Jumamosi, 13 Oktoba 2018
Neno la Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 13, 2018Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo, Mwenyezi-Mungu-anasema, Neno-la-Mungu, Ukweli, VitabuNo comments
Mwenyezi Mungu anasema, "Kumwamini Mungu si rahisi jinsi mwanadamu anaweza kuona. Mungu anavyoona, ukiwa tu na ufahamu lakini huna neno Lake kama uhai; ikiwa wewe unazingatia tu maarifa yako mwenyewe lakini huwezi kutenda ukweli au kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, basi hii ni dhihirisho kwamba huna moyo wa upendo kwa Mungu, na inaonyesha kwamba moyo wako si mali ya Mungu. Kuja kumjua Mungu kwa kumwamini; hili ndilo lengo la mwisho na ambalo mwanadamu atatafuta. Lazima ufanye juhudi ya kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ili yaweze kuonekana katika matendo yako. Kama unayo maarifa ya mafundisho ya dini pekee, basi imani yako kwa Mungu itakuwa kazi bure. Kama wewe utatenda pia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake basi imani yako inaweza kuchukuliwa kuwa kamili na kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu."
Ijumaa, 12 Oktoba 2018
Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 12, 2018Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, kula-na-kunywa-maneno-ya-Mungu, Mwenyezi-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje
Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawa ida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu. Una uwezo wa kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu kila unapofanya chochote; hata kama huelewi mapenzi ya Mungu, bado ni lazima utimize wajibu na majukumu yako kadri ya uwezo wako. Hujachelewa sana kusubiri mapenzi ya Mungu yafichuliwe kwako na kisha kuyaweka katika vitendo. Wakati uhusiano wako na Mungu umekuwa wa kawaida, basi pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu. Kila kitu kimejengwa juu ya msingi wa maneno ya Mungu. Kupitia katika kula na kunywa maneno ya Mungu, tenda kulingana na mahitaji ya Mungu, weka sawa maoni yako, usitende mambo yanayompinga Mungu au kuingilia kati mambo ya kanisa. Usifanye vitu visivyo na manufaa kwa maisha ya ndugu, usiseme maneno yasiyosaidia wengine, usifanye vitu vya kufedhehesha. Kuwa mwadilifu na mwenye heshima unapofanya mambo yote na kuyafanya ya kupendeza mbele ya Mungu. Hata ingawa kutakuwa na nyakati ambazo mwili ni dhaifu, unaweza kushikiza umuhimu mkubwa kabisa kwa kufaidi familia ya Mungu, kutotamani faida yako mwenyewe, na kutekeleza haki. Ikiwa unaweza kutenda kwa njia hii, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.
Kila unapofanya chochote, lazima uchunguze iwapo motisha yako ni sahihi. Ikiwa unaweza kutenda kulingana na matakwa ya Mungu, basi uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida. Hiki ndicho kigezo cha chini zaidi. Iwapo, unapochunguza motisha yako, kunatokea zile zisizo sahihi, na iwapo unaweza kuzikwepa na kutenda kulingana na maneno ya Mungu, basi utakuwa mtu ambaye ni mwema mbele ya Mungu, kitu ambacho kitaonyesha kuwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, na kwamba kila unachofanya ni kwa ajili ya Mungu, na sio kwa sababu yako binafsi. Ni lazima uuweke moyo wako sawa kila unapofanya ama kusema chochote, uwe mwenye haki katika matendo yako, na usiongozwe na hisia zako, au utende kulingana na mapenzi yako: Haya ndiyo maadili ambayo wale wanaoamini katika Mungu wanatenda kulingana nayo. Motisha za mtu na kimo chake vinaweza kufichuliwa katika kitu kidogo, na hivyo, kwa watu kuingia kwa njia ya kufanywa wakamilifu na Mungu, ni lazima kwanza wasuluhishe motisha yao wenyewe na uhusiano wao na Mungu. Ni pale ambapo tu uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida ndipo utaweza kufanywa mkamilifu na Mungu, na ni hapo tu ndipo ushughulikiaji, upogoaji, nidhamu, na usafishaji wa Mungu kwako utaweza kupata matokeo yanayotakiwa. Hiyo kusema, watu wanaweza kuwa na Mungu mioyoni mwao, wasitafute maslahi binafsi, wasifikirie kuhusu maisha yao binafsi ya baadaye (ikirejelea kufikiri juu ya mwili), lakini badala yake wanabeba mzigo wa kuingia katika maisha, wanajitahidi wawezavyo kutafuta ukweli, na kuitii kazi ya Mungu. Kwa namna hii, makusudi unayoyatafuta ni sahihi, na uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Inaweza kusemwa kwamba kuutengeneza uhusiano wako na Mungu ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia katika safari yako ya kiroho. Ingawa kudura ya mtu iko mikononi mwa Mungu, na imeshaamuliwa kabla na Mungu, na haiwezi kubadilishwa na yeye mwenyewe, kwamba unaweza au huwezi kufanywa mkamilifu au kupatwa na Mungu kunategemea na kama uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au la. Pengine kuna sehemu yako ambazo ni dhaifu au zenye kutotii—lakini bora tu mtazamo wako ni sawa na motisha zako ni sahihi, na bora tu umeuweka uhusiano wako na Mungu sawa na kuufanya wa kawaida, basi utastahili kufanywa mkamilifu na Mungu. Iwapo huna uhusiano sahihi na Mungu, na unatenda kwa ajili ya mwili, au familia yako, basi haijalishi unafanya kazi kwa bidii vipi, itakuwa bure. Iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, basi kila kitu kingine kitakuwa sawa. Mungu haangalii chochote kingine, bali Anaangalia tu iwapo mitazamo yako kuhusu kuamini kwa Mungu ni sawa: unayemwamini, ni kwa ajili ya nani unaamini, na ni kwa nini unaamini. Iwapo unaweza kuona vitu hivi kwa udhahiri, na unaweza kuweka mitazamo yako na matendo, basi maisha yako yatapiga hatua, na una uhakika wa kuweza kuingia kwa njia sahihi. Iwapo uhusiano wako na Mungu sio wa kawaida, na mitazamo yako kuhusu kuamini katika Mungu inaacha maadili, basi haya yatazuia mengine yote. Haijalishi jinsi unavyoamini katika Mungu, hutafaidi chochote. Iwapo tu uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida ndipo utasifiwa na Mungu unapokwepa mwili, unapoomba, unapoteseka, unapostahimili, unapotii, unapowasaidia ndugu zako, unaweka juhudi zaidi kwa Mungu, na kadhalika. Hiyo kusema, watu wanaweza kuwa na Mungu mioyoni mwao, wasitafute maslahi binafsi, wasifikirie kuhusu maisha yao binafsi ya baadaye (ikirejelea kufikiri juu ya mwili), lakini badala yake wanabeba mzigo wa kuingia katika maisha, wanajitahidi wawezavyo kutafuta ukweli, na kuitii kazi ya Mungu. Kwa namna hii, makusudi unayoyatafuta ni sahihi, na uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Inaweza kusemwa kwamba kuutengeneza uhusiano wako na Mungu ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia kwako katika safari ya kiroho. Ingawa hatima yako iko mikononi mwa Mungu, na imeshaamuliwa kabla na Mungu, na haiwezi kubadilishwa na wewe mwenyewe, kwamba unaweza au huwezi kufanywa mkamilifu au kupatwa na Mungu kunategemea na kama uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au la. Pengine kuna sehemu ndani yako ambazo ni dhaifu au zenye kutotii—lakini bora tu mtazamo wako wa nje ni sawa na motisha yako ni sahihi, na bora tu umeuweka uhusiano wako na Mungu sawa na kuufanya wa kawaida, basi utafuzu kufanywa mkamilifu na Mungu. Iwapo huna uhusiano sahihi na Mungu, na unatenda kwa ajili ya mwili, au familia yako, basi haijalishi kiwango cha kazi unayofanya kwa bidii, itakuwa bure. Iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, basi kila kitu kingine kitakuwa sawa. Mungu haangalii chochote kingine, bali anaangalia tu iwapo mitazamo yako kwa kuamini kwa Mungu ni sawa: unayemwamini, ni kwa ajili ya nani unaamini, na ni kwa nini unaamini. Iwapo unaweza kuona vitu hivi kwa udhahiri, na unaweza kuweka mitazamo yako iwe sawa na kuweza kutenda, basi maisha yako yatapiga hatua, na una uhakika wa kuweza kuingia kwenye njia sahihi. Iwapo uhusiano wako na Mungu sio wa kawaida, na mitazamo yako kwa kuamini katika Mungu inakiuka maadili, basi haya yatazuia mengine yote. Haijalishi jinsi unavyoamini katika Mungu, hutafaidi chochote. Iwapo tu uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida ndipo utasifiwa na Mungu unapoupa mwili kisogo, unapoomba, unapoteseka, unapostahimili, unapotii, unapowasaidia ndugu na dada zako, unaweka juhudi zaidi kwa Mungu, na kadhalika. Iwe kitu unachofanya kina thamani na umuhimu au hakina hutegemea iwapo makusudi yako ni sahihi na iwapo mitazamo yako ni sahihi. Siku hizi, imani ya watu wengi kwa Mungu ni kama kutazama saa kubwa huku vichwa vyao vikiwa vimeelekezwa upande mmoja—mitazamo yao imekengeuka. Kila kitu kitakuwa kizuri ikiwa mwelekeo mpya unaweza kufanyika hapa, kila kitu kitakuwa sawa ikiwa hili litatatuliwa, wakati hakutafanyika kitu ikiwa hili halitatatuliwa. Baadhi ya watu wanakuwa na tabia nzuri katika uwepo Wangu, lakini nyuma Yangu kile wanachofanya ni kupinga. Haya ni maonyesho yaliyopotoka na ya udanganyifu na aina hii ya mtu ni mtumwa wa Shetani, ni mfano halisi wa namna ile ile ya Shetani kumjaribu Mungu. Wewe ni mtu sahihi tu ikiwa unaweza kuitii kazi Yangu na maneno Yangu. Ilimradi unaweza kula na kunywa maneno ya Mungu, ilimradi kila kitu unachofanya kinapendeza mbele ya Mungu, ilimradi hufanyi mambo ya aibu, usifanye mambo ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya watu, ilimradi unaishi katika mwanga, hunyonywi na Shetani, basi uhusiano wako na Mungu utawekwa sawa.
Katika kumwamini Mungu, makusudi na mitazamo yako yanapaswa kuwekwa sawa; unapaswa kuwa na ufahamu sahihi na utendeaji sahihi wa maneno ya Mungu, kazi ya Mungu, mazingira yaliyopangwa na Mungu, mtu aliyeshuhudiwa na Mungu, na wa Mungu wa vitendo. Hupaswi kutenda kulingana na mawazo yako binafsi, au kufanya mipango yako midogo mwenyewe. Unapaswa kuweza kutafuta ukweli katika kila kitu na kusimama katika sehemu yako kama uumbaji wa Mungu na kuzitii kazi zote za Mungu. Kama unataka kutafuta kukamilishwa na Mungu na kuingia katika njia sahihi ya maisha, basi moyo wako siku zote unapaswa kuishi katika uwepo wa Mungu, usiwe fisadi, usimfuate Shetani, usimwachie Shetani fursa yoyote kufanya kazi yake, na usimruhusu Shetani kukutumia. Unapaswa kujitoa kikamilifu kwa Mungu na kumwacha Mungu akutawale.
