Jumanne, 12 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Nne

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Nne Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Elewa Mwelekeo wa Mungu na Utupilie Mbali Dhana zote Potovu Kumhusu Mungu Ni Nani Hupanga Matokeo ya Binadamu Watu Huishia Kumfafanua Mungu Kutokana na Uzoefu Wao Mwelekeo wa Mungu kwa Wale Wanaotoroka Wakati Kazi Yake Inaendelea Watu Wanaotoroka Wakati wa Kazi ya Mungu ni Wale Wanaoiacha Njia ya Kweli

Mwenyezi Mungu anasema: "Mungu huyu ambaye kwa sasa mnasadiki, mmewahi kufikiria kuhusu Yeye ni Mungu wa aina gani? Anapomwona mtu mwovu akifanya mambo maovu, je Anayachukia? (Anayachukia.) Anapoona makosa ya mtu asiyejua, mwelekeo Wake ni upi? (Huzuni.) Anapowaona watu wakiiba sadaka Yake, mwelekeo Wake ni upi? (Anawachukia.) Haya yote yako wazi, sivyo? Anapoona mtu akiwa mzembe katika kusadiki kwake Mungu, na mtu huyo akikosa kufuatilia ukweli kwa namna yoyote, mwelekeo wa Mungu ni upi? Bado hamjaelewa jambo hili, sivyo? Uzembe ni mwelekeo ambao si dhambi, na humkosei Mungu. Watu husadiki kwamba haupaswi kuchukuliwa kama kosa. Basi mnafikiria mwelekeo wa Mungu ni nini? (Hayuko radhi kujibu swali hili.) Hayuko radhi kulijibu—mwelekeo huu ni upi? Ni kwamba Mungu huwa anawadharau watu hawa, anawabeza watu hawa! Mungu hushughulikia watu hawa kwa kutowathamini. Mtazamo wake ni kuwaweka pembeni, kutojihusisha na kazi yoyote inayowahusu, ikiwemo kuwapa nuru, mwangaza, kuwarudi au kuwafundisha nidhamu. Mtu wa aina hii kwa kweli si wa thamani kwa kazi ya Mungu. Mwelekeo wa Mungu kwa watu wanaozikera tabia Yake, na kuzikosea amri Zake za kiutawala ni upi? Chuki mno kwa kupindukia! Kwa kweli Mungu hupandwa na hasira kali na watu ambao hawaghairi kuhusu kukera tabia Yake! “Hasira Kali” ni hisia tu, hali ya moyo; haiwezi kuwakilisha mwelekeo kamili. Lakini hisia hii, hali hii ya moyo, itasababisha matokeo kwa mtu huyu: Itamjaza Mungu na chukizo la kupindukia! Ni nini matokeo ya kuchukia huku kwa kupindukia? Ni kwamba Mungu atamweka pembeni mtu huyu, na kutomwitikia kwa sasa. Atasubiri watu hawa waweze kushughulikiwa kwenye kipindi cha adhabu. Hali hii inaashiria nini? Mtu huyu angali anayo matokeo? Mungu hakuwahi kunuia kumpa mtu wa aina hii matokeo! Hivyo basi si jambo la kawaida endapo Mungu kwa sasa hamwitikii mtu wa aina hii? (Ndiyo.) Mtu wa aina hii anafaa kujitayarisha vipi sasa? Wanafaa kujitayarisha kukabiliana na zile athari mbaya zilizosababishwa na tabia zao na maovu waliofanya. Huu ndio mwitikio wa Mungu kwa mtu wa aina hii. Hivyo basi Nasema waziwazi kwa mtu wa aina hii: Usishikilie imani za uwongo tena, na usijihusishe katika kufikiria makuu tena. Mungu hatavumilia watu siku zote bila kikomo; Hatastahimili dhambi zao au kutotii kwao bila kukoma. Baadhi ya watu watasema: “Nimeweza pia kuona watu wachache kama hawa. Wanapoomba wanaguswa hasa na Mungu, na wanalia kwa machungu. Kwa kawaida wao pia wanakuwa na furaha sana; wanaonekana kuwa na uwepo wa Mungu, na mwongozo wa Mungu.” Usiseme huo upuzi! Kulia kwa machungu si lazima iwe kwamba umeguswa na Mungu au unao uwepo wa Mungu, acha hata mwongozo wa Mungu. Kama watu watamghadhabisha Mungu, je, bado Mungu atawaongoza? Nikiongea kwa ujumla, wakati Mungu ameamua kumwondoa mtu, kuwaacha watu hao, tayari mtu huyo hana matokeo. Haijalishi ni vipi wanavyohisi kutosheka kujihusu wao wenyewe wakati wanapoomba, na imani kiwango kipi walichonacho katika Mungu mioyoni mwao; tayari hii si muhimu. Kitu cha muhimu ni kwamba Mungu hahitaji aina hii ya imani kwamba Mungu tayari amemsukumia mbali mtu huyu. Namna ya kuwashughulikia baadaye pia si muhimu. Kilicho muhimu ni kwamba katika muda ule ambao mtu huyu atamghadhabisha Mungu, matokeo yao tayari yameanzishwa. Kama Mungu ameamua kutomwokoa mtu wa aina hii, basi ataachwa na kuadhibiwa. Huu ndio mwelekeo wa Mungu."

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Tazama zaidi: Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Tatu

0 评论:

Chapisha Maoni