Jumatano, 19 Septemba 2018

Mapambano ya Kufa na Kupona

Mapambano ya Kufa na Kupona


Chang Moyang Mjini Zhengzhou, Mkoani Henan

"Unapoutelekeza mwili, bila shaka kutakuwa na mapambano ndani. Shetani anataka ufuate dhana za mwili, kulinda maslahi ya mwili. Hata hivyo, neno la Mungu bado linakupa nuru na kukuangaza ndani, linakupa msukumo kwa ndani na kufanya kazi kutoka ndani.
Katika hatua hii, ni juu yako kama unamfuata Mungu, au Shetani. Kila wakati ambapo ukweli unatendwa na kila wakati ambapo watu wanapofanya mazoezi ya kumpenda Mungu, kuna pambano kubwa. Unapotenda ukweli, ndani kabisa kuna pambano la kufa na kupona. Ushindi utaamuliwa tu baada ya mapigano makali. Ni machozi mangapi ya huzuni yamemwagwa" (“Kila Unapoutelekeza Mwili Kuna Pambano la Kufa na Kupona” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kila mara nilipokuwa nikisikia maneno ya Mungu katika wimbo huu, ningetafakari kuhusu yafuatayo: Je, kutenda ukweli ni kugumu kiasi hicho? Wakati watu hawauelewi ukweli, hawawezi kuutenda. Mara wanapouelewa, kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu hakutatosha? Je kungeweza kuwa kwenye uzito kweli kama “ndani kabisa kuna pambano la kufa na kupona”? Haikuwa hadi baadaye, kupitia uzoefu wangu halisi, kuwa niliona kwamba kutenda ukweli si rahisi kwa kweli. Aliyosema Mungu yanalingana kabisa na ukweli; hayajatiwa chumvi hata kidogo.

