Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwendelezo-wa-Neno-Laonekana-katika-Mwili. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwendelezo-wa-Neno-Laonekana-katika-Mwili. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 7 Mei 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Utakatifu wa Mungu (I)

Mwenyezi Mungu alisema, Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. 

Ijumaa, 6 Aprili 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I


Mwenyezi Mungu alisema, Kwa wakati huu, tunafaa kuunganisha mazungumzo yetu na sasa. Kama Mungu angeweza kufanya mambo haya madogo mbalimbali kwa binadamu Aliowaumba hapo mwanzo kabisa, hata vitu vingine ambavyo watu hawangethubutu kufikiria ama kutarajia, basi naye Mungu angewafanyia watu leo mambo kama hayo? Baadhi ya watu husema, “Ndiyo!” Kwa nini hivyo? Kwa sababu kiini cha Mungu si bandia, uzuri Wake si bandia. Kwa sababu kiini cha Mungu kwa kweli kipo, na si kitu kilichoongezewa tu na wengine na bila shaka si kitu ambacho kinabadilika na mabadiliko ya muda, mahalina enzi.

Jumapili, 1 Aprili 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia

12. Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake

(Yohana 20:26-29) Na baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwa ndani tena, na Tomaso pamoja nao: Kisha akaja Yesu, na milango imefungwa, na akasimama katikati, kisha akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso, Weka hapa kidole chako, na utazame mikono yangu; na ulete mkono wako uuweke ubavuni mwangu, na usiwe asiyeamini, bali uwe aaminiye.

Ijumaa, 30 Machi 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia


Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

3) Mungu Atumia Upinde wa Mvua Kama Ishara ya Agano Lake na mwanadamu.

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.
Kisha, hebu tuangalie sehemu hii ya maandiko kuhusu namna Mungu alivyounda upinde wa mvua kama ishara ya Agano lake na binadamu.

Jumatano, 28 Machi 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Mamlaka ya Mungu (I)

Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho? Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu?

Jumatano, 21 Machi 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa

 Mwenyezi Mungu alisema, Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa. Mlima ulikuwa unazuia njia ya kijito hiki, hivyo kijito kikauomba mlima kwa sauti yake dhaifu na ndogo, “Tafadhali naomba kupita, umesimama kwenye njia yangu na umenizibia njia yangu kuendelea mbele.” Basi mlima ukauliza, “Unakwenda wapi?” Swali ambalo kijito kililijibu, “Ninatafuta makazi yangu.” Mlima ukasema, “Sawa, endelea na tiririkia juu yangu!” Lakini kwa sababu kijito kilikuwa dhaifu sana na kichanga sana, hakukuwa na namna kwake kutiririka juu ya mlima mkubwa hivyo, hivyo hakikuwa na uchaguzi bali kuendelea kutiririka chini ya mlima ...

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)


Mwenyezi Mungu alisema, Leo Nitashiriki nawe mada mpya. Mada itakuwa ni nini? Kichwa cha mada kitakuwa “Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.” Je, hii siyo mada kubwa kidogo kuweza kuijadili? Je, inaonekana kama kitu ambacho kidogo hakiwezi kufikika? Mungu kuwa chanzo cha uhai kwa vitu vyote inaweza kuonekana ni mada ambayo watu wanahisi kutohusika nayo, lakini wote wanaomfuata Mungu wanapaswa kuielewa. Hii ni kwa sababu mada hii haihusiani kwa kuchanganulika na kila mtu anayemjua Mungu, kuweza kumridhisha na kumheshimu.

Jumanne, 20 Machi 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa ulimwengu yakinifu, watu wakikosa kuelewa vitu au jambo fulani, wanaweza kutafuta taarifa mwafaka, vinginevyo wanaweza kutumia njia mbalimbali kubaini asili ya habari kuvihusu. Lakini inapokuja kwa ulimwengu huu mwingine ambao tunauzungumzia leo—ulimwengu wa kiroho ulio nje ya ulimwengu yakinifu—watu hawana hasa mbinu au njia za kujifunzia chochote kuuhusu. Mbona Ninasema hivi? Kwa sababu, katika ulimwengu wa mwanadamu, kila kitu cha ulimwengu yakinifu hakijitengi na uwepo wa kimwili wa mwanadamu, na kwa sababu watu wanahisi kwamba kila kitu katika ulimwengu yakinifu hakitenganishwi na maisha yao ya kimwili na uhai wao wa kimwili, watu wengi wanafahamu tu kuhusu, au kuona, vitu yakinifu mbele ya macho yao, vitu vinavyoonekana kwao.

Jumamosi, 17 Machi 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Mwenyezi Mungu alisema, Kwenye mkutano  mwisho tuliweza kuzungumzia mada muhimu sana. Je, wakumbuka mada hiyo ilikuwa kuhusu nini? Hebu Niirudie. Mada ya ushirika wetu wa mwisho ilikuwa: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Je, mada hii ni muhimu kwako? Ni sehemu gani katika mada hii ni muhimu kwako? Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, au Mungu Mwenyewe? Ni sehemu ipi inakuvutia zaidi? Ni sehemu ipi unayotaka kusikiliza kuhusu zaidi? Najua ni vigumu kwako wewe kulijibu swali hilo, kwa sababu tabia ya Mungu inaweza kuonekana katika kila kipengele cha kazi Yake, na tabia Yake inafichuliwa katika kazi Yake siku zote na pahali pote, na, kutokana na hayo, inawakilisha Mungu Mwenyewe; kwenye mpango wa usimamizi wa ujumla wa Mungu, kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe vyote hivi haviwezi kutenganishwa.
Maudhui ya ushirika wetu wa mwisho kuhusu kazi ya Mungu yaliweza kuangazia mambo yaliyofanyika kitambo kwenye Biblia. Maudhui hayo yote yalikuwa hadithi kuhusu binadamu na Mungu, na yalimfanyikia binadamu na wakati huohuo yakahusisha kushiriki na maonyesho ya Mungu, hivyo basi hadithi hizi zinashikilia thamani na umuhimu mkubwa katika kujua Mungu. Baada tu ya kuumba ubinadamu, Mungu Alianza kujihusisha na binadamu na kuzungumza na binadamu, na tabia yake ikaanza kuonyeshwa kwa binadamu. Kwa maneno mengine, tangu Mungu alipojihusisha kwanza na mwanadamu, Alianza kuujuza umma kuhusu binadamu, bila kusita, kiini Chake halisi na kile Anacho na alicho. Licha ya kama watu wa awali au watu wa leo wanaweza kuona au kuelewa kiini hicho, kwa ufupi Mungu anamzungumzia mwanadamu na kufanya kazi miongoni mwa binadamu, Akifichua tabia Yake na Akionyesha kiini Chake —jambo ambalo ni ukweli, na lisilopingika na mtu yeyote. Hii inamaanisha pia kwamba tabia ya Mungu, kiini cha Mungu, na kile Anacho na alicho vyote vinatolewa daima na kufichuliwa huku naye Akifanya kazi na kujihusisha na binadamu. Hajawahi kusetiri au kumfichia binadamu chochote, lakini badala yake anatangaza kwa umma na kuachilia tabia Yake binafsi bila ya kuficha chochote. Hivyo basi, Mungu anatumai kwamba binadamu anaweza kumjua Yeye na kuielewa tabia Yake na kiini chake. Hapendi binadamu kuchukulia tabia Yake na kiini Chake kuwa mafumbo ya milele, wala Hataki mwanadamu kumchukulia Mungu kama fumbo lisiloweza kutatuliwa. Mpaka tu pale ambapo mwanadamu atakapomjua Mungu ndipo binadamu atakapojua njia ya kufuata na kuweza kuukubali mwongozo wa Mungu, na mwanadamu tu kama huyu ndiye anayeweza kuishi kwa kweli katika utawala wa Mungu, na kuishi katika mwangaza, na kuishi katikati ya baraka za Mungu.