Upo radhi kuwa mtumishi wa Shetani? Upo radhi kunyonywa na Shetani? Je, unamwamini Mungu na kumtafuta Mungu ili kwamba uweze kukamilishwa na Yeye, au ni ili uwe foili[a] katika kazi ya Mungu? Je, upo radhi kupatwa na Mungu na kuishi maisha ya maana, au upo radhi kuishi maisha tupu na yasiyo na thamani? Upo radhi kutumiwa na Mungu, au kunyonywa na Shetani? Upo radhi kuacha maneno ya Mungu na ukweli kukujaza, au kuacha dhambi na Shetani kukujaza? Litafakari na kulipima hili. Katika maisha yako ya kila siku, unapaswa kuyaelewa maneno hayo uyasemayo na mambo hayo uyafanyayo ambayo yatasababisha uhusiano wako na Mungu kuwa usio wa kawaida, halafu ujirekebishe na kuingia katika tabia sahihi. Yachunguze maneno yako, vitendo vyako, kila mwenendo wako, na fikra zako na mawazo wakati wote. Ielewe hali yako ya kweli na ingia katika njia ya kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwa njia hii tu ndipo unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Kwa kupima iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kurekebisha makusudi yako, kuielewa asili ya mwanadamu, na kujielewa mwenyewe; kupitia hili, utaweza kuingia katika uzoefu halisi, na kujinyima kwa kweli, na kupata utiifu wa makusudi. Katika masuala hayo kama unapokuwa unapitia iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kupata fursa za kukamilishwa na Mungu, utaweza kuelewa hali nyingi, ambazo kwazo Roho Mtakatifu Anafanya kazi, na utaweza kubaini mengi ya udanganyifu na njama za Shetani. Ni kupitia njia hii tu ndipo unaweza kukamilishwa na Mungu. Unaweka uhusiano wako na Mungu sawa ili kwamba ujisalimishe mwenyewe mipangilio yote ya Mungu. Ni ili utaingia kwa kina zaidi katika uzoefu halisi, na kupata kazi zaidi ya Roho Mtakatifu. Unafanya mazoezi ya kuwa na uhusianao wa kawaida na Mungu, muda mwingi, utapata huu kupitia kuunyima mwili na kupitia ushirikiano wako wa kweli na Mungu. Unapaswa kuelewa kwamba "bila moyo wa ushirikiano, ni vigumu kupokea kazi ya Mungu; ikiwa mwili haupati mateso, hakuna baraka kutoka kwa Mungu; ikiwa roho haihangaiki, Shetani hataaibishwa." Ikiwa unazitenda na kuzielewa vizuri kanuni hizi, mitazamo yako juu ya imani kwa Mungu itawekwa sawa. Katika matendo yenu ya sasa, mnapaswa kuacha mtazamo wa "kutafuta mkate ili kutuliza njaa," mnapaswa kuacha mtazamo wa "kila kitu kinafanywa na Roho Mtakatifu na watu hawawezi kuingilia." Watu wanaozungumza namna hii wote wanafikiri, "Watu wanaweza kufanya chochote kile ambacho wako radhi kukifanya, na muda utakapofika Roho Mtakatifu atafanya kazi na watu hawatakuwa na haja ya kuushinda mwili, hawatakuwa na haja ya kushirikiana, watakuwa wanahitaji tu Roho Mtakatifu kuwashawishi." Mitazamo hii yote ni ya kipuuzi. Katika mazingira haya, Roho Mtakatifu hawezi kufanya kazi. Ni mtazamo wa aina hii ndio unakuwa kizuizi kikubwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Mara nyingi, kazi ya Roho Mtakatifu inapatikana kupitia ushirikiano wa watu. Bila ushirikiano na kudhamiria, basi kutaka kubadilisha tabia ya mtu, kupata kazi ya Roho Mtakatifu, na kupata mwangaza na nuru kutoka kwa Mungu zote ni fikra za kupita kiasi; hii inaitwa "kujifurahisha mwenyewe na kumsamehe Shetani." Watu kama hawa hawana uhusiano wa kawaida na Mungu. Umepata dalili nyingi za Shetani ndani yako, na katika matendo yako ya zamani, kuna mambo mengi ambayo yamepingana na matakwa ya sasa ya Mungu. Je, unaweza kuyatelekeza sasa? Pata uhusiano wa kawaida na Mungu, fanya kulingana na makusudi ya Mungu, kuwa mtu mpya na kuwa na maisha mapya, usitazame dhambi zako za zamani, usiwe mwenye majuto kupita kiasi, kuwa na uwezo wa kusimama na kushirikiana na Mungu, na kutimiza majukumu ambayo unapaswa kufanya. Kwa njia hii, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.
Ikiwa unakubali tu maneno haya kwa mdomo baada ya kuyasoma lakini hayajaingia moyoni mwako, na huko makini kuhusu kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi inathibitisha kwamba huweki umuhimu mkubwa kwenye uhusiano wako na Mungu, mitazamo yako bado haijawekwa sawa, makusudi yako bado hayajaelekezwa kwa kumruhusu Mungu akupate, na kumkubalia Mungu utukufu, badala yake yameelekezwa kwa kuruhusu njama za Shetani kushinda na kwa kupata malengo yako binafsi. Watu wa aina hii wote wana makusudi na mitazamo isiyo sahihi. Bila kujali kile ambacho Mungu amesema au namna kilivyosemwa, hawajali na hakuna mabadiliko yanayoweza kuonekana. Mioyo yao haihisi woga wowote na hawaoni aibu. Mtu wa aina hii ni mtu aliyekanganyikiwa bila roho. Kwa kila tamshi la Mungu, baada ya kulisoma na kupata ufahamu, utaliweka katika vitendo. Bila kujali ulivyokuwa ukitenda kabla—pengine huko nyuma mwili wako ulikuwa dhaifu, ulikuwa muasi, na ulipinga—hili silo jambo kubwa, na haliwezi kuzuia maisha yako yasikue leo. Ilimradi unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu leo, basi kuna tumaini. Ikiwa kwa kila wakati unaposoma maneno ya Mungu, unakuwa na mbadiliko na kuruhusu watu wengine kuona kwamba maisha yako yamebadilika kuwa mazuri, inaonyesha kwamba una uhusiano wa kawaida na Mungu na kwamba umewekwa sawa. Mungu hashughulikii watu kulingana na dhambi zao. Ilimradi unaweza kutoasi tena na hupingi tena baada ya wewe kuelewa na kufahamu, basi Mungu atakuwa bado Ana huruma na wewe. Unapokuwa na ufahamu huu na nia ya kutafuta kukamilishwa na Mungu, basi hali yako katika uwepo wa Mungu itakuwa ya kawaida. Bila kujali unachofanya, zingatia: Mungu atafikiri nini ikiwa nitafanya hiki? Kitawaathiri vipi ndugu? Chunguza makusudi yako katika maombi, ushirika, usemi, kazi na kuhusiana na watu, na chunguza endapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au si wa kawaida. Ikiwa huwezi kutofautisha makusudi yako na fikra zako, basi huna ubaguzi, kitu ambacho kinathibitisha kwamba unaelewa kidogo sana kuhusu ukweli. Kuwa na ufahamu ulio wazi wa kila kitu ambacho Mungu hufanya, vitazame vitu kulingana na neno la Mungu na vitazame vitu kwa kusimama katika upande wa Mungu. Kwa njia hii mitazamo yako itakuwa sahihi. Kwa hiyo, kujenga uhusiano mzuri na Mungu ni kipaumbele cha juu kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu; kila mtu anapaswa kuichukulia kama kazi muhimu na kama tukio lao kubwa la maisha. Kila kitu unachofanya kinapaswa kipimwe dhidi ya iwapo una uhusiano wa kawaida na Mungu au la. Ikiwa uhusianao wako na Mungu ni wa kawaida na makusudi yako ni sahihi, basi kifanye. Ili kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, hupaswi kuogopa kupoteza maslahi binafsi, hupaswi kumruhusu Shetani kushinda, hupaswi kumruhusu Shetani kupata kitu dhidi yako, na hupaswi kumruhusu Shetani kukufanya uwe kichekesho. Kusudi kama hili ni udhihirisho kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Si kwa ajili ya mwili, badala yake ni kwa ajili ya amani ya roho, ni kwa ajili ya kupata kazi ya Roho Mtakatifu na kwa ajili ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ili kuingia katika hali sahihi, unapaswa kujenga uhusiano mzuri na Mungu, unapaswa kuweka sawa mtazamo wako wa imani kwa Mungu. Ni kumruhusu Mungu kukupata, kumruhusu Mungu kufichua matunda ya maneno Yake kwako na kukuangazia na kukupatia nuru zaidi. Kwa namna hii utaingia katika tabia nzuri. Endelea kula na kunywa maneno ya Mungu ya sasa, ingia katika njia ya sasa ya kazi ya Roho Mtakatifu, fanya kulingana na matakwa ya Mungu ya sasa, usifuate mazoea ya kale, using'ang'anie njia za zamani za kufanya mambo, na haraka ingia katika namna ya kazi ya leo. Kwa njia hii uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida kabisa na utaingia katika njia sahihi ya kumwamini Mungu.
Alhamisi, 11 Oktoba 2018
Swahili Christian Music Video | "Ni Watu Waaminifu Pekee Walio na Mfano wa Binadamu" | God Led Me Onto the Right Path of Life
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 11, 2018Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, Msururu-wa-MV-za-Ufalme, nyimbo-za-sifa, Nyimbo-za-Uzoefu-wa-Maisha, VideoNo comments
Swahili Christian Music Video | "Ni Watu Waaminifu Pekee Walio na Mfano wa Binadamu" | God Led Me Onto the Right Path of Life
I
Kwa ajili ya faida niliacha viwango vyote vya mwenendo,
na bila haya nikatumia udanganyifu kutafuta riziki yangu.
Sikujali chochote kuhusu dhamiri au maadili, chochote kuhusu uadilifu au heshima.
Niliishi tu kuridhisha tamaa na uroho wangu vilivyozidi kukua.
Kwa moyo usio na amani, nilitembea katika matope ya dhambi,
bila njia yoyote ya kuepuka giza hii isiyo na mipaka.
Utajiri wa maisha na raha za muda mfupi
hazingeweza kuficha utupu na maumivu ndani ya moyo wangu.
Ni rahisi kuandika neno "mwanadamu."
Lakini kuwa mwaminifu na mwenye kusadikika ni vigumu kuliko ngumu.
Ni nani anayeweza kuniokoa kutoka katika shimo hili la dhambi?
Ni nani anayeweza kuniokoa kutoka katika shimo hili la dhambi?
II
Sauti ya Mungu imeniongoza mbele Yake.
Leo ninaweza kumfuata Mungu na kumtumikia.
Moyo wangu umejaa utamu kutoka kwa kusoma maneno ya Mungu kila siku.
Kwa kuelewa ukweli, sasa nina kanuni za tabia za kibinadamu.
Kila kitu ninachofanya na kusema ni kulingana na maneno ya Mungu.
Kukubali uchunguzi wa Mungu katika mambo yote huufanya moyo wangu uwe mtulivu na wenye amani.
Hakuna udanganyifu, hakuna uongo, ninaishi katika nuru.
Kwa moyo ulio wazi, mimi ni mtu mwaminifu, na ninaishi kwa kudhihirisha mfano wa kibinadamu mwishowe.
Hukumu ya Mungu na kuadibu kumeniokoa,
na kuniwezesha kuzaliwa upya katika maneno ya Mungu.
Mimi nina shukrani milele kwa upendo wa Mungu na kwa wokovu wa Mungu!
Mimi nina shukrani milele kwa upendo wa Mungu na kwa wokovu wa Mungu!
Mimi nina shukrani milele kwa upendo wa Mungu na kwa wokovu wa Mungu!
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Jumatano, 10 Oktoba 2018
Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 10, 2018Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Vitabu, Wasioweka-Ukweli-katika-VitendoNo comments
Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo
Wale miongoni mwa ndugu na dada ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolewa. Katika Imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi hawatashindwa tu kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomuasi Mungu. Wakati mtu anayeamini Mungu hamtii Mungu ama kumcha Mungu lakini badala yake anamwasi Yeye, basi hii ndiyo aibu kuu zaidi kwa muumini. Ikiwa usemi na mwenendo wa muumini daima havina mpango na bila kizuizi kama asiyeamini, basi huyu muumini ni mwovu zaidi kumpiku asiyeamini; yeye ni ibilisi halisi. Wale walio kanisani ambao wanaeneza matamshi yao yenye sumu, wale miongoni mwa ndugu na dada ambao wanasambaza uvumi, kuchochea utengano na kufanya magenge wanapaswa kufukuzwa kutoka kanisani. Lakini watu hawa wamezuiwa kwa kuwa sasa ni enzi tofauti ya kazi ya Mungu, kwa sababu wamehukumiwa kuwa vyombo vya kuondolewa. Wale waliopotoshwa na Shetani wote wana tabia iliyopotoka. Lakini ilhali baadhi ya watu wana tu tabia iliyopotoka kuna wengine wasio jinsi hii, ya kuwa hawana tu tabia za kishetani zilizopotoka, lakini asili zao pia ni mbovu kupita kiasi. Yote anayoyafanya mtu huyu na kusema hayaonyeshi tu tabia yake ya kishetani, bali yeye mwenyewe ni ibilisi Shetani halisi. Anachofanya ni kuvuruga na kukatiza kazi ya Mungu, kuvuruga maisha ya kuingia ya ndugu na dada, na kuharibu maisha ya kawaida ya kanisa. Mbwa mwitu hawa waliovalia ngozi ya kondoo lazima waondolewe nje siku moja, na mtu lazima awe na mtazamo usiojizuia kwa vibaraka hawa wa Shetani; mtu lazima awe na mtazamo wa kuachwa kwao. Ni katika kufanya hili pekee ndipo mtu atakaweza kusimama upande wa Mungu na wale wasioweza kufanya hili wako katika ushirika na Shetani. Mungu daima yumo mioyoni mwa wale wanaomwamini Mungu kwa kweli na daima wana moyo wa kumcha Mungu, moyo wa kumpenda Mungu. Wale wanaomwamini Mungu lazima wayafanye mambo kwa moyo wa uangalifu na wenye busara, na yote wanayoyafanya yanapasa kulingana na matakwa ya Mungu na yaweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Hawapaswi kuwa wabishi, wakifanya watakavyo, hayo hayafai katika utaratibu mtakatifu. Watu hawawezi kuipunga bendera ya Mungu kwa madaha na kucharuka kila mahali, wakijishau na kutapeli kotekote; kutenda haya ni tendo la uasi la juu zaidi. Familia zina masharti na mataifa yana sheria, hivyo ni kwa kiasi gani zaidi ndiyo familia ya Mungu ina viwango vikali? Je, si pia ina amri za usimamiaji? Watu wana uhuru wa kutenda watakayo, lakini amri za usimamizi za Mungu haziwezi kubadilishwa kwa hiari. Mungu ni Mungu asiyewaruhusu watu kumkosea Yeye na Mungu ni Mungu anayewauwa watu—je, watu hawajui hili tayari?
