Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumatatu, 6 Mei 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Kuhusu Maisha ya Petro

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Kuhusu Maisha ya Petro

Petro ni mfano ambao Mungu aliutambulisha kwa wanadamu, na yeye ni mtu mashuhuri anayejulikana vizuri. Kwa nini mtu mnyonge kama huyo aliwekwa mahala kama mfano na Mungu na amesifiwa na vizazi vya baadaye? Bila shaka, ni wazi kwamba hili halitenganishwi na maonyesho yake na azimio lake la upendo kwa Mungu.

Jumapili, 5 Mei 2019

Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Wimbo wa Ufalme

Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Wimbo wa Ufalme

Watu wanishangilia Mimi, watu wananisifu Mimi; midomo yote inataja Mungu mmoja wa kweli, watu wote wainua macho yao kutazama matendo Yangu. Ufalme washuka duniani, nafsi Yangu ni tajiri na yenye wingi. Ni nani hangesherehekea haya? Nani hangecheza kwa furaha kwa ajili ya haya? Ee, Sayuni! Inua bango lako la ushindi ili kunisherehekea Mimi! Imba wimbo wako wa ushindi na ueneze jina Langu takatifu!

Jumamosi, 4 Mei 2019

Umeme wa Mashariki | Utangulizi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

"Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima" ni kundi la pili la matamshi yanayoonyeshwa na Kristo. Ndani yake, Kristo Anatumia utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Yanajumlisha kipindi cha kuanzia Februari 20, 1992 hadi Juni 1, 1992, na yana jumla ya matamshi arobaini na saba. Namna, maudhui na mtazamo wa maneno ya Mungu katika matamshi haya hayafanani kabisa na "Maneno ya Roho kwa Makanisa." "Maneno ya Roho kwa makanisa" inafichua na kuongoza tabia ya watu ya nje na maisha yao rahisi ya roho. Hatimaye, inaisha kwa "majaribu ya watendaji huduma."

Ijumaa, 3 Mei 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)


Neno la Mwenyezi Mungu | Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu; hii ni kwa kuwa asili potovu ya mwanadamu inatokana kabisa na Shetani na asili ya mwanadamu imemilikiwa na kupotoshwa na Shetani. Yaani, mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa uovu na ubaya wake. Mwanadamu hakui katika ulimwengu wa ukweli au mazingira matakatifu, na aidha haishi katika mwanga. Kwa hivyo, haiwezekani ukweli kumilikiwa kiasili katika asili ya kila mtu, na zaidi ya hayo, hawawezi kuzaliwa na kiini cha kumwogopa, kiini cha kumheshimu Mungu.

Alhamisi, 2 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu


Matamshi ya Mwenyezi MunguAsili na Utambulisho wa Mwanadamu

Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi. Mimi Siwalaumu mwanadamu, wala Siwaangamizi kwa ukatili au kuwatolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili. Kwa hivyo ingawa wale Waisraeli walinipigilia misumari msalabani hadharani, wao, ambao wamekuwa wanamngoja Masiha na Yehova na kumtamani sana Mwokozi Yesu, hawajasahau ahadi Yangu. Hii ni kwa sababu Sijawatelekeza.

Jumatano, 1 Mei 2019

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea. Hitaji la msingi kabisa kwenu ni kwamba myapokee waziwazi maneno yanayonenwa kwenu. Je, siyo imani iliyovurugika ikiwa unanifuata bila kufahamu kile Ninachosema? Ubora wenu wa tabia ni duni sana. Ni kwa sababu hammiliki uwezo wa kupokea kwamba hamna ufahamu hata mdogo wa kile kinachosemwa. Kwa hivyo, ni vigumu sana kutimiza matokeo yanayotamanika. Mambo mengi hayawezi kusemwa kwenu moja kwa moja na athari ya awali haiwezi kutimizwa.

Jumanne, 30 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 68



Matamshi ya Mwenyezi MunguSura ya 68

Neno Langu linatekelezwa katika kila nchi, mahali, taifa na kikundi, na neno Langu linakamilishwa katika kila pembe wakati wowote. Maafa yanayotokea kila mahali si vita kati ya watu, wala si mapigano na silaha. Hakutakuwa na vita tena baadaye. Wote wako katika mfumbato Wangu. Wote watakabili hukumu Yangu na watadhoofika kati ya maafa. Acha wale wanaonipinga na wale wasioanza kushirikiana na Mimi wateseke uchungu wa maafa mbalimbali. Acha walie na kusaga meno yao hadi milele, na kubaki katika giza daima. Hawataendelea kuishi. 

