Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Ijumaa, 19 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Matamshi ya Mwenyezi Mungu Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Mimi Naeneza kazi Yangu katika nchi za Mataifa. Utukufu Wangu unamulika kotekote ulimwenguni; mapenzi Yangu yamo katika wanadamu yakitawanyika hapa na pale, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi ambayo Nimewapa. Kuanzia wakati huu kuendelea, Nimeingia katika enzi mpya, kuwaleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Niliporudi katika “nchi Yangu,” Nilianza sehemu nyingine tena ya kazi katika mpango Wangu wa asili, ili mwanadamu aje kunijua zaidi. Nauchukua ulimwengu katika ukamilifu wake na kuona kwamba[a] ni wakati muafaka wa kazi Yangu, kwa hiyo Naharakisha mbele na nyuma kufanya kazi Yangu mpya ndani ya mwanadamu. Hii ni enzi mpya, hata hivyo, na Nimeleta kazi mpya ili Niwachukue watu wapya wengi zaidi katika enzi mpya na kuachana na wengi wa wale Nitakaowaondoa.

Jumatano, 17 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Kazi ya Mungu,kumjua mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

Kufahamu madhumuni ya kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mwanadamu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu.

Jumanne, 16 Aprili 2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu


“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu

3. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu

Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache. “Wateule wa Mungu” inarejelea nini?

Jumatatu, 15 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tabia Yako Ni Duni Sana!




Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi MunguTabia Yako Ni Duni Sana!

Ninyi nyote mmeketi katika viti vya kifahari, mkiwafundisha wale wa vizazi vijana ambao ni wa aina yenu, ukiwafanya waketi nawe. Je, mngekosaje kujua kwamba wale “watoto” wenu walikuwa tayari hawana pumzi, na kwamba hawakuwa na kazi Yangu zamani? Utukufu Wangu huangaza kutoka nchi ya Mashariki hadi nchi ya Magharibi, lakini wakati utukufu Wangu huenea mpaka mwisho wa dunia na wakati unapoanza kuinuka na kuangaza, Nitaondoa utukufu wa Mashariki na kuuletea Magharibi ili kwamba watu hawa wa giza katika Mashariki ambao wameniacha Mimi watakuwa bila mwanga unaong’aa kuanzia hapo kwendelea. Wakati huo, mtaishi katika bonde la kivuli. Ingawa watu leo ni wazuri mara mia zaidi kuliko awali, bado hawawezi kuyatosheleza mahitaji Yangu, na bado wao si ushahidi mtukufu Kwangu. 

Jumapili, 14 Aprili 2019

Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu


Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu

Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake.
Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu.
Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya.
Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana.
Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake.
Tunaondolewa vizuizi na ubaguzi wetu, tunaishi ndani ya upendo wa Mungu.
Tunatafakari, kufikiri maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu anatuangazia.
Tunaelewa moyo wa Mungu, sisi si hasi tena.

Ijumaa, 12 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Katika miaka hii miwili hadi mitatu ya kazi, kile kilichopaswa kutimizwa katika kazi ya hukumu iliyofanyika juu yenu kimetimizwa kimsingi. Watu wengi wamesahau matarajio na kudura yao ya baadaye. Hata hivyo, inapotajwa kuwa ninyi ni uzao wa Moabu, wengi wenu huchukizwa sana—nyuso zenu hubadilika, vinywa vyenu hupinda, na macho yenu hukodolea. Hamuwezi kabisa kuamini kwamba ninyi ni uzao wa Moabu. 

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili


Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote

Namna Mungu alivyoshughulikia binadamu wote wa ujinga na kutojua ulitokana kimsingi na huruma na uvumilivu. Hasira yake, kwa upande mwingine, imefichwa kwenye wingi mkubwa mno wa muda na wa mambo; haijulikani kwa binadamu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati binadamu anakabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya kuvumilia na kusamehe binadamu—yaani, wakati onyesho la mwisho la Mungu la huruma na onyo Lake la mwisho linapowafikia—kama bado wangali wanatumia mbinu zile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali huruma Yake, Mungu hataweza tena kuwapatia uvumilivu na subira yake.

Alhamisi, 11 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Kwanza



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Kwanza



Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu
Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu. Kuhusiana na kumjua Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, sehemu ya kwanza tuliyoijadili ni ipi? (Mamlaka ya Mungu.) Ya pili ilikuwa ni ipi? (Tabia ya haki ya Mungu.) Na ya tatu? (Utakatifu wa Mungu.) Tumejadili mara ngapi kuhusu mamlaka ya Mungu?