Kila moja ya kanisa lina watu wanaolivuruga kanisa, watu wanaokatiza kazi ya Mungu. Watu hawa wote ni Shetani wanaojifanya katika familia ya Mungu. Mtu wa aina hii ni mjuzi wa kuiga, akija mbele Yangu kwa heshima, akitikisa vichwa kwa kukubali na kuinama, akitenda kama mbwa wengi walio hafifu, akijitolea “yote” yake ili kufikia malengo yake mwenyewe, lakini akionyesha sura yake mbaya mbele ya ndugu. Anapomwona mtu akiuweka ukweli katika vitendo anamshambulia na kumtenga, na anapomwona mtu mbaya kumpiku yeye mwenyewe, anamsifu mno na kujipendekeza kwake, wakitenda kama viongozi wa kiimla kanisani. Inaweza kusemwa kuwa mengi ya makanisa yana aina hii ya “nyoka mwovu wa ndani,” aina hii ya “mbwa wa kupakata” kati yao. Wanatembea kwa siri kwa pamoja, wakikonyezeana na kuashiriana, na hakuna hata mmoja wao anayeweka ukweli katika vitendo. Yeyote aliye na sumu zaidi ndiye “ibilisi mkuu,” na yeyote aliye na hadhi ya juu zaidi huwaongoza, akipeperusha bendera yao juu zaidi. Watu hawa wanakuwa huru na kufanya wanachotaka kanisani, wakieneza ubaya wao, wakiachilia kifo, wakifanya watakavyo, wakisema wanachopenda, bila anayedhubutu kuwakomesha, wakijawa na tabia za kishetani. Punde tu wanapoanza kusababisha usumbufu, hewa ya kifo inaingia ndani ya kanisa. Wale wanaoweka ukweli katika vitendokatika kanisa wanaachwa na wanashindwa kufikia uwezo wao, ilhali wale wanaovuruga kanisa na kusambaza kifo wanakuwa huru na kufanya wanachotaka kanisani. Cha ziada ni, watu wengi huwafuata. Aina hii ya kanisa iko chini ya udhibiti wa Shetani na ibilisi ni mfalme wao. Iwapo watu wa kanisa hawataamka na kuwafukuza hao ibilisi wakuu, basi pia watakuja kuangamia siku moja. Kuanzia leo na kuendelea hatua lazima zichukuliwe dhidi ya kanisa la aina hii. Ikiwa wale wanaoweza kuuweka ukweli mdogo katika vitendo hawajihusishi na utafutaji, basi kanisa hilo litapigwa marufuku. Ikiwa hakuna mtu yeyote kanisani aliye radhi kuuweka ukweli katika vitendo, hakuna yeyote anayeweza kuwa shahidi kwa Mungu, basi kanisa hilo linapasa kutengwa kabisa, na miunganisho yao na makanisa mengine kukatizwa. Hili linaitwa kuzika kifo, na kumfukuza Shetani. Iwapo kuna nyoka kadhaa waovu wa ndani katika kanisa, na vilevile nzi wadogo wanaowafuata wale wasio na ufahamu kabisa, ikiwa wale wa kanisa bado hawawezi kutoa vifungu na ushawishi wa nyoka hawa baada ya wao kuona ukweli, basi hawa wajinga wataondolewa mwishoni. Ingawa nzi hawa wadogo wanaweza kuwa hawajafanya lolote baya, wao ni wenye hila hata zaidi, wadanganyifu hata zaidi na wenye kukwepa hata zaidi na kila mtu aliye namna hii ataondolewa. Hakuna yeyote atakayeachwa! Wale walio wa Shetani watarudishwa kwa Shetani, ilhali wale walio wa Mungu hakika watakwenda kutafuta ukweli; hili linaamuliwa na asili zao. Acheni wale wote wanaomfuata Shetani waangamie! Hakuna huruma watakayoonyeshwa watu hawa. Acheni wale wanaofuata ukweli wapate utoaji na muwakubalie kufurahia neno la Mungu hadi mioyo yao itosheke. Mungu ni mwenye haki; Yeye hawatendei watu kwa udhalimu. Ikiwa wewe ni ibilisi basi hutakuwa na uwezo wa kuuweka ukweli katika vitendo. Ikiwa wewe ni mtu anayetafuta ukweli basi ni wazi kuwa hutatekwa nyara na Shetani—hili halina tashwishi yoyote.