Muda fulani uliopita, nilihisi kuwa dada aliyefanya kazi nami alikuwa mwenye kiburi na kunidharau; sikuweza kujizuia ila kuzama katika hali isiyo sahihi. Nilianza kujiweka katika vikwazo kwa sababu yake. Sikuweza kulisahau jambo hili katika kazi yangu; nilikuwa mnyenyekevu katika maneno yangu na mwangalifu katika vitendo vyangu kiasi kwamba, baada ya muda mfupi, ningetazama sura yake wakati nilipozungumza au kufanya kitu, na sikuwa nikiubeba mzigo wa kazi yangu. Nilikuwa nikiishi gizani kabisa. Sikuweza kujinasua hata ingawa nilijua kuwa hali yangu ilikuwa hatari. Katikati ya mateso, kulikuwa na mwongozo wa Mungu: kuwa na mazungumzo ya dhati na dada yako, tafuta njia ya nuru. Lakini nilipofika kwa mlango wa dada yangu, nilikuwa na wazo tofauti: Dada yangu atafikiri nini nitakapozungumza kuihusu? Je, atasema kuwa kuna mambo mengi madogo mno akilini mwangu, mimi ni mzigo sana, mgumu sana kushughulika naye? Mara tu baada ya kuwa na wazo hili, ilikuwa ni kama kwamba nilikuwa nimeona ule mtazamo usio sawa katika macho yake, ule mtazamo wa kudharau. Ghafla, ujasiri wangu ulipotea tu na nikafifia, kana kwamba mwili wangu wote ulikuwa umekakamaa. kwa mara nyingine tena, maneno ya Mungu yaniletea nuru ya ndani: Ungekuwa na masuala mengi ya faragha uliyoyaona kuwa vigumu kuyazungumzia, ingekuwa vigumu kupambana kutoka katika giza. Ungekuwa radhi kuendelea hivyo? Nilijitia moyo kwa kimya: Kuwa mjasiri, kuwa mnyofu na wazi. Kutenda ukweli si kitu cha kuaibikia! Lakini wakati uo huo, hisia ya namna nyingine ilinivuta kwa ghafla: Usiseme kitu chochote—watu wengine labda wanafikiri kuwa uko sawa. Ikiwa utayazungumzia watafikiri kuwa una mambo mengi madogo mno akilini mwako na hawatakupenda tena. Wai! Ni afadhali kutosema chochote, basi! Nilipositasita kwa mara nyingine tena, Mungu aliniongoza tena: Kuwa mtu mwaminifu inamaanisha huwezi kuwa mwenye haya na hofu! Kupata nuru ya Mungu kulinisisimua, lakini kwa mshangao wangu, mara tu nilipopata nguvu kidogo, mawazo ya Shetani kwa mara nyingine tena yakafoka: Ukiyazungumzia watu wengine watajua hali yako halisi, na utakuwa mwenye taabu! Moyo wangu ghafla ukajikaza sana. Ilikuwa ni kwa njia hii ndio moyo wangu ulikuwa umevutwa huku na huko katika mapambano kati ya uzuri na hasi, nyeusi na nyeupe. Nilijua kwa uwazi: Mimi kutotaka kuzungumza ilikuwa ni haja ya kujiepusha na aibu na ubatili. Lakini kwa njia hii, hali yangu haingetatuliwa na haingekuwa na manufaa kwa kazi yangu. Kutafuta ushirika tu kutatua suala hili tu ndiyo ingekuwa na manufaa kwa kazi yangu na kuwa sambamba na mapenzi ya Mungu. Lakini wakati fikira hiyo ilinijia kuwa mara tu angejua, angeweza kuniheshimu kidogo zaidi kuliko awali, nilipoteza ujasiri wa kutenda ukweli. Nilihisi kama kwamba ningezungumza kuhusu ubaya wangu mwenyewe, singeweza kuendelea kuishi! Kwa muda mfupi nilifadhaishwa sana, na moyo wangu ulikuwa katika maumivu makubwa kama kwamba unachomwa na moto. Hii ilikuwa ngumu kama kwamba nilikuwa nimekabiliwa na uchaguzi wa uzima au kifo, na bila kujua nikalia, na yote ambayo ningefanya ni kumlilia Mungu moyoni mwangu bila kujiweza. Katika wakati huo wa kipeo, maneno ya Mungu kwa mara nyingine yalimemeteka katika akili yangu: “(Vijana) hawapaswi kuwa bila ukweli, wala kuficha unafiki na udhalimu.… Vijana wanapaswa kuwa na ujasiri wa kutoshindwa na ukandamizaji wa nguvu za giza na kubadili umuhimu wa uwepo wao” (“Maneno kwa Vijana na Wazee” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yaliniwezesha hatimaye kutuliza moyo wangu wenye wahaka: Haijalishi nini, siwezi tena kuwa chini ya dhihaka ya Shetani! Siwezi tena kumuasi Mungu; ni lazima nijinyime na kutenda ukweli. Mara nilipofanya uamuzi huo kutafuta dada yangu na kuwa na ushirika wa dhati naye, suala halikutatuliwa tu, lakini moyo wangu ulichangamka. Nilipokumbuka mapambano makali katika moyo wangu wakati huo na kuonja mateso katika mapambano yaliyofanana na ya kufa na kupona, ni hapo tu ndipo nilijua jinsi masikitiko yangu ya kujiepushia aibu yalikuwa bure. Ilikuwa ni sehemu ya maisha yangu kiasi kwamba nilikuwa naishi gizani, nikikabiliana na mwito baada ya mwito kutoka kwa Mungu lakini sikuweza kujinasua. Niliuelewa ukweli lakini sikuweza kuutenda; kwa kweli nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani! Pia nilipata uzoefu kabisa kuwa kutenda ukweli na kuwa mtu mwaminifu si rahisi.

Ilikuwa tu baada ya kupitia haya ndiyo nilielewa maneno ya Mungu: “Kila wakati ambapo ukweli unatendwa na kila wakati ambapo watu wanapofanya mazoezi ya kumpenda Mungu … ndani kabisa kuna pambano la kufa na kupona.” Maneno haya yalisemwa kuhusu hali potovu ya binadamu kwa sababu asili ya kishetani ya watu imekita mizizi kabisa katika mwili. Mwanadamu amefungwa na amezuiliwa nayo, na imekuwa maisha yetu. Tunapotenda ukweli, tunapoacha maisha yetu ya kimwili, mchakato huu ni sawa na kuzaliwa tena, kama kufa na kufufuliwa. Kwa kweli ni mashindano na mapambano ya kufa na kupona, na ni mchakato wa uchungu sana. Wakati kwa kweli hatujui asili yetu wenyewe na hatuna ridhaa ya kuteseka au kulipa gharama, bila shaka hatuwezi kutenda ukweli. Katika siku za nyuma nilidhani kuwa kutenda ukweli kulikuwa rahisi—hii ilikuwa ni kwa sababu sikuwa na ufahamu wa asili yangu potovu na sikujua jinsi upotovu wangu ulivyokuwa wa kina. Katika siku zijazo, niko radhi kujifahamu mwenyewe kwa kina zaidi kupitia uzoefu, kutafuta kutenda ukweli katika vitu vyote, na kujinyima!

0 评论:

Chapisha Maoni