Jumamosi, 23 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)" Sehemu ya Tatu



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)" Sehemu ya Tatu
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Baada ya Kuumba Viumbe Vyote, Mamlaka ya Muumba Yanathibitishwa na Kuonyeshwa kwa Mara Nyingine Tena Kwenye Agano la Upinde wa Mvua Njia na Sifa za Kipekee za Matamshi ya Muumba Ni Ishara ya Utambulisho na Mamlaka ya Kipekee ya Muumba

Mwenyezi Mungu anasema, Mamlaka ya Muumba siku zote yanaonyeshwa na kutekelezwa miongoni mwa viumbe vyote, Naye hatawali tu hatima ya viumbe vyote, lakini pia Anatawala mwanadamu, kiumbe maalum ambacho Aliumba kwa mikono Yake mwenyewe, na kinachomiliki muundo tofauti wa uhai na kinachopatikana kwa mfumo tofauti wa uhai. Baada ya kuumba viumbe vyote, Muumba hakusita kuonyesha mamlaka na nguvu Zake; kwake Yeye, mamlaka ambayo Alishikilia ukuu juu ya viumbe vyote na hatima ya mwanadamu kwa ujumla, ilianza rasmi tu pale ambapo mwanadamu alizaliwa kwa kweli kutoka kwenye mkono Wake. Alinuia kusimamia mwanadamu, kutawala mwanadamu, Alinuia kumwokoa mwanadamu, Alinuia kufaidi mwanadamu kwa kweli, kufaidi mwanadamu ambaye angetawala viumbe vyote, na Alinuia kumfanya mwanadamu kama huyo kuishi chini ya mamlaka Yake, na kujua mamlaka Yake, na kutii mamlaka Yake. Hivyo basi, Mungu akaanza kuonyesha rasmi mamlaka Yake miongoni mwa binadamu kwa kutumia matamshi Yake, na Akaanza kutumia mamlaka Yake kutambua matamshi Yake. Bila shaka, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa mbele katika sehemu zote wakati wa mchakato huu; Nimeweza kuchukua tu baadhi ya mifano mahususi, inayojulikana ambayo unaweza kuelewa na kujua upekee wa Mungu na kuelewa na kujua upekee wa mamlaka ya Mungu.

Kunao mfanano kati ya fungu kwenye Mwanzo 9:11-13 na Mafungu yaliyo hapo juu yanayohusu rekodi za Mungu kuumba ulimwengu, ilhali kunayo pia tofauti. Mfanano ni upi? Mfanano umo katika matumizi ya matamshi na Mungu kuweza kufanya kile ambacho Alinuia, na tofauti ni kwamba, fungu hili ni mazungumzo ya Mungu na binadamu, ambapo Alianzisha agano na binadamu, na Akamwambia binadamu kuhusu kile ambacho kilikuwa ndani ya agano hilo. Utiliaji mkazo huu wa mamlaka ya Mungu ulitimizwa wakati wa mazungumzo Yake na Mungu, hivi ni kusema kwamba, kabla ya uumbaji wa mwanadamu, maneno ya Mungu yalikuwa maagizo, na amri ambavyo vilitolewa kwa viumbe ambavyo Alinuia kuumba. Lakini sasa kulikuwa na mtu wa kusikiliza matamshi ya Mungu, na hivyo basi matamshi Yake yalikuwa ya mazungumzo na binadamu, na pia himizo na onyo kwa binadamu, na zaidi, kulikuwa na amri zilizotolewa kwa viumbe vyote vilivyokuwa na mamlaka Yake.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza

Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

0 评论:

Chapisha Maoni