Ijumaa, 5 Aprili 2019
Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III” Sehemu ya Pili
By Chris ZhouAprili 05, 2019Kumjua-Mungu, Neno-la-Mungu, siku-za-mwisho, Usomaji-wa-Maneno-ya-Mwenyezi-Mungu, VideoNo comments
Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Zaidi ya mwanadamu kutafuta kwa tamaa umaarufu na faida, daima anaendelea kutekeleza uchunguzi wa sayansi na utafiti wa kina, kisha bila kikomo huridhisha mahitaji yake ya mwili na tamaa; yapi tena ni matokeo ya mwanadamu? Kwanza kabisa hakuna tena usawa wa ikolojia na, pamoja na hili, miili ya wanadamu yote imetiwa doa na kuharibiwa na mazingira ya hali hii, na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na mapigo kusambaa kila mahali. Hii ni hali ambayo mwanadamu sasa hawezi kudhibiti, sivyo? Sasa kwa sababu mnaelewa hili, iwapo wanadamu hawamfuati Mungu, lakini daima wanamfuata Shetani kwa njia hii—kutumia maarifa daima kujitajirisha, kutumia sayansi kuchunguza bila kikomo siku za baadaye za maisha ya binadamu, kutumia mbinu ya aina hii kuendelea kuishi—mnaweza kutambua hitimisho ya asili ya wanadamu itakuwa vipi? Matokeo ya mwisho asilia yatakuwa yapi? Itakuwa uharibifu: kukaribia uharibifu hatua moja kwa wakati. Kukaribia uharibifu kwa hatua moja kwa wakati!”
Kujua zaidi: Swahili Gospel Praise Music "Kila Kitu Kinaishi Chini ya Sheria na Masharti Yaliyowekwa na Mungu". Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Alhamisi, 4 Aprili 2019
Wimbo wa Injili "Mwana wa Adamu Ameonekana" | Sifu Kurudi kwa Yesu Mwokozi | Watoto Wanacheza Ngoma
By Chris ZhouAprili 04, 2019Bwana-asifiwe, Msururu-wa-MV-za-Ufalme, Neno-la-Mungu, Nyimbo-za-injili, Upendo-wa-Mungu, VideoNo comments
Kutoka Mashariki ya ulimwengu (Mashariki ... Mashariki ...),
mwale wa mwanga unatokea (mwanga ... mwanga ...),
ukiangaza njia yote kwenda magharibi.
Mwana wa Adamu ameshuka duniani.
Mwokozi amerejea, Yeye ni Mwenyezi Mungu.
Akionyesha ukweli, Ameanzisha enzi mpya.
Mwana wa Adamu ameonekana. (Siyo?)
Mungu amekuja. (Eh!)
Yeye huwaletea binadamu njia ya uzima wa milele@(njia ya uzima wa milele).
Mbingu mpya, dunia mpya, enzi mpya,
binadamu wapya, njia mpya, maisha mapya.
Yerusalemu mpya umeshuka duniani.
Tumerudi kwa familia ya Mungu na tunaishi maisha ya kanisa,
kila siku tukila na kunywa neno la Mungu, tukikua katika upendo Wake.
Wewe kuja na uimbe! (Sawa!)
Nitacheza ngoma! (Ngoma!)
Maisha yetu ni ya furaha kweli (furaha kweli).
Tuko katika uwepo wa Mungu. (Tunaufurahia kweli.)
Tuna baraka za Mungu. (Tuna furaha sana.)
Ufalme wa Kristo ni nyumba kunjufu.
Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, mpendwa wetu apendezaye.
Kila mstari Anenao ni ukweli, utunyinyiziao.
Anatufundisha jinsi ya kutenda, jinsi ya kuwa waaminifu.
Tukiishi kati ya baraka za Mungu, tunampenda Mungu kwa moyo wetu wote.
Hukumu ya neno la Mungu inaishinda mioyo ya watu wote.
Wakiwa wametakaswa, watu wa Mungu humtolea ushuhuda.
Hebu tuwe wenye akili moja (tukitimiza wajibu wetu),
tukilipiza upendo wa Mungu (kuwa na ushuhuda kwa Mungu),
tukieneza injili ya Ufalme wa Mungu (injili ya Ufalme wa Mungu).
Neno la Mungu linaenea duniani kote.
