20. Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?
Qingxin Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Kuhusu kipengele cha ukweli cha "Mungu ni mwenye haki ", siku zote nilikuwa na ufahamu wa upuuzi kwa kiasi fulani. Nilidhani kuwa almradi mtu fulani hufichua upotovu katika kazi yake au hufanya makosa ambayo huiharibu kazi ya kanisa, mtu huyo atakabiliwa na rada, au kupoteza kazi yake au aathiriwe na adhabu. Hiyo ni haki ya Mungu.
Kutokana na ufahamu huu usio sahihi, pamoja na hofu ya kupoteza kazi yangu kutokana na kufanya makosa katika kazi yangu, nilifikiria juu ya utaratibu "mjanja": Wakati wowote ninapofanya kitu vibaya, mimi hujaribu niwezavyo kutowaacha viongozi wajue kwanza, na kwa haraka kujaribu kukifidia mwenyewe na kufanya kila linalowezekana ili kukisawazisha. Je, si hilo basi litanisaidia kuhifadhi kazi yangu? Kwa hiyo, wakati wowote nilipowapa ripoti juu ya kazi yangu, ningepunguza masuala makubwa kuwa madogo na masuala madogo kuwa si kitu. Iwapo wakati mwingine nilikuwa baridi ningefanya liwezekanalo ili kulifunika mbele ya viongozi na kujifanya kuwa mtendaji zaidi na chanya, nikiwa na hofu kwamba viongozi wangenifikiria kuwa asiyeweza na kuacha kunitumia. Hiyo hivyo tu, ningelindwa kwa makini sana dhidi ya viongozi katika kila kitu nilichokifanya.
Hata hivyo, Mungu huchunguza mioyo ya watu, na "hila bora" yangu haingeweza kamwe kuyaepuka macho ya Mungu. Niligundua kuwa jinsi nilivyozidi kujaribu kuyafunika mambo, ndivyo Mungu alivyozidi kunifunua katika mwanga. Kwa mfano: Wakati wowote nilipojaribu kuonyesha "talanta" yangu mbele ya viongozi, daima ningekosea vibaya na kujiaibisha mwenyewe; wakati wowote nilipojaribu kuficha hali yangu ya ubaridi, "mawingu ya giza" kwa kughafilika yangeibuka daima juu ya uso wangu na kueleweka na ndugu wa kiume na wa kike; wakati wowote nilipojaribu kuficha njia ya uzembe ambayo nilifanya kazi yangu, matokeo yake yangekuwa kama kioo kilichofichua kila kitu. ... Aibu na mateso ya dhamiri yangu kutokana na udanganyifu mara kwa mara vilinifanya nianguke, ila sikuelewa kutokana na hili nia na madhumuni ya ni kwa nini Mungu alifanya kazi kwa njia hii, wala sikuelewa jinsi Mungu alivyowaokoa watu. Nilisubiri tu kwa ubaridi kwa ujio wa "hukumu ya haki ya Mungu"–kushughulikiwa na kanisa.
Lakini hali halisi haikuendelea kama nilivyokuwa nimetarajia: Katika kazi yangu, ingawa nilikuwa nimepogolewa na kushughulikiwa kwa kutotimiza kazi yangu vizuri, niliweza kupokea mwongozo wa dhati wa ndugu wa kiume na wa kike, ambao walinieleza ni nini kilichokuwa uzembe na nini kilichokuwa kutimiza kwa uaminifu wajibu wangu. Nilielewa kwamba ni kwa kutenda tu kulingana na matakwa ya Mungu ndipo mtu anaweza kutimiza wajibu wake vizuri. Kuhusu kuingia katika uzima, mara nyingi nilizamia kabisa katika mawazo maovu ambayo singeweza kuyaondoa, yakiacha moyo katika masumbuko makali. Nilitaka kuufungua moyo wangu na kutafuta mawasiliano, lakini nilihisi aibu mno kiasi cha kutozungumza. Mwishowe, nilianguka katika giza na kupoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini baada ya kufanya jitihada zote kuzungumza, niliona kuwa ndugu wa kiume na wa kike hawakukosa tu kunicheka au kuniangalia kwa dharau kwa sababu ya hilo, badala yake walinipa msaada na himizo, wakinisaidia kuishi katika nuru na kunipa njia ya kutenda na nguvu ya kushinda dhambi. Baadaye, niliona kwamba wakati ndugu wa kiume na kike karibu na mimi walifanya makosa au kufichua upotovu, kanisa halikuwatuma nyumbani kwa sababu ya hilo. Badala yake, kanisa lilifanya kila lililowezekana kuwasiliana nao na kuwasaidia, likiwapa fursa baada ya fursa. Hata kama mtu fulani anatumwa nyumbani mwishowe, ni kwa sababu tu alikosea tabia ya Mungu mara kwa mara na bado alikataa kutubu hata baada ya kupogolewa, kushughulikiwa, na kuzungumziwa mara nyingi. Lakini hata kwa watu kama hao, kanisa bado linawasubiri kutubu na kuamka. Ikiwa kwa kweli wa hujiheshimu na kubadilika baada ya muda, kanisa bado litawapa fursa za kutenda na kuandaa matendo mema. Ukweli huu ulinifanya nione kwamba mtazamo wa Mungu ni kama jinsi wazazi hutendea kurudi kwa mwana wao mpotevu–kwa mapenzi yasio na kifani na upendo. Pia ulinifanya nione kwamba kazi ambayo Mungu hufanya ni kazi ya kuwaokoa watu, kubadili watu, na kuwakamilisha watu. Ni hapo tu nilipogundua kwamba wazo langu la "haki ya Mungu" lilikuwa la upuuzi zaidi na mbali zaidi na ukweli. Ingawa tabia ya Mungu ni ya haki, kile ambacho Yeye hufichua zaidi kwa watu wanaomfuata ni uvumilivu wa kuzidi kiasi, stahamala, na huruma–na hauna kikomo na kifani. Inaweza kusemwa kuwa upendo ambao Mungu huonyesha ni mkubwa zaidi kuliko haki Yake.
