Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumjua-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumjua-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 17 Juni 2019

Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili


Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote.

Jumamosi, 18 Mei 2019

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”



Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu.

Jumamosi, 20 Aprili 2019

Wimbo wa Kuabudu | "Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee" | How to Know God


Wimbo wa Kuabudu | "Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee" | How to Know God
Mungu huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni za kipekee,
haidhibitiwi na watu, matukio au vitu.
au kumshawishi Ajaribu njia tofauti.
Na hakuna awezaye kubadili dhana au mawazo Yake,
Mungu huhuku matendo na mawazo yote ya viumbe kwa tabia Yake ya haki.
Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba! Tabia Yake ya haki!
Na hakuna awezaye kubadili rehema au ghadhabu Yake.
Na kulingana na hili, Hutoa ghadhabu au kupeana rehema. Na ni kiini Chake tu kiwezacho kuamua njia hii.
hakuna awezaye kiuka au kushuku hili.
Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba! Tabia Yake ya haki! Tabia ya haki ya Mungu, takatifu na ya kipekee;
Hii ni asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Hakuna awezaye kuimiliki, kiumbwacho au kisichoumbwa. Ghadhabu ya Mungu ni takatifu; haiwezi kukosewa. Rehema Yake pia yabeba asili hii. Tabia Yake ya haki!
Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Hakuna mbadala wa Mungu katika Matendo Yake, kiumbwacho au kisichoumbwa. Wala hawezi kuuharibu Sodoma au kuuokoa Ninawi kama alivyofanya Mungu. Tabia Yake ya haki! Tabia Yake ya haki!

 
kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?  Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu"

Jumatano, 17 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Kazi ya Mungu,kumjua mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

Kufahamu madhumuni ya kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mwanadamu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu.

Ijumaa, 12 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili


Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote

Namna Mungu alivyoshughulikia binadamu wote wa ujinga na kutojua ulitokana kimsingi na huruma na uvumilivu. Hasira yake, kwa upande mwingine, imefichwa kwenye wingi mkubwa mno wa muda na wa mambo; haijulikani kwa binadamu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati binadamu anakabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya kuvumilia na kusamehe binadamu—yaani, wakati onyesho la mwisho la Mungu la huruma na onyo Lake la mwisho linapowafikia—kama bado wangali wanatumia mbinu zile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali huruma Yake, Mungu hataweza tena kuwapatia uvumilivu na subira yake.

Alhamisi, 11 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Kwanza



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Kwanza



Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu
Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu. Kuhusiana na kumjua Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, sehemu ya kwanza tuliyoijadili ni ipi? (Mamlaka ya Mungu.) Ya pili ilikuwa ni ipi? (Tabia ya haki ya Mungu.) Na ya tatu? (Utakatifu wa Mungu.) Tumejadili mara ngapi kuhusu mamlaka ya Mungu?

Jumatano, 10 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)” Sehemu ya Nne
Mwenyezi Mungu anasema, “Kuelewa kiini cha Mungu na kujua kiini cha Mungu kinapeana msaada usioweza kupimika kwa kuingia kwa watu katika maisha. Natumai kwamba hamtapuuza haya ama kuyaona kama mchezo; kwa sababu kumjua Mungu ni msingi muhimu na msingi wa imani ya mwanadamu kwa Mungu na ufuatiliaji wa mwanadamu wa ukweli na wokovu na kitu ambacho hakifai kuachiliwa. Iwapo mwanadamu anamwamini Mungu lakini hamjui Mungu, na iwapo mwanadamu anaishi miongoni mwa baadhi ya barua na mafundisho ya kidini, hutawahi kufikia wokovu hata kama utatenda na kuishi kulingana na maana ya juujuu ya ukweli. Hiyo ni kusema, iwapo imani yako kwa Mungu haitokani na kumjua, basi imani yako haimaanishi chochote.”

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Kujua zaidi:  Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? . Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu

Jumanne, 9 Aprili 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"

Mwenyezi Mungu anasema, “Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu. Yeye huonyesha moyo wa ndani zaidi wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na kuleta mbingu na nchi mpya na kazi mpya, na ametuletea matumaini, akimaliza maisha ambayo tuliishi katika hali isiyo dhahiri, na kuwezesha nafsi yetu nzima kuona njia ya wokovu kwa udhahiri kamili. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zimepata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, huyu si ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, tukiwa tumeamka au kuota, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu! Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ametuwezesha kuishi tena na kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele.”
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumamosi, 6 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza


Kwanza, hebu tuuimbe wimbo wa kumsifu Mungu: Wimbo wa Ufalme (I) Ufalme Umeshuka katika Ulimwengu.
Kiambata: Watu wanamshangilia Mungu, watu wanamsifu Mungu; vinywa vyote vinamwita Mungu mmoja wa kweli. Mfalme unashuka ulimwenguni.
I. Watu wanamshangilia Mungu, watu wanamsifu Mungu; vinywa vyote vinamwita Mungu mmoja wa kweli, watu wote wanainua macho yao kuyatazama matendo ya Mungu. Ufalme unashuka ulimwenguni, nafsi ya Mungu yu tajiri na mwenye ukarimu, tajiri na mwenye ukarimu. Ni nani ambaye hangeshangilia kwa ajili ya haya? (Ni nani ambaye hangeshangilia kwa ajili ya haya?) (Ni nani ambaye hangecheza kwa furaha kwa ajili ya haya?) Oo, Zayuni! (Oo, Zayuni!) Oo, Zayuni! (Oo, Zayuni!) Inua bango lako la shangwe ili kusherehekea Mungu! Imba wimbo wako wa shangwe wa ushindi na kueneza jina takatifu la Mungu!
II. Mambo yote duniani! Sasa jitakaseni kwa haraka katika kutoa sadaka kwa Mungu, katika kutoa sadaka kwa Mungu! Nyota kule mbinguni! Sasa rudini mahali penu na kuonyesha ukuu wa Mungu katika mbingu! Mungu hushughulikia sauti ya watu duniani nchini, wanaomwaga upendo usio na mwisho na heshima kwa Mungu kwenye nyimbo! Kwenye siku hii, viumbe vyote vinarudia ujana, Mungu anakuja kutembea. Wakati huu, maua hunawiri, ndege kuimba, viumbe vyote hujaa shangwe! Ndege wanaimba, viumbe vyote hujaa shangwe! Kusikikapo mlio wa saluti ya ufalme, ufalme wa Shetani ukiangamizwa chini ya kiitikio kinachovuma cha nyimbo za ufalme. Na hautawahi kuinuka tena!
III. Ni nani ulimwenguni anayethubutu kuinuka na kupinga? Mungu hushuka duniani, Mungu huleta moto, huleta hasira, huleta majanga yote, majanga yote. Falme za ulimwengu sasa ni, sasa ni ufalme wa Mungu! Juu mbinguni, mawingu yanagaagaa na kujongea kama wimbi; chini ya mbingu (chini ya mbingu), chini ya mbingu (chini ya mbingu), maji maziwani na mitoni yanabingirika na kutoa tuni ya kusisimua. Wanyama waliokuwa mapumzikoni wanajitokeza kutoka kwenye mapango yao, na watu wote waliokuwa wamelala wanaamshwa na Mungu. Siku iliyosubiriwa na kila mmoja hatimaye imewadia, hatimaye imewadia! Wanatoa nyimbo nzuri kabisa, nyimbo nzuri kabisa, kwa Mungu! Kwa Mungu! Kwa Mungu!
Ni nini mnachofikiria kuhusu kila wakati mnapouimba wimbo huu? (Ukiwa umechangamka; nasisimkwa; nafikiria namna ambavyo utukufu wa ufalme ulivyo mrembo, na mwanadamu na Mungu wataunganishwa daima dawamu.) Je, yupo yeyote aliyefikiria kuhusu umbo ambalo binadamu lazima achukue ili kuweza kuwa na Mungu? Katika kufikiria kwenu, mtu anafaa kuwa vipi ili kuweza kujiunga na Mungu na kufurahia maisha yenye utukufu yanayofuata katika ufalme? (Wanafaa kuwa wamebadilisha tabia.) Wanafaa kuwa wamebadilisha tabia, lakini kubadilisha hadi kiwango gani? Watakuwa vipi baada ya kubadilishwa tabia? (Watakuwa watakatifu.) Ni nini kipimo cha utakatifu? (Fikira na utiliaji maanani wao wote unalingana na Kristo.) Sasa ni vipi ambavyo hali hii ya kuingiliana inavyojionyesha? (Hawamzuii Mungu, wala kumsaliti Mungu, lakini wanajitolea kuwa wenye utiifu kabisa kwa Mungu na kumcha Mungu katika mioyo yao.) Baadhi ya majibu yenu yako katika njia sawa. Fungueni mioyo yenu, nyinyi nyote, na msemezane kile ambacho mioyo yenu inawaambia. (Watu wanaoishi na Mungu katika ufalme wanaweza kutekeleza wajibu wao, kutekeleza kwa uaminifu wajibu wao, kwa kutafuta ukweli na kutozuiliwa na mtu yeyote, hafla yoyote, au kifaa chochote. Na inawezekana kujiondoa kwenye ushawishi wa giza na kulinganisha mioyo yao na Mungu, na kumcha Mungu na kujiepusha na uovu.) (Mtazamo wetu wa kuangalia mambo unaweza kulinganishwa na ule wa Mungu, na tunaweza kujitenga na ushawishi wa giza. Kiwango cha chini zaidi ni kutotumiwa vibaya na Shetani, kutupa nje tabia yoyote ya upotoshaji, na kutimiza utiifu wa Mungu. Tunasadiki kwamba kuwa huru dhidi ya ushawishi wa giza ndiyo hoja kuu. Kama mtu hawezi kujitenga na ushawishi wa giza, hawezi kujipa uhuru kutoka kwenye minyororo ya Shetani, basi hajapata wokovu wa Mungu.) (Kiwango cha kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu ni binadamu akiwa na moyo mmoja na akili na Mungu. Binadamu hamzuii Mungu tena; anaweza kujua Mungu mwenyewe, kuweka ukweli katika matendo, kupata uelewa wa Mungu, kumpenda Mungu, na kulingana na Mungu. Hayo ndiyo yote ambayo mtu anahitaji kufanya.)
Uzito wa Matokeo katika Mioyo ya Watu
Yaonekana mnavyo vitu katika mioyo yenu kuhusu njia mnayofaa kutembea na mmeimarisha uelewa na ung’amuzi mzuri kuhusu vitu hivyo. Lakini kama kila kitu mlichokisema kitaishia kuwa maneno matupu au uhalisia halisi inategemea ni nini mnatilia maanani katika mazoea yako ya kila siku. Mmepata mavuno kutoka kwenye dhana zote za ukweli kupitia miaka hii, kwenye falsafa na kwenye maudhui ya ukweli. Hii inathibitisha kwamba watu siku hizi wanatilia mkazo kule kutafuta ukweli. Na kutokana na hayo, kila dhana na kila kipengele cha ukweli kwa hakika kimeweka mizizi kwenye mioyo ya baadhi ya watu. Hata hivyo, ni nini hasa Ninachoogopa sana? Kwamba ingawa wahusika wa ukweli, na nadharia hizi, yameweza kunakili mizizi yao, maudhui halisi bado hayana uzito mkubwa katika mioyo yenu. Wakati mnapokumbana na masuala, mnapopitia majaribio, mnapopitia chaguo—mtaweza kwa kiwango kipi kutumia uhalisia wa ukweli huu vizuri? Je, haya yote yatawasaidia kupitia kwenye ugumu wenu na kuwafanya kuibuka kutoka kwenye majaribio yenu baada ya kutosheleza nia za Mungu? Je, mtasimama imara katika majaribio yenu na kushuhudia kwa sauti na waziwazi kwake Mungu? Je, mmewahi kuwa na kivutio katika masuala haya awali? Mniruhusu kuuliza: Katika mioyo yenu, kwenye fikira na tafakari zenu za kila siku, ni nini hicho ambacho ni muhimu sana kwenu? Mmewahi kuja kwenye hitimisho? Ni nini mnachosadiki kuwa kitu muhimu zaidi? Baadhi ya watu husema “ni kuweka ukweli katika matendo, bila shaka”; baadhi ya watu husema “bila shaka ni kulisoma neno la Mungu kila siku”; baadhi ya watu husema “ni kujiweka mbele ya Mungu na kuomba Mungu kila siku, bila shaka”; na kisha kunao wale wanaosema “bila shaka ni kutekeleza wajibu wangu kwa njia bora kila siku”; kunao baadhi ya watu pia ambao wanasema wanafikiria wakati wote tu kuhusu namna ya kumtosheleza Mungu, namna ya kumtii Yeye katika mambo yote, na namna ya kuchukua hatua kulingana na mapenzi Yake. Je, hivi ndivyo ilivyo? Je, hivi ndivyo kila kitu kinavyohitajika kufanywa? Kwa mfano, kunao baadhi wanaosema: “Mimi ninataka tu kumtii Mungu, lakini kitu kinapofanyika siwezi kumtii Yeye.” Baadhi ya watu husema: “Nataka tu kumtosheleza Mungu. Hata kama ningemtosheleza Yeye mara moja tu, hilo lingetosha, lakini sitoweza kumtosheleza Yeye.” Na baadhi ya watu husema: “Ninataka tu kumtii Mungu. Katika nyakati za majaribio nataka kunyenyekea katika mipango Yake, huku nikitii ukuu na mipangilio Yake, bila ya malalamiko au maombi yoyote. Ilhali karibu kila wakati ninashindwa kuwa mtiifu.” Baadhi ya watu wengine husema: “Ninapokabiliwa na uamuzi, siwezi kamwe kutia ukweli katika matendo. Siku zote nataka kutosheleza mwili, siku zote nataka kutosheleza matamanio yangu ya kibinafsi ninayojitakia.” Ni nini sababu ya haya? Kabla ya jaribio la Mungu kufika, je, mmewahi kujipa changamoto nyinyi wenyewe mara nyingi, na kujijaribu nyinyi wenyewe mara nyingi? Oneni kama kweli mnaweza kumtii Mungu, kuweza kwa kweli kumtosheleza Mungu, na kuwa na hakika kutomsaliti Mungu. Tazameni kama hamwezi kujitosheleza, kutojitosheleza matamanio yenu ya kibinafsi, lakini kumtosheleza Mungu tu, bila ya chaguo lenu la kibinafsi. Je, yupo aliye hivi? Kwa hakika, kunayo hoja moja tu ambayo imewekwa mbele ya macho yenu nyinyi wenyewe. Ni kile ambacho kila mmoja wenu anavutiwa nacho, kile ambacho mnachotaka kujua zaidi, na hilo ni suala la matokeo na hatima ya kila mmoja wenu. Huenda msitambue, lakini hili ni jambo ambalo hakuna anayeweza kulikataa. Ninajua kwamba kunao baadhi ya watu ambao, tunapokuja katika ukweli wa matokeo ya binadamu, ahadi ya Mungu kwa ubinadamu, na aina gani ya hatima ambayo Mungu ananuia kumleta binadamu katika, tayari wamefanyia uchunguzi neno la Mungu katika masuala haya mara kadhaa. Kisha kunao ambao kila mara wanalitafuta na kulifikiria kwenye akili zao, na bado hawapati matokeo, au pengine wanafikia katika hitimisho fulani isiyoeleweka. Hatimaye bado hawana hakika kuhusu ni aina gani ya matokeo yanayowasubiri. Wakati wa kuyakubali mawasiliano ya ukweli, wakati wa kuyakubali maisha ya kanisa, wakati wa kutenda wajibu wao, baadhi ya watu siku zote wanataka kujua jibu wazi kwa maswali yafuatayo: Matokeo yangu yatakuwa yapi? Ninaweza kutembelea njia hii