Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumatatu, 24 Juni 2019

Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu


Neno la Mungu |  “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu

anasema, “Mungu aliumba vitu vyote kuhusiana, kupatana na kutegemeana. Alitumia njia hii na kanuni hizi kudumisha kuendelea kuishi na uwepo wa vitu vyote na kwa njia hii binadamu ameishi kwa utulivu na kwa amani na amekua na kuzaliana kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira haya hai hadi siku ya leo. Yaani, Mungu anaweka uwiano katika mazingira ya asili.

Jumapili, 23 Juni 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 43

Maneno ya Mungu | Sura ya 43

Je, Sijawakumbusha? Msiwe wenye hofu; ninyi hamjanisikiliza tu, watu wasio na fikira ninyi! Je, mtaweza kuuelewa moyo Wangu lini? Kila siku kuna nuru mpya, kila siku kuna mwanga mpya. Ni mara ngapi mmeuelewa kwa ajili yenu wenyewe? Je, Sijawaambia Mwenyewe? Bado ninyi ni wa kukaa tu kama wadudu ambao watasonga tu wanaposukumwa, lakini hamwezi kuchukua hatua ya kushirikiana na Mimi, kuufikiria mzigo Wangu. 

Jumamosi, 22 Juni 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 42


Sauti ya Mungu | Sura ya 42

Jinsi gani matendo ya Mwenyezi Mungu yalivyo makuu! Jinsi ilivyo ya ajabu! Jinsi ilivyo ya kushangaza! Tarumbeta saba zinatoa sauti, ngurumo saba zinatolewa, bakuli saba zinamwangwa—hii itadhihirika wazi mara moja na hakuwezi kuwa na shaka. Upendo wa Mungu huja juu yetu kila siku na ni Mwenyezi Mungu pekee Anayeweza kutuokoa; kama tunakabiliwa na bahati mbaya au kupokea baraka ni kwa sababu Yake kabisa, na sisi wanadamu hatuna njia ya kuamua hili. 

Ijumaa, 21 Juni 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 41


Maneno ya Mungu | Sura ya 41

Kuhusu shida zinazoibuka kanisani, usiwe na mashaka mengi. Kanisa linapojengwa haiwezekani kuepuka makosa, lakini usiwe na wasiwasi unapokabiliwa na shida hizo; kuwa mtulivu na makini. Sijawaambia hivyo? Omba Kwangu mara nyingi, na Nitakuonyesha kwa wazi nia Zangu. Kanisa ni moyo Wangu na ni lengo Langu la msingi, Nawezaje kutolipenda? Usiogope, mambo kama haya yanapotendeka kanisani, yote yanaruhusiwa na Mimi.

Alhamisi, 20 Juni 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 40


Maneno ya Mungu | Sura ya 40

Kwa nini ninyi ni wa mwendo wa polepole? Kwa nini hamsikii? Makumbusho kadhaa hayajawazindua; hili linanihuzunisha. Kwa kweli Sipendi kuwaona wanangu namna hii. Moyo Wangu unawezaje kustahimili hili? Ah! Lazima Niwafundishe kwa mkono Wangu mwenyewe. Mwendo Wangu unaendelea kuwa wa kasi. Wanangu! Inukeni haraka na mshirikiane na Mimi. Nani wanajitumia kwa dhati kwa ajili Yangu sasa? Ni nani anayeweza kujitolea kikamilifu bila malalamiko hata kidogo? Daima ninyi ni wenye kutosikia na wapumbavu! 

Jumatano, 19 Juni 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 39

Sauti ya Mungu | Sura ya 39

    Fungua macho yako na uangalie na unaweza kuona nguvu Zangu kuu kila mahali! Unaweza kuwa na uhakika na Mimi kila mahali. Ulimwengu na anga unaeneza nguvu Zangu kuu. Maneno ambayo Nimenena yametimia katika ongezeko la joto la hali ya hewa, mabadiliko ya hali ya hewa, vioja vya watu, ulemavu wa elimumwendo ya kijamii, na udanganyifu wa mioyo ya watu. Jua linakuwa jeupe na mwezi unakuwa mwekundu; Yote yako katika machafuko. Je, bado huoni haya? 