Maneno na tabia iliyowasilishwa mbele na kufichuliwa na Mungu inawakilisha mapenzi Yake, na pia inawakilisha kiini Chake halisi. Wakati Mungu anapojihusisha na binadamu, haijalishi ni nini Anachosema au kufanya, au tabia gani Anayofichua, na haijalishi ni nini binadamu anaona kuhusu kiini cha Mungu na kile Anacho na alicho, vyote vinawasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Licha ya kiwango ambacho binadamu anaweza kutambua, kufahamu, au kuelewa, vyote hivi vinawakilisha mapenzi ya Mungu—mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Hii ni zaidi ya shaka! Mapenzi ya Mungu kwa binadamu ni vile Anavyohitaji watu kuwa, kile Anachohitaji wao kufanya, namna Anavyohitaji wao kuishi, na vile Anavyowahitaji kuweza kukamilisha kutimia kwa mapenzi ya Mungu. Je, mambo haya hayawezi kutenganishwa na kiini cha Mungu? Kwa maneno mengine, Mungu huwasilisha mbele tabia Yake na vyote Alivyo navyo na kile ambacho Mungu ni wakati huohuo Akimtolea madai binadamu. Hakuna uongo, hakuna kusingizia, hakuna ufichaji, na wala hakuna kupiga chuku. Ilhali kwa nini binadamu hawezi kujua na kwa nini hajawahi kuweza kutambua waziwazi tabia ya Mungu? Na kwa nini hajawahi kutambua mapenzi ya Mungu? Kile ambacho kimefichuliwa na kuwasilishwa mbele na Mungu ndicho kile Mungu anacho Mwenyewe na maana yake , na kinaonyesha kila kipengele cha tabia Yake ya kweli—hivyo kwa nini binadamu hawezi kuona? Kwa nini binadamu hana uwezo wa kuwa na maarifa ya kina? Kunayo sababu muhimu ya haya. Na sababu yenyewe ni ipi? Tangu wakati wa uumbaji, binadamu hajawahi kumchukulia Mungu kama Mungu. Kwenye nyakati zile za mwanzo kabisa, haikujalisha ni nini Mungu alifanya kuhusiana na binadamu, yule binadamu ambaye ndiye tu alikuwa ameumbwa, binadamu alimchukulia yeye kuwa mwandani wake tu na wala si zaidi ya hapo, kama mtu wa kutegemewa, na hakuwa na maarifa yoyote wala uelewa wa Mungu. Hivi ni kusema, hakujua kwamba kile kilichowasilishwa mbele na Kiumbe huyu—Kiumbe huyu ambaye yeye alitegemea na kumwona kuwa mwandani wake—alikuwa kiini cha Mungu, na wala hakujua kwamba Kiumbe huyu ndiye anayetawala viumbe wote. Nikisema kwa urahisi, watu wa wakati huo hawakuwa na maarifa hata kidogo kumhusu Mungu. Hawakujua kwamba mbingu na nchi na mambo yote yalikuwa yameumbwa na Yeye na wala hawakujua ni wapi Alipotokea, na, zaidi hawakujua Yeye Alikuwa nani. Bila shaka, wakati huo Mungu hakumhitaji binadamu kumjua Yeye au kumfahamu Yeye au kuelewa kila kitu Alichofanya, au kufahamishwa kuhusu mapenzi Yake, kwani hizi zilikuwa nyakati za mapema zaidi baada ya uumbwaji wa mwanadamu. Wakati Mungu alipoanza matayarisho ya kazi ya Enzi ya Sheria, Mungu alifanya mambo fulani kwa binadamu na pia Akaanza kutolea binadamu madai fulani, Akimwambia namna ya kutolea Mungu sadaka na namna ya kumwabudu. Ni wakati huo ndipo binadamu alipopata mawazo machache mepesi kuhusu Mungu, ni hapo tu ndipo alipojua tofauti kati ya binadamu na Mungu na kwamba Mungu Ndiye aliyewaumba wanadamu. Wakati binadamu alipojua kwamba Mungu alikuwa Mungu na binadamu alikuwa binadamu kukawa umbali fulani kati ya Yeye na Mungu , bado Mungu hakuhitaji kwamba binadamu awe na maarifa makuu au uelewa wa kina kumhusu Yeye. Hivyo basi, Mungu anayatoa mahitaji tofauti kwa binadamu kutokana na awamu na hali za kazi Yake. Unaona nini katika