Wakati huo, sikuweza kujizuia kufikiria kifungu cha neno la Mungu. Kwa hiyo nikafungua Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo na Viongozi na Wafanyakazi wa Kanisa na kupata kifungu kifuatacho. Mungu alisema: “Ni nini kiini cha Kristo? Kiini cha Kristo ni upendo kwa binadamu; kuhusiana na wale wanaomfuata, ni upendo usio na mpaka. Kama Hana upendo au huruma, basi watu wasingekuwa na uwezo wa kumfuata hadi wakati huu. Baadhi ya watu husema: ‘Basi je, bado Mungu ni mwenye haki?’ Ndiyo! Ni sahihi kwamba Yeye bado ni mwenye haki, lakini kwa mtazamo wa tabia Yake, hali Yake ya kuwa mwenye haki ni chuki kwa upotovu na uovu wa binadamu. Je, kama Angekuwa tu mwenye haki bila upendo? Je, kama upendo usingeweza kushinda haki? Basi ingesemekana kuwa binadamu amekwisha. Kwa hiyo, Ninanena wazi na nyinyi, yaani, katika kazi Mungu Anayofanyia binadamu katika kipindi cha kupata mwili Kwake, kiini Chake dhahiri na maarufu zaidi ni upendo; ni stahamala isiyo na kipimo. Kama haikuwa upendo bali Mungu kuwaangamiza watu vile mnavyofikiria; kwa kunena uharibifu, watu waliangamizwa, na kwa kunena chuki kwa watu, watu waliadhibiwa, kulaaniwa, kuhukumiwa, na kkuadibiwa, basi hiyo itakuwa kali sana! Kama Angekuwa na hasira kwa watu, watu wangekuwa na hofu na kutetemeka na wasingewezea kusimama mbele ya macho ya Mungu .... Hii ni njia moja tu ya kuonyesha tabia ya Mungu, na mwishowe, azma Yake bado ni wokovu. Upendo Wake unadhihirika kupitia ufichuzi wote wa tabia Yake. Tafakari juu ya hili, wakati wa kuwa mwili, jambo linalofichuliwa zaidi kwa watu ni upendo. Uvumilivu ni nini? Uvumilivu ni kuwa na huruma kwa sababu kuna upendo ndani, na azma Yake bado ni kuwaokoa watu. Mungu anaweza kuwa na huruma juu ya watu kwa sababu Yeye Ana upendo. Kama vile kuna pendo la kweli kati ya mume na mke, hawaangali upungufu wa yule mwingine na hatia. Kama wangechochewa kiasi cha kuwa na hasira, wao bado wangeweza kuwa na subira. Kila kitu kimeimarishwa juu ya msingi wa upendo. Je, kama Angekuwa wa chuki? Basi mtazamo Yake usingekuwa jinsi ilivyo, kujionyesha Kwake kusingekuwa jinsi ilivyo, na matokeo yasingekuwa jinsi yalivyo. Kama Mungu tu angekuwa na chuki na hasira, na kungekuwa na hukumu na kurudi tu, na kusingekuwa na upendo ndani yake, basi hali isingekuwa muonavyo sasa na nyinyi watu msingekuwa katika hali nzuri. Je, Angeweza kuwapa ukweli?” (“Upendo wa Kweli wa Mungu kwa Wanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nilipoona kifungu hiki katika siku za nyuma, ingawa ningesema nakikubali, kwa kweli sikuwahi kamwe kukielewa na bado nilijaa shaka na hadhari kumhusu Mungu. Ni sasa tu ambapo nina ufahamu kidogo halisi wa maneno haya na ninaweza kufahamu kuwa yana umuhimu mno. Nafasi kati ya mistari imejazwa na upendo wa kina wa Mungu kwa wanadamu na ugavi Wake wenye nia njema, tegemeo na mafundisho yake kwake.
Wakatiwakati wote ambao nimekufuata Wewe, ingawa nilikuamini Wewe sikukujua Wewe. Sikuuelewa visivyo tu kwa upofu na uongo moyo Wako wa kutunza, pia nilikusababishia Wewe maumivu mengi zaidi. Kwa kweli mimi ni mtu asiyestahili mno kuja mbele Yako, na hata asiyefaa zaidi wokovu Wako. Ninastahili tu laana Yako! Lakini jinsi unavyonitendea si kwa msingi wa kutotii kwangu. Badala yake, Wewe unanipandisha hadhi kwa nguvu, kunihurumia na kunivumilia, ukinipa fursa ya kufanikisha kuzaliwa upya, Ukiniruhusu kufurahia upendo Wako wote na neema, ukiniruhusu kuona uzuri Wako na wema Wako, na kupata uzoefu wa neno Lako–Mungu ni mwenye haki na aidha ni upendo! Kuanzia sasa kwendelea, nataka kupata kujua zaidi juu ya kupendeza Kwako kwa njia ya neno Lako na kwa njia ya maisha halisi, na kujitahidi kuwa mtu ambaye ni mwaminifu, ambaye anakupenda Wewe, na kwa uaminifu kutimiza wajibu wangu kufidia upendo Wako mkubwa!
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
0 评论:
Chapisha Maoni