Ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili na Maana ya Kuteseka.
Maneno Husika ya Mungu:
Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo.
si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu! Mungu ana hamu ya mwanadamu kumpenda Yeye, lakini kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo kuteseka kwa mwanadamu huwa kwingi zaidi, na kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo majaribio ya mwanadamu huwa makubwa zaidi. Ikiwa unampenda Yeye, basi kila aina ya mateso yatakufika—na ikiwa humpendi, basi labda kila kitu kitaendelea kwa urahisi kwako, na kila kitu kinachokuzunguka kitakuwa kitulivu kwako. Unapompenda Mungu, utahisi kwamba mengi kandokando yako hayawezi kushindikana, na kwa sababu kimo chako ni kidogo sana utasafishwa; aidha, huwezi kumridhisha Mungu, na daima utahisi kwamba mapenzi ya Mungu ni ya juu sana, kwamba hayawezi kufikiwa na mwanadamu. Kwa sababu ya haya yote utasafishwa—kwa sababu kuna udhaifu mwingi ndani yako, na mengi yasiyoweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, utasafishwa ndani. Lakini lazima muone kwa dhahiri kwamba utakaso hutimizwa tu kupitia usafishaji. Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kwa rehema ya Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana. Unapojaribiwa, unapaswa kusema: "Moyo wangu ni wa Mungu, na Mungu tayari amenipata. Siwezi kukuridhisha wewe—lazima nitoe kila kitu changu ili kumridhisha Mungu." Kadri unavyomridhisha Mungu, ndivyo Mungu hukubariki zaidi, na ndivyo nguvu za upendo wako kwa Mungu huwa kuu zaidi; kwa hiyo, vilevile, utakuwa na imani na azimio, na utahisi kwamba hakuna kilicho na thamani zaidi au cha maana kuliko kutumia maisha ukimpenda Mungu. Inaweza kusemwa kwamba mwanadamu anatakiwa tu kumpenda Mungu ili kuishi bila huzuni. Ingawa kuna nyakati ambazo mwili wako ni dhaifu na unazongwa na matatizo mengi ya kweli, katika nyakati hizi utamtegemea Mungu kweli, na ndani ya roho yako utafarijiwa, na utahisi hakika, na kwamba una kitu cha kutegemea. Kwa njia hii, utaweza kushinda hali nyingi, na kwa hiyo hutalalamika kuhusu Mungu kwa sababu ya uchungu unaopitia; utataka kuimba, kucheza, na kuomba, kukusanyika na kuwasiliana kwa karibu, kumfikiria Mungu, na utahisi kwamba watu wote, mambo, na vitu vilivyo kandokando yako ambavyo vimepangwa na Mungu vinafaa. Kama humpendi Mungu, yote ambayo unategemea yatakuwa yenye kero kwako, hakuna kitakachokuwa cha kufurahisha machoni mwako; ndani ya roho yako hutakuwa huru bali wa kudhulumiwa, moyo wako daima utalalamika kuhusu Mungu, na daima utahisi kwamba unapitia mateso mengi sana, na kwamba ni udhalimu sana. Kama hufuatilii kwa ajili ya furaha, bali ili umridhishe Mungu na kutoshtakiwa na Shetani, basi ukimbizaji kama huo utakupa nguvu nyingi za kumpenda Mungu. Mwanadamu anaweza kutekeleza yote yanayonenwa na Mungu, na yote ayafanyayo yanaweza kumridhisha Mungu—hii ndiyo maana ya kuwa na hakika. Kufuatilia ridhaa ya Mungu ni kuutumia upendo wa Mungu kutia maneno Yake katika vitendo; pasipo kutia maanani wakati—hata kama wengine hawana nguvu—ndani yako bado kuna moyo unaompenda Mungu, ambao unamtamani Mungu sana, na humkosa Mungu. Hiki ni kimo halisi. Jinsi ambavyo kimo chako ni kikubwa hasa hutegemea jinsi upendo wako kwa Mungu ulivyo mkuu, kama unaweza kusimama imara wakati unajaribiwa, kama wewe ni mdhaifu hali fulani inapokujia, na kama unaweza kusimama imara wakati ambapo ndugu zako wanakukataa; majilio ya ukweli yataonyesha hasa upendo wako kwa Mungu ukoje. Inaweza kuonekana kutoka kwa kazi nyingi ya Mungu kwamba Mungu kweli anampenda mwanadamu, ni hasa tu macho ya roho ya mwanadamu bado hayajafunguliwa kabisa, na hawezi kufahamu kazi nyingi ya Mungu, na mapenzi ya Mungu, na vitu vingi ambavyo ni vya kupendeza kuhusu Mungu; mwanadamu ana upendo kidogo sana wa kweli kwa Mungu. Umemwamini Mungu kotokote katika wakati huu wote, na leo Mungu amezuia njia zote za kutoroka. Kusema kwa kweli, huna chaguo lingine ila kuifuata njia sahihi, njia sahihi ambayo umeelekezwa kwayo kwa hukumu kali na wokovu mkubwa kabisa wa Mungu. Ni baada tu ya kupitia taabu na usafishaji ndiyo mwanadamu hujua kwamba Mungu ni wa kupendeza. Baada ya kupitia mpaka leo, inaweza kusemwa kwamba mwanadamu amekuja kujua sehemu ya kupendeza kwa Mungu—lakini hili bado halitoshi, kwa sababu mwanadamu amepungukiwa sana. Lazima apate uzoefu zaidi wa kazi ya Mungu ya ajabu, na zaidi ya usafishaji wote wa mateso uliowekwa na Mungu. Ni wakati huo tu ndiyo tabia ya maisha ya mwanadamu itaweza kubadilishwa.
