Jumatano, 15 Mei 2019
Sauti ya Mungu | Sura ya 8
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguMei 15, 2019kazi-ya-Roho- Mtakatifu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, sauti-ya-Mungu, Ukweli, VitabuNo comments
Sauti ya Mungu | Sura ya 8
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa.
Jumanne, 14 Mei 2019
Sauti ya Mungu | Sura ya 7
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguMei 14, 2019Kazi-ya- Roho-Mtakatifu, maneno-ya-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Ukweli, VitabuNo comments
Sauti ya Mungu | Sura ya 7
Kuinuka kwa mazingira pande zetu zote huharakisha kurudi nyuma kwetu katika roho. Usitende kwa moyo mgumu, usipuuze kwa vyovyote vile kama Roho Mtakatifu Ana wasiwasi, usijaribu kuwa mjanja na usiwe na ridhaa kupita kiasi na kuridhika kibinafsi au kuzingatia sana matatizo yako mwenyewe; kitu pekee cha kufanya ni kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Huwezi kuyaacha maneno ya Mungu nyuma au kuyapa kisogo; lazima uyaelewae kwa makini, rudia kuomba-kusoma kwako, na uelewe maisha ndani ya maneno hayo. Usishiriki katika yale yasiyokuwa na maana kwa kuyabugia pasipo kujipa mwenyewe wakati wa kuyawaza.
Jumatatu, 13 Mei 2019
Maneno ya Mungu | Sura ya 6
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguMei 13, 2019Kristo, Neema, Neno-la-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Maneno ya Mungu | Sura ya 6
Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote Naye Anatuongoza katika dunia yote. Mara kwa mara tutakuwa karibu Naye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi. Usiwe na moyo wa kunung’unika, au Mungu hatatupa neema Yake juu yako.
Jumapili, 12 Mei 2019
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguMei 12, 2019maisha, Neno-la-Mungu, siku-za-mwisho, Usomaji-wa-Maneno-ya Mwenyezi-Mungu, VideoNo comments
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Haijalishi wewe ni mbari gani au unaishi katika ardhi gani, iwe ni Magharibi au Mashariki—huwezi kujitenganisha na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu, na huwezi kujitenga na malezi na uangalizi wa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu. Haijalishi riziki yako ni nini, kile unachokitegemea kwa ajili ya kuishi, na kile unachokitegemea kudumisha uhai wako katika mwili, huwezi kujitenganisha na kanuni ya Mungu na usimamizi wake.”
Jumamosi, 11 Mei 2019
Maneno ya Mungu | Sura ya 5
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguMei 11, 2019imani, Neema, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Roho-Mtakatifu, VitabuNo comments
Maneno ya Mungu | Sura ya 5
Milima na mito huenda ikibadilika, vijito hutiririka mbele, na maisha ya mwanadamu ni yenye uvumilivu mdogo kuliko ardhi na anga. Mwenyezi Mungu pekee ndiye maisha ya milele yaliyofufuka milele, katika vizazi hai milele! Vitu vyote na matukio viko katika mikono Yake, Shetani yuko chini ya miguu Yake.
Ijumaa, 10 Mei 2019
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 4
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguMei 10, 2019hukumu, maneno-ya-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Roho- Mtakatifu, VitabuNo comments
Daima tutakuwa tukiangalia na kusubiri, kuwa na utulivu katika roho na kutafuta kwa moyo safi. Chochote kitakachotufikia, tusishiriki kwa upofu. Twahitajika tu kuwa kimya mbele ya Mungu na daima kushiriki naye, na kisha nia Yake itafichuliwa kwetu. Roho zetu sharti daima ziwe tayari kutofautisha na sharti ziwe na bidii na zisiokubali kushindwa. Ni lazima tuteka kutoka kwa maji ya uhai mbele ya Mungu, maji ambayo huondoa kiu kutoka kwa roho zetu zilizokauka.
Alhamisi, 9 Mei 2019
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 3
By Mwenyezi Mungu ni Mchungaji WanguMei 09, 2019hukumu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Ukombozi, utukufu, VitabuNo comments
Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu. Yeye Ametimiza ukombozi na kuongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu. Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake kwa hekima Yake ya uungu na uweza Yeye Amejenga Uyahudi na kuifanya imara. Pamoja na uadhama Wake Yeye huhukumu dunia ya maovu; Yeye huhukumu mataifa yote na watu wote, ardhi na bahari na vitu vyote hai juu yao, pia wale ambao wamelewa kwa divai ya uzinzi.
