Jumapili, 6 Januari 2019

5. Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee.

Sura ya 7 Vipengele Kadhaa Vingine vya Ukweli Ambao ni wa Kiwango cha Chini Ambao Unafaa Kueleweka na Waumini Wapya
5. Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee.


Maneno Husika ya Mungu:
Leo, lazima uwe katika njia sahihi kwani unaamini katika Mungu wa vitendo. Kwa kuwa una imani katika Mungu, hupaswi tu kutafuta baraka, lakini pia kutafuta kumpenda Mungu na kumjua Mungu. Kupitia kwa kupata nuru kutoka Kwake na harakati yako mwenyewe, unaweza kula na kunywa neno Lake, kukuza ufahamu wa kweli kuhusu Mungu, na kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu unaotoka moyoni mwako.  Kwa maneno mengine, upendo wako kwa Mungu ni wa kweli zaidi, ambapo hakuna yeyote anayeweza kuharibu au kukuzuia kuonyesha upendo wako Kwake. Basi uko kwa njia ya kweli ya imani kwa Mungu. Inathibitisha kwamba wewe unamilikiwa na Mungu, kwani moyo wako umemilikiwa na Mungu na wala huwezi kumilikiwa na kitu kingine. Kutokana na tajriba yako, malipo uliyolipa, na kazi ya Mungu, wewe una uwezo wa kuendeleza upendo usioamriwa kwa Mungu. Kisha unawekwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa neno la Mungu. Ni wakati tu ambao umekuwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza ndipo unaweza kuchukuliwa kuwa umempata Mungu. Katika imani yako kwa Mungu, lazima utafute lengo hili. Huu ni wajibu wa kila mmoja wenu.
kutoka kwa "Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kupitia Mungu hakuhusu kufurahia neema Yake, lakini zaidi kuhusu kuteseka kwa sababu ya upendo wako Kwake. Kwa kuwa unafurahia neema ya Mungu, lazima pia ufurahie kuadibu Kwake—lazima upitie haya mambo yote. Unaweza kuwa na uzoefu wa nuru ya Mungu ndani yako, na unaweza pia kupitia ushughulikiaji Wake kwako na hukumu Yake. Kwa njia hiyo, unakuwa na uzoefu wa pande zote. Mungu amefanya kazi ya hukumu kwako, na Yeye pia amefanya kazi ya kuadibu kwako. Neno la Mungu limekushughulikia, lakini pia limekupa nuru, limekuangazia. Wakati unataka kukimbia, mkono wa Mungu bado unakuvuta kwa nguvu. Hizi kazi zote ni kukufahamisha kwamba kila kitu kuhusu mwanadamu kiko chini ya Mungu. Unaweza kufikiri kuamini katika Mungu ni kuhusu mateso, au kufanya mambo mengi kwa ajili Yake, au kwa ajili ya amani ya mwili wako, au ni kwa ajili ya kila jambo liende vyema kwako, kwa ajili ya kila jambo liwe la kustarehesha—lakini hakuna kati ya haya ambayo ni madhumuni watu wanapaswa kuwa nayo kwa ajili ya kuamini katika Mungu. Kama hayo ndiyo unaamini, basi mtazamo wako si sahihi na huwezi kukamilika kabisa. Matendo ya Mungu, tabia ya Mungu ya haki, hekima Yake, maneno Yake, na maajabu Yake na kutoeleweka kwa kina Kwake yote ni mambo watu wanapaswa kuelewa. Tumia uelewa huu kuachana na maombi ya kibinafsi na pia matumaini ya mtu binafsi na mawazo moyoni mwako. Ni kwa kuondoa haya tu ndio unaweza kukidhi masharti yanayotakiwa na Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio unaweza kuwa na uzima na kumridhisha Mungu. Kumwamini Mungu ni kwa ajili ya kumridhisha Yeye na kuishi kwa kudhihirisha tabia Yeye anahitaji, ili matendo na utukufu Wake yaweze kudhihirishwa kupitia kundi hili la watu wasiostahili. Huo ndio mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu, na pia lengo unapaswa kutafuta. Unapaswa kuwa na mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu na kutafuta kupata maneno ya Mungu. Unahitaji kula na kunywa maneno ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli, na hasa kuona matendo Yake ya vitendo, kuona Matendo Yake ya ajabu kotekote katika ulimwengu mzima, pamoja na kazi ya vitendo Yeye hufanya katika mwili. Kwa njia ya uzoefu wao halisi, watu wanaweza kufahamu ni jinsi gani Mungu hufanya kazi Yake kwao na mapenzi Yake kwao ni yapi. Haya yote ni kwa ili kuondoa tabia yao potovu ya kishetani. Jiondolee uchafu na udhalimu ndani yako, ondoa nia zako mbaya, na unaweza kuendeleza imani ya kweli katika Mungu. Kwa kuwa tu na imani ya kweli ndio unaweza kweli kumpenda Mungu. Unaweza tu kweli kumpenda Mungu kwa msingi wa imani yako Kwake. Je, unaweza kufanikisha kumpenda Mungu bila kumwamini Yeye? Kwa kuwa unaamini katika Mungu, huwezi kukanganyika kuhusu jambo hilo. Baadhi ya watu hujawa na nguvu mara tu wanapoona kwamba imani katika Mungu itawaletea baraka, lakini hupoteza nguvu zote mara tu wanapoona wanafaa kupitia kusafishwa. Je, hiyo ni kuamini katika Mungu? Mwishowe, imani katika Mungu inahusu utiifu kamili na mzima mbele Yake. Unaamini katika Mungu lakini bado una madai Kwake, una mawazo mengi ya kidini ambayo huwezi kuyapuuza, maslahi ya kibinafsi huwezi kuacha, na bado unatafuta baraka za mwili na unataka Mungu aokoe mwili wako, kuokoa nafsi yako—haya yote ni maonyesho ya watu wenye mtazamo usio sahihi. Hata kama watu wenye imani za kidini wana imani katika Mungu, hawatafuti mabadiliko ya tabia, hawafuatilii maarifa ya Mungu, na wanatafuta tu maslahi ya miili yao. Wengi kati yenu mna imani ambazo ni za kikundi cha kusadiki kidini. Hiyo siyo imani ya kweli katika Mungu. Kuamini katika Mungu lazima watu wamiliki moyo wa kuteseka kwa ajili Yake na hiari ya kujitoa wenyewe. Isipokuwa wakikidhi haya masharti mawili haihesabiki kama imani katika Mungu, na hawatakuwa na uwezo wa kufikia mabadiliko ya tabia. Ni watu tu wanaotafuta ukweli kwa kweli, wanaotafuta maarifa ya Mungu, na kufuatilia maisha ni wale ambao kweli wanaamini katika Mungu.
kutoka kwa "Ni Lazima Wale Wanaofaa Kufanywa Wakamilifu Wapitie Usafishaji" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni imani katika Mungu ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—hicho ndicho kiasi cha chini zaidi unachopaswa kuwa nacho katika imani yako kwa Mungu. Imani kwa Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha katika mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu, kutoka maisha ya kiasili kwenda kwa maisha katika nafsi ya Mungu, ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kutekeleza mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata.
kutoka kwa "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wengi wa watu wanaomfuata Mungu wanashughulika tu na jinsi watakavyopata baraka nyingi na kuepuka majanga. Panapotajwa kazi na usimamizi wa Mungu, wanakaa kimya na kupoteza matamanio yao yote. Wanaamini kuwa kujua maswali ya kuchosha kama hayo hakutakuza maisha yao au kuwa na faida yoyote, na kwa hivyo hata kama wamezisikia habari kuhusu usimamizi wa Mungu, wanazichukulia kikawaida. Na hawazichukulii kama kitu cha thamani kukipokea, na hata kukikubali kama sehemu ya maisha yao. Watu kama hao wana nia sahili sana katika kumfuata Mungu: kupata baraka, na ni wazembe sana kuhudhuria chochote ambacho hakihusiani na nia hii. Kwao, kuamini kwa Mungu ili kupata baraka ndilo lengo halali na la thamani kwa imani yao. Hawaathiriwi na kitu chochote ambacho hakiwezi kutekeleza lengo hili. Hivyo ndivyo ilivyo na watu wengi wanaomfuata Mungu leo. Nia yao na motisha huonekana kuwa halali, kwa sababu wakati huo huo wa kumwamini Mungu, wanatumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, wanajitolea kwa Mungu, na kutekeleza wajibu wao. Wanauacha ujana wao, wanajinyima kwa familia na kazi zao, na hata hukaa miaka mingi wakijishughulisha mbali na nyumbani kwao. Kwa ajili ya lengo lao kuu, wanabadili matamanio yao, wanabadili mtazamo wao wa nje wa maisha, hata kubadili njia wanayoitafuta, ila bado hawawezi kubadili nia ya imani yao kwa Mungu. Wanajishughulisha na usimamizi wa matamanio yao wenyewe; haijalishi njia iko mbali vipi, na ugumu na vikwazo vilivyo njiani, wanashikilia msimamo wao bila uoga hadi kifo. Ni nguvu zipi zinazowafanya wawe wa kujitolea kwa njia hii? Ni dhamiri yao? Ni sifa zao kubwa na nzuri? Ni kujitolea kwao kupigana na nguvu za maovu hadi mwisho? Ni imani yao wanayomshuhudia Mungu kwayo bila kutaka malipo? Ni utiifu wao ambao kwao wanajitolea kuacha kila kitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu? Au ni roho yao ya kujitolea ambayo kwayo wanajinyima kila mara mahitaji badhirifu ya kibinafsi? Kwa watu ambao hawajawahi kujua kazi ya usimamizi wa Mungu kutoa zaidi, kwa hakika, ni muujiza wa ajabu! Hivi sasa, wacha tusijadiliane kuhusu kiasi ambacho hawa watu wametoa. Tabia zao, hata hivyo, ni muhimu sana kuichambua. Mbali na manufaa ambayo yanahusiana nao, je, kuna uwezekano wa kuweko kwa sababu nyingine ya wale hawajawahi kumfahamu Mungu kujitolea zaidi Kwake? Kwa hili, tunagundua tatizo ambalo halikutambuliwa hapo awali: uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili kupokea malipo aliyoahidiwa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila kukubali na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika. Mambo yanapofikia hapa, nani anaweza kubadilisha mwelekeo kama huu? Na ni watu wangapi ambao wanaweza kufahamu kwa kweli jinsi uhusiano huu ulivyokosa matumaini? Naamini kuwa watu wanapojitosa wenyewe kwenye raha ya kubarikiwa, hakuna anayeweza kukisia jinsi uhusiano na Mungu ulivyo wa aibu na usiopendeza.
Jambo la kusikitisha mno kuhusu imani ya wanadamu kwa Mungu ni kuwa wanadamu wanatekeleza usimamizi wao wenyewe katikati ya kazi ya Mungu na hawasikilizi usimamizi wa Mungu. Udhaifu mkubwa wa mwanadamu unaegemea katika jinsi, wakati huo huo anatafuta kujitoa kwa Mungu na kumwabudu, mwanadamu anaunda hatima yake kamilifu na kuhesabu jinsi ya kupokea baraka kubwa zaidi na hatima iliyo bora zaidi.
kutoka kwa "Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze tu kupata uponyaji? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili tu niweze kutumia nguvu Zangu kupunga roho chafu kutoka kwenye miili yao? Na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze tu kupokea amani na furaha kutoka Kwangu? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili kuhitaji kutoka Kwangu utajiri mwingi zaidi wa dunia, na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuishi maisha hayo kwa usalama na kuwa salama salmini katika maisha yajayo? Ni wangapi wanaoniamini Mimiili waweze kuepuka tu mateso ya kuzimu na kupokea baraka za mbinguni? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili wapate tulizo lakini hawatafuti kupata chochote kutoka kwa ulimwengu ujao? Niliposhushia hasira Zangu binadamu na kuchukua furaha na amani yote aliyokuwa nayo mwanzo, binadamu akaanza kuwa na shaka. Nilipomkabidhi binadamu mateso ya kuzimu na kuchukua tena baraka za mbinguni, aibu ya binadamu iligeuka na kuwa hasira. Wakati binadamu aliponiomba Mimi kumponya, bado Sikumtambua na vilevile nilimchukia pakubwa, binadamu alienda mbali sana na Mimi na akatafuta njia za waganga na wachawi. Nilipochukua kila kitu ambacho binadamu alitaka kutoka Kwangu, kisha kila kitukilitoweka bila kuonekana tena. Kwa hivyo, Ninasema kwamba binadamu ana imani kwangu Mimi kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata.
