Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kidini. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kidini. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 13 Desemba 2018

Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | Mtu Anaweza Kuokolewa kwa Kumwamini Bwana Katika Dini?

Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | Mtu Anaweza Kuokolewa kwa Kumwamini Bwana Katika Dini?


Ndani ya dini, kuna watu wengi ambao wanaamini kwamba, ingawa wachungaji na wazee wanashikilia mamlaka katika ulimwengu wa dini na kutembea njia ya Mafarisayo wafiki, ingawa wanakubali na kuwafuata wachungaji na wazee, 

Jumapili, 24 Juni 2018

59. Uzoefu wa Kutenda Ukweli

59. Uzoefu wa Kutenda Ukweli




                     Hengxin     Jiji la Zhuzhou, Mkoa wa Hunan
Sio muda mrefu mno uliopita, nilisikia "Ushirika na Kuhubiri Kuhusu Kuingia kwa Maisha," jambo ambalo lilinielekeza kuelewa kwamba ni wale tu wanaotenda ukweli wanaoweza kupata ukweli na hatimaye kuwa wale ambao wanaomiliki ukweli na ubinadamu hivyo kupata kibali cha Mungu. Kuanzia hapo kwendelea, kwa makusudi nilifanya jitihada za kuunyima mwili wangu na kutenda ukweli katika maisha yangu ya kila siku. Wakati fulani baadaye, nilitambua kwa furaha kwamba ningeweza kutenda ukweli kiasi. Kwa mfano, siku za nyuma niliogopa kuonyesha upande wangu mwovu kwa wengine. Sasa kwa makusudi nilikuwa wazi na ndugu wa kiume na wa kike, nikichangua tabia yangu potovu. Kabla, wakati nilipopogolewa na kushughulikiwa, ningetoa udhuru na kukwepa wajibu. Sasa nilifanya jitihada makusudi kujikana badala ya kujaribu kuhalalisha tabia yangu mbaya. Katika siku za nyuma, nilipopata msuguano na wenzangu kazini, nilikuwa na mawazo finyu, uchwara na wa kuelekea kununa. Sasa nilipokabiliwa na hali hizo ningeunyima mwili wangu na kutumia stahamaha na subira na wengine. … Kila wakati nilipofikiria maendeleo yangu katika kutenda ukweli, ningejihisi kuwa na furaha mno. Nilidhani kuwa uwezo wangu wa kutenda ukweli kiasi ulimaanisha kwamba nilikuwa mweledi halisi wa ukweli. Kwa njia hii, bila kujua nikawa mwenye maringo na wa kujipongeza.
Siku moja, nilikuwa nikisomasoma “Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo” na nikapata kwa kibahati maneno yafuatayo ya Mungu: "Watu wengine husema: Ninahisi kuwa nina uwezo wa kuweka ukweli fulani katika matendo sasa, sio kwamba siwezi kuweka ukweli wowote katika matendo. Katika mazingira mengine, ninaweza kufanya mambo kulingana na ukweli, ambako kumaanisha nahesabika kama mtu anayeweka ukweli katika matendo, na nahesabika kama mtu mwenye ukweli. Kwa kweli, kinyume na hali za zamani, au kinyume na wakati ulipomwamini Mungu mara ya kwanza, kuna mabadiliko machache. Katika siku za nyuma, hukuelewa chochote, na hukujua ukweli ulikuwa nini au tabia potovu ilikuwa nini. Sasa unajua mambo fulani na unaweza kuwa na matendo fulani mazuri, lakini hii ni sehemu ndogo tu ya mabadiliko hayo; sio mabadiliko ya tabia yako kwa kweli, kwa sababu huwezi kutekeleza ukweli mkomavu na wa kina ambao unahusisha asili yako. Tofauti na siku zako zilizopita, kwa kweli una mabadiliko fulani, lakini mabadiliko haya ni mabadiliko machache tu ya ubinadamu wako, na yakilinganishwa na hali ya juu ya ukweli, wewe bado uko mbali sana na lengo. Hii ni kusema kwamba hujafikia lengo wakati unaweka ukweli katika matendo.” Baada ya kusoma maneno haya, sikuweza kujizuia kushtuka. Yote ambayo nimefanikisha yalikuwa ni tabia