Jumanne, 4 Septemba 2018

Kwaheri kwa Zile Siku za Kushindana na Majaliwa

Kwaheri kwa Zile Siku za Kushindana na Majaliwa

Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, Kupata-Furaha, ukweli,

Yixin

Kijiji cha kishamba kilichojikokota kimaendeleo, wazazi wangu waliochoka kwa sababu ya kazi zao, maisha ya shida za kifedha … kumbukumbu hizi za huzuni zilitia alama kwa mawazo yangu machanga, zilikuwa ni hisia yangu ya kwanza ya “majaliwa.” Baada ya kuanza kwenda shule, mara ya kwanza nilipomsikia mwalimu wangu akisema kwamba “Unadhibiti majaliwa yako katika mikono yako mwenyewe,” niliweka maneno haya imara mawazoni mwangu. Niliamini kuwa ingawa sikuweza kubadili ukweli kwamba nilizaliwa katika umaskini, ningeweza bado kubadili majaliwa yangu kwa kufanya kazi kwa bidii. Kwa sababu hiyo, niliweka nguvu zangu zote katika kukabiliana na “majaliwa” yangu, na kupata kipande cha mbinguni kukiita changu mwenyewe.

Kipingamizi katika Masomo Yangu

Kama tu kizazi baada ya kizazi cha wanafunzi wasiohesabika, azimio langu la kusoma na kuingia katika chuo kikuu lilikuwa hatua ya kwanza katika kubadilisha majaliwa yangu. Ili kufanikisha lengo hili, nilisoma kwa bidii. Nikiwa darasani nilisikiliza kwa makini, na nikiwa nje ya darasa wanafunzi wengine wote walipokuwa nje wakicheza, nilikuwa bado nikisoma, mara nyingi nikijishughulisha na vitabu vyangu hadi usiku wa manane. Kutokana na kusoma kwangu kwa bidii, alama zangu daima zilikuwa kati ya zile bora mno. Wakati wowote ambapo walimu wangu au wanafunzi wenzangu wangeniangalia kwa upendezwaji lingeweza kuimarisha imani yangu kuwa “Ninahitaji kuitegemea mikono yangu miwili mwenyewe ili kujichongea mahali katika ulimwengu.” Lakini njia za dunia hazitabiriki. Nilipokuwa nikijitahidia udhanifu huu mzuri, baba yangu ghafla akawa mgonjwa. Baada ya yeye kuchunguzwa tuligundua kuwa alikuwa na ugonjwa wa kudumu wa ini, na kwamba tayari ulikwa umeendelea hadi katika hatua za kati. Baba yangu alivimba mwili wake wote kwa sababu ya ugonjwa huo, na hakushindwa kufanya kazi tu, pia alilazimika kutumia fedha nyingi kwa ada za daktari. Kwa kipindi cha wakati kazi zote za nyumba, pamoja na kazi za kilimo kwa zaidi ya ekari 3 za ardhi, zilimwangukia mama yangu, na wakati huo huo mama yangu pia aliugua ugonjwa mkali wa kijinakolojia. Siku moja baba yangu aliniambia na uso uliojaa huzuni: “Binti yangu, hivi sasa familia yetu yote inamtegemea mama yako tu kwa kuikimu. Mzigo wake ni mzito sana. Inagharimu pesa nyingi kuwapeleka watoto wanne shule kusoma kwa mwaka mmoja. Kwa kweli hatuna njia yoyote ya kuwapa nyinyi nyote masomo. Wewe ndiwe mzee zaidi, hivyo unafaa kuwafikiria ndugu zako wa kiume na wa kike. Kwa nini usiache masomo ili tuweze kutenga nafasi hii kwa ajili ya ndugu zako?” Baada ya kuyasikiliza maneno ya baba yangu, nilihisi kujawa na maumivu moyoni mwangu: Daima nilitumaini kusoma kwa bidii na kuwa mtu aliyejitokeza, lakini ikiwa ningeyaridhia matakwa ya baba yangu kwamba niyaache masomo yangu, si basi matarajio yangu yote na matumaini yangu kwa ghafla yangetoweka?! Macho yangu yalijaa matone ya machozi, na nilihisi huzuni ya ghafla moyoni mwangu. Nilijua kwamba baba yangu alikuwa ameyafikiria kwa muda mrefu kabla ya kusema maneno haya, na kwa kumtazama mama yangu mgonjwa, sikuweza kumbebesha mzigo mkubwa kama huo. Kama nimekabiliwa na hali dhaifu ya kifedha ya familia yangu, sikuwa na chaguo ila kuridhiana na hali ya wakati huo na kujizuia kabisa kulia nilipoyaridhia matakwa ya baba yangu.

Kuponea Chupuchupu Kutoka kwa Maafa

Bila ya kumaliza shule ndogo ya sekondari, nilikuwa mdogo lakini nilikuwa nimejaa lengo. Ingawa sikuweza kumaliza masomo yangu, niliweka lengo la kupata kazi ya muda mfupi ili kupata pesa. Niliamini kwamba kwa njia ya kuchapa kazi bado ningeweza kubadilisha kabisa majaliwa yangu. Kabla ya muda mrefu sana, kupitia kutambulishwa na kwa jamaa wangu mmoja, nilikwenda jijini kufanya kazi kwa kiwanda kimoja cha nguo. Ili kupata fedha zaidi nilifanya kazi kwa bidii kadri nilivyoweza. Wakati ambapo watu wengine walizilinda mashine mbili nililinda nne, na wakati wengine walikwenda mapumziko ningeendelea kufanya kazi. Bosi aliona kwamba nilikuwa mtu wa kutegemewa na mwenye uwezo, na ndani ya miezi mitano ya kufanya kazi aliongeza mshahara wangu kuwa kiasi sawa na wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi huko kwa muda mrefu. Wafanyakazi wenzangu wote waliniangalia kwa wivu.

Mwaka huo nilipokuwa nikijivunia mafanikio yangu na kutaka kuendelea kufanya kazi kwa bidii, mama alinisambazia injili ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Mama aliniambia kuwa Mungu huvitawala na kuvipanga vitu vyote, na kwamba majaliwa ya kila mtu huendeshwa mikononi mwa Mungu, lakini katika mawazo yangu ya kujivunia na ya kiburi kulikuwa tu na imani kwamba “Unadhibiti majaliwa yako katika mikono yako mwenyewe,” na hasa sikusikiliza maneno ya mama yangu. Hapo, katika kukutana kwa muda mfupi na wokovu wa Mungu, sikuipokea injili iliyoenezwa na mama yangu; badala yake niliendelea kujitahidi na kupambana ulimwenguni.

Niliendelea kwa njia hii kwa miaka kadhaa, na maisha yangu yalianza kuimarika. Sikuwa tu na akiba kidogo yangu mwenyewe, lakini pia mara nyingi niliweza kutoa kidogo kwa familia yangu. Nilihisi kwamba mradi niliendelea kufanya kazi kwa bidii basi bila shaka ningekuwa na matarajio machangamfu na yasiyo na mipaka. Nilipokuwa nimepotea katika wimbi la kutafuta mali na anasa za mwili, ajali ya gari isiyotarajiwa iliponda mpango wangu wote wa maisha. Nililala kama nimepoteza fahamu katika kitanda cha hospitali kwa siku tatu usiku na mchana, na baada ya kuamka sikuweza kusema chochote. Nilikuwa tu kama bubu. Ilikuwa tu baada ya daktari kuniruhusu nitoke kitandani kutembeatembea ambapo nilitambua kwamba kutokana na hatari ya jeraha langu sikuweza kusogeza upande mzima wa kushoto wa mwili wangu. Hakukuwa na njia ambayo ningeweza kukubali uhalisi huu; nilikuwa na umri wa miaka ishirini tu! Ikiwa kutoka wakati huu kwendelea ingekuwa nipoozwe daima katika kitanda jinsi hii, si basi maisha yangu ya fahari ya ujana yangeangamizwa? Maisha yangu mazuri hata hayakuwa yameanza, na kwa kweli yangekuwa yanafika mwisho? Nilihuzunika na kuvunjika moyo; nilitaka kulia lakini hakukuwa na machozi, na sikujua jinsi ya kukabiliana na wakati ujao. … Wakati huu, mama yangu alikuja upande wangu kunifariji. Aliniambia, “Binti yangu, ni kwa sababu Mungu hukukinga ndio uliweza kuamka! Je, hujui? Daktari alisema kuwa hata kama ungeweza kuamka ungekuwa huwezi kutumia akili. Mara tu baba yako na mimi tuliposikia haya nyoyo zetu zikawa baridi. Kwa siku kadhaa zilizopita nimekuwa nikimwomba Mungu daima, nikikukabidhi mikononi mwa Mungu, nikiwa tayari kujisalimisha kwa ukuu wa Mungu. Asante kwa Mungu! Jiangalie, sasa umeamka. Huyu ni Mungu akikuhurumia. Ni mapenzi ya Mungu ya neema kwamba ajali hii ya gari ilikukumba! Ingawa tumepitia maumivu fulani katika mwili, si ni kwa njia ya kukabiliwa na hali ya aina hii ambapo tunaweza kuigeuka dunia na kumgeukia Mungu? Binti yangu, unapaswa kuanza kumwamini Mungu pamoja nami mara moja!” Nilipomwona mama akijizuia kulia huku akinienezea injili, moyo wangu hatimaye ulihisi msisimko. Mama alisema kuwa wakati nilipokuwa bila fahamu alikuwa akimwomba Mungu daima. Bila kujali kama iliwezekana niamke au la, kwa vyovyote alikuwa tayari kutii mipango ya Mungu na utaratibu. Kwa kweli hakutarajia kwamba ningeamka. Nilipokuwa nikisikiliza yote haya, nilihisi kwamba Mungu kwa kweli alikuwa mkubwa! Ingawa nilikuwa nimekataa wokovu Wake, hakuwa ameachana nami. Wakati maafa yaliponifika, ulinzi Wake ulikuwa nami daima. Alinionea huruma na kunilinda, na Aliniokoa kutoka kwa mauti. Sikuweza kujizuia kuhisi shukrani kwa Mungu. Kwa sababu ya utunzaji na ulinzi wa Mungu mwili wangu ulipona kwa kasi sana, na niliachiliwa kutoka hospitali mwezi mmoja kabla ya wakati uliopangwa.

