Jumamosi, 15 Desemba 2018

4. Sura ya tatizo la mtu asiyejua umuhimu wa jina la Mungu na asiyelikubali jina jipya la Mungu ni ipi?

IV. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Mungu na Majina Yake
4. Sura ya tatizo la mtu asiyejua umuhimu wa jina la Mungu na asiyelikubali jina jipya la Mungu ni ipi?

Umeme wa Mashariki,Yesu,Kristo,siku za mwisho,

Maneno Husika ya Mungu:
Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu angeshikilia ukweli kwamba "Yehova ni Mungu" na "Yesu ni Kristo," ukweli ambao unazingatiwa kwa kipindi kimoja, basi mwanadamu hataweza kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu, basi ataadhibiwaje? Kazi ya Mungu kamwe haijasimama, hatua Zake hazijakwama na kabla kukamilisha kazi Yake ya usimamizi, siku zote Mungu amekuwa mwenye kazi nyingi, na kamwe hajasimama. Lakini mwanadamu ni tofauti: Kutokana na kupata kiwango cha chini cha nguvu za Roho Mtakatifu, yeye huchukulia kwamba hakuna chochote kitakachobadilika; baada ya kupata ufahamu kidogo, hajipi msukumo wa kufuata nyayo za kazi mpya ya Mungu; licha ya kwamba ameona kiasi kazi ya Mungu, yeye anamchukulia Mungu kama kifaa, aina fulani ya umbo la sanamu ya mti, na anaamini kwamba Mungu atasalia kuwa hivyo daima kwani hali imekuwa hii tangu hapo awali na hata katika siku zijazo; akiwa amepata ufahamu wa kijuujuu, mwanadamu ni mwenye kiburi hivi kwamba hujisahau na kuanza kutangaza kwa fujo tabia ya Mungu na hali ya Mungu ambayo haipo; na akiwa amejifunga katika hatua moja ya Roho Mtakatifu, pasi kujali ni mtu wa aina gani ambaye anatangaza kazi mpya ya Mungu, mwanadamu huwa haikubali. Hawa ni watu ambao hawawezi kuikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu; ni watu wenye kushikilia ukale sana, na hawawezi kukubali mambo mapya. Watu kama hawa ni watu wanaomwamini Mungu lakini wakati uo huo wanamkataa Mungu. Mwanadamu anaamini kwamba wana wa Israeli walikosea "tu kumuamini Yehova na kukosa kumuamini Yesu," huku watu wengi wakiiga jukumu ambapo "humwamini Yehova tu na kumkataa Yesu" na "kusubiri kwa hamu kurejea kwa Masihi lakini wanamkataa Masihi ambaye ni Yesu". Ndiyo maana, basi, watu wengi bado wanaishi chini ya mamlaka ya Shetani baada ya kukubali hatua moja tu ya Roho Mtakatifu na bado hawapokei baraka za Mungu. Je, si hii ni kutokana na uasi wa mwanadamu? … Hata ingawa wana "uaminifu wa hali ya juu" kwa maneno yaliyozungumzwa na Mungu; maneno yao na matendo yao bado hukera kwa sababu wao huipinga kazi ya Roho Mtakatifu, na kufanya uongo na uovu. Wale wasiofuata hadi mwisho kabisa, ambao hawazingatii kazi ya Roho Mtakatifu, na ambao wanashikilia kazi ya zamani hawajakosa tu kupata uaminifu kwa Mungu, bali kwa kinyume, wamekuwa wale wanaompinga Mungu, wamekuwa wale ambao wamekanwa na enzi mpya, na watakaoadhibiwa. Kuna wa kuhurumiwa zaidi kuliko wao?
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwanadamu Akiniita Yesu Kristo kila wakati, lakini hajui kuwa nimeanza enzi mpya katika siku za mwisho na Nimeanza kazi mpya, na mwanadamu akingoja kwa hamu kufika kwa Yesu Mwokozi, basi Nitawaita watu kama hao watu wasioniamini. Ni watu ambao hawanijui, na imani yao Kwangu ni bandia. Watu hao wanaweza kushuhudia kufika kwa Yesu Mwokozi kutoka mbinguni? Wanachongoja sio kufika Kwangu, bali ni kufika kwa Mfalme wa Wayahudi. Hawatamani maangamizo Yangu ya dunia hii nzee yenye uchafu, badala yake, wanatamani kurudi kwa Yesu mara ya pili, ambapo watakombolewa; wanamtazamia Yesu kumkomboa binadamu mara nyingine kutoka kwa hii dunia iliyochafuliwa na isiyo na haki. Watu hao watakuwa vipi wale wanaokamilisha kazi Yangu katika siku za mwisho? Tamaa ya mwanadamu haina uwezo wa kufikia matakwa Yangu ama kutimiza kazi Yangu, kwani mwanadamu hutamani tu au kuenzi kazi ambayo Nimefanya hapo awali, na hawajui kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mpya kila siku na hawi mzee. Mwanadamu anajua tu kuwa Mimi ni Yehova, na Yesu, na hana ufahamu kuwa Mimi ni Mwisho, Yule Ambaye Ataleta binadamu kufika mwisho. Yale ambayo mwanadamu anatamani na kujua ni ya dhana yake mwenyewe, na ni yale tu ambayo anaweza kuyaona na macho yake mwenyewe. Hayako sambamba na kazi Ninayofanya, bali kwa mvurugano nayo.
