Alhamisi, 9 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 3

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 3

Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu. Yeye Ametimiza ukombozi na kuongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu. Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake kwa hekima Yake ya uungu na uweza Yeye Amejenga Uyahudi na kuifanya imara. Pamoja na uadhama Wake Yeye huhukumu dunia ya maovu; Yeye huhukumu mataifa yote na watu wote, ardhi na bahari na vitu vyote hai juu yao, pia wale ambao wamelewa kwa divai ya uzinzi. Kwa hakika Mungu atawahukumu hao, na kwa hakika Atakuwa mwenye hasira nao na mle uadhama wa Mungu utafichuliwa. Hukumu ya aina hiyo itakuwa papo hapo na kuwasilishwa bila kuchelewa. Ghadhabu kali ya Mungu itawachoma hao wote kwa ajili ya makosa yao ya kuchukiza na janga kubwa litawafikia wakati wowote; wao hawatajua njia ya kutoroka na hawatakuwa na mahali pa kujificha, wao watalia na kusaga meno yao kwa ajili ya uharibifu ambao wamejiletea wenyewe.

Wana wa ushindi wapendwa wa Mungu kwa hakika watakaa katika Uyahudi, kamwe wasiiache. Umati utasikiliza sauti Yake kwa makini, watatilia maanani kwa ungalifu matendo Yake, na sauti zao za sifa Kwake kamwe hazitakoma. Mungu mmoja wa kweli Ameonekana! Tutakuwa na uhakika juu Yake katika roho na kumfuata kwa karibu na kukazana kusonga mbele bila kusita. Mwisho wa dunia unajitokeza mbele yetu; maisha sahihi ya kanisa pamoja na watu, shughuli, na mambo ambayo yanatuzunguka yanaongeza mafunzo yetu. Kwa haraka chukua tena mioyo yetu ambayo inapenda dunia sana! Kwa haraka rudisha maono yetu yaliyovurugwa! Hatutasonga mbele zaidi tusije tukazidi mipaka na tutashikilia ndimi zetu ili tuweze kuishi kwa kufuata neno la Mungu, na tena hatutazozona juu ya faida zetu wenyewe na hasara. Acha upendo wako wa utajiri wa dunia ya kawaida! Jiweke huru kutoka kwa upendo wa mume wako na mabinti na wana wako! Acha maoni yako na upendeleo! Amka, kwa sababu muda ni mfupi! Iruhusu roho yako iangalie juu, angalia juu na umruhusu Mungu Achukue uongozi. Usijiruhusu kuwa kama mke wa Lutu. Kutelekezwa ni jambo la kusikitisha sana! Ni la kusikitisha kweli! Amka!
Chanzo: Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 3
Kujua zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu


0 评论:

Chapisha Maoni