Jumatatu, 11 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia”


Maneno ya Roho Mtakatifu | “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia”
Mwenyezi Mungu anasema, “Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayeitwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Itaashiria mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi, na utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna uashirio wa ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo kutakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatiao la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba “Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo” watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Anashughulika nao tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe.”

0 评论:

Chapisha Maoni