Jumanne, 21 Agosti 2018

Ninaona njia ya kumjua Mungu

Ninaona njia ya kumjua Mungu

Xiaocao Mji wa Changzhi, Mkoa wa Shanxi

Siku moja, niliona kifungu hiki kifuatacho cha neno la Mungu kwa maandishi “Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu”: “Kwenye kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. …
Tangu wakati huo akiwa na Yesu, Petro alitambua pia kwamba hulka Yake ilikuwa tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Siku zote alikuwa na mwenendo dhabiti na hakuwahi kuwa na haraka, hakupigia chuku wala kupuuza chochote, na aliyaishi maisha Yake kwa njia iliyokuwa ya kawaida na ya kuvutia. Katika mazungumzo, Yesu alikuwa mwenye madaha na uzuri, mwenye uwazi na mchangamfu ilhali pia mtulivu, na Hakuwahi kupoteza heshima Yake katika utekelezaji wa kazi Yake. Petro aliona kwamba Yesu wakati mwingine alikuwa mnyamavu, ilhali nyakati nyingine alizungumza kwa mfululizo. Wakati mwingine Alikuwa na furaha sana kiasi cha kwamba aligeuka na kuwa mwepesi na mchangamfu kama njiwa, na ilhali nyakati nyingine Alihuzunika sana kiasi cha kwamba hakuzungumza kamwe, ni kana kwamba alikuwa mama aliyeathirika na hali ya hewa. Nyakati nyingine Alijawa na hasira, kama askari jasiri anayefyatuka kuwaua adui, na wakati mwingine hata kama simba anayenguruma. Nyakati nyingine Alicheka; nyakati nyingine aliomba na kulia. Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na ukali vyote vikamfanya kuja kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache.” Baada ya kusoma kifungu hiki nilifikiri: Haishangazi kwamba Petro angeweza kufikia ujuzi wa Mungu! Yaonekana kuwa ilikuwa kwa sababu wakati aliishi pamoja na Yesu usiku na mchana, yeye binafsi alishuhudia kila neno na kila tendo la Yesu, na kutoka kwa hayo akagundua zaidi kuhusu kupendeza kwa Mungu. Sasa pia ni enzi ya wakati Mungu anakuwa mwili ili yeye mwenyewe ashuke katika ulimwengu wa mwanadamu kufanya kazi. Kama mimi pia ningekuwa na bahati ya kuweza kukutana na Mungu na kuwa na muda pamoja naye kama Petro alivyokuwa, basi si mimi pia ningemjua Mungu vizuri zaidi? Oo! Inasikitisha kwamba sasa ninaweza kusoma tu neno la Mungu lakini siwezi kuuona uso wa Kristo. Basi ningewezaje kupata ujuzi wa kweli kumhusu Mungu?

