Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo maandiko-ya-Biblia. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo maandiko-ya-Biblia. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 2 Machi 2018

Swahili Gospel Movie | “Ivunje Laana” Movie Clip: Je, Imani katika Biblia ni Sawa na Imani katika Bwana?

Swahili Gospel Movie | "Ivunje Laana" Movie Clip: Je, Imani katika Biblia ni Sawa na Imani katika Bwana?


Wachungaji wengi sana na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa kidini huamini kwamba Biblia inamwakilisha Bwana, na kwamba kuamini katika Bwana ni kuamini katika Biblia, na kuamini katika Biblia ni kuamini katika Bwana. Wao huamini kwamba mtu akiachana na Biblia basi hawezi kuitwa muumini, na kwamba mtu anaweza kuokolewa na anaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni almradi ashikilie Biblia. Je, Bibilia inaweza kweli kumwakilisha Bwana? Je, uhusiano kati ya Biblia na Bwana ni upi hasa? Bwana Yesu alisema, "Tafuta katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnadhani kuwa mna uzima wa milele: na hayo ndiyo yananishuhudia. Nanyi hamtakuja Kwangu, kwamba mpate uhai" (Yohana 5:39-40). Mwenyezi Mungu alisema, "Hata hivyo, kipi ni kikubwa? Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? … Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia! Kuwa Bwana wa Sabato, je, Asingeweza pia kuwa Bwana wa Biblia?" (Neno Laonekana katika Mwili)
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia

Jumamosi, 17 Februari 2018

Latest Swahili Gospel Movie "Wakati Wa Mabadiliko"

Latest Swahili Gospel Movie "Wakati Wa Mabadiliko"

Su Mingyue ni mhubiri wa kanisa la nyumbani huko bara China. Kwa miaka, amekuwa mtumishi aliyejitolea wa Bwana anayesisitiza kufanya kazi ya kuhubiri kwa ajili ya Bwana na kubeba mzigo wa kazi kwa ajili ya kanisa. Anaongozwa na neno la Paulo katika Biblia, akihisi kwamba kuamini tu katika Bwana kunatosha kuitwa mwenye haki na kuokolewa kwa neema. Ingawa mwanadamu bado hutenda dhambi bila kusita, dhambi zake zimesamehewa na Bwana, taswira yake itabadilishwa mara moja na kuwa takatifu na atainuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni Bwana atakapowasili. Hata hivyo, katika miaka ya hivi majuzi, kanisa limezidi kuwa lenye huzuni, waumini wamekuwa hasi na wanyonge kwa jumla, imani na upendo wao umepoa. Wafanyakazi wenza wengine huongozwa na neno la Bwana: "Si kila mtu aniitaye, Bwana, Bwana, ataingia katika ufalme wa mbinguni; lakini yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni" Wanashuku fikira kwamba "Bwana anapokuja, Ataibadili taswira ya mwanadamu mara moja na kumuinua kwenda katika ufalme wa mbinguni." Wanahisi kwamba kwa kuwa bado tunatenda dhambi siku zote, tunashindwa kufikia utakatifu kwa kiwango kikubwa na kutotii mapenzi ya Mungu, tunawezaje kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni Bwana atakapokuja? Baada ya kuwasiliana na kujadili, Su Mingyue anahisi kwamba, kuna mkanganyiko mengine kati ya maneno ya Bwana na wazo la Paulo la kubadilisha taswira ya mwanadamu mara moja Bwana ajapo. Ni wazo gani lililo sahihi hata hivyo? Su Mingyue yuko katika hali ya mtanziko na kuchanganyikiwa moyoni. Ili kupata kanisa lililo na kazi ya Roho Mtakatifu ili kutatua mkanganyiko tendaji wake, ili asiachwe na Bwana, Su Mingyue anaamua kulichunguza Umeme wa Mashariki. Kupitia kujadiliana na kuwasiliana na wahubiri wa Kanisa la Mwenyezi Mungu, Su Mingyue na wengine hatimaye wanaelewa njia ya pekee ya kuingia katika ufalme wa mbinguni …
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia

Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu!
Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?