonacho! Mungu atatubariki kabisa!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki