Jumamosi, 7 Aprili 2018

Umeme wa Mashariki | Kubagua dhidi ya Watu wa Nje ni Uovu Sana!

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

Umeme wa Mashariki | Kubagua dhidi ya Watu wa Nje ni Uovu Sana!

Xiaojin Kaunti ya Pan’an , Mkoa wa Zhejiang
Katika mwezi wa Februari mwaka wa 2007, kanisa lilipokea mpango wa kazi uitwao "Nyunyizia na Uwape Waumini Wapya ili Kuwasaidia Kukita Mizizi Haraka Iwezekanavyo." Ulisisitiza kuwa "Ni muhimu kuwatumia wale wote wanaofaa na walio na tajriba katika kuwanyunyizia waumini wapya ili kukamilisha kazi hii. Watu wasiofaa kuwanyunyizia waumini wapya hawapaswi kutumiwa; nafasi zao zinapaswa kuchukuliwa na wengine ili kuzuia kuchelewesha kazi" ("Masuala ambayo Kanisa Linakumbana nayo Sasa Ni Lazima Yatatuliwe" katika Kumbukumbu za Ushirika na Mipango ya Kazi ya Kanisa I). Baada ya kuona mpango huu, badala ya kutumia kanuni kupima iwapo dada kutoka kwa wilaya yetu aliyekuwa akinyunyizia waumini wapya alikuwa anafaa, nilikuwa tayari na mawazo dhidi yake: Mtu huyu alitekeleza wajibu wake kwa uzembe na hakulenga kula na kunywa maneno ya Mungu. Mbali na hilo, alitunza mwili wake, hivyo hakuwa anafaa kuwanyunyizia waumini wapya. La muhimu zaidi, alidhani kuwa alikuwa bora na akawa na kiburi na kuwapuuza wengine. Mara ya mwisho, alienda kwa mtu aliyesimamia kazi ya kunyunyizia ya eneo na kuongea mabaya kunihusu. Isingekuwa kwa sababu ya matakwa ya kazi yangu, kamwe singemsikiliza tena. Katika kuwaza kuhusu jambo hili, nikafanya mpango: Mbona nisijifaidi kutokana na fursa hii na nimpe mtu mwingine nafasi yake ili kamwe nisiweze kumuona tena? Je, yeye si mwenye kiburi? Nitampa mtu mwingine nafasi yake kisha nitaona jinsi alivyo mwenye kiburi!
Kama matokeo, sikupima kufaa kwa kazi yake na sikuwa ninafikiri katika kufaidika kwa kanisa. Nilikuwa tu katika haraka ya kumpa mtu mwingine nafasi yake. Baadaye, nilihamisha kiongozi wa kanisa kwenda kwa wilaya ili kutekeleza wajibu wa unyunyizaji bila kujali. Katika mtazamo wangu, mtu huyu angestahimili matatizo, alizungumza maneno yenye huruma na alikuwa anafanya kazi kwa haraka. Alikuwa wa huruma kwa watu na alikuwa anafaa sana katika kazi ya kunyunyizia. Sikufahamu kuwa mtu aliyekuwa akisimamia kazi ya kunyunyizia ya eneo na mratibu alifikiri kuwa mtu huyu hakuwa anafaa na kuwa dada yule wa kwanza alikuwa anafaa zaidi. Nilifanya nilivyoweza kuongea mazuri kuhusu kiongozi huyu wa kanisa, hata kwa kiwango cha kusema kuwa hakukuwa na mtu mwingine bora kumliko. Wakati tu ambapo sikuwa tayari kukubali mapendekezo yao, nilipokea habari zikisema kuwa kiongozi huyu wa kanisa alikuwa akichunguzwa na joka kuu jekundu. Bila chaguo lingine lolote, nilijiweka kando na huku nikiwa na kisasi nikamrejesha yule dada wa kwanza. Moyo wangu ulikuwa na wasiwasi sana na huzuni, na nilihisi kuwa sikuwa na mahali popote pa kuzungumza kuhusu mashaka yangu.