Jumanne, 18 Juni 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 38


Maneno ya Mungu | Sura ya 38

Si kwamba imani yako ni nzuri au safi, lakini badala yake, kazi Yangu ni ya ajabu! Kila kitu ni kwa sababu ya rehema Zangu! Hupaswi kuwa na tabia potovu ya ubinafsi au kiburi hata kidogo, vinginevyo kazi Yangu kwako haitaendelea. Lazima uelewe wazi kwamba iwapo watu wanaanguka au kusimama imara si kwa sababu yao, ni kwa sababu Yangu. Leo, kama huelewi vizuri hatua hii, hutaweza kuingia katika ufalme!

Jumatatu, 17 Juni 2019

Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili


Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote.

Jumapili, 16 Juni 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 36


Maneno ya MunguSura ya 36

Mwenyezi Mungu wa kweli, Mfalme katika kiti cha enzi, hutawala ulimwengu mzima, Anakabiliana na mataifa yote na watu wote, kila kitu chini ya mbingu hung’aa kwa utukufu wa Mungu. Viumbe vyote hai katika miisho ya ulimwengu vitaona. Milima, mito, maziwa, ardhi, bahari na viumbe vyote viishivyo, katika nuru ya uso wa Mungu wa kweli wamefungua mapazia yao, kuhuishwa, kama kuamka kutoka kwa ndoto, kuchipuka kwa kuvunja uchafu!

Jumamosi, 15 Juni 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 35


Sauti ya Mungu | Sura ya 35

Ngurumo saba zinatoka kwenye kiti cha enzi, zinautikisa ulimwengu, zinageuza mbingu na ardhi, na zinavuma angani! Sauti hiyo inapenya sana kiasi kwamba watu hawawezi kuepuka wala kujificha. Nuru ya ghafla ya umeme na sauti ya radi zinatumwa mbele, zikiiangusha chini mbingu na ardhi papo hapo, na watu wamekaribia kufa. Kisha, dhoruba ya mvua kali inafagia ulimwengu wote kwa kasi ya umeme, ikianguka kutoka angani! 

Ijumaa, 14 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 34


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 34

Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu zote , mwenye kutimiliza yote na Mungu wa kweli kabisa! Habebi tu nyota saba, ana Roho saba, ana macho saba, anafungua mihuri saba na kufungua hati ya kukunja yenye maandishi, lakini zaidi ya hayo Yeye anaendesha mapigo saba na vikasa saba na kufungua radi saba; zamani za kale Yeye alipiga vinumbi saba! Vitu vyote vilivyoumbwa na kufanywa kuwa kamili na Yeye vinapaswa kumsifu, kumpa adhama na kutukuza kiti Chake cha enzi.

Alhamisi, 13 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 33


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 33

Ufalme Wangu unawahitaji wale ambao ni waaminifu, wasio wanafiki, na wasio wadanganyifu. Je, si watu wenye moyo safi na waaminifu duniani hawapendwi na watu? Mimi ni kinyume kabisa cha jinsi ilivyo. Inakubalika kwa watu waaminifu kuja Kwangu; Nafurahia mtu wa aina hii, pia Ninamhitaji mtu wa aina hii. Hii ni haki Yangu hasa. Watu wengine ni wajinga; hawawezi kuhisi kazi ya Roho Mtakatifu na hawawezi kuyaelewa mapenzi Yangu.

Jumatano, 12 Juni 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 32


Sauti ya Mungu | Sura ya 32

Mwanga ni nini? Katika siku za nyuma kwa kweli mliuona mbadiliko wa kazi ya Roho Mtakatifu kama mwanga. Kuna mwanga wa kweli wakati wote, unaojumuisha ninyi kupata kile Mungu alicho kupitia kwa kunikaribia na kushirikiana na Mimi; kuwa na utambuzi katika maneno ya Mungu na kufahamu mapenzi ya Mungu katika maneno Yake—yaani, mnapokula na kunywa, mnahisi Roho wa maneno ya Mungu na kupokea maneno ya Mungu ndani yenu; kuelewa kile Alicho huku mkipitia na kupokea mwangaza wa Mungu huku mkizungumza na Yeye; na pia kupewa nuru na kuwa na utambuzi mpya katika maneno ya Mungu wakati wote huku mkifikiria na kutafakari.

Jumanne, 11 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 31


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 31

Ninawapenda wale wote wanaonitaka Mimi kwa dhati. Mkilenga kunipenda, hakika Nitawabariki kwa kiasi kikubwa. Je, mnaelewa nia Zangu? Katika nyumba Yangu, hakuna tofauti kati ya hali ya juu na chini. Kila mtu ni mwanangu, Mimi ni Baba yenu, Mungu wenu. Mimi ni mkuu na wa pekee. Ninadhibiti kila kitu ulimwenguni!
Unapaswa "kunitumikia kwa unyenyekevu na katika mafumbo" katika nyumba Yangu. Maneno haya yanapaswa kuwa kama wito wako.