Wale wasiotafuta kuendelea daima wanataka wengine wawe wabaya na watepetevu kama wao wenyewe, wale wasioweka ukweli katika vitendo wanawaonea gere wale wanaotenda ukweli. Wale wasioweka ukweli katika vitendo daima wanataka kuwadanganya wale wapumbavu na wasio na ufahamu. Mambo ambayo watu hawa wanaeneza yanaweza kukufanya usawijike, kuteleza kwenda chini, kuwa na hali isiyokuwa ya kawaida na kujawa na kiza ndani yako; yanaweza kukufanya usogezwe mbali na Mungu, na yanakufanya uuthamini mwili na kujihusisha na tamaa. Wale ambao hawapendi ukweli, ambao daima humshughulikia Mungu kwa uzembe hawana maarifa ya binafsi, na tabia zao huwashawishi watu kufanya dhambi na kuasi Mungu. Hawaweki ukweli katika vitendo wala kuwaruhusu wengine kutenda ukweli. Wanathamini dhambi na hawana chuki kwao wenyewe. Hawajifahamu wenyewe na huwakomesha wengine kujifahamu wenyewe, na huwakomesha wengine kuwa na matamanio ya kujua ukweli. Wale wanaowadanganya hawawezi kuona mwangaza na huanguka gizani, hawajijui wenyewe, na ukweli kwao si wazi na wanakuwa mbali zaidi na zaidi na Mungu. Hawaweki ukweli katika vitendo na huwakomesha wengine kutenda ukweli, wakiwaleta watu hao wajinga mbele yao. Badala ya kusema kuwa wanamwamini Mungu ingekuwa vyema kusema kuwa wanawaamini mababu zao, kwamba kile wanachoamini ni sanamu zilizo mioyoni mwao. Ingekuwa vyema kwa wale watu wanaosema kuwa wanamfuata Mungu kufungua macho yao watazame vizuri waone ni nani wanayemwamini hasa: Je, ni Mungu unayemwamini hakika, ama Shetani? Ikiwa unajua kuwa unayemwamini si Mungu ila sanamu zako mwenyewe, basi ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Ikiwa hakika hujui unayemwamini ni nani, basi, pia, ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Kusema hivi kutakuwa kukufuru! Hakuna anayekushurutisha umwamini Mungu. Msiseme kuwa mnaniamini Mimi, kwa kuwa Niliyasikia maneno hayo hapo kale wala Sitamani kuyasikia tena, kwa kuwa mnachoamini ni sanamu zilizo katika mioyo yenu na nyoka waovu wa ndani walio miongoni mwenu. Wale wanaotikisa vichwa vyao wanaposikia ukweli, wanaotabasamu sana wanaposikia mazungumzo ya kifo ni watoto wa Shetani, na wote ni vyombo vya kuondolewa. Kuna watu wengi kanisani ambao hawana ufahamu, na jambo la uongo linapotendeka wanasimama tu upande wa Shetani. Wanapoitwa vibaraka wa Shetani wanahisi kuwa wamekosewa sana. Wanasemekana kuwa hawana ufahamu, lakini daima wanasimama upande usiokuwa na ukweli. Hakujakuwa na wakati muhimu ambapo wamesimama upande wa ukweli, hakuna wakati mmoja ambapo wamesimama na kutetea mjadala juu ya ukweli, kwa hivyo je, hawana ufahamu? Kwa nini daima wanasimama upande wa Shetani? Kwa nini hawasemi neno lolote la haki ama lenye maantiki kwa ukweli? Je, hali hii kweli imetokana na kuchanganyikiwa kwao kwa ghafla? Kadri mtu anapokuwa na ufahamu mdogo, ndivyo anavyozidi kushindwa kusimama upande wa ukweli. Je, hili linaonyesha nini? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu wanapenda uovu? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu ni watoto waaminifu wa Shetani? Je, ni kwa nini daima wanaweza kusimama upande wa Shetani na kuzungumza lugha moja naye? Kila neno na tendo lao, na maonyesho yao yanathibitisha vya kutosha kuwa wao sio wapenzi wa ukweli kwa namna yoyote, lakini badala yake wao ni watu wanaochukia ukweli. Kwamba wanaweza kusimama upande wa Shetani kunadhihirisha kuwa hakika Shetani anawapenda ibilisi hawa wadogo wanaopigana kwa ajili ya Shetani katika maisha yao yote. Je, taarifa hizi za kweli si wazi sana? Ikiwa hakika wewe ni mtu unayependa ukweli, basi kwa nini huwezi kuwaheshimu wale wanaotenda ukweli, na mbona unawafuata mara moja wale wasioweka ukweli katika vitendo punde tu wanapokuwa na mabadiliko ya sura? Je, hili ni tatizo la aina gani? Sijali iwapo una ufahamu au la, sijali kwamba umelipa gharama kuu kiasi gani, sijali kuwa nguvu zako ni kuu kiasi gani na sijali ikiwa wewe ni nyoka mwovu wa ndani ama kiongozi anayepeperusha bendera. Ikiwa nguvu zako ni kuu basi ni kwa ajili tu ya usaidizi wa nguvu za Shetani; ikiwa hadhi yako iko juu, basi ni kwa sababu kuna wengi waliokuzunguka wasiotenda ukweli; ikiwa hujafukuzwa basi ni kwa kuwa sasa sio wakati wa kazi ya kufukuza, bali ni wakati wa kazi ya kuondoa. Hakuna haraka ya kukufukuza sasa. Ninahitaji tu kusubiri siku ifike ambayo utakuwa umeshaondolewa ili Nikuadhibu. Yeyote asiyeweka ukweli katika vitendo ataondolewa!
Wale wanaomwamini Mungu kwa kweli ni wale walioradhi kuweka neno la Mungu kwenye matendo, na ni wale walioradhi kutenda ukweli. Wale wanaoweza kwa kweli kuwa shahidi kwa Mungu pia ni wale walioradhi kuweka neno Lake kwenye matendo, na ni wale ambao kwa kweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wanaotumia hila na wale wanaotenda yasio haki wote ni watu wasiokuwa na ukweli na wote huleta aibu kwa Mungu. Wale walio kanisani wanaohusika na mabishano ni vibaraka wa Shetani, na ni mfano mwema wa Shetani. Mtu wa aina hii ni mwovu sana. Wale wasio na ufahamu na wasio na uwezo wa kusimama upande wa ukweli wanahifadhi nia mbovu na kufifisha ukweli. Watu hawa hata zaidi ni mawakilishi kamili wa Shetani; wamepita hali ya ukombozi na ni wazi mno kuwa wao wote ni vitu vya kuondolewa. Wale wasioweka ukweli katika vitendo hawapaswi kuruhusiwa kusalia katika familia ya Mungu, wala wale wanaobomoa kanisa kwa maksudi. Lakini sasa Sifanyi kazi ya kufukuza. Watafichuliwa tu na kuondolewa mwishoni. Hakuna kazi nyingine ya bure itakayofanywa kwa watu hawa; wale walio wa Shetani hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, ilhali wale wanaotafuta ukweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wasioweka ukweli katika vitendo hawastahili kusikia njia ya kweli na hawastahili kuwa na ushuhuda kwa ukweli. Kimsingi ukweli si kwa ajili ya masikio yao lakini badala yake unazungumzwa kwa ajili ya masikio ya wale wanaoutenda. Kabla ya mwisho wa kila