Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumatano, 27 Desemba 2017

Mazungumzo Mafupi Kuhusu “Ufalme wa Milenia Umefika”

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Mazungumzo Mafupi Kuhusu “Ufalme wa Milenia Umefika”

Mwenyezi Mungu alisema, Mnayaonaje maono ya Ufalme wa Milenia? Baadhi ya watu hutafakari sana kuuhusu na kusema kuwa Ufalme wa Milenia utadumu duniani kwa miaka elfu moja, hivyo basi ikiwa waumini wazee katika kanisa hawajaoa, je, wanapaswa kuoa? Familia yangu haina pesa, je napaswa nianze kutafuta pesa? … Ufalme wa Milenia ni nini? Je, mnajua? Watu ni nusu vipofu na wanapitia mateso mengi. Kwa hakika, Ufalme wa Milenia bado haujafika rasmi. Katika hatua ya kuwafanya wanadamu wakamilike, Ufalme wa Milenia ni mfano mdogo tu; 

Jumanne, 26 Desemba 2017

Kuhusu Majina na Utambulisho | Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu,

Kuhusu Majina na Utambulisho

Mwenyezi Mungu alisema, Iwapo unataka kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu, lazima uijue kazi ya Mungu; lazima uijue kazi Aliyofanya awali (katika Agano Jipya na la Kale), na, zaidi ya hayo, lazima uijue kazi Yake ya leo. Ndiyo kusema, ni lazima uzitambue hatua tatu za kazi ya Mungu ya zaidi ya miaka 6,000. Ukiulizwa ueneze injili, basi hutaweza kufanya hivyo bila kuijua kazi ya Mungu. Watu watakuuliza yote kuhusu Biblia, na Agano la Kale, na nini Yesu alisema na kufanya wakati huo.

Jumatatu, 25 Desemba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu Lilikujaje Kuwepo?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu Lilikujaje Kuwepo?

Kama makanisa ya Ukristo, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwepo kwa sababu ya kazi ya Mungu kupata mwili. Makanisa ya Ukristo yalipata kuwepo kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Bwana Yesu aliyepata mwili, na Kanisa la Mwenyezi Mungu lilipata kuwepo kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho. Hivyo, makanisa kotekote katika enzi yamefanyizwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mungu Aliyepata mwili.

Jumapili, 24 Desemba 2017

Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?

Watu wengi hawaelewi ni kwa nini, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu katika siku za mwisho, Bwana Yesu anaitwa Mwenyezi Mungu wakati Anapokuja kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho.

Jumamosi, 23 Desemba 2017

Ufalme wa Milenia Umewasili | Matamshi ya Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Ufalme wa Milenia Umewasili | Matamshi ya Mwenyezi Mungu

Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja. 

Ijumaa, 22 Desemba 2017

Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani – Kristo ndiye Chanzo cha Uhai na Vile Vile Bwana wa Biblia


Kristo ndiye Chanzo cha Uhai na Vile Vile Bwana wa Biblia

Biblia imejaa maneno ya Mungu na vile vile uzoefu na ushuhuda kutoka kwa mwanadamu ambao unaweza kutupa uhai na ni yenye manufaa sana kwetu. Bwana Yesu alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima: Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, bado ataishi: Na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.” (Yohana 11:25-26). Lakini kwa nini, baada ya miaka 2,000, hakuna kati ya wale walio na imani katika Bwana ambao wamesoma Biblia wamewahi kupata uzima wa milele? Inaweza kuwa kwamba Biblia haina njia ya uzima wa milele? Inaweza kuwa kwamba wakati Bwana Yesu alitekeleza kazi Yake ya ukombozi kwamba Hakuwapa binadamu njia ya uzima wa milele? Tunapaswa kufanya nini ili kuweza kupata njia ya uzima wa milele?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Alhamisi, 21 Desemba 2017

Mtu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Mtu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Binadamu amekuwa akiishi katika funiko la ushawishi wa giza, huku akiwa amezuiliwa bila ya kuwachiliwa na ushawishi wa Shetani. Nayo tabia ya binadamu, baada ya kutengenezwa na Shetani, inaendelea kuongezeka kuwa potovu. Kwa maneno mengine, binadamu huishi daima na tabia yake potovu ya kishetani, asiweze kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa hiyo, kama binadamu anataka kumpenda Mungu, lazima anyang'anywe kujidai kwake, kujigamba, kiburi, majivuno, na sifa nyingine kama hizo zinazomilikiwa na tabia ya Shetani. 

Jumatano, 20 Desemba 2017

Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watii kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. Imani kama hii ni kujidanganya, kujihakikishia, na kujishukuru. Kama imani yako haijajengwa katika msingi wa utii kwa Mungu, basi hatimaye utaadhibiwa kwa kumpinga Mungu.

Jumanne, 19 Desemba 2017

Kuijua Kazi ya Mungu Leo | Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kuijua Kazi ya Mungu Leo | Maneno ya Mwenyezi Mungu

Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (wakati wa siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima.

Jumatatu, 18 Desemba 2017

Mungu ni upendo | "Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu" | Best Swahili Gospel Worship Song

Mungu ni upendo | Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu

Sasa kwa kushangilia sana, utakatifu wa Mungu na haki
vinakua ulimwenguni kote,
ikitukuka sana kati ya wanadamu wote.
Miji ya mbinguni inacheka, falme za dunia zinacheza.
Ni nani asiyesherehekea? Ni nani asiyetoa machozi?
Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde;
jua linaaangaza kotekote.
wakiishi katika mwanga wa Mungu,
wakiwa na amani na kila mmoja.
Dunia ni ya mbingu, mbingu inaungana na dunia.
Mwanadamu ndiye ukamba unaounganisha mbingu na dunia.
Kwa sababu ya utakatifu wa mwanadamu,
kwa sababu ya upya wake,
mbingu haijifichi kutoka kwa dunia tena,
dunia haiinyamazii mbingu tena.
Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde;
hawaliabishi jina la Mungu,
wakiishi katika mwanga wa Mungu,
wakiwa na amani na kila mmoja.
Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde;
hawaliabishi jina la Mungu,
wakiishi katika mwanga wa Mungu,
wakiwa na amani na kila mmoja.
Hewa ni changamfu, ukungu mzito umetoweka,
jua linaangaza kotekote.
Hewa ni changamfu, ukungu mzito umetoweka,
jua linaangaza kotekote. Hewa ni changamfu, ukungu mzito umetoweka,
jua linaangaza kotekote.
Hewa ni changamfu, ukungu mzito umetoweka,
jua linaangaza kotekote.
Nyuso za ubinadamu zimezingirwa na tabasamu.
Ukiwa umejificha mioyoni mwao,
utamu unaenda kwa mwendo mrefu.
Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde;
hawaliabishi jina la Mungu,
wakiishi katika mwanga wa Mungu,
wakiwa na amani na kila mmoja.
Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde;
hawaliabishi jina la Mungu,
wakiishi katika mwanga wa Mungu,
wakiwa na amani na kila mmoja,
wakiwa na amani na kila mmoja,
wakiwa na amani na kila mmoja.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo za injili,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Jumapili, 17 Desemba 2017

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza | Matamshi ya Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huifahamu kamwe kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi.

Jumamosi, 16 Desemba 2017

Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yananayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake.