Jumamosi, 5 Januari 2019

3. Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Kristo wa Kweli na Makristo wa Uongo?

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu
3. Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Kristo wa Kweli na Makristo wa Uongo?

ukweli,Kristo,siku za mwisho,Roho Mtakatifu,


Maneno Husika ya Mwenyezi Mungu:
Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, Kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu.  Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, badala yake, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale Kristo bandia wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe.
kutoka kwa "Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele" katika Neno Laonekana katika Mwili
Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Huwa mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amekuwa mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, Atampa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, itadadisiwa kutoka katika dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini katika dutu Yake (Kazi Yake, Maneno Yake, Tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu.
kutoka kwa "Dibaji" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe.
…………
… Japokuwa Kristo Anamwakilisha Mungu Mwenyewe katika mwili na hufanya binafsi ambayo Mungu Mwenyewe Anapaswa kufanya, Yeye hakani kuwepo kwa Mungu mbinguni, wala kuyatangaza matendo Yake Mwenyewe kwa msisimko. Badala yake, Yeye kwa unyenyekevu Hubaki kwa siri ndani ya mwili Wake. Mbali na Kristo, wale ambao wanadai kwa udanganyifu kuwa Kristo hawana sifa Zake. Wakiwekwa sambamba dhidi ya tabia za kiburi na kujiinua za Kristo wa uongo, inakuwa dhahiri aina gani ya mwili ndiye Kristo wa kweli. Walivyo waongo zaidi, ndivyo Kristo wa uongo wanavyojionyesha wenyewe, na ndivyo wanavyoweza zaidi kufanya kazi za ishara na maajabu ya kuwahadaa binadamu. Kristo wa uongo hawana sifa za Mungu; Kristo hajachafuliwa na kipengele chochote cha dutu ya Kristo wa uongo. Mungu hupata mwili tu kukamilisha kazi ya mwili, na sio tu kuwaruhusu watu wote kumwona. Badala yake, Yeye huacha kazi Yake ithibitishe utambulisho Wake, na kuruhusu Anachofichua kushuhudia dutu Yake. Dutu Yake haikosi msingi ; utambulisho Wake haukukamatwa na mkono Wake; huamuliwa kwa kazi Yake na dutu Yake. …
Kazi na maonyesho ya Kristo huamua dutu Yake. Yeye Anaweza kukamilisha kwa moyo wa kweli kile Alichoaminiwa kufanya. Anaweza kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli, na kwa moyo wa kweli Atafute mapenzi ya Mungu Baba. Yote haya yanaamuliwa na dutu Yake. Na vile vile ufunuo Wake wa asili pia unaamuliwa na dutu Yake; sababu ya ufunuo Wake wa asili kuitwa hivyo ni kwa sababu ya maonyesho Yake siyo maigizo, au matokeo ya elimu na mwanadamu, au matokeo ya miaka mingi ya kukuzwa na mwanadamu. Hakujifunza au kujivika nayo Yeye Mwenyewe; badala yake, ni asili ndani Yake.
kutoka kwa "Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na ana uwezo wa kutoa mapepo, na kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba haya yote ni ujio wa Yesu, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuigi Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. Kazi ya Mungu haipatani na dhana za mwanadamu; kwa mfano, Agano la Kale lilitabiri juu ya ujio wa Masihi, lakini ilikuwa dhahiri kwamba Yesu Alikuja, hivyo itakuwa makosa kwa Masihi mwingine kuja tena. Yesu tayari Amekwishakuja mara moja, na yatakuwa ni makosa ikiwa Yesu Atakuja tena wakati huu. Kuna jina moja kwa kila enzi, na kila jina linaeleza sifa ya enzi. Katika dhana za mwanadamu, Mungu ni lazima siku zote Aonyeshe ishara na maajabu, ni lazima siku zote Aponye wagonjwa na kutoa mapepo, na siku zote ni lazima Awe tu kama Yesu, lakini Mungu wakati huu Hayupo kama hivyo kabisa. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine; mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Unapaswa kuelewa vizuri mambo haya.
