Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumatano, 23 Januari 2019

Ushuhuda wa Washindi | 1. Upendo wa Mungu Ulikuwa Nami Katika Gereza la Giza la Ibilisi

Ushuhuda wa Washindi | 1. Upendo wa Mungu Ulikuwa Nami Katika Gereza la Giza la Ibilisi

Yang Yi, Mkoa wa Jiangsu

Mimi ni Mkristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nimekuwa mfuasi wa Mwenyezi Mungu kwa zaidi ya miaka kumi. Katika wakati huu, kitu kimoja ambacho sitawahi kusahau ni taabu mbaya sana nilipokamatwa na polisi wa CCP muongo mmoja uliopita. Wakati huo, licha ya mimi kuteswa na kukandamizwa na ibilisi waovu, na kuwa ukingoni mwa kifo mara kadhaa, Mwenyezi Mungu alitumia mkono Wake wa nguvu kuniongoza na kunilinda, kunirudisha kwa uhai, na kunipeleka kwa usalama.... Kupitia hili, kwa kweli nilipitia uvukaji mipaka na ukuu wa nguvu ya uhai wa Mungu, na kupata utajiri wa thamani wa maisha niliyotunikiwa na Mungu.

Jumanne, 22 Januari 2019

uzoefu wa maisha | 8. Kutambua Kuwa Nimekuwa Nikiitembea Njia ya Mafarisayo

uzoefu wa maisha | 8. Kutambua Kuwa Nimekuwa Nikiitembea Njia ya Mafarisayo

Wuxin Mji wa Taiyuan, Mkoa wa Shanxi

Kitu ambacho tumezungumzia mara kwa mara katika ushirikiano wa awali ni njia ambazo zilitembewa na Petro na Paulo. Inasemekana kwamba Petro alizingatia kujijua mwenyewe na kumjua Mungu, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimpenda, ilhali Paulo alizingatia tu kazi yake, sifa na hadhi yake, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimdharau.

Jumapili, 20 Januari 2019

2. Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri

 2. Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri

Xiaoxiao Jijini Xuzhou, Mkoani Jiangsu

Kwa sababu ya mahitaji ya kazi ya kanisa, nilihamishwa mpaka mahali pengine ili kutimiza wajibu wangu. Wakati huo, kazi ya injili mahali pale ilikuwa katika hali duni, na hali ya akina kaka na dada kwa kawaida haikuwa nzuri. Lakini kwa kuwa nilikuwa nimeguswa na Roho Mtakatifu, bado nilijitwisha kila kitu nilichoaminiwa nacho kwa matumaini kamili.

Jumamosi, 19 Januari 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tano

 Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tano

Muda unapita, na kufumba na kufumbua leo imefika. Chini ya uongozi wa Roho Wangu, watu wote wanaishi katikati ya mwanga Wangu, na hakuna anayefikiria yaliyopita ama kuiwekea jana maanani. Nani hajawahi kuishi katika wakati wa sasa? Ni nani ambaye hajapitia katika siku na miezi ya ajabu katika ufalme?

Ijumaa, 18 Januari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) (Sehemu ya Tatu)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Tatu

2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu.

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

Alhamisi, 17 Januari 2019

Wakristo Ushuhuda | Mungu Aliilinda Familia Yetu Wakati wa Maafa

Wakristo Ushuhuda | 8. Mungu Aliilinda Familia Yetu Wakati wa Maafa

Wang Lan, Beijing

Agosti 6, Mwaka wa 2012

Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, mafuriko makubwa zaidi tangu miaka sitini yalipitia kijijini mwetu kwa nguvu mno. Maafa yalianguka kutoka mbinguni, maji ya mafuriko yalichanganya matope na mawe na kuharibu kijiji chote. Nyumba nyingi ziliharibiwa na maji na maporomoko ya matope.

Jumatano, 16 Januari 2019

6. Kwa nini husemwa kuwa wanadamu wapotovu wanahitaji zaidi wokovu wa Mungu aliyepata mwili?

6. Kwa nini husemwa kuwa wanadamu wapotovu wanahitaji zaidi wokovu wa Mungu aliyepata mwili?

       (Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)

     Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

    Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake;

Jumanne, 15 Januari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | 5. Ni zipi tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu?


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | 5. Ni zipi tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu?


Aya za Biblia za Kurejelea:

“Mimi nawabatiza na maji ili mtubu. Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake. Atawabatiza na Roho Mtakatifu, na moto” (MT 3:11).

Jumatatu, 14 Januari 2019

4. Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana” (YN. 5:22).

“Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu” (YN. 5:27).

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi mzima ya mpangilio wa usimamizi wa Mungu inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe. Awamu ya kwanza—uumbaji wa ulimwengu—ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na kama haikuwa hivyo, basi hakuna yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kumuumba mwanadamu;

Jumapili, 13 Januari 2019

Maonyesho ya Mungu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu"


Maonyesho ya Mungu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu"


Mwenyezi Mungu anasema, "chanzo cha uhai hutoka kwa Mungu, kwa viumbe vyote, haijalishi tofauti katika maumbile au muundo. Hata uwe kiumbe hai cha aina gani, huwezi kwenda kinyume na njia ya maisha ambayo Mungu ameweka. Katika hali yoyote, kile Napenda ni kuwa mwanadamu aelewe kwamba bila huduma, utunzaji, na utoaji wa Mungu, mwanadamu hawezi kupokea yote aliyokusudiwa kupokea, haijalishi juhudi au mapambano yake. Bila ruzuku ya uhai kutoka kwa Mungu, mwanadamu hupoteza maana ya thamani katika maisha na kupoteza madhumuni ya kusudi katika maisha."

Jumamosi, 12 Januari 2019

nyimbo za injili | Unapaswa Kupokeaje Kurudi kwa Kristo wa Siku za Mwisho?

Nyimbo za Injili | Unapaswa Kupokeaje Kurudi kwa Kristo wa Siku za Mwisho?

I
Mwili wa Mungu utajumlisha
kiini cha Mungu na maonyesho Yake.
Atakapofanywa mwili,
Ataleta
matunda ya kazi Aliyopewa
ajidhihirishe na Alete Ukweli kwa wote,
awape uhai na awaonyeshe njia.
Mwili wowote usiokuwa na dutu
Yake sio Mwili wa Mungu.

Ijumaa, 11 Januari 2019

Matamshi ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Kwanza"



Matamshi ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Kwanza"


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.

Maudhui ya video hii:

Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo

Hatima ya Binadamu na Hatima ya Ulimwengu Haviwezi Kutenganishwa na Ukuu wa Muumba Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji.