Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Ijumaa, 31 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 21

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 21
Kazi ya Roho Mtakatifu sasa imewaleta katika mbingu mpya na dunia mpya. Kila kitu kinaendelea kufanywa upya, kila kitu ki mikononi Mwangu, kinarudi ulingoni! Kwa dhana zao, watu wanashindwa kulifikiria kwa makini, na kwao haina maana, lakini ni Mimi ambaye niko kazini, na hekima Yangu iko ndani yake. Kwa hiyo mnaweza kukomesha dhana zenu zote na maoni yenu. Mnaweza kujishughulisha na kula na kunywa neno la Mungu katika utii, bila wasiwasi wowote kamwe. Kufanya kazi kwa njia hii Mimi nachukua jukumu takatifu. Kwa kweli watu hawana haja ya kuwa namna fulani.

Alhamisi, 30 Mei 2019


Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu

Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake.
Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu.
Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya.
Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake.
Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana.
Tunatafakari, kufikiri maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu anatuangazia.

Jumatano, 29 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 20

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 20
Kazi ya Roho Mtakatifu hushina mbele, ikiwaleta nyinyi ndani ya eneo mpya kabisa, ambayo ni kwamba hali halisi ya maisha ya ufalme imejitokeza mbele yako. Maneno ambayo yamesemwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja yamefichua ukina ulio ndani ya mioyo yenu na kwa hiyo picha moja baada ya nyingine zinaonekana mbele yenu. Wale wote ambao wana njaa na kiu ya haki, ambao wana nia ya kutii kwa hakika watabaki Sayuni na watakaa Yerusalemu Mpya.

Jumanne, 28 Mei 2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 19

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Kristo | Sura ya 19
Kazi ya Roho Mtakatifu inapoendelea mbele, Mungu kwa mara nyingine tena ametuingiza katika mbinu mpya ya kazi ya Roho Mtakatifu. Matokeo yake, haiepukiki kwamba baadhi ya watu wamenielewa Mimi vibaya na kufanya malalamiko Kwangu. Wengine wamenipinga na kunikataa Mimi, na wamenichunguza Mimi. Hata hivyo, bado Mimi ninasubiri kwa rehema toba yenu na mageuzi. Mabadiliko katika utaratibu wa kazi ya Roho Mtakatifu ni Mungu Mwenyewe

Jumatatu, 27 Mei 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 18

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 18
Kujenga kanisa si kitu rahisi cha kufanya! Niliweka moyo Wangu wote katika kulijenga na Shetani angefanya kila kitu ingeweza kuibomoa. Kama unataka kujengwa lazima uwe na maono; lazima uishi maisha kwa Mimi, kuwa shahidi wa Kristo, shikilia Kristo juu kwa juu, na kuwa mwaminifu Kwangu. Hupaswi kutoa visingizio, lakini badala yake kutii bila ya sharti; lazima uvumilie majaribu yoyote, na kukubali yote yanayotoka kwa Mimi.

Jumapili, 26 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 17

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 17
Kanisa linajengwa na Shetani anajaribu kwa uwezo wake kulibomoa. Anataka kubomoa ujenzi Wangu kwa njia yoyote iwezekanayo, kwa hivyo, lazima kanisa litakaswe kwa haraka. Lazima kusiwe na makapi au mabaki yoyote maovu; lazima litakaswe ili lisiwe na dosari na libaki takatifu kama awali. Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi.

Jumamosi, 25 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 16

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 16
Baada ya ushuhudiaji wa Mwana wa Adamu, Mwenyezi Mungu alijifichua kwetu hadharani kama Jua la haki. Haya ndiyo mabadiliko mlimani! Sasa inakuwa halisi zaidi na zaidi, na zaidi kuwa jambo la uhalisi. Tumeona utaratibu wa kazi ya Roho Mtakatifu, Mungu Mwenyewe ameibuka kutoka kwa mwili wa damu. Yeye hayuko chini ya udhibiti wa mwanadamu, wala anga, wala jiografia; Yeye huvuka mipaka ya nchi na bahari, Yeye hufika miisho halisi ya ulimwengu, na mataifa yote na watu wa jumuia zote wanasikiliza sauti Yake kwa utulivu. "

Ijumaa, 24 Mei 2019

Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians


Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians

I
Kama washiriki wa jamii ya wanadamu,
kama wafuasi wa Kristo wa dhati,
ni wajibu wetu, ni jukumu letu
kutoa akili zetu  na miili yetu
kwa kutimiza agizo la Mungu.
Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.
Kwa maana asili yetu, ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

Alhamisi, 23 Mei 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 15

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 15
Kuonekana kwa Mungu tayari kumetokea katika makanisa yote. Roho ndiyo anayeongea, Yeye ni moto mkali, Yeye hubeba uadhama na Anahukumu; Yeye ni Mwana wa Adamu, liyevaa vazi lililofika kwa miguu, na kufungwa mshipi kwenye matiti na ukanda wa dhahabu. Kichwa Chake na nywele Zake ni nyeupe kama sufu nyeupe, na macho Yake ni kama mwale wa moto; na miguu Yake iko kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti Yake kama sauti ya maji mengi.

Jumatano, 22 Mei 2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 14

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Kristo | Sura ya 14
Hapana muda wa kupoteza sasa. Roho Mtakatifu hutumia njia nyingi tofauti za kutuongoza katika maneno ya Mungu na kututayarisha na ukweli wote, kutakaswa, kuwa na undani wa kweli na ushirikiano na Mimi; huruhusiwi nafasi yoyote ya kuchagua. Kazi ya Roho Mtakatifu haina hisia na haijali wewe ni mtu wa aina gani. Mradi tu wewe uko tayari kutafuta na kufuata—si kutoa visingizio, si kubishana juu ya mafanikio yako mwenyewe na hasara lakini kutafuta na njaa na kiu ya haki, basi Nitakupa nuru. Bila kujali jinsi ulivyo mpumbavu na mjinga, Mimi sioni vitu kama hivyo. Naangalia kuona jinsi unavyofanya kazi kwa bidii katika hali ya kujenga.

Jumanne, 21 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 13

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 13

Katika hali yenu ya sasa nyinyi hushika dhana ya "kibinafsi"zaidi kupindukia, na madakizo ya dini ni mazito kiasi. Mmeshindwa kutenda katika roho, hamuwezi kufahamu kazi ya Roho Mtakatifu, na mmekataa mwanga mpya. Huoni jua wakati wa mchana kwa sababu wewe ni kipofu. Huwaelewi watu, umeshindwa kuwaacha wazazi wako, umekosa utambuzi wa kiroho, huijui kazi ya Roho Mtakatifu, na huna wazo la jinsi ya kula na kunywa ya neno Langu[a]

Jumatatu, 20 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 12

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 12

Ikiwa una tabia ambayo si thabiti, nyepesi kuhamaki kama upepo au mvua, kama huwezi kuendelea kusonga mbele, basi fimbo Yangu haitakuwa mbali na wewe. Unaposhughulikiwa, kadiri hali ilivyo mbaya zaidi, na kadiri unavyoteswa zaidi, ndivyo upendo wako kwa Mungu unavyoongezeka, na unaacha kushikilia dunia. Bila njia nyingine, unakuja Kwangu, na unapata tena nguvu na imani yako.

Jumapili, 19 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 11

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 11

Je, Mimi ni Mungu wako? Je, Mimi ni Mfalme wako? Je, kweli umeniruhusu Mimi kutawala kama Mfalme ndani yako? Unapaswa kutafakari kujihusu kabisa. Je, hukuchunguza na kukataa mwanga mpya na hata kuthubutu kuacha kuufuata ulipokuwa ukija? Kwa sababu ya hii utastahimili hukumu na kuanguka hadi kifo chako, utahukumiwa na kutandikwa kiboko na kiboko cha chuma na hutahisi kazi ya Roho Mtakatifu.

Jumamosi, 18 Mei 2019

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”



Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu.

Ijumaa, 17 Mei 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 10

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 10

Haupaswi kuwa na hofu ya hili na lile. Haidhuru wingi wa matatizo na hatari unazokabili, utabaki thabiti mbele Yangu; usizuiliwe na kitu chochote, ili mapenzi Yangu yaweze kufanyika. Huu utakuwa ni wajibu wako, vinginevyo utakabiliana na ghadhabu Yangu na mkono wangu uta..., na utavumilia mateso ya akili yasio na mwisho. Ni lazima uyavumilie yote, lazima uviachilie vitu vyote ulivyo navyo, na kufanya kila kitu unachoweza kunifuata Mimi, kulipa gharama zote kwa ajili Yangu.

Alhamisi, 16 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 9

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 9


Nataka kukukumbusha kwamba huwezi kuwa na wasiwasi hata kidogo juu ya neno Langu na kutokujali kwa aina yoyote hakukubaliki. Unapaswa kulisikiliza na kulitii na kutenda mambo kulingana na nia Zangu. Daima lazima uwe macho na kamwe usiwe na tabia ambayo ni ya kiburi na ya kujidai, na lazima kila wakati unitegemee Mimi ili kutupilia mbali tabia ya zamani ya asili ambayo hukaa ndani yako.

Jumatano, 15 Mei 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 8

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 8

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa.

Jumanne, 14 Mei 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 7

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 7

Kuinuka kwa mazingira pande zetu zote huharakisha kurudi nyuma kwetu katika roho. Usitende kwa moyo mgumu, usipuuze kwa vyovyote vile kama Roho Mtakatifu Ana wasiwasi, usijaribu kuwa mjanja na usiwe na ridhaa kupita kiasi na kuridhika kibinafsi au kuzingatia sana matatizo yako mwenyewe; kitu pekee cha kufanya ni kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Huwezi kuyaacha maneno ya Mungu nyuma au kuyapa kisogo; lazima uyaelewae kwa makini, rudia kuomba-kusoma kwako, na uelewe maisha ndani ya maneno hayo. Usishiriki katika yale yasiyokuwa na maana kwa kuyabugia pasipo kujipa mwenyewe wakati wa kuyawaza.

Jumatatu, 13 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 6

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 6

Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote Naye Anatuongoza katika dunia yote. Mara kwa mara tutakuwa karibu Naye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi. Usiwe na moyo wa kunung’unika, au Mungu hatatupa neema Yake juu yako.

Jumapili, 12 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Haijalishi wewe ni mbari gani au unaishi katika ardhi gani, iwe ni Magharibi au Mashariki—huwezi kujitenganisha na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu, na huwezi kujitenga na malezi na uangalizi wa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu. Haijalishi riziki yako ni nini, kile unachokitegemea kwa ajili ya kuishi, na kile unachokitegemea kudumisha uhai wako katika mwili, huwezi kujitenganisha na kanuni ya Mungu na usimamizi wake.”

Jumamosi, 11 Mei 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 5

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 5

Milima na mito huenda ikibadilika, vijito hutiririka mbele, na maisha ya mwanadamu ni yenye uvumilivu mdogo kuliko ardhi na anga. Mwenyezi Mungu pekee ndiye maisha ya milele yaliyofufuka milele, katika vizazi hai milele! Vitu vyote na matukio viko katika mikono Yake, Shetani yuko chini ya miguu Yake.

Ijumaa, 10 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 4

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 4

Daima tutakuwa tukiangalia na kusubiri, kuwa na utulivu katika roho na kutafuta kwa moyo safi. Chochote kitakachotufikia, tusishiriki kwa upofu. Twahitajika tu kuwa kimya mbele ya Mungu na daima kushiriki naye, na kisha nia Yake itafichuliwa kwetu. Roho zetu sharti daima ziwe tayari kutofautisha na sharti ziwe na bidii na zisiokubali kushindwa. Ni lazima tuteka kutoka kwa maji ya uhai mbele ya Mungu, maji ambayo huondoa kiu kutoka kwa roho zetu zilizokauka.

Alhamisi, 9 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 3

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 3

Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu. Yeye Ametimiza ukombozi na kuongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu. Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake kwa hekima Yake ya uungu na uweza Yeye Amejenga Uyahudi na kuifanya imara. Pamoja na uadhama Wake Yeye huhukumu dunia ya maovu; Yeye huhukumu mataifa yote na watu wote, ardhi na bahari na vitu vyote hai juu yao, pia wale ambao wamelewa kwa divai ya uzinzi.

Jumatano, 8 Mei 2019

Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 2

Mwenyezi Mungu anasema, Kufuata kuanza kazi kwa mtazamo mpya, kutakuwa na hatua mpya katika kazi Yangu. Kama ilivyo katika ufalme, Nitafanya mambo moja kwa moja kupitia kwa uungu, Nikiongoza kila hatua ya njia, sahihi hadi kwa maelezo madogo, na bila kutiwa najisi na nia za binadamu hata kidogo. Yafuatayo yanaeleza kwa muhtasari namna ya utekelezaji halisi: Kwa vile ni kupitia katika ugumu na usafishaji ndiyo wamepata jina la “watu”, na kama walivyo watu wa ufalme Wangu, lazima Niwafanye watii kwa mahitaji kali, ambayo ni ya juu kushinda mbinu za kazi Yangu kwa vizazi vilivyopita.

Jumanne, 7 Mei 2019

Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 1

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 1

Je, wale wanaoshuhudia maneno Yangu huyakubali kwa kweli? Je, mnanijua kwa kweli? Mmejifunza utiifu kweli? Ninyi hutumia rasilimali kwa ajili Yangu kwa uaminifu? Mmekuwa na ushuhuda thabiti, usiokubali kushindwa Kwangu mlipokabiliwa na joka kuu jekundu? Je, moyo wenu wa ibada hulifedhehesha kweli joka kuu jekundu? Ni kupitia tu kwa jaribio la maneno Yangu ndipo Naweza kutimiza lengo Langu la kulitakasa kanisa na kuwachagua wale wanaonipenda Mimi kweli. 

Jumatatu, 6 Mei 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Kuhusu Maisha ya Petro

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Kuhusu Maisha ya Petro

Petro ni mfano ambao Mungu aliutambulisha kwa wanadamu, na yeye ni mtu mashuhuri anayejulikana vizuri. Kwa nini mtu mnyonge kama huyo aliwekwa mahala kama mfano na Mungu na amesifiwa na vizazi vya baadaye? Bila shaka, ni wazi kwamba hili halitenganishwi na maonyesho yake na azimio lake la upendo kwa Mungu.

Jumapili, 5 Mei 2019

Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Wimbo wa Ufalme

Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Wimbo wa Ufalme

Watu wanishangilia Mimi, watu wananisifu Mimi; midomo yote inataja Mungu mmoja wa kweli, watu wote wainua macho yao kutazama matendo Yangu. Ufalme washuka duniani, nafsi Yangu ni tajiri na yenye wingi. Ni nani hangesherehekea haya? Nani hangecheza kwa furaha kwa ajili ya haya? Ee, Sayuni! Inua bango lako la ushindi ili kunisherehekea Mimi! Imba wimbo wako wa ushindi na ueneze jina Langu takatifu!

Jumamosi, 4 Mei 2019

Umeme wa Mashariki | Utangulizi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

"Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima" ni kundi la pili la matamshi yanayoonyeshwa na Kristo. Ndani yake, Kristo Anatumia utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Yanajumlisha kipindi cha kuanzia Februari 20, 1992 hadi Juni 1, 1992, na yana jumla ya matamshi arobaini na saba. Namna, maudhui na mtazamo wa maneno ya Mungu katika matamshi haya hayafanani kabisa na "Maneno ya Roho kwa Makanisa." "Maneno ya Roho kwa makanisa" inafichua na kuongoza tabia ya watu ya nje na maisha yao rahisi ya roho. Hatimaye, inaisha kwa "majaribu ya watendaji huduma."

Ijumaa, 3 Mei 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)


Neno la Mwenyezi Mungu | Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu; hii ni kwa kuwa asili potovu ya mwanadamu inatokana kabisa na Shetani na asili ya mwanadamu imemilikiwa na kupotoshwa na Shetani. Yaani, mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa uovu na ubaya wake. Mwanadamu hakui katika ulimwengu wa ukweli au mazingira matakatifu, na aidha haishi katika mwanga. Kwa hivyo, haiwezekani ukweli kumilikiwa kiasili katika asili ya kila mtu, na zaidi ya hayo, hawawezi kuzaliwa na kiini cha kumwogopa, kiini cha kumheshimu Mungu.

Alhamisi, 2 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu


Matamshi ya Mwenyezi MunguAsili na Utambulisho wa Mwanadamu

Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi. Mimi Siwalaumu mwanadamu, wala Siwaangamizi kwa ukatili au kuwatolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili. Kwa hivyo ingawa wale Waisraeli walinipigilia misumari msalabani hadharani, wao, ambao wamekuwa wanamngoja Masiha na Yehova na kumtamani sana Mwokozi Yesu, hawajasahau ahadi Yangu. Hii ni kwa sababu Sijawatelekeza.

Jumatano, 1 Mei 2019

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea. Hitaji la msingi kabisa kwenu ni kwamba myapokee waziwazi maneno yanayonenwa kwenu. Je, siyo imani iliyovurugika ikiwa unanifuata bila kufahamu kile Ninachosema? Ubora wenu wa tabia ni duni sana. Ni kwa sababu hammiliki uwezo wa kupokea kwamba hamna ufahamu hata mdogo wa kile kinachosemwa. Kwa hivyo, ni vigumu sana kutimiza matokeo yanayotamanika. Mambo mengi hayawezi kusemwa kwenu moja kwa moja na athari ya awali haiwezi kutimizwa.