Jumapili, 11 Februari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Injili

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?

Je, unaweza kuonyesha tabia ya Mungu ya nyakati kwa lugha inayofaa iliyo na umuhimu wa nyakati? Kupitia uzoefu wako wa kazi ya Mungu, unaweza kueleza kwa undani tabia ya Mungu? Utaielezaje vizuri, kikamilifu? Ili kupitia haya, watu wengine wapate kufahamu uzoefu wako. Utawezaje kupitisha uliyoyaona na kupitia kwa maskini hawa wa kuhurumiwa, na waumini wa kidini wa kumcha Mungu waliojitolea na waliojawa na njaa na kiu cha haki na wanaongoja uwe mchungaji wao?  Ni watu wa aina gani ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Unaweza kuwaza kweli? Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? Utahudumu vipi kama kiongozi mzuri wa wakati unaofuata? Je, unao hisia nzuri wa uongozi? Utaeleza mkuu wa kila kitu kama nini? Je, ni mkuu wa kila kitu kilicho hai na viumbe vyote duniani? Una mipango ipi ya kuendelea kwa hatua inayofuata ya kazi? Ni watu wangapi ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Je, jukumu lako ni nzito? Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, “Njia iko wapi?” Jinsi gani wanatamani mwangaza, kama nyota iangukayo kutoka angani, ianguke ghafla na kutawanya nguvu za giza zilizowakandamiza wanadamu kwa miaka mingi. Ni nani anayeweza kujua jinsi wanavyotumaini kwa hamu, na wanavyotamani hili usiku na mchana? Wanadamu hawa wanaoteseka mno wamebaki wafungwa katika jela za giza, bila tumaini la kuwachiliwa huru, hata ile siku ambayo mwanga utaonekana; ni lini hawatalia kwa uchungu tena? Roho hawa dhaifu ambao kamwe hawajapewa pumziko kwa hakika wanateseka na bahati hii mbaya. Kwa muda mrefu wamefungiwa nje na kamba zisizo na huruma na historia iliyokwama katika wakati. Ni nani amewahi kusikia sauti ya vilio vyao? Ni nani amewahi kuona nyuso zao zenye taabu? Umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyosononeka na ulivyo na wasiwasi? Anawezaje kustahimili kuona mwanadamu asiye na hatia, Aliyemuumba kwa mikono Yake Mwenyewe akiteswa na makali? Mwishowe, wanadamu ndio wasio na bahati na waliopewa sumu. Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia , ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe? Unaitafsiri vipi hali ya kutumiwa na Mungu kuishi maisha yako yasiyo ya kawaida? Je, unao kweli uamuzi na matumaini ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana ya mtu mcha Mungu anayemtumikia Mungu?
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

0 评论:

Chapisha Maoni