Maneno ya Mungu | Sura ya 28
Jumamosi, 8 Juni 2019
Maneno ya Mungu | Sura ya 28
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguJuni 08, 2019kazi-ya-Roho-Mtakatifu, maneno-ya-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, siku-za-mwisho, VitabuNo comments
Maneno ya Mungu | Sura ya 28
Unaona kwamba muda ni mfupi sana na kazi ya Roho Mtakatifu inavurumisha mbele, ikikusababisha kupata baraka kubwa hivi, kumpokea Mfalme wa ulimwengu, Mwenyezi Mungu, ambaye ni Jua ling’aalo, Mfalme wa ufalme—hii yote ni neema na huruma Yangu. Kuna nini kinachoweza kuwepo kinachoweza kukutoa kwa upendo Wangu? Tafakari kwa makini, usijaribu kuepa, subiri kwa ustahamilivu mbele Yangu kila wakati na usiwe ukizurura nje daima.
Ijumaa, 7 Juni 2019
Sauti ya Mungu | Sura ya 27
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguJuni 07, 2019Neno-Laonekana-katika-Mwili, Roho-Mtakatifu, sauti-ya-Mungu, ushuhuda, VitabuNo comments
Sauti ya Mungu | Sura ya 27
Mungu mmoja wa kweli anayetawala vitu vyote katika ulimwengu—Kristo mwenyezi! Huu ndio ushuhuda wa Roho Mtakatifu, ni ushahidi dhahiri! Roho Mtakatifu anafanya kazi kuwa na ushuhuda kila mahali, ili kusiwe na mtu yeyote mwenye shaka yoyote. Mfalme wa ushindi, Mwenyezi Mungu! Yeye ameushinda ulimwengu, Ameishinda dhambi na kufanikisha ukombozi!
Alhamisi, 6 Juni 2019
Maneno ya Mungu | Sura ya 26
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguJuni 06, 2019hukumu, kazi-ya-Roho-Mtakatifu, maneno-ya-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Maneno ya Mungu | Sura ya 26
Wanangu, yatilieni maanani maneno Yangu, sikiliza kwa utulivu sauti Yangu na Nitafichua kwako. Uwe na utulivu ndani yangu, kwa maana Mimi ni Mungu wako, Mkombozi wenu wa pekee. Mnatakiwa kutuliza mioyo yenu nyakati zote, mkae ndani yangu; Mimi ni mwamba wako, msaidizi wenu. Msiwe na nia nyingine, lakini mnitegemee kwa mioyo yenu yote na Mimi nitaonekana kwenu kwa hakika—Mimi ni Mungu wenu!
Jumatano, 5 Juni 2019
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguJuni 05, 2019sauti-ya-Mungu, siku-za-mwisho, Ufalme-wa-Mbinguni, Usomaji-wa-Maneno-ya-Mwenyezi-Mungu, VideoNo comments
Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali.
Jumanne, 4 Juni 2019
Sauti ya Mungu | Sura ya 25
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguJuni 04, 2019Neno-Laonekana-katika-Mwili, sauti-ya-Mungu, utukufu, Vitabu, wokovu-wa-MunguNo comments
Sauti ya Mungu | Sura ya 25
Mwenyezi Mungu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani, Mungu wetu Anatawala! Mwenyezi Mungu anaweka miguu Yake kwenye Mlima wa Mizeituni. Uzuri ulioje! Sikiliza! Sisi walinzi tunapaza sauti zetu: tunaimba kwa pamoja kwa sauti zetu, kwa kuwa Mungu amerudi Sayuni. Tunaona kwa macho yetu wenyewe ukiwa wa Yerusalemu. Furahieni na kuimba kwa sauti kwa pamoja, kwa kuwa Mungu ametufariji na Ameukomboa Yerusalemu.
Jumatatu, 3 Juni 2019
Maneno ya Mungu | Sura ya 24
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguJuni 03, 2019kanisa, maneno-ya-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Ukweli, VitabuNo comments
Maneno ya Mungu | Sura ya 24
Wakati unakaribia hata zaidi. Amkeni! Watakatifu wote! Nitawatamkia ninyi. Wote wanaosikia wataamka. Mimi ni Mungu ambaye mmekuwa na imani katika kwa miaka hii mingi. Leo nimekuwa mwili na kuja mbele ya macho yenu, na hii inafichua yule ambaye ananitaka kwa kweli, ambaye yuko tayari kulipa gharama yoyote kwa ajili Yangu, ambaye husikiliza neno Langu kwa kweli, na yule ambaye yuko tayari kuuweka ukweli katika matendo.