haya? Ni kipengele kipi cha tabia ya Mungu unayoitambua? Je, Mungu ni wa kweli? Yale mahitaji ambayo Mungu anampa binadamu yanastahili? Kwenye nyakati za mapema kabisa kufuatia uumbaji wa wanadamu na Mungu, wakati ambao Mungu alikuwa bado hajatekeleza kazi ya ushindi na utimilifu wa binadamu, na Alikuwa hata bado hajaongea yale maneno mengi sana kwake, Alihitaji kidogo sana kutoka kwa binadamu. Licha ya kile ambacho binadamu alifanya na namna alivyotenda—hata kama alifanya mambo fulani yaliyomkosea Mungu—Mungu alimsamehe hayo yote, na akayapuuza. Kwa sababu Mungu Alijua kile Alichokuwa Amempa binadamu, na Alijua kile kilichokuwa ndani ya binadamu, basi Alijua kiwango cha mahitaji ambayo anafaa kudai kutoka kwa binadamu. Ingawaje kiwango cha mahitaji Yake kilikuwa cha chini sana wakati huo, hii haimaanishi kwamba tabia Yake haikuwa kuu, au kwamba hekima na uweza Wake yalikuwa si yoyote ila maneno matupu. Kwa binadamu, kunayo njia moja tu ya kujua tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe: kwa kufuata hatua za kazi ya usimamizi ya Mungu na wokovu wa mwanadamu, na kuyakubali maneno ambayo Mungu anaongea akiyaelekeza kwa mwanadamu. Kujua kile Mungu anacho na alicho, na kujua tabia ya Mungu, bado binadamu angemuuliza Mungu kumwonyesha ubinafsi Wake halisi? Binadamu hatafanya hivyo, na hathubutu kufanya hivyo, kwa kuweza kuifahamu tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho, tayari binadamu atakuwa amemwona Mungu Mwenyewe wa kweli, na atakuwa tayari ameona ubinafsi Wake halisi. Haya ndiyo matokeo yasiyoepukika.
Kazi na mpango wa Mungu ulipokuwa ukiendelea mbele bila kusia, na baada ya Mungu kuanzisha agano la upinde wa mvua na binadamu kama ishara kwamba Hangewahi tena kuuangamiza ulimwengu kwa kutumia gharika, Mungu alikuwa na tamanio lililokuwa likiongezeka na kumsukuma kuwapata wale ambao wangeweza kuwa katika akili moja na Yeye. Hivyo, pia, Alikuwa na tamanio lenye udharura zaidi wa kupata wale waliokuwa na uwezo wa kutekeleza mapenzi Yake duniani, na, isitoshe, kupata kundi la watu ambao wangeweza kuwa huru dhidi ya nguvu za giza, na kutoweza kuwa watumwa wa Shetani, na kuweza kuwa na ushuhuda kwake Yeye duniani. Kupata kundi la watu kama hawa kulikuwa ni tamanio la Mungu kwa muda mrefu, Alichokuwa akisubiria tangu wakati wa uumbaji. Hivyo basi, licha ya matumizi ya gharika na Mungu ili kuuangamiza ulimwengu, au agano Lake na binadamu, mapenzi ya Mungu, hali yake ya akili, mpango, na matumaini yote yalibakia yaleyale. Kile Alichotaka kufanya, ambacho Alikuwa ametamani kwa muda mrefu kabla ya uumbaji, kilikuwa kupata wale walio miongoni mwa wanadamu ambao Alitamani kuwapata—Kupata watu wa kundi hili ambao walioweza kufahamu na kujua tabia Yake, na kuyaelewa mapenzi Yake, kundi ambalo lingeweza kumwabudu Yeye. Watu kwenye kundi kama hili wanaweza kweli kuwa na ushuhuda kwake, na wao ndio, yaweza kusemekana, wasiri Wake.
