Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kuitembea-njia-sahihi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kuitembea-njia-sahihi. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 8 Mei 2018

Umeme wa Mashariki | Niliupata Mwanga wa Kweli

Umeme wa Mashariki | Niliupata Mwanga wa Kweli


Qiuhe, Japani
Nilizaliwa katika familia ya Kikatoliki. Tangu nilipokuwa mdogo, nilihudhuria Misa kanisani na babu na bibi yangu. Kutokana na ushawishi wa mazingira yangu na imani yangu kwa Mungu, nilijifunza kuimba maandiko mengi tofauti na kufanya kaida mbalimbali za dini.
Mnamo 2009, niliwasili Japani ili kusoma. Wakati mmoja, katika chumba cha bweni cha mwanafunzi mwenzangu, kwa bahati nilikutana na kiongozi wa kikundi kidogo cha Kikristo aliyekuja kueneza injili. Nilifikiri: Waprotestanti na Wakatoliki humwamini Mungu mmoja. Wote wawili huamini katika Bwana Yesu. Matokeo yake, nilikubali mwaliko wa kiongozi huyo wa kundi ndogo kujiunga naye kanisani. Baada ya kusikiliza wachungaji wakihubiri na kusikia baadhi ya ndugu wa kiume na wa kike wakizungumza juu ya Biblia, nilipata ufahamu fulani juu ya maisha ya Bwana Yesu. Hili lilinisababisha niwe na imani zaidi katika Bwana. Hata hivyo, baada ya miezi michache, wachungaji na wahubiri walituomba kutoa zaka kila wiki. Pia, kila juma, tulipaswa kupeana vijitabu ili kueneza injili. Wakati mwingine, tulikuwa tumechoka kiasi kwamba tungesinzia wakati wa ibada ya Jumapili. Hatukuwa tena na utaratibu wa kawaida katika maisha yetu. Wakati huo, baadhi yetu tulifanya kazi na pia kusoma. Haikutubidi tu kutafuta pesa za kulipia masomo yetu, lakini pia tulihitaji fedha za gharama zetu za kila siku. Maisha yetu yalikuwa ni magumu sana tayari, lakini bado walitaka tuwape fedha zetu na nguvu zetu. Tulikuwa tunakabiliwa na shida nyingi sana na maumivu. Hatua kwa hatua, niligundua kwamba wachungaji na wahubiri hawakuwa kwa kweli watu waliomtumikia Bwana. Kwa kawaida, kwa kuwa walikuwa ndio wale ambao waliliongoza kanisa, wangepaswa kuwa wakitusaidia kukua katika maisha yetu ya kiroho. Hata hivyo, hawakuyajali maisha yetu. Hawakufikiria kabisa kuhusu matatizo yetu ya kivitendo. Badala yake, walitaka nguvu zetu na pesa zetu. Kila kitu walichokifanya kilikuwa ni cha kusaidia kupanua kanisa lao na kuimarisha hali zao na ushawishi wao. Kwa wakati huu, tulihisi kama tulikuwa tumedanganywa. Kwa hivyo, ndugu zangu kadhaa na mimi tuliliacha kanisa.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Baada ya kuacha kanisa, nilipata kanisa moja Katoliki ambalo lilikuwa juu ya mlima. Watu katika kanisa hili walikuwa Wajapani Nilihudhuria Misa mara chache lakini nilihisi kuwa halikunifaidi kiroho. Zaidi ya hayo, ilikuwa vigumu kuhudhuria ushirika, kwa hiyo nililiacha kanisa hilo pia.