kutoka kwa "Kuijua Kazi ya Mungu Leo" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, "Mimi ni Mungu!" Lakini mwishowe, hawawezi wakasimama, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. Mimi sipigi mayowe Nikisema, Mimi ni Mungu, Mimi ni Mwana Mpendwa wa Mungu! Lakini kazi Nifanyayo ni ya Mungu. Kuna haja Nipige mayowe? Hakuna haja ya kujiinua. Mungu hufanya kazi Yake Mwenyewe na hahitaji mwanadamu kumpa ruhusa ama cheo kubwa, na kazi Yake inatosha kuwakilisha utambulisho Wake na cheo. Kabla ya ubatizo Wake, si Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe? Je, Yeye hakuwa mwili wa Mungu? Hakika haiwezi kusemekana kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu baada ya kushuhudiwa? Je, hakukuwa na mwanadamu jina lake Yesu kitambo kabla Aanze kazi Yake? Huwezi kuleta njia mpya ama kumwakilisha Roho. Huwezi kueleza kazi ya Roho ama maneno Anenayo. Huwezi kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ama ile ya Roho. Huwezi kuelezea hekima, ajabu na mambo ya Mungu yasiyoeleweka, ama tabia yote ambayo Mungu humwadibu mwanadamu kupitia kwayo. Kwa hivyo madai yako ya kila mara ya kusema kuwa wewe ni Mungu hayajalishi; unalo tu jina lakini huna dutu. Mungu Mwenyewe Amekuja, lakini hakuna anayemtambua, ilhali Anaendelea na kazi Yake na Anafanya hivyo kwa uwakilishi wa Roho. Haijalishi unamwita mwanadamu ama Mungu, Bwana ama Kristo, ama umwite dada, yote ni sawa. Lakini kazi Afanyayo ni ile ya Roho na Anawakilisha kazi ya Mungu Mwenyewe. Hajali ni jina gani mwanadamu anamwita. Je, jina hilo linaweza kuamua kazi Yake? Bila kujali unachomwita, kutoka kwa mtazamo wa Mungu, Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu; Anawakilisha Roho na amekubaliwa na Yeye. Huwezi kutengeneza njia ya enzi mpya, na huwezi kuhitimisha enzi nzee na huwezi kukaribisha enzi mpya ama kufanya kazi mpya. Kwa hivyo, huwezi kuitwa Mungu!
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake.
kutoka kwa "Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kati ya hao Kristo wa uwongo, manabii waongo na wadanganyifu, hakuna wanaoitwa Mungu pia? Na mbona hao sio Mungu? Kwa sababu hawana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu. Mizizini, wao ni wanadamu, wanaowadanganya watu, sio Mungu, na hivyo hawana utambulisho wa Mungu.
kutoka kwa "Kuhusu Majina na Utambulisho" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa Mtu:
Sisi ambao tumepitia kazi ya Mungu ya siku za mwisho sote tumeweza kuona waziwazi ukweli mmoja: Kila wakati Mungu Anapofanya awamu mpya ya kazi, Shetani na roho mbalimbali waovu humfuata Yeye unyo kwa unyo, wakiiga na kuifanya kazi Yake kuonekana ya uongo ili kuwalaghai watu. Yesu Aliponya, na kuyatoa mashetani, na hivyo, ndivyo pia, Shetani na roho wa maovu wanavyofanya kwa kuponya na kutoa mashetani; Roho Mtakatifu alimpa mwanadamu tuzo ya kuongea kwa ndimi, na hivyo, pia, ndivyo pepo wabaya wanavyowafanya watu kuongea "kwa ndimi" ambazo hakuna anayeelewa. Na bado, ingawaje pepo wabaya wanafanya mambo mbalimbali yanayoshawishi mahitaji ya mwanadamu, na kutenda baadhi ya vitendo visivyo vya ulimwenguni humu ili kuweza kumlaghai yeye, kwa sababu si Shetani wala pepo hawa wabaya wameumiliki ukweli hata kidogo zaidi, hawatawahi kuweza kumpatia mwanadamu ukweli. Kuanzia sehemu hii pekee inawezekana kutofautisha kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo.