Sauti ya Mungu | Sura ya 30


Sauti ya Mungu | Sura ya 30

Amkeni, ndugu! Amkeni, kina dada! Siku Yangu haitakawishwa; wakati ni uhai, na kuushika wakati ni kuokoa uhai! Wakati hauko mbali sana! Mkifanya mitihani ya kuingia katika chuo kikuu na msipite, mnaweza kujaribu tena na mubukue kwa ajili ya mtihani. Hata hivyo, siku Yangu haitakuwa na ucheleweshaji kama huo. Kumbuka! Kumbuka! Ninakuhimiza kwa maneno haya mazuri.

Jumatatu, 10 Juni 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza


Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu  | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo. Mungu kuingia rahani kunamaanisha kwamba Hatafanya tena kazi Yake ya wokovu wa binadamu.

Jumapili, 9 Juni 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 29

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 29

Je, ulijua kwamba wakati uko karibu? Hivyo kwa muda mfupi wa hivi karibuni utanitegemea Mimi na kuyatupilia mbali mambo yote kutoka kwako ambayo hayalingani na tabia Yangu: upumbavu, upole wa kuonyesha hisia, mawazo yasiyo wazi, moyo wa upole, nia hafifu, upuuzi, hisia zilizotiwa madoido mengi, kuchanganyikiwa na ukosefu wa utambuzi. Haya lazima yatupiliwe mbali upesi iwezekanavyo. Mimi ndimi mwenyezi Mungu!

Jumamosi, 8 Juni 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 28


Maneno ya Mungu | Sura ya 28

Unaona kwamba muda ni mfupi sana na kazi ya Roho Mtakatifu inavurumisha mbele, ikikusababisha kupata baraka kubwa hivi, kumpokea Mfalme wa ulimwengu, Mwenyezi Mungu, ambaye ni Jua ling’aalo, Mfalme wa ufalme—hii yote ni neema na huruma Yangu. Kuna nini kinachoweza kuwepo kinachoweza kukutoa kwa upendo Wangu? Tafakari kwa makini, usijaribu kuepa, subiri kwa ustahamilivu mbele Yangu kila wakati na usiwe ukizurura nje daima.

Ijumaa, 7 Juni 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 27


Sauti ya Mungu | Sura ya 27

Mungu mmoja wa kweli anayetawala vitu vyote katika ulimwengu—Kristo mwenyezi! Huu ndio ushuhuda wa Roho Mtakatifu, ni ushahidi dhahiri! Roho Mtakatifu anafanya kazi kuwa na ushuhuda kila mahali, ili kusiwe na mtu yeyote mwenye shaka yoyote. Mfalme wa ushindi, Mwenyezi Mungu! Yeye ameushinda ulimwengu, Ameishinda dhambi na kufanikisha ukombozi!

Alhamisi, 6 Juni 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 26


Maneno ya Mungu | Sura ya 26

Wanangu, yatilieni maanani maneno Yangu, sikiliza kwa utulivu sauti Yangu na Nitafichua kwako. Uwe na utulivu ndani yangu, kwa maana Mimi ni Mungu wako, Mkombozi wenu wa pekee. Mnatakiwa kutuliza mioyo yenu nyakati zote, mkae ndani yangu; Mimi ni mwamba wako, msaidizi wenu. Msiwe na nia nyingine, lakini mnitegemee kwa mioyo yenu yote na Mimi nitaonekana kwenu kwa hakika—Mimi ni Mungu wenu!

Jumatano, 5 Juni 2019


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja”  Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali.

Jumanne, 4 Juni 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 25

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 25

Mwenyezi Mungu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani, Mungu wetu Anatawala! Mwenyezi Mungu anaweka miguu Yake kwenye Mlima wa Mizeituni. Uzuri ulioje! Sikiliza! Sisi walinzi tunapaza sauti zetu: tunaimba kwa pamoja kwa sauti zetu, kwa kuwa Mungu amerudi Sayuni. Tunaona kwa macho yetu wenyewe ukiwa wa Yerusalemu. Furahieni na kuimba kwa sauti kwa pamoja, kwa kuwa Mungu ametufariji na Ameukomboa Yerusalemu.