Jumatano, 10 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)” Sehemu ya Nne
Mwenyezi Mungu anasema, “Kuelewa kiini cha Mungu na kujua kiini cha Mungu kinapeana msaada usioweza kupimika kwa kuingia kwa watu katika maisha. Natumai kwamba hamtapuuza haya ama kuyaona kama mchezo; kwa sababu kumjua Mungu ni msingi muhimu na msingi wa imani ya mwanadamu kwa Mungu na ufuatiliaji wa mwanadamu wa ukweli na wokovu na kitu ambacho hakifai kuachiliwa. Iwapo mwanadamu anamwamini Mungu lakini hamjui Mungu, na iwapo mwanadamu anaishi miongoni mwa baadhi ya barua na mafundisho ya kidini, hutawahi kufikia wokovu hata kama utatenda na kuishi kulingana na maana ya juujuu ya ukweli. Hiyo ni kusema, iwapo imani yako kwa Mungu haitokani na kumjua, basi imani yako haimaanishi chochote.”

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Kujua zaidi:  Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? . Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu

Jumanne, 9 Aprili 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"

Mwenyezi Mungu anasema, “Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu. Yeye huonyesha moyo wa ndani zaidi wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na kuleta mbingu na nchi mpya na kazi mpya, na ametuletea matumaini, akimaliza maisha ambayo tuliishi katika hali isiyo dhahiri, na kuwezesha nafsi yetu nzima kuona njia ya wokovu kwa udhahiri kamili. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zimepata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, huyu si ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, tukiwa tumeamka au kuota, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu! Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ametuwezesha kuishi tena na kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele.”
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 8 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (10)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (10)


Kwa wanadamu kuendelea mbele kiasi hiki ni hali isiyo na kigezo. Kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu vinaendelea bega kwa bega, na hivyo kazi ya Mungu, pia, ni tukio kubwa lisilo na kifani. Kuingia kwa mwanadamu hadi sasa ni ajabu ambayo kamwe haijawahi kufikiriwa na mwanadamu. Kazi ya Mungu imefikia upeo wake—na, kufuatia, “kuingia” kwa mwanadamu[1] pia kumefikia kilele chake. Mungu amejishusha kwa kadiri Anavyoweza, na kamwe Hajawahi kuwalalamikia wanadamu au vitu vyote katika ulimwengu.

Jumapili, 7 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)”



