Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumatatu, 9 Aprili 2018

Umeme wa Mashariki | Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Umeme wa Mashariki | Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani kuweza kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamengoja na kumtamani kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, ili Yesu Mwokozi Arudi kwa watu ambao wamekuwa mbali Naye kwa maelfu ya miaka.

Jumamosi, 7 Aprili 2018

Umeme wa Mashariki | Kubagua dhidi ya Watu wa Nje ni Uovu Sana!

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

Umeme wa Mashariki | Kubagua dhidi ya Watu wa Nje ni Uovu Sana!

Xiaojin Kaunti ya Pan’an , Mkoa wa Zhejiang
Katika mwezi wa Februari mwaka wa 2007, kanisa lilipokea mpango wa kazi uitwao "Nyunyizia na Uwape Waumini Wapya ili Kuwasaidia Kukita Mizizi Haraka Iwezekanavyo." Ulisisitiza kuwa "Ni muhimu kuwatumia wale wote wanaofaa na walio na tajriba katika kuwanyunyizia waumini wapya ili kukamilisha kazi hii.

Ijumaa, 6 Aprili 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I


Mwenyezi Mungu alisema, Kwa wakati huu, tunafaa kuunganisha mazungumzo yetu na sasa. Kama Mungu angeweza kufanya mambo haya madogo mbalimbali kwa binadamu Aliowaumba hapo mwanzo kabisa, hata vitu vingine ambavyo watu hawangethubutu kufikiria ama kutarajia, basi naye Mungu angewafanyia watu leo mambo kama hayo? Baadhi ya watu husema, “Ndiyo!” Kwa nini hivyo? Kwa sababu kiini cha Mungu si bandia, uzuri Wake si bandia. Kwa sababu kiini cha Mungu kwa kweli kipo, na si kitu kilichoongezewa tu na wengine na bila shaka si kitu ambacho kinabadilika na mabadiliko ya muda, mahalina enzi.

Kuhusu Biblia (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kuhusu Biblia (4)

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wanaamini kwamba kuelewa na kuwa na uwezo wa kufasiri Biblia ni sawa na kutafuta njia ya kweli—lakini, kimsingi, je, vitu ni rahisi sana? Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu.

Alhamisi, 5 Aprili 2018

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wokovu

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde unapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia kwako kutakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kufuatilia kwako. Kwa njia hiyo, uzoefu na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua taswira nzima kwa ukamilifu, hutapoteza kitu maishani na hutapotea. Kama hutazijua hatua hizi za kazi, utapata hasara kwa kila mojawapo. Huwezi kugeuka baada ya siku chache tu na hutaweza kuipata njia mwafaka hata katika majuma machache.

Jumatano, 4 Aprili 2018

Kuhusu Biblia (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kuhusu Biblia (3)

Mwenyezi Mungu alisema, Sio kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana nyingi za kibinadamu, upendelevu wa kibinadamu, na ufasiri wa ajabu wa kibinadamu.

Swahili Gospel Song "Sala ya Watu wa Mungu" | Kuishi katika Upendo wa Mungu

Swahili Gospel Song "Sala ya Watu wa Mungu" | Kuishi katika Upendo wa Mungu

Watu wa Mungu wanainuliwa mbele ya kiti Chake cha Enzi,
maombi mengi mioyoni mwao.
Mungu huwabariki wote wanaorejea Kwake;
wote wanaishi katika mwanga.
Omba Roho Mtakatifu alipe nuru neno la Mungu
ili kwamba tujue kikamilifu mapenzi ya Mungu.
Tunaomba watu wote walitunze sana neno la Mungu
na waje kutafuta kumjua Mungu.
Tunaomba Mungu atupe zaidi ya neema Yake,
ili tabia zetu ziweze kubadilika.
Tunaomba Mungu atufanye wakamilifu
ili tuwe moyo na mawazo moja pamoja na Yeye.
Tunaomba Mungu atufundishe nidhamu
ili tuweze kutimiza wajibu wetu Kwake.
Tunaomba Roho Mtakatifu kila siku atuongoze
kuhubiri na kumshuhudia Mungu.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, neema
Tunaomba watu wote wajue tofauti ya mema na mabaya,
wauweke ukweli katika vitendo.
Tunaomba Mungu awaadhibu watenda maovu
na kanisa Lake lisisumbuliwe.
Tunaomba watu wote watoe upendo wa kweli kwa Mungu
wa kupendeza na mtamu sana.
Tunaomba Mungu aondoe pingamizi yote
ili tuweze kutoa vyetu vyote kwa Mungu.
Tunaomba Mungu aiweke mioyo yetu ikimpenda Mungu,
isimwache Mungu.
Tunaomba wale walioamuliwa kabla na Mungu
warudi katika uwepo Wake.
Tunaomba watu wote waimbe sifa zao kwa Mungu
ambaye amefikia utukufu.
Tunaomba Mungu awe na watu Wake,
atuweke tuendelee kuishi katika upendo wa Mungu.
Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu!
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumanne, 3 Aprili 2018