kutoka kwa "Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungui" katika Neno Laonekana katika Mwili
281 Uchungu ni Mojawapo ya Baraka za Mungu
1. Usife moyo, usiwe mnyonge, Mungu atakufichulia, Mungu atakufichulia. Njia ya kwenda katika ufalme si nyororo hivyo, hakuna kilicho rahisi vile! Unataka baraka zije kwa urahisi. Leo kila mtu atakuwa na majaribu machungu ya kukabiliana nayo, la sivyo moyo wa upendo ulio nao kwa Mungu hautaendela kuwa wenye nguvu na hutakuwa na upendo wa kweli, oo, hutakuwa na upendo wa kweli kwa Mungu. Hata kama ni hali ndogo tu, kila mtu lazima azipitie, ni kwamba tu zinatofautiana kwa kiwango fulani. Aa, hali hii ni mojawapo ya baraka za Mungu, ni wangapi, oo, ni wangapi mara nyingi hupiga magoti mbele ya Mungu kuomba baraka Zake?
2. Wewe huhisi kwamba maneno machache ya bahati huhesabika kama baraka za Mungu, ilhali huhisi kwamba uchungu ni mojawapo ya baraka Zake. Wale wanaoshiriki katika uchungu Wake hakika watashiriki katika utamu Wake. Hiyo ni ahadi ya Mungu na baraka Zake kwako. Lazima ujitolee kila kitu chako kuulinda ushuhuda wa Mungu. Hili litakuwa lengo la matendo yako, usisahau hili. Lakini sasa, umepungukiwa na imani, oo, umepungukiwa na imani na uwezo wa kutofautisha mambo na daima huwezi kuelewa neno la Mungu na makusudi Yake. Hata hivyo, usiwe na wasiwasi. Tumia muda mwingi zaidi mbele ya Mungu na usitilie maanani chakula na nguo kwa ajili ya mwili wa juu. Tafuta makusudi ya Mungu mara nyingi, na Atakuonyesha kwa wazi makusudi hayo. Pole pole utapata makusudi Yake katika kila kitu, ili kwamba Awe na njia ya kwenda katika kila mtu bila vizuizi. Itauridhisha moyo wa Mungu na utapokea baraka pamoja na Yeye milele na milele, oo, milele na milele!