Wakati tu nilipokuwa na huzuni na kusikitishwa juu ya hili na kupoteza imani yangu katika Mungu, maneno Yake yalinipa nuru: “Kumjua Mungu kunapaswa kufanywa kupitia kwa kusoma neno la Mungu na kulielewa neno la Mungu. Watu wengine husema: 'Sijamwona Mungu mwenye mwili, hivyo nitawezaje kumjua Mungu?' Neno la Mungu kwa kweli ni maonyesho ya tabia ya Mungu. Kutoka kwa neno la Mungu unaweza kuuona upendo wa Mungu kwa wanadamu, wokovu Wake wa wanadamu, na jinsi Anavyowaokoa ... kwa sababu neno la Mungu linaonyeshwa na Mungu ikilinganishwa na Mungu kumtumia mwanadamu kuliandika. Linaonyeshwa na Mungu binafsi. Ni Mungu Mwenyewe Akielezea maneno Yake mwenyewe na sauti Yake ya ndani. … Kwa sababu hayo hutolewa kutoka ndani kabisa, Akionyesha tabia Yake, mapenzi Yake, mawazo Yake, upendo Wake kwa wanadamu, wokovu Wake wa wanadamu, na matarajio Yake ya wanadamu. … Wakati mwingine Mungu huzungumza kwa mtazamo mpole na wenye huruma, na watu wanauona upendo wa Mungu kwa wanadamu; wakati mwingine Yeye huzungumza kwa mtazamo mkali, na watu wanaona tabia ya Mungu isiyoweza kukosewa. Mwanadamu ni mchafu kwa njia ya kusikitisha na hastahili kuuona uso wa Mungu, na hastahili kuja mbele za Mungu. Watu kuja mbele za Mungu sasa ni kwa neema ya Mungu tu. Hekima ya Mungu inaweza kuonekana kutokana na jinsi Mungu anavyofanya kazi na maana ya kazi Yake. Hata kama watu hawajakutana na Mungu, bado wataweza kuona mambo haya katika neno la Mungu” (“Ufahamu wa Kupata Mwili” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu kwa ghafla yalinifanya kuona mwanga. Ndiyo! Mungu katika mwili wa siku za mwisho tayari Ametumia neno Lake kuonyesha tabia Yake kwa mtu, Akimruhusu mtu kuona nguvu Zake kuu kwa njia ya neno la Mungu, mamlaka Yake ya juu kabisa, unyenyekevu Wake na kujificha kwake, na kupendeza Kwake, na zaidi ya hayo kuelewa furaha Yake na huzuni, na kujua chote Anacho Yeye na alicho. Hii inatosha kuonyesha kwamba kusoma neno la Mungu na kupitia neno la Mungu ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Nikiliondokea neno la Mungu, halafu nini hata nikimwona Mungu katika mwili? Si Mafarisayo pia walimuona Yesu wakati huo wa nyuma? Kwa hivyo mbona walimtundika Yesu msalabani? Si ni kwa sababu hawakusikiliza maneno ya Yesu, walijigamba na kwa ukaidi wakashikilia dhana zao wenyewe na mawazo yao, na kumpinga na kumshutumu Bwana Yesu kwa msingi wa maandiko kidogo waliyoyaelewa? Kwa upande mwingine, Petro aliweza kumjua Yesu kwa sababu angeachilia mawazo na dhana zake mwenyewe, kusikiliza kwa makini maneno ya Bwana Yesu, na alikuwa mzuri kwa kutafakari kwa uangalifu kila neno na sentensi zilizotamkwa na Yesu. Kwa njia ya matamshi na kazi ya Bwana Yesu alipata kujua tabia ya Mungu na chote Anacho Yeye na alicho, hatimaye akipata maarifa ya kweli ya Mungu. Si ukweli huu dhabiti unaeleza kwa utoshelevu kwamba mtu anaweza tu kumjua Mungu kupitia kwa neno Lake? Zaidi ya hayo, kutokana na kwamba kazi kuu ya Mungu katika mwili wa siku za mwisho ni kazi ya neno, si hili linanifaidi kwa kupata kumjua Mungu?

Jinsi nilivyofikiria nyuma kwa mawazo yangu ya mantiki zaidi ndivyo nilivyohisi unyonge wangu mwenyewe zaidi, ujinga, na utoto. Kila siku nilishikilia neno la Mungu mikononi mwangu, nikala na kunywa neno la Mungu, kusoma neno la Mungu, na kuwa na uzoefu wa neno ya Mungu, lakini sikulipenda neno la Mungu kwa dhati, nikifikiri kwamba ningemjua Mungu tu kwa kuona uso wa Kristo. Kwa kweli nilikuwa ninaishi maisha ya heri bila kuyafurahia! Ee Mungu! Asante kwa kufichua na kugeuza njia yangu mbaya ya kujua na kunifanya kuona njia ya kumjua Mungu. Kuanzia sasa kuendelea, nitatamani kusoma neno Lako, kutafakari neno Lako, kutafuta kuelewa furaha na huzuni Zako kwa njia ya neno Lako, na kwa kutambua zaidi kupendeza kwako nipate kukujua Wewe hata zaidi.

kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo


0 评论:

Chapisha Maoni