Jina takatifu la Mungu linasifiwa na wote.
Ufalme wa Kristo unafanyika duniani.
Hebu tuwe wenye akili moja (tukitimiza wajibu wetu),
tukilipiza upendo wa Mungu (kuwa na ushuhuda kwa Mungu),
tukieneza injili ya Ufalme wa Mungu (injili ya Ufalme wa Mungu).
Neno la Mungu linaenea duniani kote.
Jina takatifu la Mungu linasifiwa na wote.
Ufalme wa Kristo unafanyika duniani.
Ufalme wa Kristo unafanyika duniani.
kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Jumatano, 3 Aprili 2019
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji
By Chris ZhouAprili 03, 2019Kazi-ya-Mungu, kukamilishwa-na-Mungu, Neno-la-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, ushuhuda, VitabuNo comments
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji
Kama unamwamini Mungu, ni lazima umtii Mungu, uweke ukweli katika vitendo na utimize wajibu wako wote. Zaidi ya hayo, ni lazima uelewe mambo unayopaswa kupitia. Ikiwa unapitia tu kushughulikiwa, kufundishwa nidhamu na hukumu, kama wewe unaweza tu kumfurahia Mungu, lakini huwezi kuhisi wakati Mungu anakufundisha nidhamu au kukushughulikia, hili halikubaliki. Labda katika wakati huu wa usafishaji unaweza kushikilia msimamo wako. Hii bado haitoshi; ni lazima uendelee mbele. Funzo la kumpenda Mungu halina mwisho, na hakuna kamwe kikomo kwake. Watu huona kuamini katika Mungu kama jambo rahisi mno, lakini mara tu wanapopata uzoefu kiasi wa vitendo, wao hutambua kwamba imani katika Mungu si rahisi kama watu wanavyofikiria.
Jumanne, 2 Aprili 2019
Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance
By Chris ZhouAprili 02, 2019Bwana-asifiwe, kumpenda-Mungu, Msururu-wa-MV-za-Ufalme, Nyimbo-za-Kuabudu, Video, wokovu-wa-MunguNo comments
Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance
Safi na mwaminifu, kama mtoto bila hatia, mchangamfu na mwenye nguvu za ujana, wao ni kama malaika wanaokuja ulimwenguni. Bila udanganyifu, na mioyo iliyo wazi tu, wao ni waadilifu. Wanatoa mioyo yao kwa Mungu na kupata imani Yake. Wao ni watu waaminifu ambao Mungu anapenda. Kuacha maneno ya Mungu yatuongoze kila siku, tumebarikiwa na Roho Mtakatifu anatuongoza. Tunakubali uchunguzi wa Mungu, tunaishi mbele Yake. Kumpenda Mungu kweli ni kuwa na furaha. Ufalme wa Kristo ni mbinguni kwa watu waaminifu. Na ni nyumbani kwao kuzuri. Wale wanaopenda ukweli wote wana mioyo ya uaminifu. Tunafurahia kutenda ukweli. Kwa kumtii Mungu mioyo yetu ina amani. Tunamcha Mungu na kuepuka uovu, kuishi kwa maneno ya Mungu. Tukiishi katika maneno ya Mungu tumewekwa huru. Kumpenda Mungu ni kuwa na furaha kamili. Kuacha maneno ya Mungu yatuongoze kila siku, tumebarikiwa na Roho Mtakatifu anatuongoza. Tunakubali uchunguzi wa Mungu, tunaishi mbele Yake. Kumpenda Mungu kweli ni kuwa na furaha. Ufalme wa Kristo ni mbinguni kwa watu waaminifu. Na ni nyumbani kwao kuzuri. Kumpenda Mungu huleta amani na furaha. Tunaishi kwa urahisi tunapotenda kwa maneno ya Mungu. Ni Mungu na ukweli pekee vilivyo moyoni mwetu. Maneno ya Mungu yamekuwa maisha yetu yote. Kuacha maneno ya Mungu yatuongoze kila siku, tumebarikiwa na Roho Mtakatifu anatuongoza. Tunakubali uchunguzi wa Mungu, tunaishi mbele Yake. Kumpenda Mungu kweli ni kuwa na furaha. Ufalme wa Kristo ni mbinguni kwa watu waaminifu. Na ni nyumbani kwao kuzuri.
kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Sikiliza zaidi: Wimbo za Kusifu na Kuabudu 2019 “Watu wa Mungu wa Mataifa Yote Huonyesha Hisia Zao Kama Mtu Mmoja”
Jumatatu, 1 Aprili 2019
Matamshi ya Mungu | “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele”
By Chris ZhouAprili 01, 2019Neno-la-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Ufalme-wa-Mbinguni, Uzima-wa-Milele, Video, WokovuNo comments
Matamshi ya Mungu | “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele”
Mwenyezi Mungu anasema, "Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawatUfalme wa Mbinguniaweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hayo ni kwa sababu walio nayo ni maji machafu yaliyolala palepale kwa maelfu ya miaka, badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi."
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Jifunze zaidi: Filamu za Kikristo "Kumbukumbu Chungu" | Ni Vigezo Vipi vya Kuingia Kwenye Ufalme wa Mbinguni?
Jumapili, 31 Machi 2019
Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu I” Sehemu ya Tano
By Chris ZhouMachi 31, 2019Kazi-ya-Mungu, Kiumbe-Aliyeumbwa, Muumba, Neno-la-Mungu, Usomaji-wa-Maneno-ya-Mwenyezi-Mungu, VideoNo comments
Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu I” Sehemu ya Tano
Mwenyezi Mungu alisema, "Unatazama vipi haswa mamlaka ya Mungu sasa? Kwa vile sasa maneno haya yamezungumziwa kwenye ushirika, unafaa kuwa na maarifa mapya kuhusu mamlaka ya Mungu. Na kwa hivyo Nakuuliza: Mamlaka ya Mungu yanaashiria nini? Je, yanaashiria ule utambulisho wa Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria nguvu za Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria hadhi ya kipekee ya Mungu Mwenyewe? Miongoni mwa mambo yote, ni katika kitu gani umeona mamlaka ya Mungu? Uliyaona vipi? Kwa mujibu wa ile misimu minne inayopitiwa na binadamu, je, mtu yeyote anaweza kubadilisha sheria ya mabadilishano kati ya machipuko, kiangazi, mapukutiko na kipupwe? Wakati wa machipuko, miti huweza kuchomoza na kuchanua; katika kiangazi, inafunikwa na majani; katika mapukutiko inazaa matunda na katika kipupwe majani yanaanguka.
Jumamosi, 30 Machi 2019
Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”
By Chris ZhouMachi 30, 2019Kazi-ya-Mungu, Kristo, kupata-mwili, Neno-la-Mungu, Usomaji-wa-Maneno-ya-Mwenyezi-Mungu, VideoNo comments
Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”
Mwenyezi Mungu anasema, "Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili, angalau, ni lazima liwe ukweli. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. ... Kwa kuwa Yeye, kama mwili, Anahitaji kukua na kukomaa, hatua ya kwanza ya maisha Yake ni ile ya ubinadamu wa kawaida, ilhali katika hatua ya pili, kwa kuwa ubinadamu Wake una uwezo wa kuanza kazi Yake na kutekeleza huduma Yake, maisha ambayo Mungu mwenye mwili Anaishi katika kipindi cha huduma Yake ni ya ubinadamu na ya uungu kamili."
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Maonyesho ya Mungu "Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili" (Official video), Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Ijumaa, 29 Machi 2019
Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza
By Chris ZhouMachi 29, 2019Kazi-ya-Mungu, Kumjua-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, tabia-ya-Mungu, VideoNo comments
Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza
Kwanza, hebu tuuimbe wimbo wa kumsifu Mungu: Wimbo wa Ufalme (I) Ufalme Umeshuka katika Ulimwengu.
Kiambata: Watu wanamshangilia Mungu, watu wanamsifu Mungu; vinywa vyote vinamwita Mungu mmoja wa kweli. Mfalme unashuka ulimwenguni.
I. Watu wanamshangilia Mungu, watu wanamsifu Mungu; vinywa vyote vinamwita Mungu mmoja wa kweli, watu wote wanainua macho yao kuyatazama matendo ya Mungu. Ufalme unashuka ulimwenguni, nafsi ya Mungu yu tajiri na mwenye ukarimu, tajiri na mwenye ukarimu. Ni nani ambaye hangeshangilia kwa ajili ya haya? (Ni nani ambaye hangeshangilia kwa ajili ya haya?) (Ni nani ambaye hangecheza kwa furaha kwa ajili ya haya?) Oo, Zayuni! (Oo, Zayuni!) Oo, Zayuni! (Oo, Zayuni!) Inua bango lako la shangwe ili kusherehekea Mungu! Imba wimbo wako wa shangwe wa ushindi na kueneza jina takatifu la Mungu!