Jumatano, 8 Mei 2019
Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 2
By ye.fengMei 08, 2019kanisa, maneno-ya-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Roho-Mtakatifu, VitabuNo comments
Mwenyezi Mungu anasema, Kufuata kuanza kazi kwa mtazamo mpya, kutakuwa na hatua mpya katika kazi Yangu. Kama ilivyo katika ufalme, Nitafanya mambo moja kwa moja kupitia kwa uungu, Nikiongoza kila hatua ya njia, sahihi hadi kwa maelezo madogo, na bila kutiwa najisi na nia za binadamu hata kidogo. Yafuatayo yanaeleza kwa muhtasari namna ya utekelezaji halisi: Kwa vile ni kupitia katika ugumu na usafishaji ndiyo wamepata jina la “watu”, na kama walivyo watu wa ufalme Wangu, lazima Niwafanye watii kwa mahitaji kali, ambayo ni ya juu kushinda mbinu za kazi Yangu kwa vizazi vilivyopita.
Jumanne, 7 Mei 2019
Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 1
By ye.fengMei 07, 2019maneno-ya-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Ufalme, Ujenzi-wa-kanisa, VitabuNo comments
Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 1
Je, wale wanaoshuhudia maneno Yangu huyakubali kwa kweli? Je, mnanijua kwa kweli? Mmejifunza utiifu kweli? Ninyi hutumia rasilimali kwa ajili Yangu kwa uaminifu? Mmekuwa na ushuhuda thabiti, usiokubali kushindwa Kwangu mlipokabiliwa na joka kuu jekundu? Je, moyo wenu wa ibada hulifedhehesha kweli joka kuu jekundu? Ni kupitia tu kwa jaribio la maneno Yangu ndipo Naweza kutimiza lengo Langu la kulitakasa kanisa na kuwachagua wale wanaonipenda Mimi kweli.
Jumatatu, 6 Mei 2019
Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Kuhusu Maisha ya Petro
By ye.fengMei 06, 2019Enzi-ya-Neema, kazi-ya-Roho-Mtakatifu, maneno-ya-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Vitabu, YesuNo comments
Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Kuhusu Maisha ya Petro
Petro ni mfano ambao Mungu aliutambulisha kwa wanadamu, na yeye ni mtu mashuhuri anayejulikana vizuri. Kwa nini mtu mnyonge kama huyo aliwekwa mahala kama mfano na Mungu na amesifiwa na vizazi vya baadaye? Bila shaka, ni wazi kwamba hili halitenganishwi na maonyesho yake na azimio lake la upendo kwa Mungu.
Jumapili, 5 Mei 2019
Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Wimbo wa Ufalme
Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Wimbo wa Ufalme
Watu wanishangilia Mimi, watu wananisifu Mimi; midomo yote inataja Mungu mmoja wa kweli, watu wote wainua macho yao kutazama matendo Yangu. Ufalme washuka duniani, nafsi Yangu ni tajiri na yenye wingi. Ni nani hangesherehekea haya? Nani hangecheza kwa furaha kwa ajili ya haya? Ee, Sayuni! Inua bango lako la ushindi ili kunisherehekea Mimi! Imba wimbo wako wa ushindi na ueneze jina Langu takatifu!
Jumamosi, 4 Mei 2019
Umeme wa Mashariki | Utangulizi
By ye.fengMei 04, 2019Kazi-ya-Mungu, maneno-ya-Mungu, Matamshi-ya-Mwenyezi-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
"Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima" ni kundi la pili la matamshi yanayoonyeshwa na Kristo. Ndani yake, Kristo Anatumia utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Yanajumlisha kipindi cha kuanzia Februari 20, 1992 hadi Juni 1, 1992, na yana jumla ya matamshi arobaini na saba. Namna, maudhui na mtazamo wa maneno ya Mungu katika matamshi haya hayafanani kabisa na "Maneno ya Roho kwa Makanisa." "Maneno ya Roho kwa makanisa" inafichua na kuongoza tabia ya watu ya nje na maisha yao rahisi ya roho. Hatimaye, inaisha kwa "majaribu ya watendaji huduma."