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Watu wengi sasa wanamwamini Mungu ila hawajaingia katika njia iliyo sawa. Bado wanahisi watupu na watepetevu, wakati mwingine hata kuhisi kana kwamba kuishi kote ni mateso, utupu wote—hata wanatamani kufa! Hivi ndivyo mtu alivyo kabla ya moyo wake kuwa na maono. Mtu wa aina hii hajapata ukweli na hamjui Mungu bado, hivyo bado hahisi furaha nyingi ya ndani. Hususan nyinyi ambao mmepitia mateso na ugumu wakati wa kurudi nyumbani, mmeteseka na pia mna fikra za kifo na kutokuwa na radhi kuishi; huu ndio udhaifu wa mwili. Baadhi ya watu hata hufikiri kuwa ikiwa wanamwamini Mungu basi wanapaswa kuhisi ridhaa ndani yao. Katika Enzi ya Neema Roho Mtakatifu bado alitoa amani na furaha kwa watu. Sasa kuna amani na furaha kidogo sana; hakuna ridhaa kama iliyokuwa wakati wa Enzi ya Neema. Leo kumwamini Mungu kunaudhi. Unajua tu kuwa ridhaa ya mwili ni nzuri kupita chochote kingine. Hujui kile ambacho Mungu anafanyia kazi leo. Mungu anaruhusu miili yenu iteseke ili kubadilisha tabia yenu. Hata ingawa miili yenu inateseka, mna neno la Mungu na mna baraka ya Mungu. Huwezi kufariki hata ukitaka: Je, unaweza kukubali bila malalamiko kutomjua Mungu na kutopata ukweli? Sasa hasa ni kuwa bado watu hawajapata ukweli tu, na hawana maisha. Sasa watu wako katikati ya mchakato wa utafutaji wa wokovu, hivyo lazima wayapitie baadhi ya hayo wakati huu. Leo kila mtu duniani hujaribiwa: Mungu bado anaumia—je, ni vyema kwamba usiteseke? Bila kusafishwa kupitia maafa makubwa hakuwezi kuwa na imani halisi, na ukweli na uzima havitapatikana. Kutokuwa na majaribio na usafisho kusingesaidia. … Je, mateso mnayokumbana nayo sasa si sawa na mateso ya Mungu? Mnateseka pamoja na Mungu, na Mungu yuko pamoja na watu katika mateso yao, siyo? Leo nyinyi nyote mna sehemu katika mateso ya Kristo, ufalme, na subira, na kisha, mwishowe Mtapata utukufu! Aina hii ya mateso ina umuhimu. Kutokuwa na azimio hakutasaidia. Ni lazima uelewe umuhimu wa mateso ya leo na kwa nini lazima uteseke hivyo. Tafuta ukweli mdogo kutoka kwa hili na kuelewa machache ya nia ya Mungu, na kisha utakuwa na azimio la kuvumilia mateso. Ikiwa huelewi nia ya Mungu na unatafakari tu kuhusu mateso yako, basi kadri unavyozidi kuyawaza ndivyo itazidi kuwa vidumu kuvumilia—hilo lasumbua …. Hivyo, vitu hivi vyote lazima viangaliwe waziwazi, na ukweli sharti ueleweke kutoka kwa vitu hivi. Watu wanapokuwa na ukweli, wanakuwa na nguvu. Wanapokuwa na ukweli, miili yao inajawa na nguvu isiyoisha. Wanapokuwa na ukweli, wanakuwa na radhi. Bila ukweli, wao ni kama makapi laini ya tofu. Na ukweli, wao ni dhabiti na wenye kutiwa moyo, na hawahisi kuwa mateso yao ni mateso bila kujali wanavumilia mangapi. Kuteseka kwenu huku kunaleta nini? Mungu mwenye mwili bado Anateseka! Ninyi ni watu ambao wanapotoshwa na Shetani na wenye asili inayoasi dhidi ya Mungu. Nyote mmeyafanya mambo mengi yanayomuasi Mungu bila ufahamu, katika kumpinga Mungu. Mnapaswa kuhukumiwa na mnapaswa kuadibiwa. Mtu anayeugua hawezi kuogopa kuteseka anapotibiwa, hivyo ni vyema kwenu, ninyi mnaotaka tabia zenyu potovu kubadilishwa na kuupata uzima, kutoumia kidogo? Mateso yenu yanapasa kuvumiliwa; lazima yavumiliwe. Mateso haya hayaanguki juu ya yasiyo na kosa, na hata zaidi hayalazimishwi kwanu. Mnayoyapata sasa si lolote ila ugumu wa safari yenu ya mara kwa mara na uchovu mdogo kutoka kwa kazi yenu. Wakati mwingine mnapitia usafisho kiasi katika neno la Mungu. Wakati mwingine mnakuwa na ufahamu wa upotovu wenu wenyewe na kuhisi kuwa kamwe hambadiliki, na kwa kiasi mnateswa na asili yenu potovu. Wakati mwingine kuna sehemu ya neno la Mungu ambalo hamwezi kulielewa asilani, ama mioyo yenu inachomwa inaposoma neno la Mungu na mnahisi kuumizwa. Ama, ninyi hufanya kazi yenu vibaya na daima kuyafanya makosa, mkijilaumu, mkichukia kwamba hamwezi kustahimili na kwamba hamwezi kufanya kazi. Mnateseka kwa njia hizi zote,. Wakati mwingine mnawaona wengine wakiendelea na mnahisi kuwa kuendelea kwenu ni kwa asteaste sana, kwamba mnalipokea neno la Mungu polepole sana, kwamba mwanga ni nadra kabisa. Mnayapata mengine kwa njia hizi; je, kuna mateso yapi mengine kando na ya aina hizi? Hamfanyishwi kazi yoyote kubwa, na hamna wakuu ama mabwana wanaowachapa wala kuwalaani, na hakuna anayewafanya kuwa watumwa. Hamyapiti yoyote hayo, siyo? Dhiki mnazopitia sizo dhiki halisi kabisa. Fikiria kuhusu hilo kwa muda mdogo—je, hali si hiyo? Wakati mwingine mazingira yenu yanawatisha, yakiweka akili zenu katika hali ya wasiwasi, yakiwazuia kuwa na mapunziko, na mnateseka kidogo kuishi na hofu. Lazima muelewe ni nini maana ya kutoa kwenu kwa familia yenu na kutumia rasilmali yenu kwa ajili ya Mungu na kwa nini mnataka kufanya haya. Ikiwa ni ili kutafuta ukweli, kutafuta uzima, na kufanya machache ili kutimiza jukumu lenu na kulipiza upendo wa Mungu, basi hiyo ni ya haki kabisa, kitu kizuri, na ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya ulimwengu. Katika hali hii, hamtawahi kuwa na majuto, na mtaweza kuachilia familia zenu bila kujali hali. Sivyo? Ikiwa u wazi juu ya umuhimu huu basi hutakuwa na majuto, na hutakuwa mbaya. Ikiwa, hata hivyo, huji kutumia rasilmali yako kwa ajili ya Mungu, basi haina maana, na unapaswa kurudi haraka, na punde unapoona jambo hilo waziwazi tatizo litatatuliwa na hakutakuwa na haja ya wasiwasi; yote yako mikononi mwa Mungu.
