Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo siku-za-mwisho. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo siku-za-mwisho. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 24 Juni 2019

Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu


Neno la Mungu |  “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu

anasema, “Mungu aliumba vitu vyote kuhusiana, kupatana na kutegemeana. Alitumia njia hii na kanuni hizi kudumisha kuendelea kuishi na uwepo wa vitu vyote na kwa njia hii binadamu ameishi kwa utulivu na kwa amani na amekua na kuzaliana kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira haya hai hadi siku ya leo. Yaani, Mungu anaweka uwiano katika mazingira ya asili.

Jumamosi, 8 Juni 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 28


Maneno ya Mungu | Sura ya 28

Unaona kwamba muda ni mfupi sana na kazi ya Roho Mtakatifu inavurumisha mbele, ikikusababisha kupata baraka kubwa hivi, kumpokea Mfalme wa ulimwengu, Mwenyezi Mungu, ambaye ni Jua ling’aalo, Mfalme wa ufalme—hii yote ni neema na huruma Yangu. Kuna nini kinachoweza kuwepo kinachoweza kukutoa kwa upendo Wangu? Tafakari kwa makini, usijaribu kuepa, subiri kwa ustahamilivu mbele Yangu kila wakati na usiwe ukizurura nje daima.

Jumatano, 5 Juni 2019


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja”  Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali.

Jumamosi, 1 Juni 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 22

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 22
Kumwamini Mungu si jambo rahisi kufanya. Ninyi mnajiboronga, mkiteketeza kila kitu mbele yenu mkifikiri kuwa haya yote ni ya kuvutia sana, matamu mno! Kuna baadhi ambao bado wanashangilia—wao tu hawana utambuzi katika roho zao. Ni vyema kuchukua muda wa kuuweka katika muhtasari uzoefu huu. Katika siku za mwisho, kila aina za pepo huibuka kutekeleza majukumu yao, wakikaidi kwa uwazi hatua za mbele za wana wa Mungu na kushiriki katika kuuvunja ujenzi wa kanisa.

Jumapili, 12 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Haijalishi wewe ni mbari gani au unaishi katika ardhi gani, iwe ni Magharibi au Mashariki—huwezi kujitenganisha na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu, na huwezi kujitenga na malezi na uangalizi wa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu. Haijalishi riziki yako ni nini, kile unachokitegemea kwa ajili ya kuishi, na kile unachokitegemea kudumisha uhai wako katika mwili, huwezi kujitenganisha na kanuni ya Mungu na usimamizi wake.”

Jumapili, 28 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 104

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 104

Watu, matukio na vitu vyote nje Yangu vitakufa na kuwakatika hali ya kutokuwepo, ilhali watu, matukio na vitu vyote vilivyo ndani Yangu vitapata kila kitu kutoka Kwangu na kuingia katika utukufu pamoja na Mimi, kuingia katika Mlima Wangu Sayuni, makazi Yangu, na kuishi pamoja kwa amani nami milele. Niliumba vitu vyote mwanzoni na Nitamaliza kazi Yangu mwishowe, na pia Nitatawala milele kama Mfalme. Katikati, pia Ninaongoza na kuutawala ulimwengu mzima. Hakuna anayeweza kuondoa mamlaka Yangu, kwani Mimi ni Mungu mmoja Mwenyewe, na pia Nina uwezo wa kupitisha mamlaka Yangu kwawazaliwa Wangu wa Kwanza, ili wazaliwa Wangu wa kwanza waweze kutawala kandokando Yangu.

Alhamisi, 25 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 100

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 100

Ninawachukia wale wote ambao hawajajaaliwa na kuchaguliwa na Mimi. Kwa hiyo ni lazima Niwafukuze watu hawa kutoka katika nyumba Yangu mmoja baada ya mwingine, hivyo hekalu Langu litakuwa takatifu na bila doa, nyumba Yangu itakuwa mpya daima na haitakuwa nzee kamwe, jina Langu takatifu litaenezwa milele na watu Wangu watakatifu watakuwa wapendwa Wangu. Aina hii ya mandhari, aina hii ya nyumba, aina hii ya ufalme ni lengo Langu, makao Yangu nayo ni msingi wa uumbaji Wangu wa vitu vyote. Hakuna mtu anayeweza kuyayumbisha au kuyabadilisha. Mimi mwenyewe na wana Wangu wapendwa tutaishi pamoja ndani yake na hakuna mtu atakayeruhusiwa kuyakanyaga, hakuna chochote kitakachoruhusiwa kuishi humo na hata zaidi hakuna kitu chochote kibaya kitakachoruhusiwa kutokea kamwe. Yote itakuwa sifa na kushangilia tu, yote yatakuwa mandhari ambayo mwanadamu hawezi kudhania.

Jumapili, 21 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 35

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 35

Nimeanza kutenda kazi Yangu kati ya wanadamu, kuwakubalia kuishi mkondo mmoja Nami. Nitakamilisha kazi Yangu nikiwa kati yao, maana wao ni vyombo Ninavyosimamia katika mpango Wangu wote wa usimamizi—na ni mapenzi Langu ili waweze kuwa watawala wa vitu vyote. Hivyo basi Naendelea kutembea kati ya wanadamu. Kadri wanadamu pamoja Nami tuingiavyo katika enzi ya sasa, Najihisi huru kabisa, kwa sababu, hatua Yangu ni ya haraka.

Ijumaa, 19 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Matamshi ya Mwenyezi Mungu Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Mimi Naeneza kazi Yangu katika nchi za Mataifa. Utukufu Wangu unamulika kotekote ulimwenguni; mapenzi Yangu yamo katika wanadamu yakitawanyika hapa na pale, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi ambayo Nimewapa. Kuanzia wakati huu kuendelea, Nimeingia katika enzi mpya, kuwaleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Niliporudi katika “nchi Yangu,” Nilianza sehemu nyingine tena ya kazi katika mpango Wangu wa asili, ili mwanadamu aje kunijua zaidi. Nauchukua ulimwengu katika ukamilifu wake na kuona kwamba[a] ni wakati muafaka wa kazi Yangu, kwa hiyo Naharakisha mbele na nyuma kufanya kazi Yangu mpya ndani ya mwanadamu. Hii ni enzi mpya, hata hivyo, na Nimeleta kazi mpya ili Niwachukue watu wapya wengi zaidi katika enzi mpya na kuachana na wengi wa wale Nitakaowaondoa.

Jumanne, 16 Aprili 2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu


“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu

3. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu

Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache. “Wateule wa Mungu” inarejelea nini?

Ijumaa, 12 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili


Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote

Namna Mungu alivyoshughulikia binadamu wote wa ujinga na kutojua ulitokana kimsingi na huruma na uvumilivu. Hasira yake, kwa upande mwingine, imefichwa kwenye wingi mkubwa mno wa muda na wa mambo; haijulikani kwa binadamu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati binadamu anakabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya kuvumilia na kusamehe binadamu—yaani, wakati onyesho la mwisho la Mungu la huruma na onyo Lake la mwisho linapowafikia—kama bado wangali wanatumia mbinu zile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali huruma Yake, Mungu hataweza tena kuwapatia uvumilivu na subira yake.

Ijumaa, 5 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III” Sehemu ya Pili


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Zaidi ya mwanadamu kutafuta kwa tamaa umaarufu na faida, daima anaendelea kutekeleza uchunguzi wa sayansi na utafiti wa kina, kisha bila kikomo huridhisha mahitaji yake ya mwili na tamaa; yapi tena ni matokeo ya mwanadamu? Kwanza kabisa hakuna tena usawa wa ikolojia na, pamoja na hili, miili ya wanadamu yote imetiwa doa na kuharibiwa na mazingira ya hali hii, na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na mapigo kusambaa kila mahali. Hii ni hali ambayo mwanadamu sasa hawezi kudhibiti, sivyo? Sasa kwa sababu mnaelewa hili, iwapo wanadamu hawamfuati Mungu, lakini daima wanamfuata Shetani kwa njia hii—kutumia maarifa daima kujitajirisha, kutumia sayansi kuchunguza bila kikomo siku za baadaye za maisha ya binadamu, kutumia mbinu ya aina hii kuendelea kuishi—mnaweza kutambua hitimisho ya asili ya wanadamu itakuwa vipi? Matokeo ya mwisho asilia yatakuwa yapi? Itakuwa uharibifu: kukaribia uharibifu hatua moja kwa wakati. Kukaribia uharibifu kwa hatua moja kwa wakati!”

Kujua zaidi: Swahili Gospel Praise Music "Kila Kitu Kinaishi Chini ya Sheria na Masharti Yaliyowekwa na Mungu". Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?



Jumanne, 26 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Tano


Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika moyo wa Nuhu na fahamu yake, uwepo wa Mungu ulikuwepo na bila shaka, na hivyo basi utiifu wake kwa Mungu ulikuwa haujatiwa doa wala toa na ungeweza kustahimili majaribio. Moyo wake ulikuwa safi na wazi kwa Mungu. Hakuhitaji maarifa ya mafundisho ya dini mengi mno ili kujishawishi kufuata kila neno la Mungu, wala hakuhitaji ukweli mwingi kuthibitisha uwepo wa Mungu, ili akubali kile Mungu alimwaminia na kuweza kufanya chochote kile ambacho Mungu angemruhusu kufanya.

Ijumaa, 22 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II" Sehemu ya Pili


Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II" Sehemu ya Pili

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Mungu Anawajali tu Wale Wanaoweza Kutii Maneno Yake Na Kufuata Amri Zake Mungu ni Mwenye Wingi wa Rehema Kwa Wale Anaowajali, na Mwenye Hasira Kali kwa Wale Anaowachukia na Kukataa Watu Wa Siku Za Mwisho Wanaiona tu Hasira Ya Mungu Katika Maneno Yake, na Hawaipitii kwa Kweli Hasira Ya Mungu

Jumatano, 20 Machi 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi MunguMaono ya Kazi ya Mungu (3)

    Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu. Ushuhuda wa wale waliomwamini Yeye ulitolewa kwa ajili ya Yesu Kristo, na kazi waliyoifanya walifanya pia kwa ajili ya Yesu Kristo.