… Baada ya kupata mwili, Roho wa Mungu hufanya kazi kwa unyenyekevu na kwa siri, na hupitia maumivu yote ya mwanadamu bila ya malalamiko hata kidogo. Kama Kristo, Mungu hajawahi Kujishaua Mwenyewe, au kujigamba, isitoshe Hajawahi jifanya kuhusu nafasi Yake, au kuwa wa kujidai, hali ambayo inaonyesha kabisa uheshima na utakatifu wa Mungu. Hali hii inaonyesha kiini cha heshima chenye ukubwa wa maisha ya Mungu, na inaonyesha kwamba Yeye ndiye mfano halisi wa upendo. Kazi ya Makristo wa uongo na pepo wabaya kwa usahihi ni kinyume cha kazi ya Kristo: Kabla ya kitu chochote kile, pepo wabaya siku zote wanatangaza kwamba wao ni Kristo, na wanasema kwamba kama hutawasikiliza huwezi kuingia kwenye ufalme. Wanafanya kila kitu wanachoweza kuwafanya watu kukutana na wao, wanajigamba, na kujishaua wenyewe, na kujiona, au vinginevyo kutenda baadhi ya ishara na maajabu ili kuwalaghai watu —na baada ya watu hawa kulaghaiwa na kuzikubali kazi zao, wanasambaratika bila watu kuwa na habari kwa sababu kipindi kirefu kimepita tangu walipopewa ukweli. Kunayo mifano mingi, mifano mingi ya haya. Kwa sababu Makristo wa uongo si ukweli, njia, au uzima, hivyo basi hawana njia, na muda mfupi ujao au baadaye wale wanaowafuata watadhalilishwa—lakini wakati huo mambo yatakuwa yameharibika tayari na hayataweza kurekebishwa. Na hivyo, muhimu zaidi ni kutambua kwamba Kristo pekee ndiye ukweli, njia, na uzima. Makristo wa uongo na pepo wabaya kwa hakika wameondolewa ukweli; haijalishi ni mambo mangapi wanayoyasema, au vitabu vingapi wanavyoviandika, hakuna kati ya hivyo vilivyo na ukweli hata kidogo. Hali hii ni kamili. Kristo pekee ndiye Anayeweza kuuonyesha ukweli, na hii ni muhimu katika kutambua tofauti kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo. Isitoshe, Kristo hajawahi kuwalazimisha watu kumkubali au kumtambua Yeye. Kwa wale wanaomsadiki Yeye, ukweli unazidi kuwa wazi zaidi na zaidi, na namna wanavyotembea inazidi kuwa angavu zaidi na zaidi, na hii ni thibitisho kwamba Kristo pekee ndiye Anayeweza kuwaokoa watu, kwani Kristo ndiye ukweli. Makristo wa uongo wanaweza tu kuiga maneno machache, au kutamka maneno yanayogeuza weusi ukawa weupe. Hawana ukweli, na wanaweza tu kuwaletea watu giza, maangamizo, na kazi ya pepo wabaya.
kutoka kwenye Utangulizi wa Kuchanganua Kesi za Ulaghai na Kristo wa Uongo na Wapinga Kristo
Makristo wa uongo wanawezaje kutambuliwa? Ni rahisi mno. Unawaambia: "Endelea, zungumza. Nini kinachokufanya kuwa Kristo? Sema kitu kuhusu kile Mungu anacho na alicho, na kama huwezi kukisema, kukiandika ni SAWA, pia. Andika baadhi ya maneno yaliyoonyeshwa uungu—endelea, niandikie jambo. Huna tatizo kuiga baadhi ya maneno ya ubinadamu. Hebu sema mengine zaidi, zungumza kwa saa tatu na uone kama unaweza kufanya hivyo. Wasiliana ukweli nami kwa saa tatu, ongea kuhusu Alicho Mungu, na awamu hii ya kazi Yake, nizungumzie waziwazi, jaribu na uone. Na kama huwezi kuongea, basi wewe ni bandia, na ni pepo mbaya. Kristo wa kweli anaweza kuzungumza kwa siku nyingi bila ya matatizo yoyote, Kristo wa kweli Ameonyesha zaidi ya maneno milioni—na angali hajamaliza. Hakuna vipimo kuhusu ni kiwango kipi Anachoweza kuongea, Anaweza kuongea wakati wowote au mahali popote, na maneno Yake yasingeweza kuandikwa na binadamu yeyote kotekote ulimwenguni. Maneno Yake yangeweza kuandikwa na mtu yeyote yule asiyekuwa na uungu? Mtu kama huyo angeweza kuyaongea maneno haya? Nyinyi Makristo wa uongo hamna uungu, na Roho wa Mungu hayumo ndani yenu. Ungewezaje kuyaongea maneno ya Mungu? Unaweza kuyaiga baadhi ya maneno ya Mungu, lakini unaweza kuendelea hivyo kwa muda gani? Mtu yeyote aliye na akili anaweza kukariri maneno machache, kwa hivyo ongea kwa saa moja, wasiliana kwa karibu ukweli kwa saa mbili—jaribu na uone." Ukisisitiza kwao hivyo, watafichuliwa, watapigwa na bumbuazi, na watatoroka hivi karibuni. Je, hali iko hivyo? Nyinyi mnasemaje, mambo yako hivyo? Waambie haya kwao: Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima, hivyo basi onyesha ukweli wa Kristo kwangu mimi ili niweze kusikia, au kusoma. Kama utaweza, basi wewe ndiwe Kristo, na kama hutaweza, basi wewe ni pepo mbaya! Ni rahisi kutofautisha kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo. Makristo wa uongo na wapinga kristo hawana ukweli; yeyote yule ambaye ameumiliki ukweli ni Kristo, na yeyote yule anayekosa ukweli si Kristo. Je, hali iko hivyo? Waambie: "Kama huwezi kuonyesha Kristo ni nani, au kile Mungu Alicho, na unasema kwamba wewe ni Kristo, basi unadanganya. Kristo ndiye ukweli—hebu tuone ni maneno mangapi ya ukweli unayoweza kuonyesha. Kama utaiga sentensi kadhaa, basi huziwasilishi , na unazinakili pekee. Umeziiba, ni mwigo." Hapo sawa—hayo ndiyo yanayohitajika ili kuwatambua Makristo wa uongo. … Hebu tuuzungumzie ukweli: namna ambavyo Mungu Alionekana wakati Alipoonekana. Wakati Mungu Alipoanza kufanya kazi, Hakusema kwamba Yeye ni Mungu, Hakusema hivyo. Mungu Aliyaonyesha maneno mengi, na baada ya Kuyaonyesha mamia ya maelfu ya maneno, bado Hakusema kwamba Yeye ni Mungu. Mamia ya maelfu ya maneno—hicho ni kitabu kizima, takribani kurasa mia tatu au nne—na bado Hakusema kwamba Yeye ni Mungu. Baada ya kuangaziwa na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, baadhi ya watu walisema: "Jameni, haya ndiyo maneno ya Mungu, hii