kutoka kwa "Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mkitumia dhana kupima na kufafanua kwa Mungu kwa maneno, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiobadilika, na mkiwekea Mungu mipaka katika Bibilia, na kumweka katika wigo wenye mipaka wa kazi, basi hili linathibitisha kwamba mmemshutumu Mungu. Kwa sababu katika mioyo yao, Wayahudi wa Agano la Kale walimtazama Mungu kama sanamu wa udongo, kana kwamba Mungu anaweza tu kuitwa Masihi, na Yule pekee anayeitwa Masihi ndiye Mungu, na kwa sababu walitumikia na kumwabudu kana kwamba Alikuwa sanamu ya udongo (kisicho na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—wakimhukumu Yesu Asiyekuwa na hatia kwa kifo. Mungu hajatenda uhalifu wowote, ilhali mwanadamu hakumsamehe Mungu, na kumhukumu Yeye kifo bila kusita. Na ndivyo Yesu Akasulubishwa. Mwanadamu kila wakati huamini kuwa Mungu habalidiliki na humfafanua kulingana na Bibilia, kana kwamba mwanadamu ameona ndani ya usimamizi wa Mungu, kana kwamba kila kitu Atendacho Mungu kiko mikononi mwa mwanadamu. Wanadamu ni wa kufanya mzaha pakubwa, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha lugha ya kushawishi ya kujivuna. Bila kujali kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu, Bado Nasema kwamba bado humfahamu Mungu, kwamba hakuna walio wapinzani wa Mungu zaidi, na kwamba unamshutumu Mungu, kwa kuwa huna uwezo wa kuiheshimu kazi ya Mungu na kutembea katika njia ya kufanywa kuwa kamili ya Mungu. Ni kwa nini Mungu hatosheki na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hajui Mungu, kwa sababu ana dhana nyingi na kwa sababu badala ya kufuata ukweli, maarifa yake yote ya Mungu yametolewa kutoka kwenye chanzo kimoja, chenye ugumu na kisichobadilika. Hivyo, kwa kuwa amekuja duniani leo, Mungu Amesulubishwa kwa mara nyingine msalabani na mwanadamu.
kutoka kwa "Waovu Lazima Waadhibiwe" katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu kama hawa, wakaidi na washenzi wanaweza kupata baraka za Mungu? Watawezaje, kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya kweli iliyozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni, ikiwa kwamba hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kuwa huwezi kumpinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale ambao hawakumfahamu Masiha wote walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, kumkataa Yesu, kumpaka Yeye tope. Watu wasiomwelewa Yesu wote wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kuwa uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliye kurudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje, kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni asili ya watu ambayo itaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia raha ya ulimwengu wa mbinguni, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupata ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, kisha mnazikiri, wakati baada ya mwingine? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?
kutoka kwa "Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia" katika Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

0 评论:

Chapisha Maoni