Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumapili, 24 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya


Siku hizi watu wengi hawatilii maanani mafunzo yapi yanayopaswa kusomwa wakati wa upatano na wengine. Nimegundua kuwa wengi wenu hawawezi kujifunza mafunzo hata kidogo wakati wa ushirikiano na wengine. Wengi wenu mnashikilia maoni yenu mwenyewe, na wakati mnafanya kazi kanisani, unatoa maoni yako na yeye anatoa yake, moja uhusiano na mingine, bila kushirikiana kabisa. Mnajihusisha tu katika kutoa umaizi wenu wenyewe wa ndani, unaingia tu katika kuachilia huru “mizigo” ndani yenu, si kutafuta uzima hata kidogo.

Jumamosi, 23 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi


Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ni kitu ambacho kilikuwa hata zaidi kimeshaamuliwa kabla Nilipoiumba dunia. Watu huenda hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho na pia huenda hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda wale walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini, adui Yangu alipoungana katika vita na Mimi, Nilikuwa Nimeshamwambia kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kufanywa watoto wake na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake.

Ijumaa, 22 Februari 2019

Neno la Mungu | "Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya"

Neno la Mungu | “Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya”

    
    Mwenyezi Mungu anasema, "Kuonekana kwa Mungu hurejelea kuwasili Kwake duniani kufanya kazi Yake. Akiwa na utambulisho na tabia Yake, na katika mbinu Yake ya asili, Yeye hushuka miongoni mwa wanadamu kufanya kazi ya kuanzisha enzi mpya na kukamilisha enzi nyingine. Kuonekana kwa aina hii si aina fulani ya sherehe. Si ishara, picha, muujiza, au ono kuu, na hata zaidi si mchakato fulani wa kidini. Ni ukweli halisi ambao waweza kushikwa na kuonekana.

Alhamisi, 21 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Uzoefu


Katika uzoefu wote wa Petro, alikumbana na mamia ya majaribio. Ingawa watu wa leo wanafahamu neno “jaribio,” wao huchanganyikiwa kuhusiana na maana yake ya kweli na hali. Mungu hutuliza azimio la watu, husafisha imani yao, na hukamilisha kila sehemu yao—na hii hufanikishwa kimsingi kupitia majaribio, ambayo pia ni kazi ya Roho Mtakatifu iliyofichwa. Inaonekana kama kwamba Mungu amewaacha watu, na kwa hivyo wasipokuwa waangalifu, watayaona majaribio haya kama majaribu ya Shetani.

Jumatano, 20 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Matamshi ya Mwenyezi Mungu  | Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?


Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu. Hiyo haijalishi, kwani wewe bado u mfuasi wa Mungu, kwa hivyo tushirikiane kuhusu mada ya kumfuata Mungu.

Jumanne, 19 Februari 2019

Neno la Mungu | Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda


Neno la Mungu | Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda


Hatua ya kazi ya watenda-huduma ni hatua ya kwanza ya kazi ya ushindi; kwa sasa hii ni hatua ya pili ya kazi ya ushindi. Kwa nini ukamilifu unajadiliwa katika kazi ya ushindi? Ni kuujenga msingi kwa ajili ya siku za baadaye—kwa sasa hii ni hatua ya mwisho katika kazi ya kushinda, na baada ya hii, kazi ya kuwakamilisha watu itaanza rasmi wakati watakuwa wanapitia dhiki kuu. Jambo la msingi sasa ni ushindi; hata hivyo, hii pia ni hatua ya kwanza ya kukamilisha, kukamilisha ufahamu na utii wa watu, ambayo kwa kweli bado yanajenga msingi wa kazi ya kushinda.

Jumatatu, 18 Februari 2019

Neno la Mungu | Sura ya 26

Neno la Mungu | Sura ya 26

Ni nani ameshinda nyumbani Kwangu? Ni nani amesimama kwa ajili Yangu? Ni nani ameteseka kwa ajili Yangu? Ni nani ameweka ahadi yake mbele Zangu? Ni nani amenifuata hadi leo lakini hajakuwa wa kutojali? Mbona wanadamu wote wana ubaridi na hawana hisia? Mbona binadamu ameniacha? Mbona mwanadamu amechoka na Mimi? Mbona hakuna joto katika ulimwengu wa mwanadamu? Nikiwa Zayuni, Nimeonja joto lililo mbinguni, na Nikiwa Zayuni Nimefurahia baraka iliyoko mbinguni.