mtukufichuliwa, wale wanaovuruga kanisa na kukatiza kazi kwanza wataachwa upande moja. Pindi kazi itakapokamilika, watu hawa watafunuliwa mmoja baada ya mwingine kabla ya kuondolewa. Wakati wa kutoa ukweli, Siwatilii maanani kwa sasa. Ukweli wote unapofichuliwa kwa mwanadamu watu hao wanapasa kuondolewa, kwa kuwa huo pia utakuwa wakati ambapo watu wataainishwa kulingana na aina yao. Kwa sababu ya werevu wao mdogo, wale wasio na ufahamu watakuja kuangamia mikononi mwa watu waovu na watapotoshwa na watu waovu na watashindwa kurudi. Watu hawa wanapasa kushughulikiwa kwa njia hii, kwa kuwa hawaupendi ukweli, kwa sababu hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, kwa sababu wanawafuata watu waovu, wanawaunga mkono watu waovu, na kwa sababu wanashirikiana na watu waovu na kumuasi Mungu. Wanajua vema kuwa watu hao waovu wananururisha uovu lakini wanafanya mioyo yao kuwa migumu na kuwafuata, wakienda kinyume na ukweli. Je, watu hawa wasioweka ukweli katika vitendo lakini wanaofanya mambo ya uharibifu na ya chukizo wote si wanafanya maovu? Ingawa kuna wale miongoni mwao ambao wanajipa mtindo wenyewe kama “wafalme” na wale wanaofuata msururu nyuma yao, je, asili yao ya kuasi Mungu si ni sawa yote? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu hawaokoi? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu si mwenye haki? Je, si ni uovu wao wenyewe ambao umewaangamiza? Je, si ni uasi wao ambao utawavuta hadi jahanamu? Wale wanaoweka ukweli katika vitendo mwishowe wataokolewa na kufanywa wakamilifu kwa kupitia ukweli. Wale wasioweka ukweli katika vitendo mwishowe watakaribisha maangamizi kwa kupitia ukweli. Hii ndio miisho inayowasubiri wale wanaoweka ukweli katika vitendo na wale wasioutenda. Ninawashauri wale ambao hawana mpango wa kuweka ukweli katika vitendo watoke kanisani haraka iwezekanavyo ili kuepuka kutenda dhambi nyingi zaidi. Wakati utakapofika, hata majuto yatakuwa yamechelewa, na hasa wale wanaofanya magenge na kufanya migawanyiko, na wale nyoka waovu wa ndani katika kanisa lazima watoke haraka sana. Watu hawa ambao ni wenye asili ya mbwa mwitu mwovu hawana uwezo wa mabadiliko, ni heri watoke kanisani kwa nafasi inayopatikana mwanzo, wasiweze kuyavuruga maisha mazuri ya ndugu na dada tena, na hivyo kuepuka adhabu ya Mungu. Nyinyi ambao mlienda pamoja nao mtafanya vema kutumia nafasi hii kutafakari juu yenu wenyewe. Je, mtawafuata waovu nje ya kanisa, ama kusalia na kufuata kwa uaminifu wote? Lazima uzingatie jambo hili kwa makini. Ninawapa nafasi moja zaidi ya kuchagua. Ninalisubiri jibu lenu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Tufuate:Kanisa la Mwenyezi Mungu
Jumanne, 9 Oktoba 2018
Maonyesho ya Mungu "Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili" (Official video)
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 09, 2018kusoma-maneno-ya-Mwenyezi-Mungu, Maonyesho-ya-Mungu, Mwenyezi-Mungu-alivyosema, Video, Video-za-KikristoNo comments
Maonyesho ya Mungu "Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili" (Official video)
Mwenyezi Mungu alivyosema, "Hiyo ni kwa sababu Roho tayari amekwishaanza kazi, na maneno yanayonenwa sasa yanaelekezwa kwa watu ulimwenguni kote. Na hili, nusu ya kazi tayari inafanywa. Kutoka kuumbwa kwa dunia hadi sasa, Roho wa Mungu ameendeleza hii kazi kubwa, na aidha Amefanya kazi tofauti katika enzi tofauti, na katika mataifa tofauti. Watu wa kila enzi wanaiona tabia Yake tofauti, ambayo kwa asili inafichuliwa kupitia kazi tofauti Anazozifanya.
Jumatatu, 8 Oktoba 2018
Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 08, 2018Kuhusu-Maisha-ya-Kawaida-ya-Kiroho, Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo, neno-la-Mwenyezi-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho
Muumini lazima awe na maisha ya kawaida ya kiroho huu ni msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika hali halisi. Sasa hivi, je, maombi yote, kule kuja karibu na Mungu, kuimba, kusifu, kutafakari, na kule kujaribu kuelewa maneno ya Mungu ambayo mnatenda yanafikia viwango vya maisha ya kawaida ya kiroho?
Jumapili, 7 Oktoba 2018
Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (5) - Je, Hukumu ya Mungu katika Siku za Mwisho ni Adhabu au Wokovu?
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 07, 2018Filamu-za-Injili, Hukumu-ya-Mungu, iku-za-Mwisho, Sauti-Nzuri-Ajabu, VideoNo comments
Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (5) - Je, Hukumu ya Mungu katika Siku za Mwisho ni Adhabu au Wokovu?
Baadhi ya watu husoma maneno ya Mungu na kuona kwamba kunayo mambo makali ambayo ni hukumu ya wanadamu, na shutuma na laana. Wanafikiria kwamba kama Mungu huhukumu na kulaani watu, nao pia hawatashutumiwa na kuadhibiwa? Inawezaje kusemekana kwamba aina hii ya hukumu ni ya kutakasa na kuokoa wanadamu? Maneno ya Mungu yanasema: "Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu." "Ufichuzi mkali wa neno ni kwa kusudi la kukuongoza kwenye njia sahihi" (Neno Laonekana katika Mwili). Ni njia gani nzuri ya kufahamu kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho?
Jumamosi, 6 Oktoba 2018
Kiini cha Kristo Ni Mungu
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 06, 2018Kiini-cha-Kristo-Ni-Mungu, Kristo, Nyimbo, Nyimbo-za-Neno-la-Mungu, Wimbo-wa-Maneno-ya-MunguNo comments
Kiini cha Kristo Ni Mungu
Wimbo wa Maneno ya Mungu
Kiini cha Kristo Ni Mungu
I
Mungu anayekuwa mwili anaitwa Kristo,
na hivyo Kristo anayeweza kuwapa watu ukweli anaitwa Mungu.
Si kupita kiasi kusema hivyo,
kwani Ana kiini cha Mungu.
Ana tabia ya Mungu na hekima katika kazi Yake,
ambayo haifikiwi na mwanadamu.
Wale wanaojiita Kristo wenyewe
ilhali hawawezi kufanya kazi
ya Mungu ni wadanganyifu.
Wanaojifanya kuwa Kristo hatimaye wataanguka,
ingawaje wanadai kuwa Kristo,
hawana kiini chochote cha Kristo.
II
Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani,
lakini mwili hasa uliochukuliwa na Mungu.
Anapotekeleza na kutimiza kazi Yake kati ya mwanadamu.
Mwili huu hauwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote tu.
Ila mwili unaoweza kutosha kubeba kazi ya Mungu duniani.
Na kuonyesha tabia ya Mungu,
na kumwakilisha Mungu vizuri na kumpa mwanadamu uzima.
Hivyo Mungu anasema kuwa uhalali wa Kristo,
hauwezi kufafanuliwa na mwanadamu,
lakini unajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe.
Hivyo kama kwa kweli unataka kutafuta njia ya uzima,
lazima kwanza utambue,
ni katika siku za mwisho ambapo Anakuja duniani,
kumpa mwanadamu njia ya uzima.
Sio zamani, sio zamani; inafanyika leo.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwil
Ijumaa, 5 Oktoba 2018
Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 05, 2018Kusudi-la-Kazi-ya-Mungu-la-Usimamizi, Mungu-na-ukuu, Nyimbo, Nyimbo-za-Neno-la-Mungu, Wimbo-wa-Maneno-ya-MungumNo comments
Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi
Wimbo wa Maneno ya Mungu
Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi
I
Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000,
uliyogawanywa katika hatua tatu,
kila moja inaitwa enzi.
Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema,
na Enzi ya Ufalme ni awamu ya mwisho.
Ingawa kazi ya Mungu ni tofauti katika kila moja,
yote inalingana na kile ambacho binadamu wanahitaji,
ama hasa inalingana na ujanja ambao Shetani anatumia,
anapopigana na Yeye.
Kusudi la Kazi ya Mungu ni kumshinda Shetani,
kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua ujanja wote wa Shetani,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake.
II
Ni ili kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua upotovu mbaya wa Shetani,
kufunza viumbe kutofautisha mema na mabaya,
na kumjua Mtawala wa vitu vyote ni Mungu Mwenyewe.
Kuona wazi kuwa Shetani ni adui wa mwanadamu,
kuwa ni yule mwovu, mhalifu,
ili mwanadamu aweze kutofautisha mema na maovu,
ukweli na uongo,
utakatifu na uchafu, na makuu kutoka kwa ya chini.
Kusudi la Kazi ya Mungu ni kumshinda Shetani,
kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua ujanja wote wa Shetani,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake.
Kumfanya binadamu pumbavu kuwa na ushuhuda Kwake:
Sio Mungu ndiye Alileta upotovu wa mwanadamu,
na ni Mungu Mwenyewe pekee, Bwana wa uumbaji,
Anayeweza kuweka vitu vya kufurahia
na kumletea mwanadamu wokovu.
Hii ni ili waweze kujua kuwa Mungu
ni Mtawala wa vitu vyote,
kuwa Shetani ni uumbaji Wake,
ambaye baadae alichagua kumgeuka.
III
Mpango wa Mungu wa miaka 6,000 wa usimamizi
umegawanywa katika hatua tatu,
ili yafuatayo yaweze kufikiwa:
kuruhusu viumbe Wake kuwa mashahidi Wake,
kujua mapenzi Yake, na kuona kuwa ukweli ni Yeye.
Kusudi la Kazi ya Mungu ni kumshinda Shetani,
kufunua hekima ya Mungu na ukuu,
na kufichua ujanja wote wa Shetani,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake,
hivyo kumwokoa mwanadamu kutoka kwa utawala wake.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Sikiliza zaidi:Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Alhamisi, 4 Oktoba 2018
Tamko la Mia Moja na Nane
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 04, 2018Kurudi-kwa-Yesu-mara-ya-pili, mwanzo-wa-maafa, Mwenyezi-Mungu-alisema, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Tamko la Mia Moja na Nane
Ndani Yangu, wote wanaweza kupata raha na wote wanaweza kuwa huru. Wale walio nje Yangu hawawezi kupata uhuru na furaha kwa sababu Roho Wangu hayuko pamoja na watu hawa.
Jumatano, 3 Oktoba 2018
Filamu za Kikristo | "Vita" | God Saved Me From the Hands of False Shepherds (Swahili Subtitles)
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 03, 2018kusoma-maneno-ya-Mwenyezi-Mungu, kweli, Mwenyezi-Mungu, Video, Video-za-InjiliNo comments
Filamu za Kikristo | "Vita" | God Saved Me From the Hands of False Shepherds (Swahili Subtitles)
Zhang Hui alikuwa mzee katika kanisa la nyumbani la Kichina. Kila wakati alikuwa mtafutaji mwenye bidii, na alikuwa anangojea kuja kwa Bwana. Katika miaka ya hivi majuzi, alishuhudia kanisa likikumbwa na huzuni pole pole.
Jumanne, 2 Oktoba 2018
Wimbo wa Injili "Kiini cha Kristo Ni Mungu" | Differences Between the True Christ and False Christs
By Kuhusu Umeme wa MasharikiOktoba 02, 2018Kiini-cha-Kristo-Ni-Mungu, Kristo, tabia-ya-Mungu, Video, Wimbo-za-InjiliNo comments
Mungu anayekuwa mwili anaitwa Kristo,
na hivyo Kristo anayeweza kuwapa watu ukweli anaitwa Mungu.
Si kupita kiasi kusema hivyo,
kwani Ana kiini cha Mungu, Ana tabia ya Mungu na hekima katika kazi Yake,
ambayo haifikiwi na mwanadamu.
Wale wanaojiita Kristo wenyewe ilhali hawawezi kufanya kazi ya Mungu ni wadanganyifu.
Wanaojifanya kuwa Kristo hatimaye wataanguka,
ingawaje wanadai kuwa Kristo,
hawana kiini chochote cha Kristo.
Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani,
lakini mwili hasa uliochukuliwa na Mungu.
Anapotekeleza na kutimiza kazi Yake kati ya mwanadamu.
Mwili huu hauwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote tu.
Ila mwili unaoweza kutosha kubeba kazi ya Mungu duniani.
Na kuonyesha tabia ya Mungu,
na kumwakilisha Mungu vizuri na kumpa mwanadamu uzima.
Hivyo Mungu anasema kuwa uhalali wa Kristo, hauwezi kufafanuliwa na mwanadamu,
lakini unajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe.
Hivyo kama kwa kweli unataka kutafuta njia ya uzima,
lazima kwanza utambue, ni katika siku za mwisho ambapo Anakuja duniani,
kumpa mwanadamu njia ya uzima.
Sio zamani, sio zamani; inafanyika leo.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Jifunze zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Neno la Mwenyezi mungu