Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Sita
Miongoni mwa maneno haya yote, hakuna yasiyoweza kusahaulika zaidi kama yale ya leo. Awali maneno ya Mungu yalifichua hali za mwanadamu au siri za mbinguni, lakini tamko hili halifanani na yale ya wakati uliopita. Halidhihaki wala kufanya mzaha, lakini ni kitu kisichotarajiwa kabisa: Mungu aliketi chini na Akazungumza na watu kwa utulivu. Kusudi Lake ni gani?
Unaona nini Mungu anaposema, “Leo, Nimeanza kazi mpya juu ya ulimwengu. Nimewapa watu walio duniani mwanzo mpya, na Nimewaambia wote watoke nyumbani Mwangu. Na kwa kuwa kila mara watu hupenda kujideka, Nawashauri wajijue, na wasiisumbue kazi Yangu kila mara”? Ni huu "mwanzo mpya" ambao Mungu anazungumzia ni upi? Hapo awali Mungu alishawashauri watu waondoke, lakini kusudi la Mungu wakati huo lilikuwa kupima imani yao. Kwa hiyo leo, Anaponena na sauti tofauti—Anakuwa halisi au mwongo? Awali, watu hawakujua Mungu alikuwa Akizungumza kuhusu majaribio gani. Ilikuwa tu kupitia hatua ya kazi ya watendaji-huduma ndipo macho yao yaliona, na wakapitia binafsi majaribio ya Mungu. Hivyo, tangu wakati huo na kuendelea, kwa msaada wa mifano ya mamia ya majaribio ya Petro, mara nyingi watu walifanya kosa la kuamini kwamba "Yalikuwa majaribio ya Mungu." Zaidi ya hayo, katika maneno ya Mungu ukweli ulijitokeza lakini kwa nadra. Kwa hivyo, watu wakawa wa ushirikina kuhusu majaribio ya Mungu, na kwa hiyo katika maneno yote yaliyonenwa na Mungu, hawakuliamini hili kuwa kazi ya ukweli uliotekelezwa na Mungu; badala yake, waliamini kwamba Mungu, kwa sababu hakuwa na lingine la kufanya, Alikuwa hasa Anatumia maneno kuwapima watu. Ilikuwa katikati ya majaribio kama hayo, ambayo hayakuwa na tumaini lakini yalionekana kuleta tumaini, ndipo watu walifuata, na kwa hiyo Mungu aliposema “wote ambao watabaki wataelekea kupitia msiba na ukosefu kidogo mwishowe.” watu bado walijitolea kuzingatia kufuata, na hivyo hawakuwa na nia ya kuondoka. Watu walifuata katikati ya njozi kama hizo, na hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kuwa na hakika kwamba hakukuwa na tumaini—ambayo ni sehemu ya thibitisho la ushindi wa Mungu. Mtazamo wa Mungu unaonyesha kwamba Yeye hukishawishi kila kitu kimhudumie. Njozi za watu huwahimiza kutomwacha Mungu, bila kujali wakati au mahali, na kwa hiyo wakati wa hatua hii Mungu hutumia motisha za watu zenye dosari kuwafanya wawe na ushuhuda Kwake, ambao ni umuhimu mkuu wa wakati ambao Mungu asema, “Nimepata sehemu ya watu.” Shetani hutumia motisha za mwanadamu kusababisha ghasia, ilhali Mungu hutumia motisha za mwandamu kumfanya ahudumu—ambayo ni maana halisi ya maneno ya Mungu kwamba "Wanafikiri kwamba wanaweza kuingia ndani kwa hila, lakini wanaponipa pasi zao za kuingia zisizo halisi, Nazitupa ndani ya shimo la moto papo hapo—na, wanapoona 'juhudi zao za kujitahidi' zikiteketea moto, wanakata tamaa." Mungu huvishawishi vitu vyote kuvifanya vihudumu, na kwa hiyo Haepuki maoni mbalimbali ya mwanadamu, bali huwaambia watu kwa ujasiri waondoke; hii ndiyo ajabu na hekima ya kazi ya Mungu, ikichanganya maneno ya kweli na mbinu kuwa kitu kimoja, ikiwaacha watu wakiwa wenye kuchanganyikiwa na waliokanganywa. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba Mungu kweli anawataka watu watoke nyumbani Kwake, kwamba haya si aina fulani ya majaribio, na Mungu anachukua nafasi hii kusema, "Hata hivyo Mimi pia huwaambia watu kwamba wanapokosa kupata baraka, mtu yeyote asilalamike kunihusu." Hakuna anayeweza kuelewa kama maneno ya Mungu ni halisi au ya uwongo, lakini Mungu hutumia nafasi hii kuwaimarisha watu, kuwanyanganya hamu yao ya kuondoka. Hivyo, kama siku moja watalaaniwa, watakuwa wameonywa mapema kwa maneno ya Mungu, kama wasemavyo watu kwamba "Maneno yasiyovutia ndiyo mazuri." Leo, upendo wa watu kwa Mungu ni wenye ari na wa kweli, na kwa hiyo katika maneno ambayo hawangeweza kufahamu kama yalikuwa halisi au ya uwongo, walishindwa na wakaja kumpenda Mungu, ndiyo maana Mungu alisema "Tayari nimefanikisha kazi Yangu kuu." Mungu anaposema "Natumaini watapata njia yao wenyewe ya kuendelea kuishi, nami Sina mamlaka katika hili," huu ni uhalisi wa tamko la Mungu kuhusu maneno haya yote—hata hivyo watu hawafikiri hivyo; badala yake, kila mara wamefuata bila kutilia maanani maneno ya Mungu hata kidogo. Kwa hivyo, Mungu anaposema "katika siku za baadaye, hakutakuwa tena na maneno yoyote kati yetu, hatutakuwa tena na jambo la kuzungumzia, hatutaingiliana, kila mmoja wetu atashika njia yake," maneno haya ni ukweli, na hayajatiwa doa hata kidogo. Chochote ambacho watu hufikiria, hivyo ndivyo kutokuwa na urazini kwa Mungu kulivyo. Tayari Mungu amekuwa na ushuhuda mbele ya Shetani, na Mungu alisema kwamba Atawafanya watu wote wasimwache haijalishi wakati au mahali—kwa hivyo hatua hii ya kazi imeshakamilishwa, na Mungu hayasikilizi malalamiko ya mwanadamu. Hata hivyo Mungu amelifafanua hili tangu mwanzo, kwa hivyo watu wanaachwa wakiwa wadhaifu, wanalazimika kuomba radhi. Vita kati ya Mungu na Shetani vinategemea mwanadamu kikamilifu. Watu hawawezi kujidhibiti, wao ni makaragosi kweli, huku Mungu na Shetani ndio wanaovuta kamba bila kuonekana. Mungu anapowatumia watu kuwa na ushuhuda Kwake, Yeye hufanya kila Awezalo kufikiri, Hufanya chochote kiwezekanacho, kuwatumia watu kumfanyia huduma, Akiwasababisha watu kutawaliwa na Shetani, na, zaidi ya hayo, kuongozwa na Mungu. Na wakati ambapo ushuhuda ambao Mungu anataka utolewe umemalizika, Yeye huwatupa watu upande mmoja na kuwaacha wakiteseka, huku Mungu anajifanya kwamba Hana shughuli nao. Wakati ambapo Anataka tena kuwatumia watu, Yeye huwaokota kwa mara nyingine na kuwatumia—na watu hawana ufahamu wa hili hata kidogo. Wao ni kama tu ng'ombe au farasi anayetumiwa jinsi atakavyo bwana wake, hakuna kati yao aliye na mamlaka juu yake mwenyewe. Hili linaweza kuonekana kuwa la kusikitisha kidogo, lakini haijalishi kama watu wana mamlaka juu yao wenyewe au la, kumfanyia Mungu huduma ni heshima, si kitu cha kumfadhaisha mtu. Ni kana kwamba Mungu anapaswa kutenda hivi. Je, kuweza kuridhisa hitaji la Mwenye Uweza si jambo la kujivunia? Kwa hiyo unaonaje? Je, umewahi kufanya azimio lako kutoa huduma kwa Mungu? Yawezekana kwamba bado unataka kushikilia haki yako ya kutafuta uhuru wako mwenyewe?
Hata hivyo, yote afanyayo Mungu ni mazuri, na yanastahili kuigwa, na mwanadamu na Mungu ni, hata hivyo, tofauti. Kwa msingi huu, unapaswa kumpenda Mungu kwa moyo wa utu bila kujali kama Mungu anastahi upendo wako au la. Maneno ya Mungu yanaonyesha kwamba pia kuna huzuni nyingi ndani ya moyo wa Mungu. Ni kwa ajili ya maneno ya Mungu tu ndio watu wanasafishwa. Lakini kazi hii, hata hivyo, ilifanyika jana—na kwa hiyo ni nini hasa ambacho Mungu atafanya kufuatia? Mpaka sasa, hii inabaki kuwa siri, na hivyo watu hawana uwezo wa kuielewea au kuifahamu, na wanaweza tu kufuata mkondo wa Mungu. Hata hivyo, yote ambayo Mungu asema ni kweli, yote hutimia—hili halina shaka!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
0 评论:
Chapisha Maoni