Hii iliendelea hadi siku moja niliposoma katika kifungu katika mahubiri ya mtu: “Jinsi viongozi huwatendea dada na ndugu wale ambao huona hawasikizani, wale ambao huwapinga, wale ambao huwa na mitazamo iliyo tofauti kabisa nao—hili ni suala kuu sana na linapaswa kushughulikuwa kwa makini. Iwapo hawataingia katika ukweli, hakika watambagua na kumpiga mtu huyu wanapokumbana na suala la aina hii. Aina hii ya kitendo kwa ufupi inafichua asili ya joka kuu jekundu na kumsaliti Mungu. Iwapo kiongozi ni mtu ambaye hutafuta ukweli, ambaye huwa na dhamiri, na akili, atatafuta ukweli na aushughulikie ipasavyo" ("Viongozi Wasiojali Ambao Hawafanyi Kazi yao Njema Ni Lazima Wafutwe" Katika Kumbukumbu za Ushirika na Mipango ya Kazi ya Kanisa I). Wakati huu, singejizuia kufikiria kuhusu uhamishaji wa hivi karibuni wa mfanyakazi wa kunyunyizia wa wilaya. Wakati huo, Mungu alinizuia kufanya kitendo kibaya ili kuilinda kazi Yake mwenyewe, jambo ambalo lilizuia mpango wangu kufaulu. Hata hivyo, asili ya kishetani na sumu ya joka kuu jekundu iliyokuwa ndani yangu ilipata mwangaza kikamilifu. Mpango wa kazi ulisisitiza kwa wazi kufanya chochote kiwezekanacho ili kuwanyunyizia waumini wapya na kuhamisha wafanyakazi wanaofaa wa kunyunyiza. Lakini licha ya dharura ya Mungu ya kuwaokoa watu, na bila kufikiri kuhusu kufanya kazi vyema, iligharimu uhuru wa kutobagua na kumshambulia aliyenikosea. Katika kufanya hivyo, mimi sikuwa ninatumia njia sawa za kudharau kama joka kuu jekundu ili kuwaondoa watu wa nje? Hii ilikuwaje kumtumikia Mungu? Ilikuwa tu kuwadhulumu watu na kuwaadhibu. Ilikuwa kupinga na kuvuruga kazi ya kanisa. Kwa hakika nimeharibiwa na Shetani na nimekuwa mfano wa joka kuu jekundu kikamilifu. Vitendo vyangu havikuwa tofauti na vile vya joka kuu jekundu. Joka kuu jekundu hutumia njia za kusikitisha ili kuwaondoa watu wa nje. Pia nilikuwa ninaitoa nafasi ya aliyenikosea kwa mtu mwingine kwa kusingizia kuweka mipango ya kazi katika utendaji. Joka kuu jekundu huwapandisha vyeo linaowapenda na nilikuwa ninampandisha mtu cheo ambaye mimi binafsi nilidhani alikuwa mwema na ambaye alipatana na maoni yangu. Joka kuu jekundu hufuata kanuni ya kishetani ya “Nitii au uangamie.” Pia nilitumia "mamlaka" yangu kulipiza kisasi kwa mtu aliyenikosea na ambaye alikuwa na wazo kunihusu. Joka kuu jekundu hugeuza ukweli; halina haki na linapendelea. Nilikuwa na hisia nilipomshutumu mtu ambaye hakukubaliana na matakwa yangu bila kufikiria. Niliendelea kunena mazuri kuhusu mtu niliyempenda hata kwa kiwango cha kutia chumvi, kunena kinyume na ukweli. … Sasa ninaona kuwa sumu ya joka kuu jekundu imekita mizizi ndani yangu. Tayari imekuwa sehemu ya maisha yangu, kwa kiwango kuwa inaathiri kila kipengele cha tabia yangu. Sumu ya joka kuu jekundu hunifanya mwenye dhambi na mwenye nia mbaya; hufanya moyo wangu kuwa mchafu, wa kulaaniwa, na mbaya, hii hunifanya kumpinga mtu kiujinga. Isingekuwa kwa sababu ya nuru ya Mungu, ningekuwa ningali ninaishi katika uovu wangu mwenyewe na bado ningekuwa ninatafakari kuhusu mipango yangu iliyofeli. Hakika singejua kwamba nilikuwa nimepoteza fikira na dhamiri zangu kabisa na kuwa tabia yangu ilikuwa inakosea tabia ya Mungu.
Mwenyezi Mungu, mahusiano yako yamenifanya kuona kuwa asili yangu ni mbovu sana na ya kusikitisha. Mimi ni mfano kamili wa joka kuu jekundu; tabia yangu haina utofauti wowote na joka kuu jekundu. Kutoka sasa, niko tayari kufuata ukweli kwa utendaji. Nitajichunguza kwa kulinganisha mawazo, maneno na matendo yangu na neno la Mungu, na kutambua asili ya joka kuu jekundu ndani yangu. Nitaona kiini chake kwa wazi na hakika nitalichukia, kuligeuka, na kuwa mwanamume halisi aliye na ubinadamu wa kuufariji moyo Wako.

Ushuhuda-wa-Kuipitia-Hukumu-ya-Kristo

Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

0 评论:

Chapisha Maoni