Jumapili, 19 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 11

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 11

Je, Mimi ni Mungu wako? Je, Mimi ni Mfalme wako? Je, kweli umeniruhusu Mimi kutawala kama Mfalme ndani yako? Unapaswa kutafakari kujihusu kabisa. Je, hukuchunguza na kukataa mwanga mpya na hata kuthubutu kuacha kuufuata ulipokuwa ukija? Kwa sababu ya hii utastahimili hukumu na kuanguka hadi kifo chako, utahukumiwa na kutandikwa kiboko na kiboko cha chuma na hutahisi kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa haraka utapiga magoti katika ibada wakati huo ukilia kwa huzuni. Nimewaambia daima na daima Nimewaeleza na Nimewaambia kila kitu. Fikiria nyuma kulihusu, ni wakati upi Nimewahi kukosa kuwaambia kitu? Hata hivyo, kuna watu fulani ambao wanashikilia kufanya mambo kwa njia ambayo si sahihi. Wamepotea katika ukungu wa shaka ambao unazuia jua na kamwe hawauoni mwanga. Je, hii si kwa sababu fikira yao ya “nafsi” ni yenye nguvu sana ama mawazo yao wenyewe ni makubwa sana? Unawezaje kuniona Mimi katika macho yako? Unawezaje kuwa na nafasi kwa ajili Yangu katika roho yako? Wakati umefeli, wakati hauko sawa, na wakati umeishiwa na uchaguzi, hapo tu ndipo unaomba Kwangu. Basi, mbona usifanye mambo kivyako sasa? Watu kama hawa daima wanaangamizwa na nafsi zao nzee!

Watu wengine hawawezi kupata njia, na hawawezi kufuata mwanga mpya. Wanashiriki tu kuhusu kile ambacho wameona awali, hakuna kitu kipya kwao. Mbona hivyo? Mnaishi ndani yenu na mmeniacha Mimi nje ya mlango. Unaona mbinu ya kazi ya Roho Mtakatifu ikibadilika, lakini daima wewe ni mwangalifu sana kuhusu kuwa mwenye makosa; unawezaje kwa kweli kumcha Mungu? Je, umelitafuta katika ukimya wa uwepo wa Mungu? Unatafakari tu: “Je, Roho Mtakatifu kweli anafanya kazi hivyo?” Watu wengine wameshuhudia kwamba ni kazi ya Roho Mtakatifu, lakini bado wana mambo kusema kuihusu. Watu wengine wanakiri kwamba ni neno la Mungu, lakini hawalikubali. Kila dhana tofauti inawafurika, na hawaelewi kazi ya Roho Mtakatifu, wakiwa wazembe na wa ovyoovyo, bila hiari ya kulipa gharama na kuwa wenye bidii katika uwepo Wangu. Roho Mtakatifu amewapa nuru, lakini hawatakuja mbele Yangu kuwasiliana kwa karibu na kunitafuta. Badala yake, wanafuata tamaa zao wenyewe, wakifanya chochote wapendacho; ni nini nia yao?

Chanzo: Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 11
Tufuate: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

0 评论:

Chapisha Maoni