Jumapili, 2 Juni 2019
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 23
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguJuni 02, 2019hukumu, Matamshi-ya-Mwenyezi-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Ukweli, VitabuNo comments
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 23
Kwa ndugu wote ambao wameisikia sauti Yangu: Mmeisikia sauti ya hukumu Yangu kali na mmevumilia mateso yaliyokithiri. Hata hivyo, mnapaswa kujua kwamba katika sauti Yangu kali kumejificha nia Zangu! Ninawafundisha nidhamu ili muweze kuokolewa. Mnapaswa kujua kwamba kwa wana Wangu wapendwa, Nitawafundisha nidhamu na kuwapogoa na kuwafanya muwe wakamilifu hivi karibuni. Moyo Wangu una hamu sana, lakini ninyi hamuelewi moyo Wangu na hamtendi kulingana na neno Langu.
Jumamosi, 1 Juni 2019
Sauti ya Mungu | Sura ya 22
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguJuni 01, 2019kazi-ya-Roho-Mtakatifu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, sauti-ya-Mungu, siku-za-mwisho, VitabuNo comments
Sauti ya Mungu | Sura ya 22
Kumwamini Mungu si jambo rahisi kufanya. Ninyi mnajiboronga, mkiteketeza kila kitu mbele yenu mkifikiri kuwa haya yote ni ya kuvutia sana, matamu mno! Kuna baadhi ambao bado wanashangilia—wao tu hawana utambuzi katika roho zao. Ni vyema kuchukua muda wa kuuweka katika muhtasari uzoefu huu. Katika siku za mwisho, kila aina za pepo huibuka kutekeleza majukumu yao, wakikaidi kwa uwazi hatua za mbele za wana wa Mungu na kushiriki katika kuuvunja ujenzi wa kanisa.
Ijumaa, 31 Mei 2019
Maneno ya Mungu | Sura ya 21
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguMei 31, 2019kazi-ya-Roho-Mtakatifu, maneno-ya-Mungu, Maombi, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Maneno ya Mungu | Sura ya 21
Kazi ya Roho Mtakatifu sasa imewaleta katika mbingu mpya na dunia mpya. Kila kitu kinaendelea kufanywa upya, kila kitu ki mikononi Mwangu, kinarudi ulingoni! Kwa dhana zao, watu wanashindwa kulifikiria kwa makini, na kwao haina maana, lakini ni Mimi ambaye niko kazini, na hekima Yangu iko ndani yake. Kwa hiyo mnaweza kukomesha dhana zenu zote na maoni yenu. Mnaweza kujishughulisha na kula na kunywa neno la Mungu katika utii, bila wasiwasi wowote kamwe. Kufanya kazi kwa njia hii Mimi nachukua jukumu takatifu. Kwa kweli watu hawana haja ya kuwa namna fulani.
Alhamisi, 30 Mei 2019
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguMei 30, 2019maneno-ya-Mungu, Mfuateni-Mwanakondoo-na-Kuimba-Nyimbo-Mpya, Upendo-wa-Mungu, Video, Wimbo-wa-KuabuduNo comments
Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu
Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake.
Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu.
Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya.
Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake.
Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana.
Tunatafakari, kufikiri maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu anatuangazia.
Jumatano, 29 Mei 2019
Maneno ya Mungu | Sura ya 20
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguMei 29, 2019kanisa, kazi-ya-Roho-Mtakatifu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Ukweli, VitabuNo comments
Maneno ya Mungu | Sura ya 20
Kazi ya Roho Mtakatifu hushina mbele, ikiwaleta nyinyi ndani ya eneo mpya kabisa, ambayo ni kwamba hali halisi ya maisha ya ufalme imejitokeza mbele yako. Maneno ambayo yamesemwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja yamefichua ukina ulio ndani ya mioyo yenu na kwa hiyo picha moja baada ya nyingine zinaonekana mbele yenu. Wale wote ambao wana njaa na kiu ya haki, ambao wana nia ya kutii kwa hakika watabaki Sayuni na watakaa Yerusalemu Mpya.
Jumanne, 28 Mei 2019
Matamshi ya Kristo | Sura ya 19
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguMei 28, 2019hukumu, kanisa, kazi-ya-Roho-Mtakatifu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Matamshi ya Kristo | Sura ya 19
Kazi ya Roho Mtakatifu inapoendelea mbele, Mungu kwa mara nyingine tena ametuingiza katika mbinu mpya ya kazi ya Roho Mtakatifu. Matokeo yake, haiepukiki kwamba baadhi ya watu wamenielewa Mimi vibaya na kufanya malalamiko Kwangu. Wengine wamenipinga na kunikataa Mimi, na wamenichunguza Mimi. Hata hivyo, bado Mimi ninasubiri kwa rehema toba yenu na mageuzi. Mabadiliko katika utaratibu wa kazi ya Roho Mtakatifu ni Mungu Mwenyewe