Leo, hebu tuendelee kuzifuata nyayo za Mungu na kufuata nyayo za kazi Yake, ili tuweze kufichua fikira na mawazo ya Mungu, na kila kitu kinachomhusu Mungu, vyote ambavyo “vimehifadhiwa kwenye ghala” kwa muda mrefu. Kupitia mambo haya tutajua hatimaye tabia ya Mungu, kukielewa kiini cha Mungu, tutamruhusu Mungu kuingia kwenye mioyo yetu, na kila mmoja wetu ataweza kukaribia Mungu kwa utaratibu, na kupunguza umbali wetu na Mungu.
Sehemu ya kile tulichozungumzia wakati wa mwisho ilihusiana na kwa nini Mungu alianzisha agano na binadamu. Wakati huu, tutakuwa na ushirika kuhusu vifungo vya maandiko zilizo hapa chini. Hebu tuanze kwa kuyasoma maandiko.
Ibrahimu
1. Mungu Amwahidi Ibrahimu Mwana
(Mwa 17:15-17) Mungu akamwambia Abrahamu, na Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara. Nami nitambariki, na pia nitakupa mwana kutoka kwake: naam, Nitambariki, na yeye atakuwa mama wa mataifa; na wafalme wa za watu watatoka kwake. Kisha Abrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka, akasema moyoni, Je, mtoto atazaliwa kwa mtu wa umri aliye namiaka mia moja? Na Sara, aliye na umri wa miaka tisini, atazaa?” Kwa maneno mengine wanandoa hawa wazee walikuwa na umri mwingi sana wa kupata watoto. Naye Ibrahimu alifanya nini baada ya Mungu Kumwahidi? Aliuangukia uso wake akicheka, na kujiambia, “Je, mtoto atazaliwa kwa mtu wa umri aliye na miaka mia moja?” Ibrahimu aliamini kwamba haikuwezekana—hivi alimaanisha kwamba alisadiki ahadi ya Mungu kwake haikuwa chochote ila mzaha. Kutoka mtazamo wa binadamu, ahadi isingeweza kutimizika na binadamu, na vilevile isingeweza kutimizika na Mungu na ilikuwa haiwezekani kwa Mungu. Pengine, kwa Ibrahimu, ahadi hii ilikuwa ya kuchekesha. Mungu alimuumba binadamu, lakini yaonekana kwamba hajui kwamba mtu aliyezeeka sana hawezi kupata watoto; Anafikiria kwamba Anaweza kuniruhusu kupata mtoto, Anasema kwamba atanipa mtoto—kwa kweli hilo haliwezekani!. Na hivyo, Ibrahimu akaangukia uso wake na kucheka, akijifikiria yeye mwenyewe: Haiwezekani—Mungu anafanya mzaha na mimi, hili haliwezi kuwa kweli. Hakutilia maanani maneno yake Mungu. Hivyo, katika macho ya Mungu, Ibrahimu alikuwa binadamu wa aina gani? (Mwenye haki) Ni wapi ulipojifunza kwamba alikuwa mwenye haki? Wewe unafikiria kwamba wale wote ambao Mungu anawaita ni wenye haki, na watimilifu, na watu wanaotembea na Mungu. Wewe unashikilia mafundisho ya dini! Lazima uone waziwazi kwamba wakati Mungu anapomfasili mtu, Hafanyi hivyo kiholela. Hapa, Mungu hakusema kwamba Ibrahimu alikuwa mwenye haki. Katika moyo Wake, Mungu anavyo viwango vya kupima kila mtu. Ingawaje Mungu hakusema ni mtu wa aina gani ambaye Ibrahamu alikuwa, kwa mujibu wa mwenendo wake, Ibrahimu alikuwa na imani ya aina gani kwake Mungu? Ilikuwa ya kidhahania kidogo? Au alikuwa mwenye imani kuu? La, hakuwa! Kicheko na fikira zake zilionyesha yeye alikuwa nani, hivyo imani yako kwamba alikuwa mwenye haki ni ndoto ya kufikiria kwako, ni matumizi yasiyo na mwelekeo ya mafundisho ya dini, usiopaswa. Je, Mungu alikiona kicheko cha Ibrahimu na maonyesho yake madogo, [a] Alijua kuyahusu? Mungu alijua. Lakini Mungu