Sasa ninyi nyote mnapitia dhiki kiasi ya majaribio. Baadhi yenu mna ukweli fulani; wengine hawana. Baadhi ya watu huupokea kwa njia hii; wengine hupokea kwa njia nyingine. Bila kujali unavyoupokea, mradi kuna ukweli ndani yako na unaupokea kwa njia sahihi, mateso yako yatakuwa na maana na thamani, utakuwa na ushupavu, na utafanikiwa hadi mwisho. Usipopokea ukweli ila upokee tu fikra za mwanadamu na mawazo, basi kuteseka kwako hakuna maana kwa sababu hujaupata ukweli.
kutoka kwa "Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Lazima uvumilie mateso kwa ajili ya ukweli, lazima ujitoe kwa ajili ya ukweli, lazima uvumilie udhalilishaji kwa ajili ya ukweli, na kupata ukweli zaidi lazima upate mateso zaidi. Hili ndilo unalopaswa kufanya. Msitupilie mbali ukweli kwa ajili ya maisha ya amani ya familia, na lazima msiipoteze heshima na uadilifu wa maisha kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Unapaswa kufuata yote ambayo ni ya kupendeza na mema, na unapaswa kufuata njia katika maisha ambayo ni ya maana zaidi. Kama wewe unaishi maisha ya kishenzi, na wala hufuati malengo yoyote, je, si huko ni kupoteza maisha Yako? Ni nini unachoweza kupata kutoka kwa maisha ya aina hii? Unapaswa kuziacha starehe zote za mwili kwa ajili ya ukweli mmoja, na hupaswi kutupilia mbali ukweli wote kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Watu kama hawa hawana uadilifu au heshima; hakuna maana ya kuwepo kwao!
kutoka kwa "Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Jambo fulani linafanyika linalokutaka uvumilie hali ngumu, wakati huo unapaswa ufahamu ni nini mapenzi ya Mungu, na ni jinsi gani unapaswa kuyajali mapenzi ya Mungu. Usijiridhishe mwenyewe: Jiweke kando kwanza. Hakuna kitu kilicho duni kuliko mwili. Ni lazima udhamirie kumridhisha Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako. Katika mawazo kama hayo, Mungu atakupa nuru ya kipekee katika jambo hili, na moyo wako pia utapata faraja. Jambo lolote likikutendekea, liwe dogo au kubwa, ni sharti kwanza ujiweke pembeni na kuuona mwili kama kitu duni zaidi kuliko vitu vyote. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo unavyochukua uhuru zaidi; ukiuridhisha mara hii, wakati mwingine utataka zaidi, na jinsi hili linaendelea, ndivyo unapata kuupenda mwili hata zaidi. Mwili mara zote una tamaa kupita kiasi, mara zote mwili unakutaka uuridhishe, na kwamba uutosheleze kwa ndani, iwe ni katika chakula unachokula, unachokivaa, au kuwa na hasira katika matendo yako, au kuushawishi udhaifu na uzembe wako… Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo tamaa yake inaongezeka, na jinsi mwili unavyopotoka zaidi, hadi kufikia kiwango ambacho miili ya watu inahodhi dhana nzito, na kutomtii Mungu, na kujiinua, na kuanza kuishuku kazi ya Mungu. … Inasemekana kuwa kulikuwepo na mkulima aliyeona nyoka barabarani aliyekuwa ameganda. Huyu mkulima alimchukua yule nyoka na kumweka kifuani mwake, na baada ya yule nyoka kuamka alimuuma yule mkulima hadi akafa. Miili ya wanadamu ni kama yule nyoka: asili yake ni kuyadhuru maisha