ndiyo sauti ya Roho Mtakatifu!" Mwanzoni, walisadiki kwamba ilikuwa ni sauti ya Roho Mtakatifu; baadaye, walisema kwamba ilikuwa sauti ya Roho wale saba, ya Roho aliyezidi na aliyekuwa mara saba. Waliita "sauti ya Roho saba," au "matamko ya Roho Mtakatifu." Haya ndiyo waliyoyasadiki mwanzoni. Ni baadaye tu, baada ya Mungu kuyatamka maneno mengi, mamia ya maelfu ya maneno, ndipo Alipoanza kushuhudia maana ya kupata mwili, na maana ya kuonekana kwa Neno katika mwili— na hapo tu ndipo watu walianza kujua, wakisema: "Jameni! Mungu amepata mwili! Ni kupata mwili kwa Mungu Anayetuzungumzia sisi!" Hebu tazama namna kazi ya Mungu ilivyo fiche na yenye unyenyekevu. Hatimaye, baada ya Mungu kumaliza kuyaonyesha maneno Yake yote ambayo lazima Angeyaonyesha, bado Hakusema kwamba Yeye ni Mungu Alipofanya kazi na kuhubiri, bado Hakuwahi kusema, "Mimi ni Mungu! Nyinyi lazima mnisikilize Mimi." Hakuwahi kuongea hivyo. Na bado Makristo wa uongo wanasema wao ni Kristo kabla ya hata kutamka maneno machache. Je, hawa wanaweza kukosa kuwa bandia? Mungu wa kweli ni mfiche na mnyenyekevu, na kamwe Hajishaui; Shetani na pepo wabaya, kinyume cha mambo ni kwamba, wanapenda kujishaua, ambayo ni njia nyingineyo ya kuwatambua.
kutoka kwa "Majibu ya Maswali" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (I)
Sasa, kama watu watajaribu kuwalaghai, angalieni kama wanaweza kuionyesha sauti ya Mungu. Hali hii itathibitisha kama wamemiliki au la kiini cha uungu. Kama hawawezi kuzungumzia kuhusu kile Mungu anacho na alicho, na hawawezi kuonyesha mambo na sauti ya Mungu, basi kwa kweli hawana kiini cha Mungu, na hivyo wao ni bandia. Kunao wale wanaosema: Tumewaona baadhi ya watu wakiongea maneno ambayo hakuna mwanadamu angeweza kuyasema. Wanaweza pia kuongea unabii, na kuongea bila ya kutatizwa kwa mambo ambayo hakuna mtu angeyajua wala kuyaona—hivyo basi, wao ni Mungu? Mnawezaje kutofautisha haya mambo hasa kuhusu watu kama hawa? Kama ambavyo imesemwa tu, kama wao ni Mungu, basi lazima waweze kuongea kuhusu kile Mungu anacho na alicho, na kuweza kuzungumzia siri za ufalme wa Mungu; ni mtu kama huyu tu ndiye anayeweza kusemekana kuwa mwili wa Mungu. Kama kunao watu wanaoweza kuongea mambo ambayo wengine hawajui, wanaoweza kuwaambia kuhusu siku zao za usoni, na wanaoweza kusema kile kitakachofanyikia nchi, haya si lazima yawe maneno ya Mungu; pepo wabaya wanaweza pia kusababisha mambo haya. Kwa mfano, kama leo utawaambia: "Ni nini kitakachonifanyikia katika siku za usoni?" watakuambia ni janga aina gani litakalokupata wewe, au watakuambia ni lini utakapokufa, au vinginevyo watakuambia ni nini kitakachofanyikia familia yako. Katika matukio mengi, mambo haya huja kuwa kweli. Lakini kuweza kuzungumzia mambo kama haya si kile Mungu Alicho, wala si sehemu ya kazi ya Mungu. Lazima uwe wazi kuihusu hoja hii. Haya ndiyo mambo madogomadogo ambayo pepo wabaya wanatia fora kwayo; Mungu hajihusishi na mambo kama haya. Tazama ni kazi gani ambayo Mungu Amefanya kila wakati Amepata mwili. Mungu Anafanya kazi ya kumwokoa mwanadamu, Hatabiri