Jumatano, 13 Machi 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Tatu”


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Tatu”
Dhamira Zangu kadhaa zimefichwa ndani ya matamshi ya sauti Yangu. Ila mwanadamu hajui na hafahamu chochote kuhusu haya, huku akiendelea kuyapokea na kuyafuata maneno Yangu kutoka nje, bila kung’amua roho Yangu na kuelewa mapenzi Yangu kutoka ndani ya maneno Yangu. Hata ingawa Nimeyaweka maneno Yangu wazi, kuna yeyote aliyeelewa? Nilitoka Sayuni Nikaja miongoni mwa wanadamu. Kwa sababu Nimejivisha ubinadamu wa mwanadamu wa kawaida na kujivika ngozi ya mwanadamu, wanadamu hulitambua umbo Langu tu kwa nje ila hawatambui uhai uliomo ndani Yangu, wala hawatambui Mungu Roho, wanajua tu mtu wa mwili.

Jumatatu, 4 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (4)


Mnapaswa kujua kuhusu hadithi ya ndani na uumbaji wa Biblia. Ufahamu huu haushikiliwi na wale ambao hawajakubali kazi mpya ya Mungu. Wao hawajui. Waelezee mambo haya ya kiini, na hawatakuwa pamoja nawe wenye kushikilia sana elimu ya vitabuni na sheria kuhusu Biblia. Wao huchunguza kwa uthabiti kile ambacho kimetabiriwa: Kauli hii imeshatimia? Kauli ile imeshatimia? Kukubali kwao injili ni kwa mujibu wa Biblia; wao huhubiri injili kulingana na Biblia. Wao huyategemea maneno ya Biblia kumwamini Mungu; bila Biblia, wao hawatamwamini Mungu. Hii ndiyo njia ambayo wao huishi, kuichunguza Biblia hivyo.

Alhamisi, 21 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Uzoefu


Katika uzoefu wote wa Petro, alikumbana na mamia ya majaribio. Ingawa watu wa leo wanafahamu neno “jaribio,” wao huchanganyikiwa kuhusiana na maana yake ya kweli na hali. Mungu hutuliza azimio la watu, husafisha imani yao, na hukamilisha kila sehemu yao—na hii hufanikishwa kimsingi kupitia majaribio, ambayo pia ni kazi ya Roho Mtakatifu iliyofichwa. Inaonekana kama kwamba Mungu amewaacha watu, na kwa hivyo wasipokuwa waangalifu, watayaona majaribio haya kama majaribu ya Shetani.

Jumatano, 13 Februari 2019

Filamu za Injili | “Siri ya Utauwa” (3) - Siri ya Kupata Mwili kwa Mungu


Filamu za Injili | “Siri ya Utauwa” (3) - Siri ya Kupata Mwili kwa Mungu


     Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili na akawa Bwana Yesu aliyekuja kuwakomboa wanadamu, na Mafarisayo wa Kiyahudi wakasema kwamba Bwana Yesu alikuwa mwanadamu tu. Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili na amekuwa Mwenyezi Mungu ambaye Amekuja kufanya kazi Yake ya hukumu, wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa kidini pia wanasema kwamba Mwenyezi Mungu ni mwanadamu tu, kwa hiyo tatizo ni lipi hapa? Kwa upande wa nje, Mungu mwenye mwili Anaonekana kuwa mtu wa kawaida. Lakini ndani Roho wa Mungu anaishi ndani Yake; Anaweza kuonyesha ukweli, kuonyesha sauti ya Mungu na kufanya kazi ya Mungu, kwa hiyo Mungu mwenye mwili ni mwanadamu, au ni Mungu?

Jumatano, 6 Februari 2019

Je, Kanisa la Mwenyezi Mungu Lina Malengo Yapi?

Je, Kanisa la Mwenyezi Mungu Lina Malengo Yapi?

     Kanisa la Mwenyezi Mungu hunyunyizia na kuwaongoza waumini wake kwa mujibu kamili wa maneno ya Mungu katika Biblia na Neno Laonekana Katika Mwili yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, ili kwamba kila muumini anaweza, chini ya uongozi, utolewaji, unyunyiziwaji, na uongozwaji wa maneno ya Mwenyezi Mungu, kuelewa ukweli wote katika maneno ya Mungu, kumiliki mtazamo sahihi juu ya maisha na maadili, kuwa na malengo sahihi ya kufuatilia, kufuata njia ya Mungu, kushikilia maagizo ya Mungu, kumtukuza Mungu kwa kuwa nuru na chumvi ya dunia, na kusifiwa na Mungu, na kuwa na sifa kamili kurithi ahadi za Mungu.