angebadilisha kile Alichokuwa ameamua kufanya? La! Wakati Mungu alipopangilia na kuamua kwamba Angemchagua binadamu huyu, suala hilo lilikuwa tayari limekamilishwa. Si fikira za binadamu wala mwenendo wake ungemshawishi au kuhitilafiana na Mungu hata chembe; Mungu Asingebadilisha kiholela mpango Wake, wala Asingebadilisha au kuharibu mpango Wake kwa sababu ya mwenendo wa binadamu, hali ambayo ingekuwa ujinga. Nini, basi, kimeandikwa katika Mwanzo 17:21-22? “Lakini agano langu Nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sara atakuzalia wakati kama huu mwaka ujao. Na akaacha kuzungumza naye, na Mungu akapanda kutoka kwa Ibrahimu.” Mungu hakutilia maanani hata chembe kile Ibrahimu alichofikiria au kusema. Na sababu ya kutotilia maanani Kwake ni gani? Kutotilia maanani kwake kulikuwa kwa sababu, wakati huo Mungu hakuhitaji kwamba mwanadamu awe mwenye imani kuu au kwamba aweze kuwa na maarifa kuu kuhusu Mungu, au, vilevile, aweze kuelewa kile kilichofanywa na kusemwa na Mungu. Hivyo, hakuhitaji kwamba binadamu aelewe kabisa kile Alichoamua kufanya, au watu Alioamua kuchagua, au kanuni za vitendo Vyake, kwani kimo cha binadamu hakikutosha tu. Wakati huo, Mungu alichukulia kile ambacho Ibrahimu alifanya na vyovyote alivyojiendesha yeye mwenyewe kuwa kawaida. Hakushutumu, au kukemea, lakini alisema tu: “Sara atakuzalia Isaka wakati huu uliopangwa mwaka ujao.” Kwa Mungu, baada Yake kuyatangaza maneno haya, suala hili hatimaye lilikuwa kweli hatua kwa hatua; katika macho ya Mungu, kile ambacho kilikuwa kikamilishwe na mpango Wake kilikuwa tayari kimetimizwa. Baada ya kuikamilisha mipangilio ya hayo, Mungu aliondoka. Kile binadamu hufanya au kufikiria, kile binadamu huelewa, mipango ya binadamu—hakuna chochote kati ya hivi vyote kinacho uhusiano wowote na Mungu. Kila kitu hufanyika kulingana na mpango wa Mungu, kikiendana na nyakati na awamu zilizowekwa na Mungu. Hivyo ndivyo kanuni ya kazi ya Mungu inavyoenda. Mungu haingilii kati chochote kile binadamu anafikiria au kujua, ilhali Haachi mpango Wake, wala kuacha kazi Yake kwa sababu binadamu hasadiki wala kuelewa. Kweli hizi hivyo basi zinakamilishwa kulingana na mpango na fikira za Mungu. Hivi ndivyo hasa tunavyoona kwenye Biblia: Mungu Alisababisha Isaka kuzaliwa wakati ule Aliokuwa amepanga. Je, kweli zinathibitisha kwamba tabia na mwenendo wa binadamu vilizuia kazi ya Mungu? Havikuzuia kazi ya Mungu! Je, imani ndogo ya binadamu kwa Mungu, na dhana zake na fikira kumhusu Mungu viliweza kuathiri kazi ya Mungu? La, havikuathiri! Hata kidogo! Mpango wa usimamizi wa Mungu hauathiriwi na binadamu, suala, au mazingira yoyote. Kila kitu Anachoamua kufanya kitakamilika na kukamilishwa kwa wakati na kulingana na mpango Wake, na kazi Yake haiwezi kutatizwa na binadamu yeyote. Mungu hatilii maanani baadhi ya ujinga na kutojua kwa binadamu, na hata Hupuuza upinzani na dhana fulani za binadamu Kwake; badala yake, Anafanya kazi ambayo lazima Afanye bila ya kusita. Hii ni tabia ya Mungu na ni onyesho la kudura Yake.

