Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumatano, 13 Machi 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Tatu”


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Tatu”
Dhamira Zangu kadhaa zimefichwa ndani ya matamshi ya sauti Yangu. Ila mwanadamu hajui na hafahamu chochote kuhusu haya, huku akiendelea kuyapokea na kuyafuata maneno Yangu kutoka nje, bila kung’amua roho Yangu na kuelewa mapenzi Yangu kutoka ndani ya maneno Yangu. Hata ingawa Nimeyaweka maneno Yangu wazi, kuna yeyote aliyeelewa? Nilitoka Sayuni Nikaja miongoni mwa wanadamu. Kwa sababu Nimejivisha ubinadamu wa mwanadamu wa kawaida na kujivika ngozi ya mwanadamu, wanadamu hulitambua umbo Langu tu kwa nje ila hawatambui uhai uliomo ndani Yangu, wala hawatambui Mungu Roho, wanajua tu mtu wa mwili.

Jumanne, 12 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Nne

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Nne Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Elewa Mwelekeo wa Mungu na Utupilie Mbali Dhana zote Potovu Kumhusu Mungu Ni Nani Hupanga Matokeo ya Binadamu Watu Huishia Kumfafanua Mungu Kutokana na Uzoefu Wao Mwelekeo wa Mungu kwa Wale Wanaotoroka Wakati Kazi Yake Inaendelea Watu Wanaotoroka Wakati wa Kazi ya Mungu ni Wale Wanaoiacha Njia ya Kweli

Mwenyezi Mungu anasema: "Mungu huyu ambaye kwa sasa mnasadiki, mmewahi kufikiria kuhusu Yeye ni Mungu wa aina gani? Anapomwona mtu mwovu akifanya mambo maovu, je Anayachukia? (Anayachukia.) Anapoona makosa ya mtu asiyejua, mwelekeo Wake ni upi? (Huzuni.) Anapowaona watu wakiiba sadaka Yake, mwelekeo Wake ni upi? (Anawachukia.) Haya yote yako wazi, sivyo? Anapoona mtu akiwa mzembe katika kusadiki kwake Mungu, na mtu huyo akikosa kufuatilia ukweli kwa namna yoyote, mwelekeo wa Mungu ni upi? Bado hamjaelewa jambo hili, sivyo? Uzembe ni mwelekeo ambao si dhambi, na humkosei Mungu. Watu husadiki kwamba haupaswi kuchukuliwa kama kosa. Basi mnafikiria mwelekeo wa Mungu ni nini? (Hayuko radhi kujibu swali hili.)

Jumatatu, 11 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia”


Maneno ya Roho Mtakatifu | “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia”
Mwenyezi Mungu anasema, “Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayeitwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa.

Jumamosi, 9 Machi 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote”


Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote”
    Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote. Yeye ndiye Mungu wa viumbe vyote. Yeye si Mungu wa Waisraeli pekee, na Yeye si Mungu wa Wayahudi pekee; Yeye ni Mungu wa viumbe vyote. …

Jumatano, 6 Machi 2019

Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa nyuma wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; hii ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii moyoni mwake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu.

Jumanne, 5 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu


Kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, bila shaka, ikirejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu.

Jumatatu, 4 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (4)


Mnapaswa kujua kuhusu hadithi ya ndani na uumbaji wa Biblia. Ufahamu huu haushikiliwi na wale ambao hawajakubali kazi mpya ya Mungu. Wao hawajui. Waelezee mambo haya ya kiini, na hawatakuwa pamoja nawe wenye kushikilia sana elimu ya vitabuni na sheria kuhusu Biblia. Wao huchunguza kwa uthabiti kile ambacho kimetabiriwa: Kauli hii imeshatimia? Kauli ile imeshatimia? Kukubali kwao injili ni kwa mujibu wa Biblia; wao huhubiri injili kulingana na Biblia. Wao huyategemea maneno ya Biblia kumwamini Mungu; bila Biblia, wao hawatamwamini Mungu. Hii ndiyo njia ambayo wao huishi, kuichunguza Biblia hivyo.

Jumapili, 3 Machi 2019

Neno la Mungu | Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa


    Katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili ili kufanya kazi Aliyopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja yeye mwenyewe ili kufanya kazi kati ya wanadamu kwa lengo la kuwakamilisha wale watu ambao wanaipendeza nafsi Yake. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo Yeye hufanya tu hiyo kazi wakati wa siku za mwisho. Ni wakati wa siku za mwisho tu ambapo Mungu alipata mwili ili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa. 

Jumamosi, 2 Machi 2019

Neno la Mungu | Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu


Neno la Mungu | Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu


    Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu.

Ijumaa, 1 Machi 2019

Neno la Mungu | Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu

Neno la Mungu | Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu


Unampenda Mungu kiasi gani hasa leo? Na unajua kiasi gani hasa kuhusu yote ambayo Mungu amefanya ndani yako? Haya ni mambo unayopaswa kujifunza. Mungu anapowasili duniani, yote ambayo Amefanya ndani ya mwanadamu na kumkubalia mwanadamu kuona ni ili mwanadamu atampenda na kumjua Yeye kweli. Kwamba mwanadamu anaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu na ameweza kufikia umbali huu ni, kuhusiana na jambo moja, kwa sababu ya upendo wa Mungu, na kuhusiana na jambo lingine, ni kwa sababu ya wokovu wa Mungu;

Alhamisi, 28 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 8


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 8

 Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa Roho, sauti Yake huelekezwa kwa wanadamu wote. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa mwanadamu, sauti Yake huelekezwa kwa wote wafuatao uongozi wa Roho Wake. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu (kile ambacho watu hutaja kama mtazamaji), Anaonyesha neno Lake moja kwa moja kwa watu ili watu wamwone kama mtoa maoni, na huonekana kwamba kutoka kinywani Mwake hutoka mambo yasiyo na kikomo ambayo mwanadamu hayajui, mambo ambayo mwanadamu hawezi kuelewa.

Jumatano, 27 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)


  Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)


Katika nyakati zilizopita, watu walijifundisha wenyewe kuwa na Mungu na kuishi katikati ya roho kila wakati, ambao, ukilinganishwa na utendaji wa leo, ni mafundisho rahisi ya kiroho tu. Utendaji kama huu huja kabla ya kuingia kwa watu katika njia sahihi ya maisha, na ni mbinu ya juujuu zaidi na rahisi zaidi kati ya mbinu zote za utendaji. Ni utendaji wa hatua za mwanzoni kabisa za imani ya watu kwa Mungu. Ikiwa watu wataishi kila mara kwa utendaji huu, watakuwa na hisia nyingi sana, na hawataweza kuingia katika uzoefu ambao ni wa kina na wa kweli.