hadi mwisho wake? Mwelekeo wa Mungu kwake binadamu ni upi? Baadhi ya watu huwa hata na wasiwasi: Nimefanya baadhi ya mambo siku zilizopita, nimesema baadhi ya mambo, sikumtii Mungu, nimefanya mambo fulani ambayo yamemsaliti Mungu, kulikuwa na masuala fulani ambapo sikumtosheleza Mungu, niliuumiza moyo wa Mungu, nilimfanya Mungu kunikasirikia, nilimfanya Mungu kunichukia na kuniona kwamba ninachukiza, hivyo basi pengine matokeo yangu hayajulikani. Ni haki kusema kwamba watu wengi zaidi wanahisi wasiwasi kuhusu matokeo yao wenyewe. Hakuna anayethubutu kusema: “Nahisi kwa uhakika wa asilimia mia moja kwamba nitaishi Ninao uhakika wa asilimia mia moja kwamba ninaweza kuzitosheleza nia za Mungu; mimi ni mtu anayefuata moyo wa Mungu; mimi ni mtu anayesifiwa na Mungu.” Baadhi ya watu hufikiria ni vigumu hasa kufuata njia ya Mungu, na kwamba kutia ukweli katika matendo ndilo jambo gumu zaidi la kufanya. Kwa hivyo, watu hawa hufikiria hawawezi kusaidika, na hawathubutu kuwa na matumaini ya kuwa na matokeo mazuri. Au pengine wanasadiki kwamba hawawezi kutosheleza nia za Mungu, na kuweza kuishi; na kwa sababu ya haya watasema kwamba hawana matokeo, na hawawezi kufikia hatima nzuri. Licha ya jinsi watu hufikiria, kila mmoja anastaajabu kuhusu matokeo yao mara nyingi. Kuhusu masuala ya siku zao za usoni, kuhusu maswali ya kile watakachopata wakati Mungu atakapomaliza kazi Yake, watu hawa siku zote wanapiga hesabu, siku zote wanapanga. Baadhi ya watu wanalipia bei mara dufu; baadhi ya watu wanaacha familia zao na kazi zao; baadhi ya watu wanakata tamaa katika ndoa zao; baadhi ya watu wanakubali bila kulalamika kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu; baadhi ya watu huacha nyumba zao ili kutenda wajibu wao; baadhi ya watu huchagua ugumu, na kuanza kufanya kazi ambazo ni chungu zaidi na zinachosha zaidi; baadhi ya watu huchagua kuutoa utajiri wao, kujitolea kila kitu chao; na bado baadhi ya watu huchagua kufuata ukweli na kufuatilia kumjua Mungu. Haijalishi namna mnavyochagua kutenda, namna mnavyotenda ndiyo muhimu zaidi? (Si muhimu.) Ni vipi tunavyoelezea kwamba si muhimu, basi? Kama namna hiyo si muhimu, basi ni nini muhimu? (Tabia nzuri kwa nje si wakilishi wa kutia ukweli katika matendo.) (Kile ambacho kila mmoja anafikiria si muhimu. Cha msingi hapa ni kama tumeweza kutia ukweli katika matendo, na kama tunampenda Mungu.) (Maangamizi ya wapinga Kristo na viongozi bandia hutusaidia kuelewa kwamba tabia ya nje si jambo muhimu zaidi. Kwa nje wanaonekana kuwa wamejinyima mengi, na wanaonekana kuwa radhi kulipa bei, lakini kwa kuchambua tunaweza kuona kwamba hawana moyo kabisa unaomcha Mungu; kwa mitazamo yote wanampinga Yeye. Siku zote wanasimama pamoja na Shetani katika nyakati za hatari, na kuingilia kazi ya Mungu. Hivyo basi, utiliaji maanani mkuu hapa ni upande gani tutasimama wakati ukiwadia, na mitazamo yetu.) Nyote mnaongea vyema, na yaonekana kwamba tayari mnao msingi wa uelewa wa na kiwango cha kuweza kutia ukweli wenu katika matendo, nia za Mungu, na kile Mungu anahitaji kutoka kwa binadamu. Kwamba mnaweza kuongea hivi ni jambo la kugusa kweli. Ingawa kuna maneno machache yasiyofaa hapa na pale, kauli zenu tayari zinakaribia ufafanuzi unaostahili ukweli Hii inathibitisha kwamba mmeimarisha uelewa wenu halisi wa watu matukio, na vifaa vilivyo karibu nanyi, mazingira yenu yote ambayo Mungu amepanga, na kila kitu mnachoweza kuona. Uelewa huu unakaribia ukweli. Hata ingawa kile mnachosema si pana kabisa, na maneno machache hayafai sana, uelewa wenu tayari unakaribia uhalisi wa ukweli. Kuwasikiliza mkiongea kwa njia hii kunanifanya Mimi kuhisi vizuri sana.
Imani za Watu Haziwezi Kubadilishwa na Ukweli