Kushikilia KushughulikiaMambo kwa Njia Mbaya

Ingawa nilikuwa nimefurahia upendo wa Mungu na huruma Yake, bado sikuelewa umuhimu wa kweli wa kumwamini Mungu, kwa hiyo sikuchukulia kuwa na imani katika Mungu kama jambo kubwa. Haikuwa hadi baada ya mwili wangu kupona kiasi ambapo mama alipendekeza kwamba nitafute kazi karibu na nyumbani ili niweze kupata riziki, na kwamba alitumaini kwamba ningetumia muda wangu  wa ziada zaidi kwa kuitenda imani yangu katika Mungu. Lakini sikuwa tayari kuishi maisha ya aina hii. Nilisubiri mpaka jeraha langu la mguu lilipopona kabisa na kisha kuondoka nyumbani bila kusita ili kufanya kazi ya muda. Wakati wa kazi hii nilikuwa na uhusiano na mvulana mmoja, na baada ya kufanya urafiki kwa kipindi cha muda, aliniposa, akiniahidi kuwa angenipenda kwa maisha yetu yote. Nilifikiria jinsi masomo yangu yalikuwa yamezuiwa kwa miaka, jinsi nusu ya njia pia nilipatwa na ajali ya gari, na jinsi baada ya jitihada hizi bado sikuweza kubadilisha majaliwa yangu. Kwa hiyo wakati huu niliweka matumaini yangu ya kubadilisha majaliwa yangu kwa ndoa hii. Kama ningeolewa na mtu ambaye alikuwa tayari kuniahidi kunipenda kwa maisha yangu yote, basi sehemu ya mwisho ya maisha yangu ingekuwa ya furaha na yenye furaha kamili. Nilibeba maono haya ya maisha mazuri nami katika ukumbi wa ndoa. Lakini bila kutarajia, mara tu nilipoolewa, haikuwa kabisa jinsi nilivyofikiri ingekuwa. Mara nyingi mume wangu angegombana nami kwa sababu ya mambo madogo, na mama mkwe wangu pia alikuwa baridi kwangu, na hata angemchochea mume wangu kubishana nami. … Niliishi katika mateso na hakukuwa na yeyote wa kunifariji. Aidha, familia niliyoolewa kwayo iliishi mbali sana, kwa hiyo hapakuwa na mtu yeyote karibu nami ambaye ningeweza kupata ili kutoa hisia zangu kwake. Nikiwa na hisia hii ya kutokuwa na msaada, yote niliyoweza kufanya ni kurudi tena na kutafuta kazi ya muda. Kutokana na mume wangu na mimi kuishi katika maeneo mawili tofauti, haikuchukua muda mrefu kwetu kuhisi kama wasiojuana. Baada ya miaka mitano ya ndoa, mume wangu alileta suala la talaka, akiniambia kuwa alikuwa amekutana na mwanamke mwingine aliyempenda zaidi. Nilipomsikia akisema hayo, mawazo yangu yalihisi kuwa matupu kabisa, na nikajiuliza, “Nitafanya nini? Kila mtu husema kuwa talaka kwa mwanamke ni sawa na kuwa nusu hai, kwa hiyo ninafaaje kuishi sehemu ya mwisho ya maisha yangu?” Nilipokuwa nikitia sahihi cheti changu cha talaka, nilikuwa peke yangu nikibeba mizigo katika treni kurudi nyumbani, na nilianza kulia bila kuzuilika. Nilikuwa na hisia kubwa ya uchungu ambao watu hupitia wanapoishi ulimwenguni humu, na nilikuwa na hata hisia kubwa zaidi ya upweke usio na kifani ulionikabili. Ulikuwa ulimwengu mkubwa mno lakini hapakuwa na mahali ambapo ningeweza kukaa. Nilihisi kuhuzunika sana. Kwa kweli nilitaka kujiua ili kuyamaliza yote. Lakini nilifikiri juu ya wazazi wangu ambao walikuwa wanazeeka kila uchao, na nilihisi hisia ya kusita: Kama ningekufa, huzuni ya wazazi wangu ingewafanyia nini! Lilikuwa haliwezekani. Singeweza kufa kwa njia hiyo. Lazima nifute machozi yangu kabisa, kuamua kutojiua na kuendelea kuishi.

Kurudi kwa Mwana Mpotevu

Niliporudi nyumbani, mama tena alishiriki neno la Mungu kwangu. Nilitumia kitabu kilichokuwa mikononi mwa mama na kusoma maneno ya Mungu: “Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo” (“Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Wewe na yule mwovu mmepita katika maelefu ya miaka ya dhoruba na tufani. Wewe pamoja naye, mnampinga Mungu, ambaye alikuwa chanzo cha maisha yenu. Hutubu, wala kujua kwamba umefikia hatua ya maangamizi. Unasahau kwamba yule mwovu amekujaribu, amekutesa; unasahau asili yako. Vivyo hivyo, yule mwovu amekuwa akikuharibu hatua baada ya hatua, hata mpaka sasa. Moyo wako na roho yako vimekufa ganzi na vimeoza. Hulalamiki tena juu ya dhiki ya dunia, huamini tena kwamba dunia si ya haki. Wala hujali tena juu ya uwepo wa Mwenye Uweza. Hii ni kwa sababu umemchukulia mwovu kuwa baba yako wa kweli, na huwezi kutengana naye. Hii ndiyo siri iliyomo moyoni mwako” (“Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Baada ya kuyasoma maneno ya Mungu, nilielewa. Mungu ni Muumba na Mtawala wa mbingu na ardhi na vitu vyote, na aidha Yeye ndiye chanzo cha uzima kwa wanadamu. Majaliwa ya kila mtu hutawaliwa na kudhibitiwa na mikono ya Mungu. Lakini kwa kweli sikumwamini Mungu na sikuwa na maarifa ya kweli ya ukuu wa Mungu. Bado nilitegemea mbegu ya Shetani iliyopanda kwa kina ndani yangu ili kuishi, ikiniambia kuwa “Unadhibiti majaliwa yako katika mikono yako mwenyewe.” Bado nilijaribu bila kufaulu kujitegemea na kuutembea ulimwengu nikitafuta kipande cha mbinguni, nikitupa ukuu wa Mungu na mipango. Nilifikiria nyuma kwa muongo uliopita, jinsi ili kubadili majaliwa yangu nilisoma kwa bidii na kujitahidi kupata pesa. Baadaye, baada ya kuhusika katika ajali ya gari, Mungu aliniokoa na kunisaidia kunusurika kutoka kwa maafa, na kuuruhusu mwili wangu kupona haraka. kimaajabu Lakini bado sikuwa nimekuja kuuona ukweli licha ya majaribio ya mama kunishawishi. Sikupokea injili na kuja mbele ya Mungu, badala yake nilitegemea lengo na hamu kufanya mipango yangu, kuelewa ni njia gani maisha yangu yangechukua wakati ujao. Halafu mara nyingine tena niliweka furaha katika maisha yangu mwenyewe kwa ndoa. Nilidhani nilikuwa nimempata mtu kuolewa naye ambaye angeendelea kuwa wangu na kunipenda maisha yangu yote, na kwamba bila shaka ningekuwa na furaha, lakini hatimaye ndoa iliyokosa kufanikiwa ilinisababishia mateso yasiyokwisha. … Nilishikilia maneno kwamba “Unadhibiti majaliwa yako katika mikono yako mwenyewe,” nikiamini kwamba kwa kutegemea kazi yangu ya bidii ningeweza kubadilisha majaliwa yangu, na kwamba hatimaye kungekuwa na siku ambapo bila shaka ningekuwa na mafanikio. Lakini baada ya miaka mingi sana, baada ya kutiwa kovu na kuviliwa, baada ya ushinde mkubwa, kando na maumivu na mateso hakukuwa na kitu kingine ambacho nilikuwa nimepata. Ni kwa kuangalia tu nyuma juu ya jinsi nilivyoitegemea sumu ya Shetani kuishi, jinsi hili lilikuwa katika ushindani na majaliwa yangu, nilipoona kwamba sikuyatambua mamlaka ya Mungu, kwamba kwa kuutegemea uwezo wangu mwenyewe nilikuwa nikiupuuza ukuu wa Mungu. Kwa kweli lilikuwa jambo la upumbavu na ujinga! Ingawa nilijitenga na Mungu na kukataa kusikiliza sauti ya Mungu, Mungu bado alinisamehe na kunivumilia, na alinisubiri kwa utulivu, na akaunda mazingira yangu ili kuuchangamsha moyo wangu na nafsi yangu. Kupitia mamangu kunisambazia injili mara nyingine tena nilirudishwa mbele ya Mungu. Katika wakati huu nina majuto yasiyo na kikomo, lakini nimejaa shukrani na deni katika moyo wangu kwa Mungu, na siwezi kuyazuia machozi kuchiririka usoni mwangu.

Kupata Furaha

Kurudi mbele ya Mungu na kufurahia kunyunyiziwa na neno la Mungu kuliponya roho yangu iliyojeruhiwa kidogo kidogo. Baadaye, dada mmoja jirani alipata habari kuhusu talaka yangu na alitaka kunijulisha kwa mwenzi fulani. Wakati huu nilitafuta maoni ya mama kwa bidii. Mama hakunifanyia uamuzi, badala yake alinitaka niombe ili kutafuta mapenzi ya Mungu. Nilikuja mbele ya Mungu kuomba, nikitoa suala la ndoa yangu katika mikono ya Mungu. Baada ya kuomba, nilihisi kuwa na amani sana moyoni mwangu, na lilinifanya kukumbuka kifungu kutoka kwa neno la Mungu: “Majaliwa ya mwanadamu inadhibitiwa na mikono ya Mungu. Wewe huna uwezo wa kujidhibiti mwenyewe: Licha ya mwanadamu yeye mwenyewe daima kukimbilia na kujishughulisha, anabakia bila uwezo wa kujidhibiti. Kama ungejua matarajio yako mwenyewe, kama ungeweza kudhibiti majaliwa yako mwenyewe, ingekuwa wewe bado ni kiumbe? … Hatima ya mwanadamu iko mikononi mwa Muumba, hivyo ni jinsi gani mwanadamu anaweza kujidhibiti mwenyewe?” (“Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ni kweli. Majaliwa yangu yanadhibitiwa na mikono ya Mungu. Aina yoyote ya ndoa ambayo natakiwa kuwa nayo imeamriwa na kupangwa na Mungu. Siwezi kufanya uchaguzi peke yangu, kama nilivyofanya awali, nikitegemeza matakwa yangu na viwango vyangu. Maisha yoyote ambayo nitaishi katika sehemu ya karibuni ya maisha yangu, mwanamume wa aina y0yote ninayeweza kumpata, naamini kwamba hili lote limeamuliwa na kupangwa na Mungu. Kitu ambacho ninahitaji kufanya sasa ni kutafuta mapenzi ya Mungu, kufuata uongozi wa Mungu, na kutii ukuu wa Mungu.

Siku tuliyokutana niliona kwamba hakuwa mtu mrefu sana, wala hakuwa mzuri sana kwa kuzungumza. Kulingana na viwango vyangu vya awali vya kuchagua mume, kwa kweli ningemtafuta mwenzi ambaye angeweza kuzungumza vizuri, au ambaye alikuwa mrefu na mzuri, lakini wakati huu sikufanya kukataa huko kwa haraka. Badala yake, nilikubali tupate kujuana kwa muda kwanza. Katika siku zilizofuata niligundua kwamba ingawa hakuwa wa kuvutia au mwenye njozi za mapenzi, alikuwa mwaminifu na mwenye kuwafikiria wengine, imara katika kazi zake, na la muhimu zaidi, aliiunga mkono imani yangu kwa Mungu. Nilihisi kwamba ni lazima awe ndiye mume ambaye Mungu alinipangia. Baada ya kujuana kwa muda tulifunga ndoa. Baada ya kufunga ndoa, familia ya mume wangu ilikuwa nzuri sana kwangu, na wote waliiunga mkono imani yangu kwa Mungu. Wakati ndugu wa kiume na wa kike wanapokusanyika nyumbani kwetu, wote huwasalimu wageni wetu kwa furaha. Mimi hujihisi mwenye furaha sana, na moyo wangu huhisi kuridhika sana. Katika moyo wangu nina shukrani kwa neema na baraka za Mungu. Mungu anasema: “Unapotambua kwa kweli kwamba Mungu anao ukuu juu ya hatima ya binadamu, unapoelewa kwa kweli kwamba kila kitu ambacho Mungu amekupangilia na kukuamulia ni chenye manufaa makubwa, na ni ulinzi mkubwa, basi unahisi maumivu yako yakipungua kwa utaratibu, na uzima wako wote unaanza kutulia, kuwa huru na kukombolewa” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Maneno ya Mungu yalinifanya nitambue kwamba ni Mungu peke yake anayeelewa kila kitu ambacho kila mtu huhitaji. Yeye huangalia kwa makini taabu zetu zote, na ni Yeye peke yake aliye na ukuu juu yetu na hupanga kila kitu kwa njia bora mno inavyowezekana. Siku hizi nimepata wokovu wa Mungu na kuja mbele Yake. Mimi hufurahia kunyunyiziwa na kuruzukiwa na neno la Mungu, na kwa njia ya uzoefu wangu katika kazi, familia na ndoa, nimeweza kutatua utawala wa shetani ulioishi ndani yangu na kuniambia kuwa “Unadhibiti majaliwa yako katika mikono yako mwenyewe.” Nimekuja kutambua kwamba haya ni maneno ya shetani ambayo huwadanganya na kuwapotosha wanadamu, yakiwadanganya ili wajitenge na Mungu. Wakati huo huo, nimekuja kuwa na ufahamu dhahiri kwamba jamii ya binadamu iliumbwa na Mungu, kwamba maisha yetu yote hutawaliwa na kusimamiwa na Mungu, na kwamba hakuna mtu anayeweza kuepuka hili, wala hawezi kudhibiti hili. Sisi hujaribu bila mafanikio kujitegemea wenyewe kubadilisha majaliwa yetu, tukiishia tu kupigwa na kuviliwa. Hili ni onyesho la mamlaka ya Muumbaji. Mungu ameniokoa kutoka kumilikiwa na Shetani. Nimerudi mbele ya Mungu, Mungu ameniongoza kuuelewa ukweli, na hatimaye ninatembea katika njia ya kweli na sahihi ya maisha ya binadamu. Kupitia mambo niliyoyapitia, nimekuja kutambua kwa kweli kwamba utajiri wote na cheo na mambo yote ya kimwili katika ulimwengu huu ni matupu, kwamba unaweza tu kulitegemea neno la Mungu ili kuishi. Ni wakati huo tu ambapo moyo wako utakuwa imara na wenye amani. Huu ndio upendo mkubwa zaidi na baraka ambazo Mungu amenipa. Ninapoendelea na safari yangu, ninaguswa na kitu kimoja tu: Watu wajinga ambao humpinga Mungu huishi na mateso mengi sana, na ni watu wenye hekima tu wanaoutii ukuu wa Mungu wanaokombolewa na ni wenye furaha!

    Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

0 评论:

Chapisha Maoni