Jumapili, 27 Januari 2019

Nyimbo za Dini | Ni kwa Kufanya Kazi Katika Mwili Pekee Ndiyo Mungu Anaweza Kumpata Binadamu

Nyimbo za Dini | Ni kwa Kufanya Kazi Katika Mwili Pekee Ndiyo Mungu Anaweza Kumpata Binadamu

I
Kupitia neno la Mungu la utendaji,
unyonge wa mwanadamu na uasi
yanahukumiwa na kufichuliwa.
Kisha wanadamu wanapokea wanachohitaji
Wanaona kuwa Mungu amekuja
katika ulimwengu huu wa binadamu.

Kazi ya Mungu wa utendaji ina nia ya kumwokoa kila mmoja
kutoka kwa ushawishi wa Shetani,
kuwaokoa kutoka kwa uchafu na kwa tabia yao
iliyopotoshwa na Shetani.
Kupatwa na Mungu kunamaanisha kufuata mfano Wake
kama mfano kamili wa mwanadamu.
Mfuate Mungu wa matendo, ishi ubinadamu wa kawaida.
fuata maneno Yake na mahitaji,
fuata kile Anachosema kabisa.
na ufanikishe kile Anachotaka, kisha utapatwa na Mungu.
II
Mungu alichukua mwili,
Akiruhusu watu kuona matendo Yake.
Roho Wake alichukua mwili,
ili mwanadamu amguse Mungu,
ili watu wamtazame Mungu na kuja kumjua.
Kwa njia hii ya matendo pekee ndiyo
Mungu huwafanya watu kuwa wakamilifu.
Wale wanaoweza kuishi maisha yao kulingana na Yeye
na kufuata moyo Wake, ni wale wanaopatwa na Mungu.
Kupatwa na Mungu kunamaanisha kufuata mfano Wake
kama mfano kamili wa mwanadamu.
Mfuate Mungu wa matendo, ishi ubinadamu wa kawaida.
fuata maneno Yake na mahitaji,
fuata kile Anachosema kabisa.
na ufanikishe kile Anachotaka, kisha utapatwa na Mungu.
III
Kama Mungu angenena tu mbinguni na asije chini duniani,
watu wangewezaje kumjua Yeye?
Na maneno matupu tu kuonyesha kazi Yake,
na sio maneno Yake kama ukweli.
Mungu anakuja kama mfano,
ili mwanadamu amwone na kumgusa,
amwone na kupatwa na Yeye.
Kupatwa na Mungu kunamaanisha kufuata mfano Wake
kama mfano kamili wa mwanadamu.
Mfuate Mungu wa matendo, ishi ubinadamu wa kawaida.
fuata maneno Yake na mahitaji,
fuata kile Anachosema kabisa.
na ufanikishe kile Anachotaka, kisha utapatwa na Mungu.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

0 评论:

Chapisha Maoni