Kazi ya Usimamizi wa Mungu na Wokovu wa Mwanadamu Yaanza kwa Sadaka ya Isaka ilivyotolewa na Ibrahimu

Baada ya kumpa mtoto Ibrahimu, maneno ambayo Mungu alikuwa ametamka kwa Ibrahimu yakawa yametimizwa. Hii haimaanishi kwamba mpango wa Mungu ulifikia mwisho hapa; kinyume cha mambo ni kwamba, mpango wa ajabu wa Mungu wa usimamizi na wokovu wa mwanadamu ndipo ulikuwa tu umeanza, na baraka Yake ya mwana kwa Ibrahimu ilikuwa tu ni utangulizi wa mpango wa usimamizi Wake kwa ujumla. Wakati huo, ni nani aliyejua kwamba vita vya Mungu na Shetani vilikuwa vimeanza kimya kimya wakati Ibrahimu alipomtoa Isaka?

Mungu Hajali Kama Binadamu Ni Mjinga—Anahitaji Tu Binadamu Awe Mkweli

Kisha, hebu tuangalie kile Mungu alimfanyia Ibrahimu. Ukiangalia Mwanzo 22:2, Mungu alimtolea Ibrahimu amri ifuatayo: “Naye akasema, Umchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, uende mpaka nchi ya Moria; na huko umtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo Nitakaokuambia.” Maana ya Mungu ilikuwa wazi: Alikuwa akimwambia Ibrahimu amtoe mtoto wake wa pekee Isaka, ambaye alimpenda, kwa minajili ya sadaka ya kuteketezwa. Tukiiangalia amri ya Mungu leo, je ingali inakinzana na dhana za binadamu? Ndiyo! Kile alichokifanya Mungu wakati huo ni kinyume sana na dhana za binadamu na hakieleweki kwa binadamu. Katika dhana zao, watu husadiki yafuatayo: Wakati binadamu hakusadiki, na akafikiria ni jambo lisilowezekana, Mungu Alimpa mwana, na baada ya kupata mtoto, Mungu alimwomba amtoe mwana wake—haiwezekani! Mungu kwa hakika alinuia kufanya nini? Kusudio halisi la Mungu lilikuwa nini? Alimpa Ibrahimu mtoto bila masharti yoyote, ilhali pia Alimwomba Ibrahimu aweze kutoa bila masharti. Maji yalikuwa yamezidi unga? Katika mtazamo wa mtu wa pembeni, hapa maji hayakuwa tu yamezidi unga lakini pia ilikuwa kwa kiasi fulani hali ya “kuunda tatizo pasipo na tatizo” Lakini Ibrahimu mwenyewe hakusadiki kwamba Mungu alikuwa akihitaji mengi sana. Ingawaje alikuwa na wasiwasi fulani, na alimshuku kidogo Mungu, alikuwa tayari bado kumtoa mtoto wake. Wakati huu, ni nini unachoona ambacho kinathibitisha kuwa Ibrahimu alikuwa radhi kumtoa mtoto wake? Ni nini kinazungumzwa kwenye sentensi hizi? Maandishi asilia yanaelezea yafuatayo: “Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda hadi mahali alipoambiwa na Mungu.” (Mwa 22:3). “Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu; Abrahamu akajenga madhabahu huko, akazipanga kuni tayari, na akamfunga Isaka mwanawe, na akamweka juu ya madhabahu juu ya zile kuni. Abrahamu akanyosha mkono wake, akakichukua kisu ili amchinje mwanawe.” (Mwa 22:9-10). Wakati Ibrahimu alipounyosha mkono wake, na kukichukua kisu ili kumwua mtoto wake, Mungu aliviona vitendo vyake? Naam aliviona. Mchakato wote—kuanzia mwanzo, wakati Mungu alipomwomba Ibrahimu kumtoa Isaka, hadi pale ambapo Ibrahimu alikiinua kisu chake ili kumwua mtoto wake—hilo lilionyesha Mungu moyo wa Ibrahimu, na haijalishi kuhusu ujinga wake wa awali, kutojua kwake, na kutomwelewa Mungu kwake, wakati huo moyo wa Ibrahimu kwa Mungu ulikuwa kweli, na wenye uaminifu, na kwa kweli alikuwa akienda kumrudisha Isaka, mtoto aliyepewa yeye na Mungu, ili arudi kwa Mungu. Ndani yake, Mungu aliuona utiifu—utiifu uleule ambao Yeye Alitamani.