Jumatatu, 3 Juni 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 24


Maneno ya Mungu | Sura ya 24
Wakati unakaribia hata zaidi. Amkeni! Watakatifu wote! Nitawatamkia ninyi. Wote wanaosikia wataamka. Mimi ni Mungu ambaye mmekuwa na imani katika kwa miaka hii mingi. Leo nimekuwa mwili na kuja mbele ya macho yenu, na hii inafichua yule ambaye ananitaka kwa kweli, ambaye yuko tayari kulipa gharama yoyote kwa ajili Yangu, ambaye husikiliza neno Langu kwa kweli, na yule ambaye yuko tayari kuuweka ukweli katika matendo.

Jumapili, 2 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 23

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 23
Kwa ndugu wote ambao wameisikia sauti Yangu: Mmeisikia sauti ya hukumu Yangu kali na mmevumilia mateso yaliyokithiri. Hata hivyo, mnapaswa kujua kwamba katika sauti Yangu kali kumejificha nia Zangu! Ninawafundisha nidhamu ili muweze kuokolewa. Mnapaswa kujua kwamba kwa wana Wangu wapendwa, Nitawafundisha nidhamu na kuwapogoa na kuwafanya muwe wakamilifu hivi karibuni. Moyo Wangu una hamu sana, lakini ninyi hamuelewi moyo Wangu na hamtendi kulingana na neno Langu.

Jumamosi, 1 Juni 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 22

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 22
Kumwamini Mungu si jambo rahisi kufanya. Ninyi mnajiboronga, mkiteketeza kila kitu mbele yenu mkifikiri kuwa haya yote ni ya kuvutia sana, matamu mno! Kuna baadhi ambao bado wanashangilia—wao tu hawana utambuzi katika roho zao. Ni vyema kuchukua muda wa kuuweka katika muhtasari uzoefu huu. Katika siku za mwisho, kila aina za pepo huibuka kutekeleza majukumu yao, wakikaidi kwa uwazi hatua za mbele za wana wa Mungu na kushiriki katika kuuvunja ujenzi wa kanisa.

Ijumaa, 31 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 21

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 21
Kazi ya Roho Mtakatifu sasa imewaleta katika mbingu mpya na dunia mpya. Kila kitu kinaendelea kufanywa upya, kila kitu ki mikononi Mwangu, kinarudi ulingoni! Kwa dhana zao, watu wanashindwa kulifikiria kwa makini, na kwao haina maana, lakini ni Mimi ambaye niko kazini, na hekima Yangu iko ndani yake. Kwa hiyo mnaweza kukomesha dhana zenu zote na maoni yenu. Mnaweza kujishughulisha na kula na kunywa neno la Mungu katika utii, bila wasiwasi wowote kamwe. Kufanya kazi kwa njia hii Mimi nachukua jukumu takatifu. Kwa kweli watu hawana haja ya kuwa namna fulani.

Alhamisi, 30 Mei 2019


Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu

Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake.
Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu.
Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya.
Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake.
Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana.
Tunatafakari, kufikiri maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu anatuangazia.

Jumatano, 29 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 20

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 20
Kazi ya Roho Mtakatifu hushina mbele, ikiwaleta nyinyi ndani ya eneo mpya kabisa, ambayo ni kwamba hali halisi ya maisha ya ufalme imejitokeza mbele yako. Maneno ambayo yamesemwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja yamefichua ukina ulio ndani ya mioyo yenu na kwa hiyo picha moja baada ya nyingine zinaonekana mbele yenu. Wale wote ambao wana njaa na kiu ya haki, ambao wana nia ya kutii kwa hakika watabaki Sayuni na watakaa Yerusalemu Mpya.

Jumanne, 28 Mei 2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 19

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Kristo | Sura ya 19
Kazi ya Roho Mtakatifu inapoendelea mbele, Mungu kwa mara nyingine tena ametuingiza katika mbinu mpya ya kazi ya Roho Mtakatifu. Matokeo yake, haiepukiki kwamba baadhi ya watu wamenielewa Mimi vibaya na kufanya malalamiko Kwangu. Wengine wamenipinga na kunikataa Mimi, na wamenichunguza Mimi. Hata hivyo, bado Mimi ninasubiri kwa rehema toba yenu na mageuzi. Mabadiliko katika utaratibu wa kazi ya Roho Mtakatifu ni Mungu Mwenyewe

Jumatatu, 27 Mei 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 18

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 18
Kujenga kanisa si kitu rahisi cha kufanya! Niliweka moyo Wangu wote katika kulijenga na Shetani angefanya kila kitu ingeweza kuibomoa. Kama unataka kujengwa lazima uwe na maono; lazima uishi maisha kwa Mimi, kuwa shahidi wa Kristo, shikilia Kristo juu kwa juu, na kuwa mwaminifu Kwangu. Hupaswi kutoa visingizio, lakini badala yake kutii bila ya sharti; lazima uvumilie majaribu yoyote, na kukubali yote yanayotoka kwa Mimi.

Jumapili, 26 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 17

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 17
Kanisa linajengwa na Shetani anajaribu kwa uwezo wake kulibomoa. Anataka kubomoa ujenzi Wangu kwa njia yoyote iwezekanayo, kwa hivyo, lazima kanisa litakaswe kwa haraka. Lazima kusiwe na makapi au mabaki yoyote maovu; lazima litakaswe ili lisiwe na dosari na libaki takatifu kama awali. Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi.

Jumamosi, 25 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 16

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 16
Baada ya ushuhudiaji wa Mwana wa Adamu, Mwenyezi Mungu alijifichua kwetu hadharani kama Jua la haki. Haya ndiyo mabadiliko mlimani! Sasa inakuwa halisi zaidi na zaidi, na zaidi kuwa jambo la uhalisi. Tumeona utaratibu wa kazi ya Roho Mtakatifu, Mungu Mwenyewe ameibuka kutoka kwa mwili wa damu. Yeye hayuko chini ya udhibiti wa mwanadamu, wala anga, wala jiografia; Yeye huvuka mipaka ya nchi na bahari, Yeye hufika miisho halisi ya ulimwengu, na mataifa yote na watu wa jumuia zote wanasikiliza sauti Yake kwa utulivu. "

Ijumaa, 24 Mei 2019

Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians


Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians

I
Kama washiriki wa jamii ya wanadamu,
kama wafuasi wa Kristo wa dhati,
ni wajibu wetu, ni jukumu letu
kutoa akili zetu  na miili yetu
kwa kutimiza agizo la Mungu.
Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.
Kwa maana asili yetu, ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

Alhamisi, 23 Mei 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 15

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 15
Kuonekana kwa Mungu tayari kumetokea katika makanisa yote. Roho ndiyo anayeongea, Yeye ni moto mkali, Yeye hubeba uadhama na Anahukumu; Yeye ni Mwana wa Adamu, liyevaa vazi lililofika kwa miguu, na kufungwa mshipi kwenye matiti na ukanda wa dhahabu. Kichwa Chake na nywele Zake ni nyeupe kama sufu nyeupe, na macho Yake ni kama mwale wa moto; na miguu Yake iko kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti Yake kama sauti ya maji mengi.

Jumatano, 22 Mei 2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 14

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Kristo | Sura ya 14
Hapana muda wa kupoteza sasa. Roho Mtakatifu hutumia njia nyingi tofauti za kutuongoza katika maneno ya Mungu na kututayarisha na ukweli wote, kutakaswa, kuwa na undani wa kweli na ushirikiano na Mimi; huruhusiwi nafasi yoyote ya kuchagua. Kazi ya Roho Mtakatifu haina hisia na haijali wewe ni mtu wa aina gani. Mradi tu wewe uko tayari kutafuta na kufuata—si kutoa visingizio, si kubishana juu ya mafanikio yako mwenyewe na hasara lakini kutafuta na njaa na kiu ya haki, basi Nitakupa nuru. Bila kujali jinsi ulivyo mpumbavu na mjinga, Mimi sioni vitu kama hivyo. Naangalia kuona jinsi unavyofanya kazi kwa bidii katika hali ya kujenga.

Jumanne, 21 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 13

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 13

Katika hali yenu ya sasa nyinyi hushika dhana ya "kibinafsi"zaidi kupindukia, na madakizo ya dini ni mazito kiasi. Mmeshindwa kutenda katika roho, hamuwezi kufahamu kazi ya Roho Mtakatifu, na mmekataa mwanga mpya. Huoni jua wakati wa mchana kwa sababu wewe ni kipofu. Huwaelewi watu, umeshindwa kuwaacha wazazi wako, umekosa utambuzi wa kiroho, huijui kazi ya Roho Mtakatifu, na huna wazo la jinsi ya kula na kunywa ya neno Langu[a]

Jumatatu, 20 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 12

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 12

Ikiwa una tabia ambayo si thabiti, nyepesi kuhamaki kama upepo au mvua, kama huwezi kuendelea kusonga mbele, basi fimbo Yangu haitakuwa mbali na wewe. Unaposhughulikiwa, kadiri hali ilivyo mbaya zaidi, na kadiri unavyoteswa zaidi, ndivyo upendo wako kwa Mungu unavyoongezeka, na unaacha kushikilia dunia. Bila njia nyingine, unakuja Kwangu, na unapata tena nguvu na imani yako.

