Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 35
Nimeanza kutenda kazi Yangu kati ya wanadamu, kuwakubalia kuishi mkondo mmoja Nami. Nitakamilisha kazi Yangu nikiwa kati yao, maana wao ni vyombo Ninavyosimamia katika mpango Wangu wote wa usimamizi—na ni mapenzi Langu ili waweze kuwa watawala wa vitu vyote. Hivyo basi Naendelea kutembea kati ya wanadamu. Kadri wanadamu pamoja Nami tuingiavyo katika enzi ya sasa, Najihisi huru kabisa, kwa sababu, hatua Yangu ni ya haraka.
Wanadamu hawa wanawezaje kudumisha mwendo huu? Nimefanya kazi nyingi kwa watu wasiojali na walio butu, lakini hawajafaidi chochote kwa kuwa hawanijali wala kunipenda Mimi. Nimeishi kati ya watu wote na kuwatazama waendapo juu na chini ya ardhi. Wale wote wanaoainishwa kama “wanadamu” wananipinga Mimi, kana kwamba “kunipinga Mimi” kulikuwa katika maelezo ya kazi yao. Inaonekana kwamba kama hawangeitekeleza hii kazi, basi wangekuwa kama yatima mzururaji, asiyepangwa na mtu yeyote. Hata hivyo, Mimi Siwahukumu watu kwa udhalimu kulingana na matendo na tabia zao. Bali, Mimi husaidia na kuwaruzuku kwa mujibu wa kimo chao. Kwa kuwa wanadamu ndio wahusika wakuu wa mpango Wangu wote wa usimamizi, Natoa ushauri zaidi kwa walio katika hii nafasi ya “binadamu” ili waweze kuiigiza kwa moyo wote na kwa uwezo wao wote, ili igizo hili Ninaloliongoza liweze kufanikiwa kikamilifu. Hili ndilo ombi Langu kwa wanadamu. Je, yawezekana kuwa bila ombi hili, hawataweza kutenda wajibu wao kadri ya uwezo wao? Naweza kutimiza kile watu wanachohitaji Kwangu, lakini wao hawawezi kutimiza Ninachohitaji kwao? Haiwezi kusemwa kuwa Nawatesa wanadamu kwa uwezo. Hili ndilo ombi Langu la mwisho: Nawasihi kwa juhudi na uaminifu wote. Hawawezi kwa kweli kufanya Ninachowauliza? Nimekuwa nikiwapa watu kwa miaka mingi, lakini Sijapokea chochote kutoka kwao. Ni nani amewahi kunipa Mimi chochote? Je, damu, jasho, na machozi Yangu ni kama tu mawingu milimani? Nimewapa watu “chanjo” mara nyingi, na kuwaambia kwamba mahitaji Yangu kwao hayakuwa ya kushurutisha. Kwa nini, basi, watu huniepuka Mimi daima? Je, ni kwa sababu Nitawachukulia kama vifaranga wadogo, kuuawa punde washikwapo? Je, Mimi ni katili na asiye na huruma hivyo? Wanadamu daima hunipima kwa dhana zao. Je, dhana zao juu Yangu zinafanana na uhalisi wa[a] Mimi mbinguni? Sichukulii dhana za watu kuwa vyombo vya furaha Yangu. Bali, Naiona mioyo yao kama vitu vya kuthaminiwa. Hata hivyo, Nahisi kuchoshwa kabisa na dhamiri zao, kwa kuwa kulingana na wao, Mimi Mwenyewe sina dhamiri. Hivyo basi Nimefafanua kauli za ziada juu ya mada hiyo. Hata hivyo, Nakataa kukosoa dhamiri zao moja kwa moja; badala yake, Naendelea kuwaelekeza kwa uvumilivu na utaratibu. Hata hivyo, wanadumu ni dhaifu, na wasioweza kufanya kazi yoyote.