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)”
Mwenyezi Mungu alisema, "Kwa kweli, Mungu hana mahitaji sana kwa wanadamu—au angalau, hana mahitaji kama watu wanavyodhani. Bila matamshi ya Mungu, au udhihirishaji wowote wa tabia Yake, matendo, au maneno, basi kumjua Mungu kungekuwa kugumu sana kwenu, kwa sababu watu wangelazimika kukisia nia ya Mungu na mapenzi Yake, kitu ambacho ni kigumu sana kwao. Lakini kutokana na hatua ya mwisho ya Kazi Yake, Mungu amenena maneno mengi, kufanya kiwango kikubwa cha kazi, na kufanya mahitaji mengi kwa wanadamu. Katika maneno Yake, na kiwango kikubwa cha kazi Yake, amejulisha watu anachokipenda, anachokichukia, na wanafaa kuwa aina gani ya watu. Baada ya kuelewa vitu hivi, ndani ya nyoyo watu wanafaa kuwa na maelezo sahihi ya mahitaji ya Mungu, kwa kuwa hawamwabudu tena yule Mungu asiye yakini, au kumfuata Mungu katika ukosefu uyakini na udhahania na utupu; badala yake, watu wanaweza kusikia maneno ya Mungu, wanaweza kuelewa viwango vya mahitaji ya Mungu, na kuvifikia, na Mungu hutumia lugha ya wanadamu kuwaambia watu yale yote wanafaa kujua na kulewa. Leo, kama watu hawafahamu mahitaji ya Mungu kwao, kile Mungu alicho, kwa nini wanamwamini Mungu, na jinsi wanafaa kumwamini Mungu na jinsi wanavyojichukulia mbele Zake, basi kuna shida hapa. Sasa hivi tu kila mmoja wenu amezungumza kuhusu kipengele kimoja; mnafahamu kuhusu mambo fulani, yawe ni mambo mahususi au ya jumla—lakini Ningependa kuwaambia mahitaji ya Mungu ya kweli, kamili, na mahususi kwa wanadamu. Ni maneno machache tu, na rahisi sana. Yawezekana tayari mnayajua haya maneno. Mahitaji sahihi ya Mungu kwa wanadamu na wale ambao wanamfuata ni kama ifuatavyo. Mungu anahitaji mambo matano kutoka kwa wale wanaomfuata; imani ya kweli, ufuasi wenye uaminifu, utiifu kamili, ufahamu wa kweli na heshima za kutoka moyoni.
Katika mambo haya matano, Mungu anahitaji kuwa watu wasimshuku tena, wala kumfuata wakitumia fikira zao au mitazamo ikosayo uyakini na iliyo dhahania; Ni lazima wamfuate Mungu bila fikira au dhana zozote. Mungu anahitaji kuwa wote wanaomfuata wafanye hivyo kwa uaminifu, sio kwa shingo upande au bila kujizatiti. Mungu anapokupa mahitaji yoyote, au kukujaribu, kukuhukumu, kukushughulikia na kukupogoa, au kukuadhibu na kukuangamiza, unapaswa kuwa mtiifu kabisa Kwake. Hufai kuuliza kilichosababisha, au kuweka masharti, au hata uongee kuhusu sababu. Utiifu wako lazima uwe usio na shaka. Kumjua Mungu ni kipengele ambacho watu wengi wanakosea. Mara kwa mara wanamlazimishia Mungu misemo, matamshi, na maneno ambayo hayahusiani na Yeye, wakiamini kuwa haya maneno ndiyo ya kweli kuhusu kumfahamu Mungu. Kumbe hawajui kuwa hii misemo, ambayo inatoka kwa fikira za watu, ung'amuzi wao, na busara zao, havina uhusiano wowote na kiini cha Mungu. Na kwa hiyo, Ninataka kukwambia kuwa, katika ufahamu wa watu unaotamaniwa na Mungu, Mungu haulizi tu kwamba umtambue Mungu na maneno Yake, lakini kuwa ufahamu wako juu ya Mungu ni sahihi. Hata kama unaweza kusema sentensi moja tu, au una ufahamu mdogo tu, huu ufahamu mdogo ni sahihi na wa kweli, na unalingana na kiini cha Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa Mungu hapendi sifa na wao kumtukuza Yeye kwa hali isiyo halisi na yenye nia mbaya. Zaidi ya hayo, Anachukia watu wanapomchukulia kama hewa. Anachukia ambapo, wakati wa majadiliano juu ya mada kuhusu Mungu, watu wanazungumza kimzaha, wakiongea kwa hiari bila ya kujali, wakiongea wapendavyo; zaidi ya hayo, anawachukia wale wanaojifanya wanamjua Mungu, na wanaringa kuhusu ufahamu wa Mungu, wakijadili mada kuhusu Mungu bila mipaka au kipimo. La mwisho Kati ya yale mahitaji matano lilikuwa ni kumheshimu Mungu kutoka moyoni. Hili ndilo hitaji kuu la Mungu kwa wale wote wanaomfuata. Wakati mtu ana ufahamu wa kweli na sahihi kumhusu Mungu, anaweza kumheshimu Mungu na kuepuka maovu. Heshima hii hutoka ndani ya moyo wake, ni ya hiari, na sio kwa sababu Mungu amemshurutisha. Mungu hataki utoe zawadi ya mwelekeo wowote wa kupendeza, au tabia, au mienendo ya nje Kwake; badala yake, anataka kwamba umheshimu na umwogope kutoka ndani ya moyo wako. Heshima hii inaafikiwa kutokana na mabadiliko katika tabia ya maisha yako, kwa sababu una ufahamu juu ya Mungu, kwa sababu unaelewa matendo ya Mungu, kwa sababu ya uelewa wako wa kiini cha Mungu, na kwa sababu umetambua ukweli kuwa wewe ni mmoja wa viumbe wa Mungu. Na kwa hiyo, nia yangu ya kutumia neno “kutoka moyoni” kwa kurejelea heshima hapa ni kwamba wanadamu waelewe kuwa heshima ya watu kwa Mungu inapaswa kutoka ndani ya mioyo yao.