Kunao baadhi ya watu wanaoweza kuvumilia ugumu; wanaweza kulipia bei; tabia yao ya nje ni nzuri sana; wanaheshimika sana; na wanatamaniwa na wengine. Mnafikiria nini: Je, tabia kama hii ya nje inaweza kuchukuliwa kama ya kutia ukweli katika matendo? Mnaweza kusema kwamba mtu huyu anatosheleza nia za Mungu? Kwa nini mara kwa mara watu wanamwona mtu wa aina hii na kufikiria kwamba wao wanamtosheleza Mungu, wanafikiria kwamba wanatembelea njia ile ya kutia ukweli katika matendo, kwamba wanatembea katika njia ya Mungu? Kwa nini baadhi ya watu hufikiria kwa njia hii? Upo ufafanuzi mmoja tu kwa haya. Na ufafanuzi huu ni upi? Sababu ni kwamba kwa kiasi kikubwa cha watu, maswali kama kutia ukweli katika matendo ni nini, kutosheleza Mungu ni nini, ni nini kuwa na uhalisia wa ukweli—maswali haya hayako wazi sana. Hivyo basi kunao baadhi ya watu ambao mara nyingi wanadanganywa na wale ambao kwa nje wanaonekana wa kiroho, wanaonekana wa kilodi, wanaonekana kuwa na taswira za ukuu. Kuhusiana na watu hao wanaoweza kuzungumzia barua na falsafa, na ambao hotuba na vitendo vyao vinaonekana kuwa vyenye kustahili uvutiwaji, wale wanaowatamani hawajawahi kuangalia kiini halisi cha vitendo vyao, kanuni zinazoendesha vitendo vyao, shabaha zao ni nini. Na hawajawahi kuangalia kama watu hawa wanatii Mungu kwa kweli, na kama wao ni watu wanaomcha Mungu kwa kweli na kujiepusha na uovu au la. Hawajawahi kutambua kile kiini halisi cha ubinadamu cha watu hawa. Badala yake, kutoka kwenye hatua ya kwanza ya kujua na kuzoeana nao, hatua kwa hatua wanaanza kuwapenda watu hawa, kuwatukuza watu hawa, na hatimaye watu hawa wanakuwa sanamu zao. Aidha, katika akili za baadhi ya watu, sanamu hizi wanazoziabudu, wanaosadiki wanaweza kuacha familia na kazi zao, na kulipa ile bei kwa juujuu—sanamu hizi ndizo ambazo kwa kweli zinatosheleza Mungu, ndizo zile zinazoweza kupokea kwa kweli matokeo mazuri na hatima nzuri. Katika akili zao, sanamu hizi ndizo wale watu ambao Mungu husifu. Ni nini husababisha watu kuwa na aina hii ya kusadiki? Ni nini kiini halisi cha suala hili? Ni nini matokeo hali hii inaweza kuleta? Hebu na tuzungumzie kwanza suala la kiini chake halisi.
Masuala haya kuhusiana na mitazamo ya watu, vitendo vya watu, ni kanuni gani ambazo watu wanachagua kutenda, na kile ambacho kwa kawaida kila mtu anatilia mkazo, kimsingi haya yote hayahusu mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu hata kidogo. Bila kujali kama watu wanazingatia masuala ya juujuu au yale ya kina, wanazingatia barua na falsafa au uhalisia, watu hawatii yale ambayo wanafaa kutii zaidi, na hawajui kile wanachofaa kujua zaidi. Sababu ya hali hii kuwa hivi ni kwamba watu hawaupendi ukweli kamwe. Hivyo basi, watu hawako radhi kutumia muda na jitihada zao katika kutafuta na kuendeleza kanuni katika neno la Mungu. Badala yake, wanapendelea kutumia njia za mkato, na kujumlisha kile wanachoelewa, kile wanachojua, kuwa vitendo vizuri na tabia nzuri. Muhtasari huu nao huwa shabaha yao ya binafsi ya kufuata, unakuwa ukweli wa kutendwa. Athari ya moja kwa moja ya haya yote ni kwamba watu wanatumia tabia nzuri ya kibinadamu kama kisawazisho cha kutia ukweli katika matendo yao, hali ambayo inatosheleza pia matamanio ya watu ili kupata fadhila na Mungu. Hii inawapa watu mtaji wa kushindania ukweli na kutoa sababu ili kumshawishi Mungu na kuingia katika mzozo Naye. Wakati uo huo, watu wanamweka Mungu kando kwa njia za ufidhuli, na kuiweka ile sanamu ya mioyo yao katika nafasi ya Mungu. Kunayo sababu moja tu ya chanzo cha haya ambayo huwafanya watu kuwa na vitendo wasivyovijua, mitazamo wasiyoijua, au mitazamo na vitendo vya upande mmoja, na leo Nitawaelezea kuhusu haya. Sababu ni kwamba ingawa watu wengi wanaweza kumfuata Mungu, kumwomba Yeye kila siku, na kusoma neno la Mungu kila siku, hawaelewi kwa hakika nia za Mungu. Hiki ndicho chanzo cha tatizo. Kama mtu huelewa moyo wa Mungu, huelewa kile anachopenda Mungu, kile humchukiza Mungu, kile anachotaka Mungu, kile anachokataa Mungu, ni mtu wa aina gani ambaye Mungu humpenda, ni mtu wa aina gani ambaye Mungu hampendi, ni kiwango kipi ambacho Mungu hutumia katika kutoa mahitaji Yake kwa binadamu, ni mtazamo gani ambao Anauchukua katika kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, je, mtu huyu anaweza bado kuwa na mawazo yake ya kibinafsi? Wanaweza tu kuenda na kumwabudu mtu mwingine? Mtu wa kawaida anaweza kuwa sanamu yao? Kama mtu anaelewa nia za Mungu, mtazamo wake ni wenye kirazini zaidi kuliko hapo. Hawatamwabudu kama Mungu kiongozi aliyepotoka kiholela, wala hawataweza, huku wakitembea njia ya kutia ukweli katika matendo, kusadiki kwamba kutii kiholela katika sheria au kanuni chache rahisi ni sawa na kutia ukweli katika matendo.
Kunayo Maoni Mengi Yanayohusu Kiwango Ambacho Mungu Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu

Hebu na turudi katika mada hii na tuendelee kuzungumzia suala la matokeo.
Kwa sababu kila mmoja anajali matokeo yake, je, mnajua namna ambavyo Mungu huamua matokeo hayo? Na ni kwa njia gani ambayo Mungu huanzisha matokeo ya mtu? Na ni kiwango gani ambacho Mungu hutumia kuasisi matokeo ya mtu? Na wakati ambapo matokeo ya mtu yangali bado hayajaasisiwa, ni nini anachofanya Mungu ili kufichua matokeo haya? Je, yupo anayejua haya? Kama Nilivyosema tu, kunao baadhi ambao tayari wamefanyia uchunguzi neno la Mungu kitambo sana. Watu hao wanatafuta dalili fulani kuhusu matokeo ya mwanadamu, kuhusu kategoria ambazo matokeo haya yamegawanywa, na kuhusu matokeo tofauti yanayosubiria aina tofauti ya watu. Wanataka pia kujua namna neno la Mungu linavyoanzisha matokeo ya binadamu, aina za kiwango ambacho Mungu hutumia, na njia ambayo Yeye huasisi matokeo ya binadamu. Ilhali mwishowe watu hawa hawafanikiwi kupata chochote. Kwa hakika, yapo mambo machache yenye thamani yanayozungumzwa kuhusu suala hili miongoni mwa neno la Mungu. Kwa nini hali iko hivi? Ili mradi matokeo ya binadamu yangali hayajafichuliwa, Mungu hataki kumwambia yeyote kuhusu kile kitakachofanyika mwishowe, wala Hataki kumfahamisha yeyote kuhusu hatima yao kabla ya wakati kufika. Sababu ya kufanya hivi ni kwamba Mungu kufanya hivyo hakutaleta manufaa yoyote kwa binadamu. Sasa hivi, Nataka kuwaambia tu kuhusu namna Mungu huasisi matokeo ya binadamu, kuhusu kanuni Anazotumia katika kazi Yake ili kuyaasisi matokeo ya binadamu, na kuonyesha matokeo haya, pamoja na kiwango Anachotumia ili kuanzisha kama mtu ataweza kuishi au la. Hiki sicho kile ambacho mnajali zaidi kuhusu? Hivyo basi, ni vipi ambavyo watu hufahamu njia ambayo Mungu anaanzisha matokeo ya binadamu? Mlizungumzia kidogo kuhusu suala hili muda mfupi uliopita. Baadhi yenu mlisema kwamba ni swali la kutenda wajibu wao kwa uaminifu, kugharamika kwa ajili ya Mungu; baadhi ya watu walisema kumtii Mungu na kutosheleza Mungu; baadhi ya watu walisema kudhibitiwa na Mungu; na baadhi ya watu walisema kuishi maisha ya hadhi ya chini…. Wakati mnapotia ukweli huu katika matendo, wakati mnapotenda kanuni za kufikiria kwenu, je mnajua kile Mungu anachofikiria? Mmewahi kufikiria kama kuendelea hivi ni kutosheleza nia za Mungu au la? Kama kunatilia maanani kiwango cha Mungu? Kama kunatilia maanani mahitaji ya Mungu? Ninasadiki kwamba watu wengi zaidi hawalifikirii suala hili kwa undani. Wanatumia tu bila kutilia maanani sehemu ya neno la Mungu, au sehemu ya mahubiri, au viwango vya watu fulani wa kiroho ambao wanawaabudu, na kujilazimisha kufanya hivi na vile. Wanasadiki kwamba hii ndiyo njia sahihi, na hivyo basi wanaendelea kuitii, kuifanya, liwalo liwe hatimaye. Baadhi ya watu hufikiria: “Nimesadiki kwa miaka mingi siku zote nimetenda mambo kwa njia hii; nahisi kuwa nimemtosheleza kabisa Mungu; ninahisi pia kuwa nimejifunza mengi kutoka kwa haya. Kwani nimekwishaelewa ukweli mwingi katika kipindi hiki, na nimeelewa mambo mengi ambayo sikuyaelewa awali—hasa, wingi wa fikira na mitazamo yangu imebadilika, maadili ya maisha yangu yamebadilika sana, na ninao uelewa mzuri sana wa ulimwengu huu.” Watu kama hao wanasadiki kwamba haya ni mavuno, na ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi ya Mungu kwa binadamu. Kwa maoni yenu, kwa viwango hivi na vitendo vyenu nyote vimewekwa pamoja—je, mnatosheleza nia za Mungu? Baadhi ya watu watasema kwa uhakika wote: “Bila shaka! Tunatenda kulingana na neno la Mungu; tunatenda kulingana na kile ambacho ndugu alihubiri na kushiriki nasi; siku zote tunafanya wajibu wetu, siku zote tunamfuata Mungu, hatujawahi kumwacha Mungu. Hivyo basi tunaweza kusema kwa imani kamili kwamba tunamtosheleza Mungu. Haijalishi ni kiasi kipi tunachoelewa kuhusu nia za Mungu, haijalishi ni vipi tunavyoelewa neno la Mungu, siku zote tumekuwa kwa njia ya kutafuta kuweza kutangamana na Mungu. Kama tutachukua hatua kwa usahihi, na kutenda kwa usahihi, basi matokeo yatakuwa sahihi.” Je, mnafikiria nini kuhusu mtazamo huu? Je, ni kweli? Pengine wapo wale wanaosema: “Sijawahi kufikiria kuhusu mambo haya awali. Mimi nafikiria tu kwamba nikiendelea kutimiza wajibu wangu na kuendelea kutenda kulingana na mahitaji ya neno la Mungu, basi nitasalia. Sijawahi kufikiria swali la kama ninaweza kutosheleza moyo wa Mungu, na sijawahi kufikiria kama ninatimiza kiwango kinachohitajika na Yeye. Kwa sababu Mungu hajawahi kuniambia, wala kunipatia maagizo yoyote kwa uwazi, ninasadiki kwamba mradi tu niendelee kupiga hatua mbele, Mungu atatosheka na Yeye hafai kuwa na mahitaji yoyote ya ziada kwangu mimi.” Je, kusadiki huku ni sahihi? Kulingana na Ninavyojua, njia hii ya kutenda, njia hii ya kufikiria, na mitazamo hii—yote yanakuja na madoido fulani na kiasi kidogo cha upofu. Ninaposema hivi, pengine wapo baadhi yenu mnaohisi kuvunjika moyo: “Yaani upofu? Kama ni ‘upofu,’ basi tumaini letu la wokovu, tumaini letu la kuishini dogo mno, na halina uhakika, hapo ni kweli? Je, wewe kulitamka hivyo lilivyo si sawa na kutumwagilia maji baridi?” Haijalishi kile mnachosadiki, mambo Ninayoyasema na kufanya hayanuii kukufanya ninyi kuhisi kama mnamwagiliwa maji baridi. Badala yake, yananuia kuboresha uelewa wenu wa nia za Mungu, na kuboresha ung’amuzi wenu kuhusu kile ambacho Mungu anafikiria, kile ambacho Mungu anataka kukamilisha ni mtu wa aina gani ambaye Mungu anapenda, nini kinachukiza Mungu, nini Mungu anadharau, ni mtu wa aina gani ambaye Mungu anataka kumpata, na ni mtu wa aina gani ambaye Mungu anatupilia mbali. Yananuia kupatia akili zenu uwazi, kuwasaidia kujua wazi ni kiwango kipi vitendo na fikira za kila mmoja wenu yamepotea kutoka kwa kiwango kinachohitajika na Mungu. Je, inahitajika kuzungumzia mada hii? Kwa sababu Ninajua mmesadiki kwa muda mrefu, na mmesikiliza mahubiri mengi, lakini kwa hakika haya ndiyo mambo yanayokosekana zaidi. Mmerekodi kila ukweli katika daftari zenu, mmerekodi pia kile ambacho nyie wenyewe mnasadiki kibinafsi kuwa muhimu katika akili zenu na katika mioyo yenu. Na mnapanga kukitumia kumridhisha Mungu mnapotenda, kukitumia wakati mnahitaji usaidizi, au kukitumia kupitia nyakati ngumu zilizo mbele yenu, au mnaacha ukweli huu uandamane na ninyi mnapoishi maisha yenu tu. Lakini kulingana na Ninavyojua, iwapo mnatenda tu, namna mnavyotenda hasa si muhimu. Nini, basi, ndicho kitu cha muhimu sana? Ni kwamba wakati unatenda, moyo wako hujua kwa uhakika wote kama kila kitu unachofanya, kila kitendo, ndicho kile anachotaka Mungu au la; kama kila kitu unachofanya ni sahihi au la, kila kitu unachofikiria ni sahihi au la, na matokeo na shabaha katika moyo wako yanatosheleza nia za Mungu au la, kama yanatilia maanani mahitaji ya Mungu au la, na kama Mungu anayaidhinisha au la. Haya ni mambo muhimu.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Matamshi ya Mungu | "Unajua Nini Kuhusu Imani?