Leo, Nimechukua hatua rasmi kuingia katika eneo la kuadibu kusio na mipaka, na Ninaifurahia pamoja na wanadamu. Pia Nawaongoza kwa mkono, nao wana nidhamu njema chini ya uongozi Wangu; hakuna anayethubutu kunipinga Mimi. Wote wapo chini ya uongozi Wangu, wakiteleza wajibu Niliowapa, kwa kuwa hili lipo katika “maelezo ya kazi” zao. Kati ya mambo yote yaliyo mbinguni na chini ya mbingu ni nani huthubutu kutotii mipango Yangu? Ni nani asiye katika mfumbato Wangu? Ni nani asiyetamka sifa na fadhili kwa maneno Yangu na kazi Zangu? Wanadamu huajabia matendo Yangu, hivyo basi wao hujitoa kwa mkondo wa kazi Yangu kwa ajili ya kila hatua Yangu ndogo. Ni nani awezaye kuacha? Ni nani anayeweza kuondoka kutoka kwa kazi Niliyoipanga? Kwa ajili ya amri Yangu ya utawala, wanadamu hawana budi ila kusalia; bila hiyo, wote wangepenyeza kimya kimya kutoka “mstari wa mbele” na kuwa “watoro.” Nani asiye na hofu ya kifo? Je, watu wako tayari kweli kujitoa mhanga? Simlazimishi yeyote, kwa sababu Nilipata ufahamu wa asili ya wanadamu hapo kale. Kwa hivyo, Nimekuwa kila mara Nikifanya miradi ambayo watu hawajawahi kufanya hapo awali. Kwa kuwa hakuna mtu ambaye angeifanya kazi Yangu, Nimeingia vitani binafsi kukumbana na mapambano ya kufa na kupona dhidi ya Shetani. Siku hizi, Shetani amekithiri kupita kiasi. Kwa nini Nisichukue fursa hii kuringia kiini cha kazi Yangu ili kufichua nguvu Zangu? Kama Nilivyosema hapo awali, Natumia ujanja wa Shetani kama foili[b]; je, hii sio fursa mwafaka? Sasa tu ndio Naonyesha tabasamu ya kufurahishwa, maana Nimetimiza lengo Langu. Sitakimbia huku na huku tena na kuomba ‘msaada’ wa wanadamu. Nimeacha kutangatanga huku na huko, na Siishi tena maisha ya mzururaji. Tangu sasa kuendelea, Nitaishi kwa amani. Wanadamu pia watakuwa salama salmini, kwa maana siku Yangu imewadia. Hapa duniani Nimeishi maisha ya shughuli nyingi mno ya mwandamu, maisha ambamo matukio mengi ya udhalimu yanaonekana yamefanyika. Kwa macho ya wanadamu, Nimeshiriki raha na masikitiko yao, na vilevile shari zao. Kama wanadamu, Mimi, pia, Nimeishi duniani na chini ya mbingu. Hivyo basi wameniona Mimi daima kama kiumbe kilichoumbwa. Kwa kuwa wanadamu hawajaniona Mimi mbinguni, hawajatumia juhudi nyingi Kwangu. Hata hivyo, hali ilivyo leo, watu hawana budi ila kukubali kuwa Mimi ni Bwana wa majaliwa yao na mnenaji anenaye kutoka mawinguni. Hivyo basi wanadamu wamegusisha vichwa vyao ardhini wakiabudu mbele Yangu. Je, hii sio ithibati ya marejeo Yangu ya ushindi? Je, hili silo onyesho la ushindi Wangu dhidi ya majeshi yote ya uhasama? Watu wote wamekuwa na jakamoyo kwamba dunia inakaribia mwisho, na kwamba binadamu utapitia utakaso mkuu. Hata hivyo, hawawezi kwa ukweli kutimiza kwa kufahamu kile Ninachouliza, kwa hiyo hawana budi ila kulia chini ya kuadibu Kwangu. Nini kinachoweza kufanyika? Ni nani aliyewaambia hawa wanadamu kutotii? Ni nani aliyewaambia kuingia katika enzi ya mwisho? Kwa nini walizaliwa kama wanadamu katika nyakati hizi zinazotangulia mwisho wa dunia? Kila kitu kimepangwa na Mimi binafsi. Ni nani anayeweza kulalamika?