yao—na ikipata mbinu yake kikamilifu, maisha yako yanapotea. Mwili ni wa Shetani. Kuna tamaa kupita kiasi ndani yake, hujithamini wenyewe, unafurahia faraja, na kushangilia burudani, kujiachilia katika uvivu na uzembe, na baada ya kuuridhisha kwa kiwango fulani mwishowe utakuangamiza. Hivi ni kusema, ukiuridhisha sasa, wakati mwingine utakuomba zaidi. Daima mwili una tamaa na matakwa kupita kiasi, na unajinufaisha kutokana na wewe kuutosheleza mwili na kukufanya uufurahie hata zaidi na kuishi katika starehe zake—na ikiwa hutaushinda, mwishowe utajipotosha. Iwapo utapata uzima mbele za Mungu, na namna hatima yako itakavyokuwa, inategemea uasi wako dhidi ya mwili utakuwa wa namna gani. Mungu amekuokoa, na kukuteua na kukuamulia kabla, bado ikiwa leo hauko radhi kumridhisha, hauko radhi kuuweka ukweli katika vitendo, hauko radhi kuuasi mwili wako kwa moyo umpendao Mungu kwa dhati, hatimaye utajiangamiza mwenyewe, na kwa hivyo utapitia mateso mengi. Ikiwa mara zote unautosheleza mwili, Shetani atakumeza hatua kwa hatua, na kukuacha bila uzima, au upako wa Roho, hadi siku itafika ambayo ndani utakuwa giza. Ukiishi katika giza, utakuwa umetekwa nyara na Shetani, hutakuwa na Mungu tena, na wakati ule utaukataa uwepo wa Mungu na kumwacha.
kutoka kwa "Kumpenda Mungu Tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita.
kutoka kwa "Kumpenda Mungu Tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu anawataka watu kuweka ukweli katika matendo kimsingi kushughulikia mambo yaliyo ndani yao, kushughulikiwa fikira zao, na dhana zao ambazo haziufuati moyo wa Mungu. Roho Mtakatifu anawagusa watu ndani, na kuendeleza kazi Yake ndani yao, na kwa hivyo katika tukio lolote kuna vita: kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, huwa kuna vita vikali, na japokuwa mambo yanaweza kuonekana shwari katika miili yao, ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona—na ni baada tu ya hivi vita vikali, baada ya kutafakari kwa kina, ndipo ushindi au kushindwa kunaweza kuamuliwa. Mtu anashindwa kujua ama acheke au alie. Kwa sababu motisha nyingi ndani ya watu zina makosa, ama kwa sababu kazi kubwa ya Mungu inakinzana na dhana zao, watu wakiuweka ukweli katika vitendo vita vikali huzuka kisirisiri. Baada ya kuuweka huu ukweli katika vitendo, kisirisiri watu watakuwa wamemwaga machozi mengi sana ya huzuni kabla ya kuamua kumridhisha Mungu. Ni kwa sababu ya vita hivi watu huvumilia shida na usafishaji; huku ni kuteseka kwa kweli. Vita vikikukabili, kama unaweza kusimama kweli upande wa Mungu, utaweza kumridhisha. Kuteseka katika harakati ya kutenda ukweli hakuepukiki; ikiwa, wanapoweka ukweli katika vitendo, kila kitu ndani yao kingekuwa sawa, basi wasingehitaji kufanywa wakamilifu na Mungu, na kusingekuwa na vita, na hawangeteseka. Ni kwa sababu kuna mambo mengi ndani ya watu ndipo hawafai kutumiwa na Mungu, na tabia nyingi za uasi wa mwili, ndipo watu wanapaswa kujifunza funzo la kuasi dhidi ya mwili kwa kina zaidi. Huku ndiko Mungu anaita kuteseka ambako Alimtaka mwanadamu kushiriki Naye.