Jumatatu, 29 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 98

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 98

Mambo yote yatakuja juu ya kila mmoja wenu, na yatawawezesha kujua zaidi juu Yangu na kuwa na uhakika zaidi juu Yangu. Yatawawezesha kunijua, Mungu mmoja Mwenyewe, kunijua Mimi Mwenye uweza, kunijua Mimi Mungu Mwenyewe mwenye mwili. Baadaye, Nitatoka katika mwili, Nirudi Sayuni, Nirudi katika nchi nzuri ya Kanaani, ambayo ni makazi Yangu, ndiyo hatima Yangu, na ndio msingi ambao niliumba vitu vyote. Sasa hakuna yeyote kati yenu anayeelewa maana ya maneno ambayo Ninasema, hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kuelewa maana ya maneno haya.

Jumapili, 28 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 104

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 104

Watu, matukio na vitu vyote nje Yangu vitakufa na kuwakatika hali ya kutokuwepo, ilhali watu, matukio na vitu vyote vilivyo ndani Yangu vitapata kila kitu kutoka Kwangu na kuingia katika utukufu pamoja na Mimi, kuingia katika Mlima Wangu Sayuni, makazi Yangu, na kuishi pamoja kwa amani nami milele. Niliumba vitu vyote mwanzoni na Nitamaliza kazi Yangu mwishowe, na pia Nitatawala milele kama Mfalme. Katikati, pia Ninaongoza na kuutawala ulimwengu mzima. Hakuna anayeweza kuondoa mamlaka Yangu, kwani Mimi ni Mungu mmoja Mwenyewe, na pia Nina uwezo wa kupitisha mamlaka Yangu kwawazaliwa Wangu wa Kwanza, ili wazaliwa Wangu wa kwanza waweze kutawala kandokando Yangu.

Jumamosi, 27 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 65

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 65

Maneno Yangu daima yanaendeleza barabara, yaani yanaonyesha udhaifu wenu wa jaala, vinginevyo bado mgekuwa mnakokota visigino vyenyu, bila wazo la muda gani ulioko sasa. Fahamu hili! Mimi Hutumia njia ya upendo ili kuwaokoa. Bila kujali jinsi nyinyi mlivyo, bila shaka Nitakamilisha mambo ambayo Nimekubali bila kufanya kosa lolote. Je, Ninaweza, Mwenyezi Mungu Mwenye haki, kufanya kosa? Je, hiyo siyo dhana ya mtu? Niambieni, kila kitu Mimi Hufanya na kusema si kwa ajili yenu?

Ijumaa, 26 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 97

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 97

Nitafanya kila mtu aone matendo Yangu ya ajabu na kusikia maneno Yangu ya hekima. Ni lazima iwe kila mtu na ni lazima iwe juu ya kila suala. Hii ni amri Yangu ya utawala na ni ghadhabu Yangu. Nitahusisha kila mtu na kila jambo ili watu wote kutoka mwisho mmoja wa ulimwengu hadi mwingine wataona kwa macho yao wenyewe, la sivyo Sitaacha kamwe. Ghadhabu Yangu imemwagwa kikamilifu na hakuna hata chembe imezuiwa. Inaelekezwa kwa kila mtu mmoja ambaye anakubali jina hili (hivi karibuni itageuzwa juu ya mataifa yote ya dunia). Na ghadhabu Yangu ni nini? Ni kali kiasi gani?

Alhamisi, 25 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 100

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 100

Ninawachukia wale wote ambao hawajajaaliwa na kuchaguliwa na Mimi. Kwa hiyo ni lazima Niwafukuze watu hawa kutoka katika nyumba Yangu mmoja baada ya mwingine, hivyo hekalu Langu litakuwa takatifu na bila doa, nyumba Yangu itakuwa mpya daima na haitakuwa nzee kamwe, jina Langu takatifu litaenezwa milele na watu Wangu watakatifu watakuwa wapendwa Wangu. Aina hii ya mandhari, aina hii ya nyumba, aina hii ya ufalme ni lengo Langu, makao Yangu nayo ni msingi wa uumbaji Wangu wa vitu vyote. Hakuna mtu anayeweza kuyayumbisha au kuyabadilisha. Mimi mwenyewe na wana Wangu wapendwa tutaishi pamoja ndani yake na hakuna mtu atakayeruhusiwa kuyakanyaga, hakuna chochote kitakachoruhusiwa kuishi humo na hata zaidi hakuna kitu chochote kibaya kitakachoruhusiwa kutokea kamwe. Yote itakuwa sifa na kushangilia tu, yote yatakuwa mandhari ambayo mwanadamu hawezi kudhania.