Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumanne, 12 Februari 2019

Gospel Movie Clip “Siri ya Utauwa” (4) - Mungu Mwenye Mwili pekee Ndiye Anaweza Kufanya Kazi ya Hukumu Katika Siku za Mwisho



Umeme wa Mashariki unashuhudia kwamba Mungu amepata mwili katika siku za mwisho kufanya kazi ya hukumu Mwenyewe. Lakini kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria ilifanywa kwa kumtumia Musa. Kwa hiyo kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho haiwezi kufanywa kwa namna hiyo hiyo, kwa kuwatumia watu? Kwa nini Mungu anahitaji kupata mwili na kuifanya Mwenyewe? Mwenyezi Mungu asema, "Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu" (Neno Laonekana katika Mwili).

Jumatatu, 11 Februari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” (Sehemu ya Kwanza)



Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” (Sehemu ya Kwanza)


    Mwenyezi Mungu anasema, "Katika kila aina ya kazi ya Mungu kuna maono yanayofahamika na mwanadamu; maono yanayofuatwa na matarajio mwafaka ya Mungu kwa mwanadamu. Bila haya maono kama msingi, mwanadamu hawezi kuwa na uwezo wa utendaji na pia hangeweza kumfuata Mungu bila kuyumbayumba. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu au hayaelewi mapenzi ya Mungu, basi yote ayafanyayo ni bure na yasiyoweza kukubalika na Mungu.

Jumapili, 10 Februari 2019

Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Saba


Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Saba


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.

Maudhui ya video hii:
Hakuna Anayeweza Kubadilisha Hoja Kwamba Mungu Anashikilia Ukuu juu ya Hatima ya Binadamu
Mtazamo na Matendo Bora ya Mtu Anayependa Kujinyenyekeza katika Mamlaka ya Mungu
Kumkubali Mungu kama Bwana Wenu wa Kipekee Ndiyo Hatua ya Kwanza katika Kutimiza Wokovu

Baadhi ya Makala: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)” Sehemu ya Kwanza"

Jumamosi, 9 Februari 2019

nyimbo za injili | Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu


Nyimbo za InjiliToa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu

I
Kama washiriki wa jamii ya wanadamu,
Kama wafuasi wa Kristo wa dhati,
ni wajibu wetu, ni jukumu letu
kutoa akili zetu na miili yetu
kwa kutimiza agizo la Mungu.
Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.
Kwa maana asili yetu, ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

Ijumaa, 8 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Tatu

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Tatu

Namna Ambavyo Mungu Huanzisha Matokeo Ya Binadamu na Kiwango Ambacho Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu

Kabla ya kuwa na mitazamo au hitimisho zako binafsi, unafaa kwanza kuelewa mwelekeo wa Mungu kwako, kile ambacho Mungu anafikiria, na kuamua kama kufikiria kwako ni sahihi au la. Mungu hajawahi kutumia vipimo vya muda katika kuasisi matokeo ya mtu, na Hajawahi kutumia kiwango cha mateso yaliyovumiliwa na mtu katika kuasisi matokeo yake.

Alhamisi, 7 Februari 2019

Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu

Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu


(1) Mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Mafundisho ya Ukristo yanatoka kwa Biblia, na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu yanatoka kwa ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu tangu wakati wa uumbaji wakati wa kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Hiyo ni kusema, Agano la Kale, Agano Jipya, na Biblia ya Enzi ya Ufalme–Neno Laonekana Katika Mwili–zilizoonyeshwa Bwana Yesu aliyekurudi wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, ni imani za msingi na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu.

Jumatano, 6 Februari 2019

Je, Kanisa la Mwenyezi Mungu Lina Malengo Yapi?

Je, Kanisa la Mwenyezi Mungu Lina Malengo Yapi?

