Jumapili, 17 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Ingawaje Mungu aliunda agano na wanadamu kutumia upinde wa mvua, hakuwahi kuambia yeyote kwa nini alifanya hivi, kwa nini alianzisha agano hili, kumaanisha hakuwahi kuambia mtu fikira Zake halisi. Hii ni kwa sababu hakuna mtu anayeweza kufahamu kina cha upendo ambao Mungu anao kwa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake mwenyewe, na hakuna pia mtu anayeweza kutambua ni kiasi kipi cha maumivu moyo Wake uliteseka wakati Alipoangamiza binadamu. Hivyo basi, hata kama Angeambia watu namna Anavyohisi, hawawezi kumwamini. Licha ya kuwa katika maumivu, angali Anaendelea na hatua inayofuata ya kazi Yake. Siku zote Mungu Anautoa upande wake bora zaidi na mambo bora zaidi kwa wanadamu huku yeye Mwenyewe Akistahimili kimyakimya mateso yote. Mungu kamwe hafichui mateso haya. Badala yake, Anayavumilia na kusubiri kwa kimya. Ustahimilivu wa Mungu si wa kimya tu, usio na hisia, au usio na suluhu, wala si ishara ya unyonge. Ni kwamba upendo na kiini cha Mungu siku zote yamekuwa bila nafsi. Huu ni ufunuo wa kiasili wa kiini na tabia Yake na maonyesho halisi wa utambulisho wa Mungu kama Muumba wa kweli.”

Tazama zaidi: Neno la Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Kwanza

0 评论:

Chapisha Maoni