Sasa yafikirie hayo matakwa matano: kuna yeyote kati yenu anaweza kupata matatu ya kwanza? Ambapo Ninamaanisha uaminifu wa kweli, ufuasi wenye uaminifu, na utiifu kamili. Kuna wowote kati yenu wanaoweza mambo haya? Najua Nikisema yote matano, basi bila kuuliza hapatakuwa na hata mmoja kati yenu anayeweza—lakini nimeyapunguza hadi matatu. Tafakari kama umeyapata au la. Je, “uaminifu wa kweli” ni rahisi kuupata? (La, sio rahisi.) Sio rahisi, kwa kuwa mara nyingi watu humtilia Mungu mashaka. Na, je, “ufuasi wenye uaminifu”? Huu “uaminifu” una maana gani? (Sio kwa shingo upande ila kwa moyo wote.) Sio kwa shingo upande ila kwa moyo wote. Mmegonga ndipo! Kwa hiyo, je, mna uwezo wa kupata hili hitaji? Inabidi mjitahidi zaidi—siyo? Kwa sasa bado hamjapata hili hitaji. Kuhusu “utiifu kamili”—je, mmepata hilo? (Hapana.) Bado hamjapata hilo, pia. Mara nyingi nyinyi si watiifu na ni waasi, mara nyingi hamsikilizi, au kupenda kutii, au kutaka kusikia. Haya ndiyo mahitaji matatu ya msingi wanayopata watu baada ya kuingia katika maisha yao, na bado hamjayapata. Kwa hiyo, kwa wakati huu, mna uwezo mkubwa? Leo, baada ya kunisikia nikisema maneno haya, mna wasiwasi? (Ndiyo.) Ni sawa kuwa mna wasiwasi—. Msiwe na wasiwasi Ninahisi wasiwasi kwa niaba yenu. Sitakwenda katika mahitaji hayo mengine mawili; bila shaka, hakuna anayeweza kuyafikia. Mna shauku. Kwa hivyo mmebaini malengo yenu? Malengo yapi, kuelekeza upande gani, mnapaswa kuyafuata, na kujitolea jitihada zenu? Mna lengo? (Ndiyo.) Lengo lenu ni lipi? (Kuutafuta ukweli, kuutafuta ufahamu wa Mungu katika maneno Yake, na kwa hakika kupata heshima na utiifu kwa Mungu.) Hebu niongee waziwazi: mnapofikia mahitaji haya matano, mtakuwa mmemridhisha Mungu. Kila mojawapo ni ishara, ishara ya watu wakiingia katika maisha wakiwa wamefikia ukomavu, na lengo la mwisho la hii. Hata kama Ningechukua moja kati ya mahitaji na kuongea kwa kina kulihusu na kinachohitajika, haiwezi kuwa rahisi kupata; ni lazima mpitie kiwango fulani cha matatizo na kufanya kiasi fulani cha juhudi. Na ni aina gani ya mawazo mnapaswa kuwa nayo? Yanapaswa kuwa sawa na yale ya mgonjwa wa saratani anayesubiri kwenda kwenye meza ya upasuaji. Na ni kwa nini Ninasema haya? Kama ungependa kumwamini Mungu, na kumpata Mungu na kupata ridhaa Yake, basi kama hutapitia katika kiasi fulani cha shida, au kufanya kiwango fulani cha juhudi, hutaweza kupata vitu hivi. Umesikia mahubiri mengi, lakini kuyasikia hakumaanishi kuwa haya mahubiri ni yako; ni lazima uyachukue na kuyageuza yawe kitu ambacho ni chako, ni lazima uyasimilishe maishani mwako, na kuyaleta katika uwepo wako, ukiyaruhusu maneno na mahubiri haya yakuongoze katika maisha yako, na kuleta dhamana na maana ya uhai katika maisha yako—na hivyo basi itakuwa ni thamani kuwa uliyasikia maneno haya. Kama maneno haya Ninayoyanena hayaleti mabadiliko yoyote katika maisha yenu, au thamani yoyote katika uwepo wako, basi hakuna haja ya kuyasikiliza. Mnaelewa haya, ndiyo? Baada ya kuelewa haya, basi kilichobaki ni juu yenu wenyewe. Ni lazima mfanye kazi! Ni lazima muwe na bidii katika kila jambo! Msiwe huku na kule—wakati unapita upesi! Wengi wenu wameamini kwa zaidi ya miaka kumi. Tazama nyuma kwa hii miaka zaidi ya kumi ya imani katika Mungu: Umenufaika kiasi gani? Na mmesalia na miongo mingapi ya haya maisha? Sio mirefu. Sahau kuhusu iwapo kazi ya Mungu inakusubiri, iwapo Amekuachia nafasi, iwapo Atafanya kazi ile ile tena; usizungumze kuhusu hili. Unaweza kurudisha nyuma miaka yako kumi iliyopita? Kwa kila siku inayopita, na kila hatua unayochukua, siku ambazo unazo hupunguzwa kwa siku moja. Muda haumsubiri mwanadamu yeyote! Utanufaika tu kutokana na imani kwa Mungu kama utaichukulia kama kitu kikubwa zaidi maishani mwako, muhimu zaidi kuliko chakula, mavazi, au kitu kingine chochote! Kama huwa unaamini tu unapokuwa na wakati, na huwezi kutoa umakini wako wote kwa imani yako, kama siku zote umetatizwa na vurugu, basi hutafaidi chochote. Unaelewa hili, ndio? Tutaishia hapa kwa leo. Tuonane wakati ujao! (Shukrani kwa Mungu!)"


kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili


Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?