chache nzuri? Bado niko mbali na kutenda ukweli kwa uhalisi? Je, nini basi, nilifikiri, inamaanisha kutenda ukweli kwa uhalisi? Nilianza kuchunguza jibu halisi la swali hili. Baadaye, katika ushirika wa mwanadamu, niliona maneno yafuatayo: "Wale ambao kwa shauku hutenda ukweli wanaweza kumudu gharama na wako tayari kuzikubali shida zinazohusika. Kwa dhahiri, mioyo yao imejaa furaha na raha. Wale ambao wako tayari kutenda ukweli hawatawahi kufanya kitu tu kwa namna isiyo ya dhati kamwe kwa sababu hawafanyi tu kwa sababu ya monyesho. Dhamiri na sababu wanazomiliki kama wanadamu wa kawaida huwalazimisha kutenda sehemu yao kama viumbe wa Mungu. Kwao, kutenda ukweli ndicho kiini cha kuwa binadamu; ni sifa ambayo yule aliye na ubinadamu wa kawaida anapaswa kumiliki" ("Ukweli Lazima Utendwe Kwa Moyo" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo na Viongozi na Wafanyakazi wa Kanisa). Baada ya kusoma hili, hatimaye nilielewa: Wataalamu halisi wa ukweli wanaweza kutenda ukweli kwa sababu wanaelewa kusudi la kufanya hivyo. Wao hujua kwamba kutenda ukweli ndiyo maana ya kuwa binadamu, sifa ambyao wanadamu wanapaswa kuwa nayo. Kwa hiyo, hawafanyi hivyo kwa maonyesho; huwa wanauona kama wajibu wao. Wako tayari kuvumilia shida na kulipa gharama; hawana malengo ya kibinafsi na tamaa. Lakini nilitendaje ukweli? Wakati nikifichua tabia zangu potovu, huenda nilikuwa wazi na kuzifunua kwa ndugu zangu wa kiume na wa kike, lakini katika moyo wangu nilikuwa nikifikiria, "Mnaona jinsi ninavyotenda ukweli? Ninaweza kuweka wazi tabia zangu potovu. Hilo linanifanya kuwa bora kuliko ninyi, naam?" Wakati nilipopogolewa na kushughulikiwa, naweza kuwa sikutoa udhuru kwa sauti, lakini ndani nilikuwa nikisema "Ona? Huwa sitoi udhuru tena. Nimekuwa mzuri sana. Labda ninastahili kama mtu ambaye yuko tayari kuukubali ukweli sasa, naam?" Wakati nilipokuwa na msuguano na wenzangu kazini, huenda kwamba nilijaribu kwa makusudi kujizuia mwenyewe na kuepuka mlipuko wowote, lakini moyoni mwangu nilikuwa nikifikiria, "Mnaona? Mimi si kama nilivyokuwa kabla, kuwa uchwara na mwenye mawazo finyu. Nimebadilika, naam?" … Wakati nilipofikiri jinsi nilivyokuwa nikitenda ukweli, hatimaye niligundua kuwa sikuwa kwa kweli natenda ukweli. Nilikuwa nimejaa nia zangu na tamaa zangu. Nilikuwa nikilifanya kwa sababu ya maonyesho. Nilitaka watu wengine kunipenda na kunisifu. Ningewezaje kusema kwamba nilikuwa nikitenda ukweli kwa sababu nilielewa umuhimu wake? Nilikuwa nikifanyaje hili ili kumridhisha Mungu wangu? Nilikuwa nikifanya hili ili kujiridhisha na kujionyesha kwa wengine. Nilikuwa nikimshutumu na kumlaghai Mungu. Kwa uhalisi, nilikuwa nausaliti ukweli. Kanuni yangu inayodaiwa kuwa "kutenda ukweli" ilikuwa tu kufuata desturi. Lilikuwa ni zoezi la kizuizi, kukoma kwa tabia fulani mbaya. Lilikuwa tu badiliko la nje. Nilikuwa na bado niko mbali sana na kufikia viwango vinavyotakiwa kwa mweledi wa ukweli. Hata hivyo, sio tu kuwa nilifikiri kwa kujipujua kwamba nilikuwa mweledi wa ukweli, hata nilikuja kuwa wa kujipongeza kama matokeo. Tabia yangu ilikuwa kweli iliyovuka mpaka!
Mungu, asante kwa nuru Yako na mwongozo Wako. Asante kwa kunionyeshea kwamba sikuwa mweledi wa kweli wa ukweli na kwamba utekelezaji wangu wa ukweli haukufikia viwango Vyako. Kuanzia siku hii kwendelea, niko tayari kuchunguza nia zangu mwenyewe na kushikilia viwango vinavyohitajiwa kutenda ukweli. Nitajioondolea uchafu na kuwa mweledi wa ukweli.


