Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 97
Nitafanya kila mtu aone matendo Yangu ya ajabu na kusikia maneno Yangu ya hekima. Ni lazima iwe kila mtu na ni lazima iwe juu ya kila suala. Hii ni amri Yangu ya utawala na ni ghadhabu Yangu. Nitahusisha kila mtu na kila jambo ili watu wote kutoka mwisho mmoja wa ulimwengu hadi mwingine wataona kwa macho yao wenyewe, la sivyo Sitaacha kamwe. Ghadhabu Yangu imemwagwa kikamilifu na hakuna hata chembe imezuiwa. Inaelekezwa kwa kila mtu mmoja ambaye anakubali jina hili (hivi karibuni itageuzwa juu ya mataifa yote ya dunia). Na ghadhabu Yangu ni nini? Ni kali kiasi gani?
Je, ghadhabu Yangu inamwangukia mtu wa aina gani? Watu wengi wanafikiri kuwa ghadhabu ni hasira kali kabisa, lakini hii haiielezi kikamilifu. Ghadhabu Yangu na amri Zangu za utawala ni sehemu mbili zisizotenganishwa; Ninapozifanya amri Zangu za utawala kuwa sheria, ghadhabu hufuata nyuma yake. Kwa hiyo ghadhabu ni nini? Ghadhabu ni kiwango cha hukumu Ninachotoa kwa watu na ni kanuni ya kufanywa kuwa sheria kwa amri Yangu yoyote ya utawala. Yeyote anayekosea mojawapo ya amri Zangu, ghadhabu Yangu itakuwa kulingana na kiwango chake, kulingana na amri ambayo imekosewa. Pamoja na ghadhabu huja amri Zangu za utawala, na pamoja na amri Zangu za utawala huja ghadhabu. Amri Zangu za utawala na ghadhabu hufanya uzima usiotenganishwa. Ni hukumu kali zaidi na hakuna mtu anayeweza kuikosea. Watu wote wanapaswa kuizingatia, la sivyo wataona vigumu kuepuka kupigwa chini na mkono Wangu. Watu hawakuwahi kujifunza jambo hilo katika enzi zote (ingawa watu wengine waliteseka machungu yaliyosababishwa na maafa makubwa, bado hawakutambua kulihusu; lakini hili hasa linaanza kufanywa kuwa sheria sasa), lakini leo ninawafichulia yote, ili muweze kuepuka kusababisha kosa.
Watu wote wanapaswa kusikia sauti Yangu na kuamini maneno Yangu, vinginevyo Sitatenda lolote wala kufanya kazi yoyote. Maneno Yangu yote na matendo ni mifano ambayo mnapaswa kufuata; hayo ni mifano yenu bora na hayo ni mifano ya ninyi kufuata. Sababu ya Mimi kuwa mwili ni kwamba muweze kuona kile Nilicho na nilicho nacho katika ubinadamu Wangu. Katika siku zijazo, Nitawaruhusu kushuhudia kile Nilicho na nilicho Nacho katika uungu Wangu. Mambo lazima yaende hatua kwa hatua kwa njia hii. Vinginevyo, watu hawataweza kuamini kabisa, na hawatakuwa na ujuzi kunihusu. Badala yake watakuwa tu bila uwazi na kutoweza kutofautisha kuhusu maono na hawataweza kuwa na ufahamu wa wazi wa Mimi. Maneno Yangu yameonyesha kuwa nafsi Yangu imeonekana kwenu kabisa, watu tu ndio wapumbavu na wasiojua, kwa hiyo wanasikia maneno Yangu na bado hawanijui Mimi. Watu bado wananikataa Mimi kama kupata mwili kwa sasa, kwa hiyo Ninatumia ghadhabu Yangu na amri Zangu za utawala ili kuadhibu enzi hii ya zamani mbovu na ya uasherati na kumwaibisha Shetani na ibilisi kabisa. Hii ndiyo njia pekee, ni hatima ya wanadamu, na ni mwisho ambao unawasubiri wanadamu. Matokeo yake ni hitimisho lililopita kwamba hakuna mtu anayeweza kubadilisha au kujitetea asamehewe. Mimi tu ndiye Nina uamuzi wa mwisho; huu ni usimamizi Wangu na ni mpango Wangu. Watu wote wanapaswa kuamini na kushawishika katika moyo na kwa neno. Wale ambao wanapata bahati nzuri katika maisha haya bila shaka watateseka milele yote, huku wale wanaoteseka katika maisha haya hakika watabarikiwa katika milele yote—hii Nimeiamua kabla na hakuna mtu anayeweza kuibadilisha. Hakuna mtu anayeweza kubadili moyo Wangu na hakuna mtu anayeweza kuongeza hata neno moja zaidi kwa maneno Yangu, sembuse wao kuruhusiwa kuondoa neno lolote kiholela; hakika Nitawaadibu wakosaji wote.
Mafumbo Yangu yanafichuliwa kwenu kila siku—je, mnayaelewa kweli? Je, mna hakika kuyahusu? Je, unaweza kung’amua wakati Shetani anakudanganya? Hii inaamuliwa kwa mujibu wa vimo vyenu katika maisha. Kwa kuwa Ninasema kwamba vitu vyote vimeamuliwa kabla na Mimi, kwa nini basi ninapata mwili mimi binafsi kuwakamilisha wanangu wazaliwa wa kwanza? Zaidi ya hayo, kwa nini nimefanya kazi nyingi sana ambazo watu wanazifikiria kama zisizo na maana? Je, ni Mimi Niliyechanganyikiwa? Kumbuka hili! Kila kitu Ninachofanya hakifanyiki tu ili kuwapata wana Wangu wazaliwa wa kwanza lakini la muhimu zaidi vinafanywa kumwaibisha Shetani. Ingawa ananikiuka, bado Nina uwezo wa kuwafanya wazawa wake waasi dhidi yake, na kugeuka kunisifu. Hii ni hasa ili hatua ifuatayo ya kazi itaendelea vizuri, na kwamba ulimwengu wote utafurahi na kunisifu na vitu vyote vinavyopumua vitanipigia goti na kunitukuza; hiyo kweli itakuwa siku ya utukufu. Ninashikilia vitu vyote mikononi Mwangu na wakati radi saba zitakapozuka vitu vyote vitakuwa vimekamilishwa kabisa, visibadilike kamwe, vyote vimetengenezwa. Kutoka wakati huo kuendelea maisha mapya ya mbingu na nchi mpya yataingiwa, kuingia katika hali mpya kabisa, na maisha ya ufalme yataanza. Lakini hali ni vipi ndani ya ufalme? Watu hawawezi kuuelewa wazi kabisa (kwa sababu hakuna mtu aliyewahi kuonja maisha ya ufalme kabla, na hivyo yamefikiriwa tu katika akili za watu na kufikiriwa ndani ya mioyo yao). Katika kugeuka kutoka kwa maisha ya kanisa hadi kwa maisha ya ufalme, ambayo ni kugeuka kutoka hali ya sasa hadi hali ya baadaye, mambo mengi yatatokea wakati huu ambayo watu hawajawahi kufikiria awali. Maisha ya Kanisa ni utangulizi wa uingiaji katika maisha ya ufalme, hivyo kabla ya maisha ya ufalme kutokea Sitaacha jitihada yoyote katika kuendeleza maisha ya kanisa. Maisha ya kanisa ni nini? Ni kila mtu, ikiwa ni pamoja na wanangu wazaliwa wa kwanza, akila, kunywa na kufurahia maneno Yangu na kunijua, hivyo kupokea uchomaji na utakaso Wangu, ili kuelewa amri Zangu za utawala, hukumu Yangu na ghadhabu Yangu, ili aweze kuepuka kusababisha kosa katika maisha ya ufalme. Na maisha ya ufalme ni nini? Maisha ya Ufalme ni pale ambapo wanangu wazaliwa wa kwanza wanaanza kutawala kama wafalme pamoja na Mimi, wakitawala watu wote na mataifa yote ( wanangu wazaliwa wa kwanza na Mimi tu ndio tunaweza kufurahia maisha ya ufalme). Ingawa wana Wangu na watu Wangu kutoka kwa watu wote na mataifa yote wataingia katika ufalme, hawawezi kufurahia maisha ya ufalme. Uzima wa ufalme unaweza kufurahiwa tu na wale wanaoingia katika ulimwengu wa kiroho. Hivyo ni wanangu wazaliwa wa kwanza tu na Mimi tunaoweza kuishi katika mwili, wakati wana wangu na watu wangu wanaendelea kuishi katika mwili. (Lakini huu sio mwili ambao umepotoshwa na Shetani. Huu