Jumapili, 19 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 11

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 11

Je, Mimi ni Mungu wako? Je, Mimi ni Mfalme wako? Je, kweli umeniruhusu Mimi kutawala kama Mfalme ndani yako? Unapaswa kutafakari kujihusu kabisa. Je, hukuchunguza na kukataa mwanga mpya na hata kuthubutu kuacha kuufuata ulipokuwa ukija? Kwa sababu ya hii utastahimili hukumu na kuanguka hadi kifo chako, utahukumiwa na kutandikwa kiboko na kiboko cha chuma na hutahisi kazi ya Roho Mtakatifu.

Jumamosi, 18 Mei 2019

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”



Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu.

Ijumaa, 17 Mei 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 10

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 10

Haupaswi kuwa na hofu ya hili na lile. Haidhuru wingi wa matatizo na hatari unazokabili, utabaki thabiti mbele Yangu; usizuiliwe na kitu chochote, ili mapenzi Yangu yaweze kufanyika. Huu utakuwa ni wajibu wako, vinginevyo utakabiliana na ghadhabu Yangu na mkono wangu uta..., na utavumilia mateso ya akili yasio na mwisho. Ni lazima uyavumilie yote, lazima uviachilie vitu vyote ulivyo navyo, na kufanya kila kitu unachoweza kunifuata Mimi, kulipa gharama zote kwa ajili Yangu.

Alhamisi, 16 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 9

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 9


Nataka kukukumbusha kwamba huwezi kuwa na wasiwasi hata kidogo juu ya neno Langu na kutokujali kwa aina yoyote hakukubaliki. Unapaswa kulisikiliza na kulitii na kutenda mambo kulingana na nia Zangu. Daima lazima uwe macho na kamwe usiwe na tabia ambayo ni ya kiburi na ya kujidai, na lazima kila wakati unitegemee Mimi ili kutupilia mbali tabia ya zamani ya asili ambayo hukaa ndani yako.

Jumatano, 15 Mei 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 8

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 8

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa.

Jumanne, 14 Mei 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 7

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 7

Kuinuka kwa mazingira pande zetu zote huharakisha kurudi nyuma kwetu katika roho. Usitende kwa moyo mgumu, usipuuze kwa vyovyote vile kama Roho Mtakatifu Ana wasiwasi, usijaribu kuwa mjanja na usiwe na ridhaa kupita kiasi na kuridhika kibinafsi au kuzingatia sana matatizo yako mwenyewe; kitu pekee cha kufanya ni kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Huwezi kuyaacha maneno ya Mungu nyuma au kuyapa kisogo; lazima uyaelewae kwa makini, rudia kuomba-kusoma kwako, na uelewe maisha ndani ya maneno hayo. Usishiriki katika yale yasiyokuwa na maana kwa kuyabugia pasipo kujipa mwenyewe wakati wa kuyawaza.

Jumatatu, 13 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 6

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 6

Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote Naye Anatuongoza katika dunia yote. Mara kwa mara tutakuwa karibu Naye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi. Usiwe na moyo wa kunung’unika, au Mungu hatatupa neema Yake juu yako.

Jumapili, 12 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Haijalishi wewe ni mbari gani au unaishi katika ardhi gani, iwe ni Magharibi au Mashariki—huwezi kujitenganisha na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu, na huwezi kujitenga na malezi na uangalizi wa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu. Haijalishi riziki yako ni nini, kile unachokitegemea kwa ajili ya kuishi, na kile unachokitegemea kudumisha uhai wako katika mwili, huwezi kujitenganisha na kanuni ya Mungu na usimamizi wake.”

Jumamosi, 11 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 5

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 5

Milima na mito huenda ikibadilika, vijito hutiririka mbele, na maisha ya mwanadamu ni yenye uvumilivu mdogo kuliko ardhi na anga. Mwenyezi Mungu pekee ndiye maisha ya milele yaliyofufuka milele, katika vizazi hai milele! Vitu vyote na matukio viko katika mikono Yake, Shetani yuko chini ya miguu Yake.