Ijumaa, 5 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III” Sehemu ya Pili


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Zaidi ya mwanadamu kutafuta kwa tamaa umaarufu na faida, daima anaendelea kutekeleza uchunguzi wa sayansi na utafiti wa kina, kisha bila kikomo huridhisha mahitaji yake ya mwili na tamaa; yapi tena ni matokeo ya mwanadamu? Kwanza kabisa hakuna tena usawa wa ikolojia na, pamoja na hili, miili ya wanadamu yote imetiwa doa na kuharibiwa na mazingira ya hali hii, na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na mapigo kusambaa kila mahali. Hii ni hali ambayo mwanadamu sasa hawezi kudhibiti, sivyo? Sasa kwa sababu mnaelewa hili, iwapo wanadamu hawamfuati Mungu, lakini daima wanamfuata Shetani kwa njia hii—kutumia maarifa daima kujitajirisha, kutumia sayansi kuchunguza bila kikomo siku za baadaye za maisha ya binadamu, kutumia mbinu ya aina hii kuendelea kuishi—mnaweza kutambua hitimisho ya asili ya wanadamu itakuwa vipi? Matokeo ya mwisho asilia yatakuwa yapi? Itakuwa uharibifu: kukaribia uharibifu hatua moja kwa wakati. Kukaribia uharibifu kwa hatua moja kwa wakati!”