Jumapili, 17 Februari 2019

Ishini Katika Upendo wa Mungu | "Wimbo wa Mapenzi Matamu" | Best Swahili Christian nyimbo za kuabudu


Ishini Katika Upendo wa Mungu | "Wimbo wa Mapenzi Matamu" | Best Swahili Christian nyimbo za kuabudu


Kinani mwa moyo wangu, ni mapenzi Yako. Ni matamu sana, nakaa karibu yako.
Kukutunza hukoleza moyo wangu; kukutumikia na mawazo yangu yote.
Kuongoza moyo wangu, ni mapenzi Yako; mimi hufuata nyayo zako za mapenzi.
Mimi hujisogeza kulingana na macho Yako; mapenzi yanaonyesha furaha ya moyo wangu.

Jumamosi, 16 Februari 2019

Neno la Mungu | Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Neno la Mungu | Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

    Mwenyezi Mungu anasema, "Wale waliofanywa kuwa wakamilifu hawawezi tu kuwa watiifu baada ya kushindwa, lakini wanaweza pia kuwa na maarifa wa kazi ya hukumu, kubadilisha tabia yao na kumjua Mungu. Wanapitia njia ya kumpenda Mungu na wamejazwa na ukweli. Wanajua namna ya kupitia kazi ya Mungu, wanaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu, na wanayo hiari zao wenyewe. Wale waliokamilishwa ni wale walio na ufahamu halisi wa ukweli kutokana na kupitia neno la Mungu. Wale walioshindwa ni wale wanaojua kuhusu ukweli lakini hawajakubali maana halisi ya ukweli."

Yaliyopendekezwa:  APP Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Ijumaa, 15 Februari 2019

Nyimbo za Injili | "Njia Yote Pamoja na Wewe" Mungu ni Upendo

Nyimbo za Injili | "Njia Yote Pamoja na Wewe" Mungu ni Upendo 


Nilikuwa kama mashua, ikielea baharini.
Ulinichagua, na mahali pazuri Uliniongoza.
Sasa katika familia Yako, nikipewa joto na upendo Wako,
nina amani kabisa.
Unanibariki, Unatoa maneno Yako ya hukumu.
Bado sijui jinsi ninavyokosa kuithamini neema Yako.
Kila mara nikiasi, kwa namna fulani nikiuumiza moyo Wako.

Alhamisi, 14 Februari 2019

Nyimbo za Kuabudu "Upendo wa Kweli wa Mungu" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitle)


Nyimbo za Kuabudu | "Upendo wa Kweli wa Mungu" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitles)


Leo naja mbele ya Mungu tena,
naona uso Wake wa kupendeza.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
nimeacha siku zangu za zamani za kuzurura nyuma yangu.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
kufurahia neno Lake kunanijaza na furaha.

Jumatano, 13 Februari 2019

Filamu za Injili | “Siri ya Utauwa” (3) - Siri ya Kupata Mwili kwa Mungu


Filamu za Injili | “Siri ya Utauwa” (3) - Siri ya Kupata Mwili kwa Mungu


     Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili na akawa Bwana Yesu aliyekuja kuwakomboa wanadamu, na Mafarisayo wa Kiyahudi wakasema kwamba Bwana Yesu alikuwa mwanadamu tu. Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili na amekuwa Mwenyezi Mungu ambaye Amekuja kufanya kazi Yake ya hukumu, wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa kidini pia wanasema kwamba Mwenyezi Mungu ni mwanadamu tu, kwa hiyo tatizo ni lipi hapa? Kwa upande wa nje, Mungu mwenye mwili Anaonekana kuwa mtu wa kawaida. Lakini ndani Roho wa Mungu anaishi ndani Yake; Anaweza kuonyesha ukweli, kuonyesha sauti ya Mungu na kufanya kazi ya Mungu, kwa hiyo Mungu mwenye mwili ni mwanadamu, au ni Mungu?