Tangu uumbaji wa ulimwengu, Nimetembea kati ya wanadamu, Nikiishi nao katika kuishi kwao duniani. Katika vizazi vilivyotangulia, hata hivyo, hakuna mtu hata mmoja aliyechaguliwa na Mimi; kila mmoja alikataliwa na kimya Changu. Hii ni kwa sababu watu hao wa kale hawakunitumikia kwa kujitolea kwa roho moja; hivyo basi Nami wala sikuwapenda kipekee. Walikuwa wamechukua “vipawa” vya Shetani na kisha wakageuka na kunitolea Mimi; kwa kufanya hivyo, je, huu haukuwa udanganyifu Kwangu? Wakati sadaka hizo zilikuwa zinatolewa, Sikufichua ghadhabu Yangu; badala yake, Nilijaribu kubadili mpango wao kwa matumizi Yangu mwenyewe kwa kuongezea “vipawa” hivi kwa vifaa vinavyotumika katika usimamizi Wangu. Baadaye, mara tu vilipokuwa vimesindikwa na mtambo, Ningechoma masalio yaliyoharibika. Ijapokuwa kizazi hiki cha sasa cha wanadamu hakijanitolea Mimi “vipawa” vingi, Siwakaripii kwa hilo. Watu hawa wamekuwa daima masikini na wenye mkono mtupu; hivyo, kwa kutazama uhalisi wa hali yao, Sijawahi kuwaitisha kisichowezekana baada ya Mimi kuja katika ulimwengu wa wanadamu. Bali, baada ya kuwapa “vifaa,” Nimetafuta tu “bidhaa iliyokamilishwa” Ninayotaka, maana hili ndilo jambo pekee la kuweza kutimizwa na wanadamu. Nimeishi miaka mingi kwenye taabu, Nikijifunza maana ya kuishi kama mwanadamu, kabla ya kutoa ombi la kufaa. Lau Singekuwa na uzoefu wa maisha ya mwanadamu, Ningeelewaje maswala wanayoyaona magumu kujadili? Hata hivyo, wanadamu hawayaoni hivi; wao husema tu Mimi ni Mungu mwenye nguvu, Mungu Mwenyewe wa ajabu. Je, hii siyo hasa dhana ambayo wanadamu wote wamekuwa nayo kote katika historia na hata mpaka leo? Nilisema kuwa ardhini hakuna yeyote anayeweza kunijua Mimi kweli asilimia mia moja. Usemi huu una maana yake; hii sio porojo tu. Nina uzoefu na Nimeona hili Mimi Mwenyewe, kwa hivyo Nina ufahamu wa utondoti. Iwapo Singekuja chini kwa ulimwengu wa wanadamu, ni nani angekuwa na nafasi ya kunijua Mimi? Ni nani angeyasikiliza maneno Yangu binafsi? Ni nani angeona umbo Langu kati yao? Tangu nyakati za zamani Nilikuwa daima Nimefichwa mawinguni. Nilitabiri hapo mapema kwamba Ningeshuka chini kwa ulimwengu wa wanadamu katika siku za mwisho kuwa mfano wao mzuri. Ndio maana siku hizi watu wana bahati kupanua peo zao. Je, hii si fadhili Niliyowakidhi nayo? Je, yawezekana kuwa hawataelewa neema Yangu kabisa? Mbona wanadamu ni wasiojali hisia za wengine na ni butu sana? Baada ya kuja umbali huu, mbona bado hawajaamka? Nimekuwapo humu ulimwenguni kwa miaka mingi lakini nani anijuaye? Si ajabu Nawaadibu watu. Inaonekana kwamba wao ndio vyombo vya kuweka mamlaka Yangu katika matumizi; inaonekana kwamba wao ni risasi kwenye bunduki Yangu ambazo, Nikishalipua, zote zitapotea. Hili ndilo wazo lao. Nimewaheshimu wanadamu daima; Sijawahi kuwanyonya kwa udhalimu au kuwafanyia biashara kama watumwa. Hii ni kwa sababu Siwezi kuwaacha, wala wao hawawezi kuniwacha Mimi. Hivyo basi, mshikamano wa kufa kupona umeundwa kati Yetu. Daima Nawatunza na kuwapenda wanadamu. Ijapokuwa hisia hiyo haijawahi kuwa ya maafikiano, wamenitazama Mimi daima, ndio maana Naendelea kutumia juhudi kwao. Nawapenda watu kama hazina Yangu mwenyewe, maana wao ndio “rasilimali” ya usimamizi Wangu duniani; hivyo basi Sitawaangamiza kamwe. Mapenzi Yangu kwa wanadamu hayatabadilika. Je, wanaweza kusadiki kwa kweli katika kiapo Changu? Watawezaje kuniridhisha? Huu ndio wajibu wa wanadamu wote; hili ndilo “zoezi la nyumbani” Nililowaachia. Ni tumaini Langu kwamba wote watafanya bidii kulikamilisha.
Aprili 23, 1992
Tanbihi:
a. Maandishi ya asili yanaacha “uhalisi wa.”
b. foili—Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
b. foili—Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
0 评论:
Chapisha Maoni