Ushuhuda-wa-Kuipitia-Hukumu-ya-Kristo

Know more Kujua zaidi:Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki 

Ijumaa, 11 Mei 2018

"Imani katika Mungu" (3) - Je, Kazi ya Mungu na Kuonekana kwa Mungu Kunaleta Nini katika Jamii ya Dini?

"Imani katika Mungu" (3) - Je, Kazi ya Mungu na Kuonekana kwa Mungu Kunaleta Nini katika Jamii ya Dini?

Utambulisho


Kila wakati ambapo Mungu anakuwa mwili na kuonekana ili kufanya kazi Yake, nguvu za uovu za Shetani hupinga na kulaani njia ya kweli kwa ghadhabu. Kwa njia hii, vita vinatokea ndani ya dunia ya kiroho ambavyo hugawanya na kufunua ulimwengu wa dini. Bwana Yesu alisema, “Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani: sikuja kuleta amani, bali upanga”(Mathayo 10:34). Wakati ambapo Bwana Yesu alionekana na kufanya kazi katika Enzi ya Neema, dini ya Kiyahudi iligawanyika katika vikundi vingi. Sasa kwa kuonekana kwa Mwenyezi Mungu na kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, ulimwengu wa dini unapatwa na mfichuo mkubwa; ngano na magugu mwitu, kondoo na mbuzi, wanawali wenye busara na wanawali wapumbavu, na watumishi wazuri na watumishi wabaya —wote wanafunuliwa, kila mmoja na aina yake. Hekima ya Mungu na maajabu kweli ni ya kina sana!
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatano, 9 Mei 2018

"Imani katika Mungu" (2) - Je, Njia Inayoshutumiwa na CCP na Miongoni mwa Watu wa Dini Siyo Njia ya kweli?


"Imani katika Mungu" (2) - Je, Njia Inayoshutumiwa na CCP na Miongoni mwa Watu wa Dini Siyo Njia ya kweli?

Utambulisho
Watu wengi hutafuta na kuchunguza njia ya kweli pasipo kutegemeza vitendo hivi katika maneno na kazi ya Mungu. Badala yake, wao hufuata mitindo ya ulimwengu wa dini na wanaamini kwamba kile ambacho serikali ya kikomunisti ya China na ulimwengu wa dini inalaani sio njia ya kweli—je, hii ni njia sahihi ya kuelekea? Biblia inasema, “dunia nzima hukaa ndani ya maovu."(1 Yohana 5:19). “Hiki ni kizazi kiovu” (Luka 11:29). Hivyo inaweza kuonekana kwamba mifumo ya kisiasa ya kukana Mungu na ulimwengu wa dini hakika utakana na kuishutumu njia ya kweli. Wakati ambapo Bwana Yesu alifanya kazi Yake katika Enzi ya Neema, serikali ya Kiyahudi na ya Kirumi zilimpinga na kumtia hatiani kwa hasira, na mwishowe Bwana Yesu alisulubishwa msalabani. Je, si huu ni ukweli wa hali? Mwenyezi Mungu anapokuja kufanya kazi Yake katika siku za mwisho, Anapitia uasi mkali na shutuma ya serikali ya China na ulimwengu wa dini. Hili linaonyesha nini? Je, si hili linastahili sisi kulitafakari?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumapili, 29 Aprili 2018

Latest Swahili Christian Movie "Imani katika Mungu" | Hufunua Fumbo la Imani Katika Mungu

Latest Swahili Christian Movie "Imani katika Mungu" | Hufunua Fumbo la Imani Katika Mungu

Utambulisho
Yu Congguang huhubiri injili kwa niaba ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wakati wa kuhubiri injili, aliandamwa na serikali ya Kikomunisti ya China. Alikimbia milimani, ambapo alipokea msaada kutoka kwa Zheng Xun, mfanyakazi mwenza wa kanisa la nyumba la mahali pale. Walipokutana mara ya kwanza, walihisi kama tayari walikuwa wamejuana kwa muda mrefu. Zheng Xun alimpeleka Yu Congguang kwenye kibanda cha makuti ambapo yeye na wafanyakazi wenzake walikusanyika. Huko, mjadala ulijitokeza miongoni mwa Zheng Xun na wafanyakazi wenzake kuhusu kama muumini katika Mungu anapaswa kutii wale walio madarakani au la. Yu Congguang alitoa ushirika kwa kuzingatia suala hili na kuondoa kuchanganyikiwa kwao. Ushirika wa Yu Congguang ulikuwa wa manufaa sana kwao, na wote wakaanza kutafuta na kujifunza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Hata hivyo, Mzee Sun kutoka kanisa la mahali pale alipopata habari kwamba Yu Congguang alikuwa shahidi kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu, alifanya kila kitu ambacho angeweza kulizuia kanisa na kuwazuia wafuasi kutafuta njia ya kweli. Sun alikwenda katika nyumba moja hadi nyingine kumtafuta Yu Congguang, na hata kuwahamasisha wafuasi kumripoti Yu kwa polisi na kumkamata …
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Injili

Soma Zaidi:  Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumamosi, 28 Aprili 2018

"Mji Utaangushwa" (5) - Mji mkuu wa dini wa Babeli Umekusudiwa Kuangamia Chini ya Ghadhabu ya Mungu!

"Mji Utaangushwa" (5) - Mji mkuu wa dini wa Babeli Umekusudiwa Kuangamia Chini ya Ghadhabu ya Mungu!

Utambulisho
Ulimwengu wa dini humkaidi na kumlaani Mwenyezi Mungu, ukitenda matendo maovu yasiyohesabika, na wamekuwa kambi ya Shetani ambayo humpinga Mungu vikali. Mji mkuu wa dini wa Babeli umekusudiwa kuangamia chini ya ghadhabu ya Mungu! Ufunuo unatabiri, "Ole, ole ule mji mkuu Babeli, ule mji ulio na uwezo! kwani hukumu yako imekuja katika saa moja" (Ufunuo 18:10). Mwenyezi Mungu asema, "Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo" (Neno Laonekana katika Mwili).



Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?