kutoka kwa "Unajua Nini Kuhusu Imani?" katika Neno Laonekana katika Mwili
Unachofuata ni cha kukuwezesha kupata amani baada ya kumwamini Mungu—watoto wako wawe huru kutokana na magonjwa, ili mme wako apate kazi nzuri, ili mwana wako apate mke mwema, binti wako apate mme anayeheshimika, ili ndume na farasi wako walime shamba vizuri, kwa mwaka wa hali ya anga nzuri kwa mimea yako. Hili ndilo unalolitafuta. Harakati yako ni kuishi kwa starehe, ili ajali isipate familia yako, ili upepo ukupite, ili uso wako usiguswe na changarawe, ili mazao ya familia yako yasipate mafuriko, ili usiguzwe na majanga yoyote, kuishi katika mikono ya Mungu, kuishi kwenye kiota chenye joto. Mwoga kama wewe, anafuata mwili kila wakati—je, una moyo, una roho? Si wewe ni mnyama? Nakupa njia ya ukweli bila kukuuliza chochote, ilhali hauifuati. Je, wewe ni wale wamwaminio Mungu? Nahifadhi uhai wa ukweli wa binadamu juu yako, ila hauufuati. Je, una tofauti kati ya nguruwe na mbwa? Nguruwe hawafuati maisha ya binadamu, hawafuati kutakaswa, na hawaelewi maana ya maisha. Kila siku wanapokula na kushiba, wanalala. Nimekupa njia ya ukweli, ila hujaipata: Wewe u mkono mtupu. Je, unakubali kuendelea na maisha haya, maisha ya nguruwe? Umuhimu wa watu hao kuwa hai ni nini? Maisha yako ni ya kudharauliwa na kutoheshimika, unaishi huku ukiwa na uchafu na uzinzi, na hufuati lengo lolote; je, si maisha yako ni ya kutoheshimika kwa yote? Je, una ujasiri wa kumtazamia Mungu? Ukiendelea kuwa na uzoefu wa haya, je, si utakosa kupata chochote? Umepewa njia ya ukweli, lakini kama utaipata ama hapana inategemea na kutafuta kwako.
kutoka kwa "Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama wewe hufurahia tu neema ya Mungu, na maisha ya familia yenye amani au baraka yakinifu, basi hujampata Mungu, na imani yako kwa Mungu haijafaulu. Mungu tayari ametekeleza hatua moja ya kazi ya neema katika mwili, na tayari amempa mwanadamu baraka yakinifu—lakini mwanadamu hawezi kufanywa mkamilifu na neema, upendo, na rehema pekee. Katika uzoefu wa mwanadamu yeye hukabiliwa na baadhi ya upendo wa Mungu, na huuona upendo na rehema ya Mungu, lakini baada ya kupitia kwa kipindi fulani cha wakati, yeye huona kwamba neema ya Mungu na upendo na rehema Yake hayawezi kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na hayana uwezo wa kufichua kile ambacho ni potovu ndani ya mwanadamu, wala hayawezi kumwondolea mwanadamu tabia yake potovu, au kufanya kuwa kamilifu upendo na imani yake. Kazi ya Mungu ya neema ilikuwa kazi ya kipindi kimoja, na mwanadamu hawezi kutegemea kufurahia neema ya Mungu ili kumjua Mungu.
kutoka kwa "Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu. Wale wanaotumia upendo kwa Mungu kusitawisha maisha yao yasiyopendeza na kujaza utupu katika mioyo yao ni wale ambao wanataka kuishi katika raha, si wale ambao kweli wanatafuta kumpenda Mungu. Upendo wa aina hii ni kinyume na matakwa ya mtu, harakati ya ridhaa ya hisia, na Mungu hahitaji upendo wa aina hii. Upendo wako, basi, ni upendo wa aina gani? Ni kwa ajili gani unampenda Mungu? Je, ni kiasi gani cha upendo wa kweli, ulicho nacho kwa Mungu sasa? Upendo wa watu wengi kati yenu ni kama uliotajwa hapo awali. Upendo wa aina hii unaweza tu kudumisha hali kama ilivyo; hauwezi kufikia uthabiti wa milele, wala kuchukua mizizi katika mtu. Aina hii ya upendo ni ule wa ua ambalo halizai matunda baada ya kuchanuka na hatimaye kunyauka. Kwa maneno mengine, baada ya wewe kumpenda Mungu mara moja kwa jinsi hii na hakuna mtu wa kukuongoza kwa njia ya mbele, basi utaanguka. Kama unaweza tu kumpenda Mungu katika nyakati za kumpenda Mungu na kutofanya mabadiliko katika tabia ya maisha yako baadaye, basi utaendelea kufunikwa na ushawishi wa giza, bila uwezo wa kutoroka, na bila uwezo wa kujinasua kwa minyororo ya kutumiwa na kupumbazwa na Shetani. Hakuna mtu kama huyu anayeweza kukubaliwa na Mungu; mwishowe, roho zao, nafsi na mwili bado ni mali ya Shetani. Hili ni bila ya shaka. Wale wote ambao hawawezi kukubaliwa kikamilifu na Mungu watarudi mahali pao pa awali, yaani, kwa Shetani, na watakwenda chini kwa ziwa liwakalo moto wa jahanamu kukubali hatua ya pili ya adhabu kutoka kwa Mungu. Wale wanaokubaliwa na Mungu ni wale ambao wanamkataa shetani na kutoroka kutoka kwa miliki ya Shetani. Watu kama wale watahesabiwa rasmi miongoni mwa watu wa ufalme. Hivi ndivyo watu wa ufalme huja kuwa. Je, uko tayari kuwa mtu wa aina hii? Je, uko tayari kukubaliwa na Mungu? Je, uko tayari kutoroka kutoka miliki ya Shetani na kurudi kwa Mungu? Je, sasa wewe ni mali ya Shetani au umehesabiwa miongoni mwa watu wa ufalme? Mambo hayo lazima yote yawe wazi na hayahitaji maelezo zaidi.