Kwa binadamu, Mungu hufanya mengi yasiyoeleweka na yaliyo ya ajabu. Wakati Mungu anapotaka kupangilia mtu, mpango huu mara nyingi unakinzana na dhana za binadamu, na huwa haueleweki kwa binadamu huyo, ilhali ni ukosefu wa mwafaka huu na kutofahamu ndiyo majaribio ya Mungu na mtihani wake kwa binadamu. Ibrahimu, huku haya yakiendelea, aliweza kuonyesha utiifu kwa Mungu uliokuwa ndani yake, jambo ambalo ndilo lililokuwa sharti muhimu zaidi la yeye kuweza kushibisha mahitaji ya Mungu. Hapo tu, wakati Ibrahimu alipoweza kutii mahitaji ya Mungu, alipomtoa Isaka ndipo Mungu Alipohisi kwa kweli utulivu na kukubaliwa na Mungu—kwa Ibrahimu, ambaye Alikuwa amemchagua. Hapo tu ndipo Mungu alipokuwa na hakika kwamba mtu huyu Aliyekuwa amemchagua Yeye alikuwa kiongozi muhimu ambaye angetekeleza ahadi Yake na mpango Wake wa usimamizi wa baadaye. Ingawaje lilikuwa tu jaribio na mtihani, Mungu alihisi furaha, Alihisi upendo wa binadamu kwake Yeye, na Alihisi akiwa ametulizwa na binadamu kwa mara ya kwanza. Wakati huu ambao Ibrahimu alipokiinua kisu chake ili kumwua Isaka, Mungu alimsimamisha? Mungu hakumruhusu Ibrahimu kumpa Isaka, kwani Mungu hakuwa na nia yoyote ya kumtoa uhai Isaka. Hivyo, Mungu alimsimamisha Ibrahimu kwa wakati mwafaka. Kwake Mungu, utiifu wa Ibrahimu ulikuwa tayari umepita mtihani, kile alichofanya kilitosha, naye Mungu tayari alikuwa ameona matokeo ya kile Alichokuwa amenuia kufanya. Je, matokeo haya yalimtosheleza Mungu? Yaweza kusemekana kwamba matokeo haya yalimtosheleza Mungu na kwamba ndiyo ambayo Mungu alitaka, na ndiyo ambayo Mungu alikuwa ametamani kuyaona. Je, hili ni kweli? Ingawaje, katika miktadha tofauti, Mungu anatumia njia tofauti za kupima kila mtu. Kwa Ibrahimu Mungu aliona kile Alichotaka, Aliona kwamba moyo wa Ibrahimu ulikuwa wa kweli, na kwamba utiifu wake haukuwa na masharti na ilikuwa hali hii hasa ya “kutokuwa na masharti” ambayo Mungu alitamani. Watu mara nyingi husema, tayari nimetoa hii, tayari nimeachana na ile—kwa nini bado Mungu hajatosheka na mimi? Kwa nini Anaendelea kuniweka katika majaribio? Kwa nini Anaendelea kunijaribu? Hii yaonyesha ukweli mmoja: Mungu bado hajauona moyo wako, na bado hajapata moyo wako. Hivi ni kusema, Hajauona uaminifu kama wakati ule ambao Ibrahimu aliweza kukiinua kisu chake ili kumuua mtoto wake kwa mkono wake mwenyewe na kumtoa kwa Mungu. Bado Hajauona utiifu wako usio na masharti, na hajatulizwa na wewe. Ni jambo la kiasili, hivyo basi, kwamba Mungu anaendelea kukujaribu. Je, haya si kweli? Tutaachia hapa kwa mada hii. Halafu, tutasoma “Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu.”
3. Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu
(Mwa 22:16-18) … Nimeapa kwa nafsi yangu, akasema BWANA, kwa kuwa umetenda jambo hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee: Kwamba katika kubariki Nitakubariki, na katika kuzidisha Nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulio kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa; kwa sababu umeitii sauti yangu.
Huu ni ukamilifu wa maelezo ya baraka za Mungu kwa Ibrahimu. Ingawaje ni fupi, maudhui yake ni mengi: Yanajumuisha sababu ya, na usuli wa, zawadi ya Mungu kwa Ibrahimu, na kile ambacho Alimpa Ibrahimu. Unao pia mhemko wa furaha na msisimko Aliotumia Mungu kutamka maneno haya, , pamoja na udharura wa tamanio Lake la kupata wale wanaoweza kusikiliza maneno Yake. Katika haya, tunaona upendo wa Mungu kwa, na wema Wake kwa, wale wanaotii maneno Yake na kufuata amri Zake. Hivyo, pia, tunaiona gharama Anayolipia ili kupata watu, na utunzaji na fikira Anazotumia kuweza kuwapata. Zaidi ya hayo, kifungu hicho, kilicho na maneno “Nimeapa kwa nafsi yangu,” kinatupa hali ya nguvu ya machungu na maumivu Aliyoyapitia Mungu, na Mungu pekee, usiri wa kazi hii ya mpango wa usimamizi. Ni kifungu cha kuchokonoa fikira, na kile ambacho kilikuwa na umuhimu maalum kwa, na ilikuwa na athari nyingi ajabu kwa wale waliokuja baadaye.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili 

Juni 13, 2014