Umeme wa Mashariki | Dibaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Mwenyezi Mungu alisema, Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno “Mungu” na mafungu ya maneno kama “kazi ya Mungu”, hawamjui Mungu, na kwa kiwango cha chini zaidi hawaijui kazi ya Mungu.

Neno la Mungu Humwongoza Mtu Kuishi Maisha Mapya | Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana

Neno la Mungu Humwongoza Mtu Kuishi Maisha Mapya | Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana

Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana
I
Mwenyezi Mungu mwenye mwili, tunaimba nyimbo za sifa kubwa Kwako.
Wewe hutuleta katika maisha ya ufalme.
Sisi watu wa ufalme tu katika karamu yako ya fahari,
tukifurahia maneno Yako, tukitakaswa upotovu wetu.
Neno Lako hutuongoza na sisi kukufuata kwa karibu.
Ni neema ya Mungu kwamba tabia yetu ya kishetani imetupiliwa mbali.
Sisi hufurahia neno la Mungu na kuishi maisha mapya mbele Zake.
Kutunza moyo wa Mungu, kumpenda Yeye kwa dhati, kumshukuru na kumsifu.
La la la la la ... la la la la la ...
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

II
Kumini kwamba neno la Mungu ni ukweli na linaweza kutupa maisha.
Sisi hufanya ushirika kuhusu neno la Mungu na kuuelewa ukweli, na Roho Mtakatifu Akifanya kazi juu yetu.
Twajimimina mbali sisi wenyewe, kuwa sahili na wazi, na kufanya mazoezi ya kuwa mtu mwaminifu.
Ukweli hutufanya kuwa walioachiliwa na huru, ukijaza moyo wetu na furaha.
Maisha yetu ya kanisa yanapendeza sana, na watakatifu wote wamekuwa hai.
Sisi hufanya ushirika juu ya ukweli na kusaidiana, na maisha yetu hukua kwa kasi.
Kukubali hukumu, kutenda ukweli, na kuishi katika neno la Mungu.
Ishi kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli kutosheleza moyo wa Mungu.
La la la la la ... la la la la la …
III
Sisi ndugu huratibu kwa mpangilio na sote tuna furaha.
Sisi huwasilishiana maneno ya Mungu na kushiriki matukio, tukitekeleza majukumu yetu kwa uratibu.
Kutii kweli, kuingia uhalisi na kumfanya Mungu aridhike.
Kuishi katika upendo wa Mungu, sisi humsifu Mungu milele.
La la la la la ... la la la la la ...

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya 

Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatatu, 2 Aprili 2018

Umeme wa Mashariki | Maonyo Matatu

Umeme wa Mashariki | Maonyo Matatu

Mwenyezi Mungu alisema, Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla ya kuuamua mwisho wenu, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu.

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kristo

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. 

Jumapili, 1 Aprili 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia

12. Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake

(Yohana 20:26-29) Na baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwa ndani tena, na Tomaso pamoja nao: Kisha akaja Yesu, na milango imefungwa, na akasimama katikati, kisha akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso, Weka hapa kidole chako, na utazame mikono yangu; na ulete mkono wako uuweke ubavuni mwangu, na usiwe asiyeamini, bali uwe aaminiye.