ni umuhimu wa wana Wangu wazaliwa wa kwanza kutawala pamoja nami kama wafalme.) Roho za watu wengine wote zitachukuliwa, roho na miili itachukuliwa na kutupwa Kuzimuni. Hiyo ni kusema kuwa watu hawa wataangamia kabisa na watakoma kuwepo (na bado wanapaswa kupitia katika utumwa wote na ukatili wa Shetani, kama vile shida na maafa). Mara hii itakapofanyika, watu wanaweza kuingia rasmi kwenye njia sahihi ya maisha ya ufalme na Nitaanza kufichua matendo Yangu rasmi (kufichuliwa waziwazi na sio kufichwa). Kutoka wakati huo kuendelea, hakika hakutakuwa na kutanafusi tena na machozi. (Kwa maana hakutakuwa na kitu chochote ambacho kinaweza kuwaumiza watu, au kuwafanya kulia au kuwasababishia mateso, na hii inahusu wana Wangu na watu Wangu pia; lakini kuna jambo moja ambalo linastahili kusisitizwa, ambalo ni kwamba wana Wangu na watu Wangu watakuwa miili milele.) Wote watakuwa wenye furaha na kuonekana wenye furaha. Hakitakuwa kitu chochote cha kimwili, kitakuwa kitu ambacho hakiwezi kuonekana kwa macho ya kimwili. Wale ambao ni wanangu wazaliwa wa kwanza watakuwa na uwezo wa kufurahia pia; hili ni tendo Langu la ajabu na mamlaka Yangu.
Ninatamani kwamba ninyi muwe na uwezo wa kutafuta mapenzi Yangu na muuhurumie moyo Wangu wakati wote. Raha isiyodumu inaweza kuharibu maisha yako yote, wakati mateso ya muda mfupi yanaweza kukaribisha baraka ya milele. Usiwe mwenye huzuni; hii ndiyo njia ambayo lazima itembewe. Nimesema mara nyingi kabla: “Kwa wale wanaogharimika kwa ajili Yangu kwa dhati, hakika Nitakubariki sana.” Baraka ni nini? Siyo tu zile zinazopatikana leo, lakini zaidi ya hayo ni zile zitakazofurahiwa katika siku zijazo—hizi tu ndizo baraka za kweli. Mnaporudi katika Mlima Sayuni, mtaonyesha shukrani isiyo na mwisho kwa mateso yenu ya sasa, kwa maana hii ni baraka Yangu. Kuishi sasa katika mwili ni kuwa juu ya Mlima Sayuni (kumaanisha ya kuwa unaishi ndani Yangu), wakati kuishi katika mwili kesho kutakuwa siku ya utukufu, na hii hata zaidi ni kuwa juu ya Mlima Sayuni. Baada ya kusikia maneno haya Ninayosema, kisha mnaelewa maana ya Mlima Sayuni. Mlima Sayuni ni kisawe cha ufalme, na pia ni ulimwengu wa kiroho. Katika Mlima Sayuni wa leo, ninyi mko katika mwili mkipata faraja na kupata neema Yangu; juu ya Mlima Sayuni wa siku zijazo, mtakuwa katika mwili mkifurahia baraka ya kutawala kama wafalme. Hii lazima bila shaka isipuuzwe. Na msiruhusu nyakati ambapo baraka zinaweza kupatikana zipite hata kidogo; leo ni leo, hata hivyo, na ni tofauti sana na kesho. Unapokuja kufurahia baraka, utafikiri kuwa neema ya leo haistahili kutajwa. Hili ndilo Ninalokuaminia, na ni ushauri Wangu wa mwisho.
Chanzo: Sura ya 97
Tufuate: Utangulizi wa programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu | Injili ya kurudi kwa Bwana Yesu
0 评论:
Chapisha Maoni