     Kanisa la Mwenyezi Mungu hunyunyizia na kuwaongoza waumini wake kwa mujibu kamili wa maneno ya Mungu katika Biblia na Neno Laonekana Katika Mwili yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, ili kwamba kila muumini anaweza, chini ya uongozi, utolewaji, unyunyiziwaji, na uongozwaji wa maneno ya Mwenyezi Mungu, kuelewa ukweli wote katika maneno ya Mungu, kumiliki mtazamo sahihi juu ya maisha na maadili, kuwa na malengo sahihi ya kufuatilia, kufuata njia ya Mungu, kushikilia maagizo ya Mungu, kumtukuza Mungu kwa kuwa nuru na chumvi ya dunia, na kusifiwa na Mungu, na kuwa na sifa kamili kurithi ahadi za Mungu.

Jumanne, 5 Februari 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 2. Utangulizi Mfupi Kuhusu Usuli wa Kuonekana kwa Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho Nchini China


    China ni nchi ambamo joka kubwa jekundu hukaa, na ni mahali ambapo pamempinga na kumshutumu Mungu zaidi sana katika historia. China ni kama ngome ya mapepo na gereza linalodhibitiwa na shetani, lisilopenyeka na lisiloingilika. Zaidi ya hayo, utawala wa joka kubwa jekundu husimama ukilinda katika ngazi zote na umeanzisha ulinzi katika kila kaya. Matokeo yake, hakuna mahali pagumu zaidi ya hapa kueneza injili ya Mungu na kufanya kazi ya Mungu.

Jumatatu, 4 Februari 2019

Ushuhuda wa Maisha | 11. Kiini cha Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi

Ushuhuda wa Maisha | 11. Kiini cha Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi

Zhou Li Mji wa Xintai, Mkoa wa Shandong

     Wakati fulani kitambo, tulihitaji kuzichora wilaya katika eneo letu, na kwa msingi wa kanuni zetu kwa ajili ya uteuzi wa viongozi, kulikuwa na ndugu mmoja wa kiume aliyekuwa mtaradhia mzuri kiasi. Nilitayarisha kumpandisha cheo hadi kuwa kiongozi wa wilaya. Siku moja nilipokuwa nikizungumza na ndugu huyu, alitaja kwamba alihisi kuwa nilikuwa mwenye nguvu sana katika kazi yangu, mkali sana, na kwamba katika mkusanyiko pamoja nami hapakuwa na furaha nyingi .... Niliposikia jambo hili, nilihisi kuwa nilikuwa nimedunishwa. Nilihisi vibaya sana; mara moja nikakuza maoni fulani ya ndugu huyu, na sikukusudia tena kumpandisha cheo kuwa kiongozi wa wilaya.

Jumapili, 3 Februari 2019

Ushuhuda wa Maisha | 6. Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa

Ushuhuda wa Maisha | 6. Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa


Ding Ning Mji wa Heze, Mkoa wa Shandong

     Katika siku chache zilizopita, kanisa limepanga mabadiliko katika kazi yangu. Nilipopokea wajibu huu mpya, niliwaza, "Ninahitaji kuchukua fursa hii ya mwisho kuita mkutano na ndugu zangu wa kiume na wa kike, niongee nao wazi juu ya mambo, na niwaache na picha nzuri." Kwa hiyo, nilikutana na mashemasi kadhaa, na kufikia mwisho wa wakati wetu pamoja, nikasema, "Nimeulizwa kuondoka hapa na kuenda kwa kazi tofauti.

Jumamosi, 2 Februari 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | ""Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu"""


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu"


  Mwenyezi Mungu anasema, "Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu."

Alhamisi, 31 Januari 2019

Kanisa la Mwenyezi Mung|7. Roho Ya Majivuno Kabla ya Kuanguka

Kanisa la Mwenyezi Mung | 7. Roho Ya Majivuno Kabla ya Kuanguka

Baixue Mji wa Shenyang

Kwa sababu ya mahitaji ya kazi, nilihamishiwa hadi sehemu nyingine ya kazi. Wakati huo, nilikuwa na shukurani sana kwa Mungu. Nilihisi kwamba nilikuwa ninapungukiwa sana, lakini kwa njia ya ukuzwaji mtakatifu na Mungu, nilipewa nafasi ya kutimiza wajibu wangu katika eneo la kazi la ajabu hivyo. Niliweka nadhiri kwa Mungu moyoni mwangu: Ningefanya lote ninaloweza kumlipa Mungu.