Jumatatu, 27 Mei 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 18

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 18
Kujenga kanisa si kitu rahisi cha kufanya! Niliweka moyo Wangu wote katika kulijenga na Shetani angefanya kila kitu ingeweza kuibomoa. Kama unataka kujengwa lazima uwe na maono; lazima uishi maisha kwa Mimi, kuwa shahidi wa Kristo, shikilia Kristo juu kwa juu, na kuwa mwaminifu Kwangu. Hupaswi kutoa visingizio, lakini badala yake kutii bila ya sharti; lazima uvumilie majaribu yoyote, na kukubali yote yanayotoka kwa Mimi. Lazima ufuate chochote Roho Mtakatifu hufanya ili Akuongoze wewe, lazima uwe na roho hodari na uwezo wa kutofautisha mambo. Ni lazima uelewe watu na usifuate wengine kwa upofu, weka macho yako ya kiroho nga’vu na umiliki elimu kamilifu ya mambo. Watu ambao ni wa akili sawa na Mimi lazima wawe shahidi Kwangu Mimi na kupigana vita vya kuamua dhidi ya Shetani. Lazima uwe kwote umejengwa na kupigana vita. Mimi nipo miongoni mwenu, Ninawasaidia na Mimi ndiye kimbilio lenu.

Shughuli ya kwanza ni kujitakasa, kuwa mtu aliyebadilika, na kuwa na mwenendo imara. Lazima uishi kwa Mimi katika mazingira mazuri na mabaya, na kama uko nyumbani au katika sehemu zingine, usisite kwa sababu ya mtu mwingine, au kwa sababu ya baadhi ya tukio au kitu. Lazima usimame imara na kuishi kama Kristo Alivyofanya kudhihirisha Mungu Mwenyewe katika maisha yako mwenyewe. Lazima ufanye shughuli zako na kutimiza wajibu wako kama kawaida; hii haitendeki yote mara moja, lakini lazima iendelezwe. Lazima uchukue Moyo Wangu kama moyo wako, dhamira Zangu lazima ziwe mawazo yako, lazima ufikirie hali yote kwa ujumla, ruhusu Kristo Aanzie kwako, na kujiunga pamoja kutumikia. Lazima uende kwa kasi sawa na kazi ya Roho Mtakatifu na ujiegemeze katika mbinu ya wokovu wa Roho Mtakatifu. Lazima ujifanye tupu na kuwa mtu asiye na hatia na mtu aliye wazi. Lazima ushiriki kwa kawaida pamoja na ndugu na dada zako, muwe na uwezo wa kufanya mambo katika roho, pendaneni, ruhusu nguvu za wengine kusawazisha udhaifu wako, tafuta kujengwa katika kanisa. Ni wakati huo tu ambapo utakuwa na sehemu katika ufalme.
Chanzo: Sauti ya Mungu | Sura ya 18

0 评论:

Chapisha Maoni