kutoka kwa "Kumpenda Mungu Tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuona kama una kibali cha Mungu ni hasa kutazama mambo kama vile iwapo una Roho Mtakatifu akifanya kazi kwako, kama Roho Mtakatifu anakupa nuru na kukuongoza, na kama unaambatana na neema fulani. Watu wengine walipofanya kazi yao mara ya kwanza, walikuwa na nguvu nyingi, kana kwamba hawangeishiwa kamwe. Lakini ni jinsi gani kwamba wanapoendelea wanaonekana kupoteza nguvu hizo? Mtu waliyekuwa wakati ule na mtu waliye sasa ni kama watu wawili tofauti. Kwa nini walibadilika? Sababu ilikuwa nini? Ni kwa sababu imani yao kwa Mungu ilienda njia mbaya kabla ya kufika kwenye njia sahihi. Walichagua njia mbaya. Kulikuwa na kitu kilichofichika ndani ya utafutaji wao wa awali, na kwa wakati muhimu jambo hilo liliibuka. Ni nini kilichofichwa? Ni matarajio ambayo yako ndani ya mioyo yao wakati wanamwamini Mungu, matarajio kuwa siku ya Mungu inawadia hivi karibuni ili upweke wao utafika mwisho; matarajio kwamba Mungu atabadilishwa na kwamba mateso yao yote yataisha. Wote wanaingoja kwa hamu siku ambayo wanaweza kurudi nyumbani ili kuungana tena na familia zao, wakati hakuna mateso tena, wakati ambapo wako huru kabisa, wakati wanaweza kumwamini Mungu bila vikwazo vyovyote na wengine, na kila mtu anaweza kuishi katika mazingira mazuri ambapo anaweza kuvaa vizuri na kula vizuri. Je, si wote wana tumaini hili? Mawazo haya yapo katika kina cha mioyo yao kwa sababu mwili wa mwanadamu hauko tayari kuteseka na hungoja kwa hamu siku bora wakati wowote unapopitia mateso. Mambo haya hayatafichuliwa bila hali sahihi.[a] Wakati hakuna hali, kila mtu ataonekana kuwa sawa hasa, ataonekana kwa kweli kuwa na kimo, kuelewa ukweli vizuri zaidi, na kuonekana kuwa na nguvu nyingi kuliko kawaida. Siku moja, wakati hali itatokea, mawazo haya yote yatatoka. Akili yao itaanza kupambana, na wengine wataanza kuanguka. Sio kwamba Mungu hakufungulii njia ya kuepa, au kwamba Mungu hakupi neema Yake, na kwa hakika si kwamba Mungu hajali kuhusu matatizo yako. Ni kwamba kuvumilia maumivu haya sasa ni baraka yako, kwa sababu lazima ustahimili mateso kama hayo ili uokolewe na kuishi, na imeshapangiwa kabla. Kwa hivyo ili mateso haya yakupate wewe ni baraka yako. ... maana ya sababu yake ni ya kina sana, yenye umuhimu sana.
kutoka kwa "Wale ambao Wamepoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Wako Hatarini Zaidi" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Mnapaswa kila mara kuwa waangalifu. Ingawa mnaishi mahali pachafu hamjawekwa mawaa na uchafu na mnaweza kuishi ubavuni mwa Mungu, mkipokea ulinzi Wake mkuu. Mmechaguliwa miongoni mwa wote walio katika nchi hii ya manjano. Je, ninyi sio watu waliobarikiwa zaidi? Kama kiumbe aliyeumbwa, unapaswa bila shaka kumwabudu Mungu na kufuatilia maisha yenye maana. Usipomwabudu Mungu na uishi katika mwili mchafu, basi wewe siye mnyama tu aliye ndani ya vazi la mwanadamu? Kama binadamu, unapaswa kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso. Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu, kama Petro. Katika ulimwengu huu, mwanadamu huvaa mavazi ya ibilisi, hula chakula kinachotolewa na ibilisi, na hufanya kazi na kutumika chini ya Shetani, na kukanyagiwa ndani ya uchafu wake. Usipoelewa maana ya maisha au njia ya kweli, basi ni nini maana ya maisha yako? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale wanaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?
kutoka kwa "Utendaji (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili
(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?
Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, umepokea utukufu mkuu na wokovu wa Mungu kabisa. Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu wake kutoka kwa Israeli, watu wake wateule, hadi kwako, ili kufanya kusudio lake lijidhihirishe kwenu kama kundi. Kwa hiyo, ninyi ndinyi mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu. Pengine utayakumbuka maneno haya: "Kwa maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda mfupi tu, inatufanyia utukufu mzito wa milele unaozidi kuwa mwingi sana." Zamani, mlisikia msemo huu, lakini hakuna aliyeelewa maana kamili ya maneno yale. Leo, unajua vyema umuhimu wa maneno yale. Maneno haya ndiyo yatakayotimizwa na Mungu katika enzi za mwisho. Yatatimia kwa wale walioteswa na joka kuu jekundu katika sehemu linakoishi. Joka kuu jekundu humtesa Mungu na ni adui wa Mungu, kwa hiyo katika nchi hii, wanaomwamini Mungu wanateswa na kudhihakiwa. Ndiyo sababu maneno haya yatakuja kuwa kweli kwenu nyie kundi la watu. Kazi inapotekelezwa katika nchi inayompinga Mungu, kazi Yake yote inakabiliwa na vizuizi vya kupita kiasi, na mengi ya maneno Yake hayawezi kutimizwa katika wakati ufaao: ndiyo maana, watu husafishwa kwa ajili ya neno la Mungu. Hiki pia ni kipengele cha mateso. Ni vigumu kabisa kwa Mungu kutekeleza kazi yake katika nchi yenye joka kuu jekundu, lakini ni kupitia ugumu huu ndipo Mungu Hupiga hatua katika kazi Yake ili kudhihirisha hekima Yake na matendo Yake ya ajabu. Mungu Huchukua fursa hii kuwakamilisha watu hawa wa kikundi hiki. Kwa ajili ya mateso ya watu, tabia yao na hulka ya kishetani ya watu katika nchi hii najisi, Mungu Anafanya kazi Yake ya kutakasa na ushindi, ili, kutokana na hili, apokee utukufu na kuwapata wale wote wanaoshuhudia matendo Yake. Huu ndio umuhimu wa kujitoa kwa Mungu kwa ajili ya kikundi hiki cha watu. Ina maana kuwa Mungu hufanya kazi ya ushindi kupitia wale wanaompinga. Kwa hiyo, kufanya vile kunadhihirisha nguvu za Mungu. Kwa maneno mengine, ni wale tu walio katika nchi najisi ndiyo wanaostahili kuurithi utukufu wa Mungu na ni hili tu ambalo litafanya nguvu kuu za Mungu kuwa maarufu. Ndiyo maana Nasema kuwa utukufu wa Mungu unapatikana katika nchi najisi na kwa wale wanaoishi humo. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu. Hii ni kama tu ilivyokuwa katika kazi ya Yesu; Angetukuzwa tu kati ya Wafarisayo waliomdhihaki. Isingelikuwa mateso na usaliti wa Yuda, Yesu asingelidhihakiwa na kudharauliwa, na hata zaidi kusulubiwa, na hivyo asingelipokea utukufu. Kila mara Mungu Anapofanya kazi katika wakati fulani na kila mara anapofanya kazi Yake kwa kupitia mwili, huwa Anapokea utukufu na papo hapo huwapata Anaotaka kuwapata. Huu ndio mpango wa kazi ya Mungu na hivi ndivyo anavyosimamia kazi Yake.
Katika mpango wa Mungu wa miaka elfu kadhaa, kazi inayofanywa ndani ya mwili ni katika sehemu mbili: Kwanza ni kazi ya kusulubiwa, ambayo kwayo anatukuzwa; nyingine ni kazi ya ushindi na ukamilifu katika nyakati za mwisho, ambayo kwayo pia Atapokea utukufu. Huu ni usimamizi wa Mungu. Hivyo basi, usichukulie kazi ya Mungu au agizo Lake kwako kuwa rahisi sana. Ninyi ndinyi warithi wa uzito wa milele wa utukufu wa Mungu, hili liliteuliwa na Mungu. Katika sehemu hizo mbili za utukufu wa Mungu, moja inafichuliwa ndani yako; ukamilifu wa sehemu moja ya utukufu Wake umepewa ili uwe urithi wako. Huku ndiko kutukuzwa kutoka kwa Mungu na mpango wake uliopangwa kitambo. Kutokana na ukuu wa kazi aliyoifanya Mungu katika nchi ambako joka kuu jekundu linaishi, kazi kama hii, ikipelekwa katika sehemu nyingine, ingezaa tunda zuri kitambo na ingekubaliwa na mwanadamu kwa urahisi. Na kazi kama hii ingekuwa rahisi sana kukubaliwa na viongozi wa dini wa Magharibi wanaomwamini Mungu, kwani kazi ya Yesu ni kama kielelezo. Ndio maana Hawezi kutekeleza hatua hii ya kazi ya utukufu mahali pengine; yaani, kwa kuwa kuna uungaji mkono kwa watu wote na utambulisho wa mataifa yote, hamna mahali ambapo utukufu wa Mungu unaweza "kupumzikia." Na huu ndio umuhimu wa kipekee wa hatua hii ya kazi katika nchi hii. Kati yenu, hamna mtu mmoja