kile kitakachowafanyikia watu, wataishi kwa muda gani, ni watoto wangapi watakaowapata, au ni lini janga litakapowapata. Je, Mungu amewahi kuyatabiri mambo kama haya? Hajawahi. Sasa, nyinyi mnasema nini, Mungu Anayajua mambo kama haya? Bila shaka Anayajua, kwani Aliumba mbingu na ardhi na vitu vyote. Mungu tu ndiye Anayevijua kwa njia bora zaidi, ilhali kunayo mipaka kuhusu kile ambacho pepo wabaya wanajua. Pepo wabaya wana uwezo wa kujua nini? Pepo wabaya wanajua hatima ya mtu, au nchi, au taifa. Lakini hawajui chochote kuhusu usimamizi wa Mungu, hawajui hatima ya mwanadamu itakuwa vipi, au ni wapi ambapo mwisho wa kweli wa mwanadamu unapatikana, isitoshe hawajui ni lini ulimwengu utafika mwisho na ufalme wa Mungu kuwasili, au maonyesho mazuri ya ufalme wa mbinguni yatakuwa vipi. Hawajui chochote kuhusu haya yote, hakuna yeyote kati yao anayeyajua. Mungu pekee ndiye Anayejua masuala kama haya, na hivyo Mungu ni Mjua-yote, ilhali kile pepo wabaya wanachojua kinao ufinyu mkubwa sana. Tunajua kwamba manabii wakubwa zaidi wa ulimwengu walikuwa waliongea kuhusu kile kitakachofanyika kwenye siku za mwisho, na leo maneno yao yametimizwa—lakini hawakujua chochote kuhusu kazi ambayo Mungu Anafanya kwenye siku za mwisho, isitoshe hawakujua kile ambacho Mungu Amekuja kutimiza, au namna ambavyo Ufalme wa Milenia utakavyofikiwa, au ni nani atakayeingia kwenye ufalme wa Mungu na kuishi. Wala, na kuongezea hayo, hawakujua chochote kuhusu kile kitakachofanyika baadaye, kwa ufalme wa Mungu. Hakuna pepo mbaya anayejua masuala kama hayo; Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayejua, na hivyo pepo wabaya hawawezi kamwe kujua chochote kinachohusu mpango wa usimamizi wa Mungu. Kama utawaambia, "Hatima yangu ni nini? Nini kitakachofanyikia familia yangu?" baadhi ya pepo wabaya wataweza kukuambia jibu dhahiri. Lakini ukiwaambia, "Kwenye siku za usoni, nitakuwa na hatima katika imani yangu kwa Mungu? Nitaishi?" hawatajua. Pepo wabaya wanao ufinyu mkubwa sana kuhusu kile wanachojua. Kama pepo mbaya anaweza kusema tu mambo machache finyu, anaweza kuwa Mungu? Hawezi kuwa—ni pepo mbaya. Wakati pepo mbaya anaweza kuwaambia watu mambo wasiyoyajua, kuwaambia kuhusu siku zao za usoni, na hata kuwaambia namna ambavyo walikuwa na mambo ambayo wameyafanya, kama kunao wale wanaofikiria kwamba kufanya hivi kunao uungu kwa kweli, je, huoni kwamba watu hao ni wa kukejeliwa? Hii inathibitisha kwamba wewe hujui Mungu kabisa. Unaziona mbinu ndogo za pepo wabaya kuwa zenye uungu kabisa, na kuwachukulia kama Mungu. Je, unajua kuihusu kudura ya Mungu? Hivyo, kama leo tunayo maarifa kuihusu kudura na kazi ya Mungu, hakuna pepo mbaya, haijalishi ni ishara na maajabu gani ambayo wanatenda, anayeweza kutulaghai, kwani kwa hakika lipo jambo japo moja ambalo tuna hakika nalo: Pepo wabaya si ukweli, hawawezi kufanya kazi ya Mungu, wao si Muumba, hawawezi kumwokoa mwanadamu, na wanaweza kumpotosha tu mwanadamu.
kutoka kwa “Utofauti kati ya Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)

0 评论:

Chapisha Maoni