kutoka kwa "Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa yote unayotafuta ni kukamilishwa na Mungu na kubarikiwa mwishoni kabisa, basi mtazamo wa imani yako katika Mungu si safi. Unapaswa kuwa ukitafuta jinsi ya kuona matendo ya Mungu katika maisha ya kweli, jinsi ya kumridhisha Yeye wakati anafichua mapenzi Yake kwako, kutafuta jinsi ya kutoa ushahidi kwa maajabu Yake na hekima, na jinsi ya kuonyesha nidhamu na ushughulikiaji Wake kwako. Haya yote ni mambo unapaswa kuwa ukijaribu kuelewa sasa. Kama upendo wako kwa Mungu ni ili tu uweze kushiriki katika utukufu wa Mungu baada ya Yeye kukukamilisha, bado haitoshi na haiwezi kukidhi mahitaji ya Mungu. Unahitaji kuwa na uwezo wa kutoa ushuhuda kwa matendo ya Mungu, kutosheleza mahitaji Yake, na kuwa na uzoefu wa kazi Amefanya kwa watu kwa njia ya vitendo. Iwe ni maumivu, machozi, au huzuni, lazima uyapitie yote kwa vitendo. Haya yote ni ili uweze kuwa shahidi wa Mungu. Je, ni chini ya utawala wa nini hasa sasa unateseka na kutafuta ukamilifu? Je, ni kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu? Je, ni kwa ajili ya baraka za mwili au kwa ajili ya matarajio ya baadaye? Dhamira zako zote, motisha, na malengo ya kibinafsi ya kufuatilia lazima yarekebishwa na hayawezi kuongozwa na mapenzi yako mwenyewe. Kama mtu mmoja anatafuta ukamilifu kupokea baraka na kutawala katika madaraka, wakati yule mwingine anafuatilia ukamilifu kumridhisha Mungu, kwa ajili ya kweli kuwa shahidi wa matendo ya Mungu, je, ni ipi kati ya njia hizi mbili za ufuatiliaji ungeweza kuchagua? Ukichagua ya kwanza, basi bado uko mbali sana na viwango vya Mungu. Nilisema kabla ili kuruhusu matendo Yangu kujulikana wazi katika ulimwengu wote na kwamba ningetawala kama Mfalme katika ulimwengu. Kwa upande mwingine, kilichokabidhiwa kwenu ni kwenda kutoa ushuhuda kwa matendo ya Mungu, si kwa ajili yenu kuwa wafalme na kuonekana ulimwenguni wote. Wacha ulimwengu wote ujazwe na matendo ya Mungu. Wacha kila mtu ayaone na ayakiri. Hili linasemwa kuhusiana na Mungu Mwenyewe, na kile wanadamu wanapaswa kufanya ni kutoa ushuhuda kwa ajili ya Mungu. Je, unajua kiasi gani kuhusu Mungu sasa? Je, unaweza kutoa ushuhuda kwa Mungu kiasi gani? Je, ni lengo gani la Mungu kumkamilisha mwanadamu? Mara baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, je, unapaswa kuonyesha kujali jinsi gani kuelekea mapenzi Yake? Kama uko tayari kukamilishwa na tayari kutoa ushuhuda kwa matendo ya Mungu kulingana na kile unachoishi kwa kudhihirisha, kama una hii nguvu ya msukumo, basi hakuna lililo ngumu sana. Wanachohitaji watu sasa ni kujiamini. Kama una hii nguvu ya msukumo, basi ni rahisi kuachilia chochote chenye uhasi, ubatili, uvivu na mawazo ya mwili, falsafa za maisha, tabia ya uasi, hisia, na mengineyo.
kutoka kwa "Ni Lazima Wale Wanaofaa Kufanywa Wakamilifu Wapitie Usafishaji" katika Neno Laonekana katika Mwili
Jifunze zaidi:  Umeme wa Mashariki

0 评论:

Chapisha Maoni