anayepokea ulinzi wa sheria; badala yake, unaadhibiwa na sheria, na ugumu mkubwa zaidi ni kuwa hapana mtu anayekuelewa, awe ni jamaa yako, wazazi wako, marafiki wako, ama watendakazi wenzako. Hakuna anayekuelewa. Mungu "Anapokukataa," hapana uwezekano wako kuendelea kuishi duniani. Hata hivyo, watu hawawezi kumwacha Mungu; huu\ ndio umuhimu wa ushindi wa Mungu kwa watu, na huu ni utukufu wa Mungu. Kile ambacho umerithi wakati huu, kimepiku walichorithi mitume na manabii na ni kikuu zaidi kuliko alichopokea Musa na Petro. Baraka haziwezi zikapokewa kwa siku moja au mbili; sharti zipatikane kwa kujitolea kwingi. Yaani, lazima uwe na upendo uliosafishwa, imani kuu, na ukweli mwingi ambao Mungu Anakuagiza uufikie; zaidi ya hayo, sharti uelekeze uso wako kwa haki wala usikubali kushindwa, na lazima uwe na upendo usiofikia kikomo kwa Mungu. Azimio linahitajika kutoka kwako, na vilevile mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Upotovu wako lazima utibiwe, na lazima ukubali mipango ya Mungu pasipo kulalamika, na hata uwe mtiifu hadi kifo. Hicho ndicho unachopaswa kutimiza. Hili ndilo lengo la Mungu la mwisho, na matakwa ya Mungu kwa watu wa kundi hili. Anapokukarimia mengi, anakutaka wewe badala yake na kukufanyia matakwa yanayokufaa. Kwa hiyo, kazi yote ya Mungu haipo bila sababu, na kutokana na hili inaonekana ni kwa nini Mungu kila mara hufanya kazi ya hali ya juu na yenye mahitaji makali. Ndiyo maana unafaa kujawa na imani katika Mungu. Kwa ufupi, kazi yote ya Mungu hufanywa kwa ajili yako, ili kwamba uweze kupokea urithi Wake. Hii sio kwa ajili ya utukufu wa Mungu bali ni kwa ajili ya wokovu wako na kufanya kundi hili la watu walioteswa na nchi najisi kuwa wakamilifu. Sharti uelewe mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo Nawahimiza wale wote wasiojua, wasio na hisia na ufahamu: Usimjaribu Mungu wala kumpinga tena. Mungu Ameshavumilia mateso yote ambayo mwanadamu hajaweza kupitia, na hapo awali Ameteseka na kudhihakiwa kwa niaba ya mwanadamu. Je, nini kingine ambacho huwezi kukiachilia? Je, ni nini muhimu zaidi kuliko mapenzi ya Mungu? Ni nini zaidi kuliko upendo wa Mungu? Ni kazi ambayo ina ugumu mara mbili zaidi kwa Mungu kufanya katika nchi najisi. Ikiwa mtu atatenda dhambi kimakusudi na akifahamu, kazi ya Mungu itaendelezwa kwa muda mrefu zaidi. Katika tukio lolote, hili silo pendeleo la yeyote wala si la maana kwa yeyote. Mungu Hafungwi na wakati; kazi Yake na utukufu Wake huchukua mstari wa mbele. Kwa hiyo, hata ikichukua muda mrefu, Hataacha kutoa dhabihu yoyote ikiwa ni kazi Yake. Hii ndiyo silika ya Mungu: Hatapumzika hadi pale kazi Yake itakapokamilika. Ni pale tu ambapo wakati unapowadia na anapokea sehemu ya pili ya utukufu wake ndipo kazi Yake itakapokwisha. Mungu Asipokamilisha sehemu ya pili ya utukufu wake ulimwenguni, Siku Yake haitawadia, mkono wake hauwezi kuwaachilia wateule wake, utukufu wake hautashuka juu ya Israeli na mpango wake kamwe hauwezi kukamilishwa. Unapaswa kuona kuwa mapenzi Yake na kazi Yake si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Kwa sababu kazi ya leo ni kubadilisha wale waliopotoshwa, wale waliokufa ganzi, na kutakasa walioumbwa kisha kushughulikiwa na Shetani, si kuumba Adamu na Hawa, ama hata kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake. Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayvodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake. Huu ndio undani wa hadithi ya hatua hii ya kazi ya Mungu. Lazima ufahamu wala usirahisishe mambo. Kazi ya Mungu ni tofauti na kazi nyingine. Uzuri wake hauwezi kutambuliwa na akili za mwanadamu wala hekima Yake kupatikana vile. Mungu Haumbi kila kitu wala kuharibu kila kitu. Bali, Anabadilisha viumbe vyote na kutakasa vyote vilivyonajisiwa na Shetani. Kwa hiyo, Mungu Ataanzisha kazi kuu, na huu ndio umuhimu wa kazi ya Mungu. Baada ya kusoma maandishi haya, je, unaamini kuwa kazi ya Mungu ni rahisi vile?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Yaliyopendekezwa: Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Mwenyezi Mungu
0 评论:
Chapisha Maoni