Alhamisi, 28 Machi 2019
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya
By Chris ZhouMachi 28, 2019Neno-la-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, tabia-ya-Mungu, Upendo-wa-Mungu, VitabuNo comments
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya
Nyote mmeshuhudia wenyewe kazi ambayo Nimefanya miongoni mwenu, ninyi wenyewe mmesikia maneno ambayo Nimenena, nanyi mnajua mtazamo Wangu kuelekea kwenu, kwa hiyo mnapaswa kujua kwa nini Ninafanya kazi hii miongoni mwenu. Nitawaambia ukweli—ninyi ni vifaa tu vya kazi Yangu ya ushindi katika siku za mwisho; ninyi ni vyombo vya kupanua kazi Yangu miongoni mwa nchi za Mataifa. Mimi huzungumza kupitia kwa udhalimu wenu, uchafu wenu, upinzani na uasi wenu ili kupanua bora zaidi kazi Yangu ili jina Langu lienee miongoni mwa nchi za Mataifa, yaani, kuenea miongoni mwa nchi yoyote nje ya Israeli.
Jumatano, 27 Machi 2019
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unajua Nini Kuhusu Imani?
By ye.fengMachi 27, 2019baraka, Kiumbe-Aliyeumbwa, Neno-Laonekana-katika-Mwili, ushuhuda, utukufu-wa-Mungu, VitabuNo comments
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unajua Nini Kuhusu Imani?
Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binadamu huelewa kidogo sana, na binadamumwenyewe amepungukiwa sana; yeye anakuwa tu na imani ndani Yangu bila kujali na bila kujua. Ingawa hajui imani ni nini wala ni kwa nini anayo imani ndani Yangu, anaendelea kufanya hivyo kwa shauku mno. Kile Ninachomwomba binadamu, si tu yeye kuniita Mimi kwa shauku kwa njia hii au kuniamini Mimi kwa mtindo huu wa kukosa mwelekeo. Kwani kazi Ninayoifanya ni yake binadamu kunijia Mimi na kunijia Mimi, wala si kwa binadamu kuvutiwa na kuniangalia Mimi kwa njia mpya kwa sababu ya kazi Yangu.
Jumanne, 26 Machi 2019
Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Tano
By ye.fengMachi 26, 2019Kazi-ya-Mungu, maneno-ya-Mungu, siku-za-mwisho, tabia-ya-Mungu, Usomaji-wa-Maneno-ya-Mwenyezi-Mungu, VideoNo comments
Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Tatu
Mwenyezi Mungu anasema, “Katika moyo wa Nuhu na fahamu yake, uwepo wa Mungu ulikuwepo na bila shaka, na hivyo basi utiifu wake kwa Mungu ulikuwa haujatiwa doa wala toa na ungeweza kustahimili majaribio. Moyo wake ulikuwa safi na wazi kwa Mungu. Hakuhitaji maarifa ya mafundisho ya dini mengi mno ili kujishawishi kufuata kila neno la Mungu, wala hakuhitaji ukweli mwingi kuthibitisha uwepo wa Mungu, ili akubali kile Mungu alimwaminia na kuweza kufanya chochote kile ambacho Mungu angemruhusu kufanya.
Jumatatu, 25 Machi 2019
Wimbo wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Watu wa Mungu wa Mataifa Yote Huonyesha Hisia Zao Kama Mtu Mmoja” | Praise and Thank God's Love
Wimbo wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Watu wa Mungu wa Mataifa Yote Huonyesha Hisia Zao Kama Mtu Mmoja” | Praise and Thank God's Love
Uangalie ufalme wa Mungu, ambako Mungu anatawala juu ya yote.
Kutoka wakati uumbaji ulipoanza mpaka siku ya sasa,
wana wa Mungu waliongozwa wakipitia taabu.
Katika milima na mabonde walienda. Lakini sasa katika nuru Yake wanakaa.
Nani asiyelia juu ya udhalimu wa jana?Ni nani asiyelia machozi kwa ajili ya maisha magumu leo?