Jumapili, 26 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 17

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 17
Kanisa linajengwa na Shetani anajaribu kwa uwezo wake kulibomoa. Anataka kubomoa ujenzi Wangu kwa njia yoyote iwezekanayo, kwa hivyo, lazima kanisa litakaswe kwa haraka. Lazima kusiwe na makapi au mabaki yoyote maovu; lazima litakaswe ili lisiwe na dosari na libaki takatifu kama awali. Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo; lazima mle na mnywe maneno Yangu zaidi na, muhimu zaidi, lazima mweze kuyala na kuyanywa nyinyi wenyewe. Jiandaeni wenyewe na ukweli wote, njooni mbele Yangu ili nifungue macho yenu ya kiroho na kuwaruhusu kuona siri zote zilizo rohoni.... Wakati kanisa linaingia awamu yake ya ujenzi, vita vya watakatifu dhidi ya Shetani[a] vinaanza. Vipengele mbalimbali vya Shetani vya kutisha Vinawekwa mbele yenu; je, mnaacha na kurudi nyuma au mnainuka na kuendelea mkinitegemea Mimi? Weka hadharani vipengele vya Shetani vyenye upotovu na viovu, bila hisia wala huruma! Pambana na Shetani hadi kifo! Mimi ni msaada wenu na ni lazima muwe na roho ya mwana wa kiume! Shetani yuko katika hekaheka zake za kifo cha mwisho lakini bado hataweza kuhepa hukumu Yangu. Shetani yuko chini ya miguu Yangu na pia anakanyagwa chini ya miguu yenu—ni ukweli!

Wale wapinga dini wote na wale ambao hubomoa ujenzi wa kanisa hawafai kuvumiliwa hata kidogo na nitawahukumu mara moja. Weka Shetani hadharani, mkanyagie chini ya miguu, muangamize kabisa na usimuachie pa kujificha. Kila aina ya mapepo na vizuka hakika wataonyesha maumbile yao ya kweli mbele Yangu na Nitawatupa wote kuzimu ambamo hawatawahi kuwa huru; wote wako chini ya miguu yetu. Kama unataka kupigana vita vizuri kwa ajili ya ukweli, basi kwanza kabisa, usimpe Shetani nafasi ya kufanya kazi, na ili kufanya hivi mtastahili kuwa na nia moja na muweze kutumika katika kushirikiana, acheni dhana zenu za kibinafsi, maoni, mitazamo na njia za kufanya mambo, tuliza moyo wako ndani Yangu, zingatia sauti ya Roho Mtakatifu, kuwa makini na kazi ya Roho Mtakatifu na uwe na uzoefu wa maneno ya Mungu kwa kina. Lazima uwe na nia moja tu, ambayo ni kwamba mapenzi Yangu yaweze kutendeka. Hupaswi kuwa na nia nyingine. Lazima uangalie Kwangu kwa moyo wako wote, angalia hatua Zangu na Ninavyotenda mambo kwa karibu, na wala usiwe mzembe kabisa. Roho yako lazima iwe amilifu, macho yako yakiwa wazi. Kwa kawaida, wale ambao nia na malengo yao si sahihi, wale ambao wanapenda kuonekana na wengine, wenye hamu ya kutenda mambo, wenye tabia ya kukatiza, walio imara katika mafundisho ya dini, watumishi wa Shetani, nk., watu hawa wanapoinuka wanakuwa ugumu kwa kanisa na kula na kunywa kwa ndugu kunakuwa si kitu; unapompata mtu wa aina hii jifanye kisha mpige marufuku mara moja. Kama muda baada ya muda hawabadiliki basi watateseka sana. Kama wale wanaoendelea katika njia zao kwa ukaidi wanajitetea na kujaribu kufunika dhambi zao, kanisa linapaswa kuwaondoa mara moja na kutowaachia nafasi ya kuendelea. Usipoteze mengi kwa kujaribu kuokoa machache, na uzingatie makubwa.
Macho yako ya kiroho lazima sasa yafunguke, na kutofautisha aina kadhaa za watu kanisani:
Je, ni mtu wa ina gani anaelewa masuala ya kiroho na anajua roho?
Je, ni mtu wa ina gani haelewi masuala ya kiroho?
Je, ni mtu wa ina gani ana roho waovu ndani yake?
Je, ni mtu wa ina gani ana Shetani anafanya kazi juu yake?
Je, ni mtu wa ina gani ambaye ana tabia ya kukatiza?
Je, ni mtu wa ina gani ambaye Roho Mtakatifu anatenda kazi kwake?
Je, ni mtu wa ina gani huonyesha kuzingatia kuelekea mzigo wa Mungu?
Je, ni mtu wa ina gani anaweza kutenda mapenzi Yangu?
Je, ni nani shahidi Wangu mwaminifu?
Jua ya kwamba nuru ambayo Roho mtakatifu hupatia makanisa yote ni maono ya leo ya juu zaidi. Msichanganyikiwe kuhusu mambo haya, lakini badala yake lazima mchukuwe muda wa kuyafikiria kabisa—hii ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya maisha yenu! Kama huelewi mambo haya yaliyo machoni pako basi hutakuwa na uwezo wa kusonga mbele, utakuwa katika hatari ya majaribu na ufungwa wakati wowote, na huenda ukavamiwa. Jambo kuu sasa ni kuzingatia kuweza kuwa karibu na Mimi moyoni mwako, kufanya ushirika zaidi na Mimi, na chochote unachokosa au kutafuta utafidiwa kupitia kuwa karibu na Mimi na kufanya ushirika na Mimi. Maisha yako hakika yatashughulikiwa na utakuwa na nuru mpya. Mimi kamwe siangalii jinsi mlikuwa wajinga awali na siyakumbuki makosa yenu. Mimi huangalia jinsi mnavyonipenda: Je, mnaweza kunipenda zaidi ya mambo mengine yote? Naangalia kuona iwapo mnaweza kugeuka nyuma na kunitegemea kuondoa ujinga wenu au la. Baadhi ya watu husimama Kwangu, kunipinga hadharani, na kuhukumu watu wengine; hawajui maneno Yangu, na hata uwezekano wao wa kuona uso Wangu uko chini. Wote wale walio mbele Yangu ambao hunifuata kwa dhati, ambao wana mioyo yenye njaa na kiu cha haki, Nitawapa nuru, kuwafichulia, kuwaruhusu kuniona kwa macho yenu na kugusa mapenzi Yangu wenyewe; hakika moyo Wangu utafichuliwa kwenu, ili mpate kuelewa. Lazima muweze kutenda yale ambayo naangaza ndani yenu kulingana na maneno Yangu, vinginevyo mtahukumiwa. Fuata mapenzi Yangu na hamtapotea
Kwa wote wale wanaotafuta kuingia ndani ya maneno Yangu, neema na baraka vitaongezeka mara mbili juu yenu, mtapata nuru mpya kila siku, ufahamu mpya kila siku na kujisikia mpya katika kula na kunywa maneno Yangu kila siku; utayaonja kwa kinywa chako mwenyewe: Ni tamu jinsi gani! … Lazima uwe makini, na usitosheke unapokuwa na ufahamu kiasi na ladha kiasi ya utamu—cha msingi ni kuendelea kutafuta mbele! Baadhi ya watu hufikiria ya kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kweli ajabu na halisi—huyu kweli ni mtu wa Mwenyezi Mungu anafichuliwa wazi, na ishara na maajabu kubwa zaidi viko mbele. Kuwa makini na macho wakati wote, angalia kabisa kwenye chanzo, kuwa mtulivu mbele Yangu, zingatia na usikilize kwa makini, na kuwa na uhakika kuhusu maneno Yangu. Haiwezekani kuwa na utata; kama una shaka hata kidogo basi Nina hofu kuwa utapotea zaidi ya malango. Kuwa na maono wazi, simama kwenye sakafu ngumu, fuata mkondo huu wa maisha na uufuate popote ufikapo; usisite hata kidogo kabisa. Kula, kunywa na kutoa sifa tu, tafuta kwa moyo mtakatifu na usikate tamaa. Leta chochote usichokielewa mbele Yangu zaidi na hakikisha usiwe na moyo wa mashaka ili uepuke kupata hasara kubwa. Endelea! Endelea! Kaa karibu! Jikwamue kutoka kwa vizuizi na usijichafue. Endelea kwa moyo wote na usirudi nyuma. Lazima utoe moyo wako wakati wote na kamwe usiwahi kuupoteze muda wowote. Roho Mtakatifu daima ana kazi mpya ya kutenda, hutenda mambo mapya na ana nuru mpya kila siku; “kugeuka sura mlimani”—mwili mtakatifu wa kiroho wa Mungu umeonekana! Jua lenye haki hutoa nuru na huangaza, mataifa yote na watu wote wameona uso Wako mtakatifu. Nuru Yangu itaangaza juu ya wale wote wanaokuja mbele Yangu. Maneno yangu ni nuru, yakiwaongoza mbele. Hamtageuka kushoto au kulia mnapotembea lakini mtatembea ndani ya nuru Yangu, na kukimbia kwenu hakutakuwa kazi isiyo na matunda. Lazima muone kazi ya Roho Mtakatifu kwa uwazi na mapenzi Yangu yako pale ndani yake. Siri zote zimefichwa na zitafunuliwa kwenu hatua kwa hatua. Wekeni maneno Yangu akilini wakati wote na mje mbele Yangu kufanya ushirika zaidi na Mimi. Kazi ya Roho Mtakatifu huendelea. Tembeeni katika nyayo Zangu; maajabu makuu yako mbele na yatafunuliwa kwenu moja baada ya lingine. Ni wale tu ambao wanajali, wanaosubiri na ambao wako macho watayaona. Hakikisha usiwe mlegevu. Mpango wa usimamizi wa Mungu unakaribia hatua yake ya mwisho, ujenzi wa kanisa utafanikiwa, idadi ya washindi tayari imewekwa, mwana wa kiume mshindi atafanyika na wataingia katika ufalme na Mimi, kuchukua ufalme Nami, kutawala mataifa kwa fimbo ya chuma na kuwa katika utukufu pamoja!
Tanbihi:
a. Maandishi ya asilia huondoa "dhidi ya Shetani."
Chanzo: Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 17
Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

0 评论:

Chapisha Maoni