Kujua zaidi: Swahili Gospel Praise Music "Kila Kitu Kinaishi Chini ya Sheria na Masharti Yaliyowekwa na Mungu". Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?



Ijumaa, 29 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza

Kwanza, hebu tuuimbe wimbo wa kumsifu Mungu: Wimbo wa Ufalme (I) Ufalme Umeshuka katika Ulimwengu. 
 Kiambata: Watu wanamshangilia Mungu, watu wanamsifu Mungu; vinywa vyote vinamwita Mungu mmoja wa kweli. Mfalme unashuka ulimwenguni. 

 I. Watu wanamshangilia Mungu, watu wanamsifu Mungu; vinywa vyote vinamwita Mungu mmoja wa kweli, watu wote wanainua macho yao kuyatazama matendo ya Mungu. Ufalme unashuka ulimwenguni, nafsi ya Mungu yu tajiri na mwenye ukarimu, tajiri na mwenye ukarimu. Ni nani ambaye hangeshangilia kwa ajili ya haya? (Ni nani ambaye hangeshangilia kwa ajili ya haya?) (Ni nani ambaye hangecheza kwa furaha kwa ajili ya haya?) Oo, Zayuni! (Oo, Zayuni!) Oo, Zayuni! (Oo, Zayuni!) Inua bango lako la shangwe ili kusherehekea Mungu! Imba wimbo wako wa shangwe wa ushindi na kueneza jina takatifu la Mungu!

Jumamosi, 2 Machi 2019

Neno la Mungu | Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu


Neno la Mungu | Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu


    Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu.

Alhamisi, 28 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 8


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 8

 Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa Roho, sauti Yake huelekezwa kwa wanadamu wote. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa mwanadamu, sauti Yake huelekezwa kwa wote wafuatao uongozi wa Roho Wake. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu (kile ambacho watu hutaja kama mtazamaji), Anaonyesha neno Lake moja kwa moja kwa watu ili watu wamwone kama mtoa maoni, na huonekana kwamba kutoka kinywani Mwake hutoka mambo yasiyo na kikomo ambayo mwanadamu hayajui, mambo ambayo mwanadamu hawezi kuelewa.

Jumapili, 10 Februari 2019

Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Saba


Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Saba


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.

Maudhui ya video hii:
Hakuna Anayeweza Kubadilisha Hoja Kwamba Mungu Anashikilia Ukuu juu ya Hatima ya Binadamu
Mtazamo na Matendo Bora ya Mtu Anayependa Kujinyenyekeza katika Mamlaka ya Mungu
Kumkubali Mungu kama Bwana Wenu wa Kipekee Ndiyo Hatua ya Kwanza katika Kutimiza Wokovu

Baadhi ya Makala: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)” Sehemu ya Kwanza"

Jumatano, 6 Februari 2019

Je, Kanisa la Mwenyezi Mungu Lina Malengo Yapi?

Je, Kanisa la Mwenyezi Mungu Lina Malengo Yapi?

     Kanisa la Mwenyezi Mungu hunyunyizia na kuwaongoza waumini wake kwa mujibu kamili wa maneno ya Mungu katika Biblia na Neno Laonekana Katika Mwili yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, ili kwamba kila muumini anaweza, chini ya uongozi, utolewaji, unyunyiziwaji, na uongozwaji wa maneno ya Mwenyezi Mungu, kuelewa ukweli wote katika maneno ya Mungu, kumiliki mtazamo sahihi juu ya maisha na maadili, kuwa na malengo sahihi ya kufuatilia, kufuata njia ya Mungu, kushikilia maagizo ya Mungu, kumtukuza Mungu kwa kuwa nuru na chumvi ya dunia, na kusifiwa na Mungu, na kuwa na sifa kamili kurithi ahadi za Mungu.

Jumamosi, 2 Februari 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | ""Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu"""


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu"


  Mwenyezi Mungu anasema, "Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu."

Jumatatu, 28 Januari 2019

nyimbo za kuabudu 2019 | "Mungu Anashuka na Hukumu" | Christ of the Last Days Has Appeared


Nyimbo za Kuabudu 2019 | "Mungu Anashuka na Hukumu" | Christ of the Last Days Has Appeared


Anapokuja chini katika taifa la joka kuu jekundu,
Mungu anageuka kuutazama ulimwengu na unaanza kutingika.
Je, kuna mahali popote ambapo hapatapata hukumu Yake?
Ama kuishi katika janga Analotoa?
Kila mahali Aendapo anamwaga mbegu ya janga,
lakini kupitia kwayo Anatoa wokovu na kuonyesha upendo Wake.
Mungu anatamani kuwafanya watu zaidi kumjua, kumwona na kumheshimu.
Hawajamwona kwa muda mrefu, lakini sasa Yeye ni wa kweli kabisa.

Jumapili, 27 Januari 2019

Nyimbo za Dini | Ni kwa Kufanya Kazi Katika Mwili Pekee Ndiyo Mungu Anaweza Kumpata Binadamu

Nyimbo za Dini | Ni kwa Kufanya Kazi Katika Mwili Pekee Ndiyo Mungu Anaweza Kumpata Binadamu

I
Kupitia neno la Mungu la utendaji,
unyonge wa mwanadamu na uasi
yanahukumiwa na kufichuliwa.
Kisha wanadamu wanapokea wanachohitaji
Wanaona kuwa Mungu amekuja
katika ulimwengu huu wa binadamu.

Ijumaa, 18 Januari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) (Sehemu ya Tatu)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Tatu

2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu.

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

Ijumaa, 11 Januari 2019

Matamshi ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Kwanza"



Matamshi ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Kwanza"


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.

Maudhui ya video hii:

Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo

Hatima ya Binadamu na Hatima ya Ulimwengu Haviwezi Kutenganishwa na Ukuu wa Muumba Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji.