Jumatano, 3 Oktoba 2018

Filamu za Kikristo | "Vita" | God Saved Me From the Hands of False Shepherds (Swahili Subtitles)

Filamu za Kikristo | "Vita" | God Saved Me From the Hands of False Shepherds (Swahili Subtitles)

Zhang Hui alikuwa mzee katika kanisa la nyumbani la Kichina. Kila wakati alikuwa mtafutaji mwenye bidii, na alikuwa anangojea kuja kwa Bwana. Katika miaka ya hivi majuzi, alishuhudia kanisa likikumbwa na huzuni pole pole.
Roho yake mwenyewe ilififia pia na hakuwa na chochote cha kuhubiri. Zaidi ya hayo, bibi yake alifariki kwa ghafla, jambo lililomuathiri sana. Alikutana na mashahidi wawili kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa sadfa tu. Kupitia kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, roho yake yenye kiu ilipokea unyunyiziaji na chakula na aliweza kufurahia utamu wa kazi ya Roho Mtakatifu. Alihitimisha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu na akakubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Lakini wachungaji na watumishi wenzake kutoka kwa kanisa lake wanapogundua kuwa anaamini Mwenyezi Mungu, wanafanya kila kitu wawezacho kumzuia na kumvuruga. Juhudi zao za kutumia cheo na pesa ili kumjaribu Zhang Hui zinapokosa kufua dafu, wanaamua kutumia harusi ya mwanawe ili kumshurutisha kuacha njia ya kweli. Vita vya kiroho vinaanza kimya kimya … Je, Zhang Hui ataweza kumtegemea Mungu amwezeshe kubaini hila za watumishi wenzake? Je, ataweza kuepuka mitego yao na vikwazo na kurudi kusimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu?

0 评论:

Chapisha Maoni